Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  8 Rabi' I 1445 Na: HTS 1445 / 04
M.  Jumamosi, 23 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai: Chombo cha Kisiasa, sio cha Kimahakama

Uadilifu wa Kweli Unaweza tu Kupatikana Kupitia Utekelezaji wa Sheria za Kiislamu chini ya Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)

Pambizoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Karim Khan, alikutana na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, Mwenyekiti wa Baraza la Enzi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Sudan, mnamo Ijumaa, Septemba 22, 2023. Kulingana na ripoti, Karim Khan alimfahamisha Al-Burhan kwamba uchunguzi kuhusu ukiukaji huko Darfur utajumuisha viongozi wa jeshi, akiwemo yeye mwenyewe. Kama ilivyoripotiwa na Al-Arabiya, Mwendesha Mashtaka Mkuu huyo alisema kwamba mahakama italeta tu mashtaka ya ukiukaji huko Darfur endapo kuna ushahidi wa kutosha. Aliongeza kuwa wanayo mamlaka ya kuchunguza matukio huko Darfur yanayohusisha pande zote, na kusisitiza kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliwapatia haki ya kuchunguza matukio ya Darfur.

Inajulikana vyema kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ni moja ya zana za kisiasa za Ulaya, zinazotumika kutia shinikizo vibaraka wa Marekani na kuitumiwa kama karata wakati wowote inapotumikia maslahi yake. Ulaya haijali kuhuku damu ya Waislamu au ukiukaji wa hadhi yao. Machoni mwa wengi, Ulaya na Amerika hushiriki hatia katika uhalifu anuwai. Historia ya Ulaya, haswa Uingereza na Ufaransa, imeshuhudia vitendo dhidi ya Waislamu ambavyo kamwe sio vya kupendeza.

Kile Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai alichokifanya kwa Al-Burhan, na udhalilifu aliomfanyia, kinaonekana na wengine kama njia ya kuwashinikiza viongozi wa jeshi ambao wanachukuliwa kuwa vibaraka wa Marekani nchini Sudan. Shinikizo hili linalenga kuwasukuma kufanya makubaliano na vibaraka wa Ulaya, haswa Uingereza, ambao wanajumuisha vikosi vya uhuru na mabadiliko. Haya yanajiri baada ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Enzi, Malik Agar, kuwashutumu kuwa wafuasi wa kisiasa wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), wakionyesha kuondolewa kwao katika nafasi za madaraka ambazo walikuwa karibu sana. Katika maelezo yake, Malik Agar alisema: "Jaribio lao la kurudi madarakani kupitia mapinduzi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka yameshindwa, na wamegundua kuwa sio sehemu tena ya mahesabu ya awamu hii." Maoni haya yalitiliwa nguvu na Abdel Fattah al-Burhan katika hotuba yake mnamo Alhamisi, Septemba 22, 2023, kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo alionyesha kuwa kutakuwa na kipindi kifupi cha mpito na uundwaji ya serikali ya kiraia inayojumuisha watu huru . Hii inamaanisha kubatilishwa kwa Muundo wa Makubaliano ambayo hapo awali yapeana mamlaka ya mpito kwa watu wa Ulaya, vikiwemo vikosi vya uhuru na mabadiliko.

Kwa kweli inasikitisha kuwa nchi yetu ni jukwaa la njama za mkoloni kafiri magharibi, zinazo tekelezwa na vibaraka wao kutoka kwa jeshi na raia, wote wakitafuta viti vibovu vya madaraka vinavyo endeshwa na mkoloni wa kafiri mwenyewe na kupitia zana zake.

Watu wa Darfur, na hakika watu wote wa Sudan, hawatarajii haki kutoka kwa maadui wa Ummah wa Kiislamu waliomo ndani ya miduara ya utawala au kutoka kwa zile taasisi zao zinazoitwa "za haki". Haki ya kikweli, kama wanavyoamini, itatawala tu wakati dunia itakapoangazwa na nuru ya Khilafah Rashida njia ya Utume, ambayo itarudi hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na itawahisabu wale waliofanya uhalifu dhidi ya Ummah na wanadamu kwa jumla. Katika kusudi kama hilo, na wafanye kazi wenye kufanya kazi.

[إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا * وَنَرَاهُ قَرِيبًا]

“Hakika wao wanaiona iko mbali, * Na Sisi tunaiona iko karibu.” [Al-Ma'arij: 6-7].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu