Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  5 Muharram 1445 Na: HTS 1445 / 01
M.  Jumapili, 23 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Suluhisho Haliko nchini Togo au Mahali Pengine Popote, Bali liko katika Kushikamana Amri ya Mwenyezi Mungu ya Kusimamisha Khilafah

(Imetafsiriwa)

Leo, Jumapili, 22/7/2023, huko Lome, mji mkuu wa Togo, kongamano linaoitwa la mashauriano la viongozi wa kisiasa na wawakilishi wa mashirika ya umma kutoka jimbo la Darfur ulizinduliwa. Ilisemekana kwamba lilikuwa ni kwa ajili ya kuweka makubaliano yenye kupelekea msimamo wa umoja kuhusiana na kuzuia athari za vita juu ya mshikamano wa jamii huko Darfur.

Miongoni mwa washiriki mashuhuri katika kongamano hilo walikuwa Muhammad Hassan al-Ta'Shi, mjumbe wa zamani wa Baraza la Enzi Kuu, na Nasr al-Din Abd al-Bari, Waziri wa zamani wa Sheria. Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan, Baraza la Mpito, Al-Hadi Idris, aliiambia Sudan Tribune kwamba hatakuwa miongoni mwa washiriki katika mkutano uliopangwa wa ushauri huko Togo. Pia, Harakati ya Haki na Usawa ilitangaza, kupitia msemaji wake rasmi, Hassan Ibrahim, kwamba hawatashiriki katika mkutano huo, akisisitiza kwamba mkutano huo unafanyika kwa mwaliko wa vikosi vya msaada wa haraka, na ushiriki wa idadi ya watu Watu wa Darfur ambao wanaunga mkono, na washauri kwa kiongozi wake, Muhammad Hamdan Dagalo. Msemaji wa vikosi vya ukombozi wa Sudan pia alikataa ushiriki wa mkuu wa jumuiko hilo, At-Taher Hajar. Ni wazi kwamba kongamano hili ni mwaliko wa vikosi vya msaada wa haraka. Hii ni licha ya kukanusha kwa Youssef Ezzat, mshauri wa Hemedti, ambaye alisema kwamba atashiriki na waraka bila kubainisha ni nani aliyeitisha kongamano hilo.

Inaonekana kwamba kongamano hili ni idhini kutoka Marekani, kwa sababu wengi wa washiriki ni watu wake, na wengi wa wapinzani ni watu wa Ulaya, nayo, yaani, Marekani, inataka kuvifanya Vikosi vya Msaada wa Haraka kulidhibiti jimbo la Darfur endapo litajitenga katika siku zijazo, Mwenyezi Mungu awapishe mbali.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunaonya juu ya uzito wa kile kinachotokea nchini Sudan, na njama zinapangwa dhidi yake na Kafiri mkoloni, ambazo zinatekelezwa kwa mikono ya baadhi ya wanati wake, hata ikiwa hiyo inahusisha umwagaji damu, fedheha, uporaji wa mali, na uharibifu wa nchi. Kwa hivyo, tunasema kwa vikosi vyote vya kijeshi (jeshi, Vikosi vya Msaada wa Haraka, na harakati za kisilaha), na kwa nguvu zote za kisiasa katika mielekeo yao tofauti: kiasili ni kwamba nyinyi ni Waislamu, na Uislamu unakuhitajini kujisalimisha kwa hukmu zake na kushikamana na sheria yake, kwa hivyo muogopeni Mwenyezi Mungu katika viumbe vyake, rudisheni akili zenu, tubuni kwa Mola wenu, acheni kumwaga damu ya watu bila ya haki, na ondoeni mikono yenu kutokana na kutekeleza ajenda ya makafiri.

Enyi mlio na ikhlasi miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi, ipeni Nusra (msaada wa nyenzo) Hizb ut Tahrir ili iregeshe maisha kamili ya Kiisilamu, ambayo yanamridhisha Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu