Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Safar 1444 Na: HTS 1444 / 06
M.  Jumapili, 11 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa kuzingatia Udhalilifu wa Watawala wa Sudan, Balozi wa Marekani anakaimu kama Mtawala Mkuu wa Sudan
(Imetafsiriwa)

Balozi wa Marekani nchini Sudan, John Godfrey, mnamo Jumamosi tarehe 10/09/2022, alitembelea El Fasher katika jimbo la Darfur, na kufanya mkutano na serikali ya jimbo hilo, na kusema kuwa ziara yake imekuja kwa lengo la kufahamu hali ya mambo kwa ujumla Darfur, na kinachofuata ni utabikishaji wa Mkataba wa Amani wa Juba, pamoja na kubainisha masuala ya maendeleo na utulivu. Pia imepangwa kuwa balozi na wanachama wa Congress wanaoandamana naye, na afisa wa USAID Mervyn Ferro wakati wa ziara yao ya siku tatu; watatembelea kambi ya wakimbizi ya Zamzam, na kufanya mikutano na viongozi wa Idara ya Wenyeji na kamati za upinzani, na pia kutembelea Chuo Kikuu cha El Fasher na kijiji cha Tora, kaskazini mwa El Fasher.

Anachofanya balozi wa Marekani nchini Sudan ni uingiliaji wa wazi katika mambo ya ndani ya nchi, na ni kiini cha majukumu ya raisi wa nchi, au mwakilishi wake, kwa hiyo je balozi wa Marekani amekuwa mtawala mkuu wa Sudan? ! Anakutana na watawala wa majimbo, anakutana na raia wa jimbo, na anazungumzia masuala ya maendeleo na utulivu na amali zengine za mtawala!

Uingiliaji huu haufanyiki katika nchi inayoheshimika ambayo inadai kuwa huru, bali unatokea nchini Sudan licha ya madai ya sheria za kimataifa, zinazozuia mabalozi kuingilia kwa njia yoyote ile mambo ya ndani ya nchi mwenyeji, kama ilivyoelezwa katika Ibara ya (41-) 1) ya Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia Yafuatayo: “Bila ya upendeleo kwa fadhila na kinga walizopewa, watu wanaonufaika na fadhila na kinga hizi wana wajibu wa kuheshimu sheria na kanuni za nchi waliyoitabanni, na pia wana wajibu wa kutoingilia masuala ya ndani ya nchi hii.

Magharibi (Amerika na Ulaya) na mabalozi wao nchini Sudan hawaichukulii Sudan kuwa ni dola huru na inayojitawala, hivyo inajuzu kwa mabalozi wote, kwani wanaingilia mambo madogo madogo katika masuala yake, na watawala wa zamani na wa sasa wa Sudan hawasubutu kuwazuia, hata kwa nusu ya neno. Lau dola ya Khilafah ingekuwa imesimama, balozi wa mojawapo ya dola za kikoloni au raia wake asingesubutu kuingia katika nchi yetu bila ya idhini ya Khalifah.

Watu wa Sudan na nchi nyingine za Kiislamu lazima wafanye kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itapata ubwana halisi kwao juu ya nchi yao, na kukata mkono wa mkoloni kafiri kutoka humo. Bali si Amerika wala Uingereza na nchi zote zenye ulafi katika nchi za Kiislamu zitakuwa na ubalozi au balozi huko, kama ilivyotajwa katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah, ambayo itaregea hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, na ambayo Hizb ut Tahrir inaiwasilisha kwa Ummah ili kuisoma, kusimamisha Khilafah kwa msingi wake, na utabikishaji wa hukmu zake. Kwa mujibu wa ibara yake ya 189, inayofafanua uhusiano wa Khilafah na dola nyingine zilizopo duniani, inasema yafuatayo: “Tatu: dola ambazo hatuna mikataba nazo, na dola za kikoloni halisi kama Uingereza, Marekani, Ufaransa, na dola ambazo zina mezea mate nchi yetu kama vile Urusi, zinachukuliwa kuwa dola za kivita kihukmu, kwa hivyo tahadhari zote zinachukuliwa. Sio sawa kuanzishwa uhusiano wowote wa kidiplomasia nayo. Raia wa nchi hizi wanaweza kuingia katika nchi yetu, lakini wakiwa na pasipoti na visa maalum kwa kila mtu binafsi na kwa kila safari, isipokuwa ikiwa nchi hiyo itakuwa nchi ya kivita kivitendo.”

[وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.” [Al-Munafiqun:8]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu