Alhamisi, 02 Rajab 1446 | 2025/01/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Jumada I 1445 Na: 1445 / 06
M.  Alhamisi, 07 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mateso ya Wanawake Kwa Sababu ya Vita Yanathibitisha Haja ya Haraka ya Mfumo wa Kiwahyi ili Kuyapangua Machafuko haya
(Imetafsiriwa)

Katika taarifa moja ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mnamo tarehe 6/12/2023, kuhusu vita vya Sudan, ambapo alishutumu jeshi pamoja na Vikosi vya Msaada wa Haraka, alisema: "RSF na wanamgambo washirika wao wamewahangaisha wanawake na wasichana katika maeneo mbalimbali ya Sudan, kupitia unyanyasaji wa kingono, kuwashambulia majumbani mwao, kuwateka nyara kutoka mitaani, na kuwalenga wale waliojaribu kukimbilia usalama nje ya mpaka...” Taarifa hiyo ilisema: “Kulingana na uchambuzi wa kiangalifu wa sheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na ukweli uliopo, nimeamua kuwa wanachama wa SAF na RSF wamefanya uhalifu wa kivita nchini Sudan.”

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, tunathibitisha yafuatayo:

Kuendelea kwa mashambulizi ya kimpangilio kwa wanawake na watoto kutokana na vita vya Sudan, na mandhari za kutisha zinazopeperushwa na vyombo vya habari, yanaonyesha ukatili wa nyoyo; wao ni kama mawe, bali ni wakatili zaidi, kwani ripoti zilifichuliwa kuhusu wahasiriwa, wanawake na watoto, waliouawa majumbani mwao kwa silaha mbele ya familia zao, bila kusahau silaha zisizodhibitiwa zinazoua watu. Mashambulizi haya hutokea kila siku. Ama habari zinazovujishwa na mahabusu ni za aibu!

Uhalifu huu wa kutisha ni matokeo ya kufuata hatua za Marekani, ambazo ziliibua vita na kuhakikisha kuendelea kwake kupitia Jukwaa la Jeddah, ambalo hukutana na kuahirishwa ili faili libaki mikononi mwa Marekani huku mashini ya vita ikichukua (uhai wa) wanawake na watoto.

Kuhusu ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa, inasimama kimya ikitazama na hata inashirikiana na Marekani katika kutekeleza mkakati wake wa kuigawanya Sudan katika vijidola vidogo ndani ya mfumo mpya wa Sykes-Picot. Inasaidiwa katika hili na kila mtu aliyeshiriki katika mazungumzo kwa niaba ya watu wa Sudan.

Enyi Wanawake wa Kiislamu: Chini ya Uislamu, wanawake waliheshimiwa na kuenziwa, kwa uangalizi na ulinzi dhidi ya kushambuliwa kwa aina yoyote ile, na walikuwa ni heshima iliyolindwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwafukuza Mayahudi wa Banu Qaynuqa kutoka Madina, pindi mmoja wao alipofunua nguo ya mwanamke wa Kiislamu ili kumcheka.

Enyi Watu Wanyoofu Wenye Nguvu na Ulinzi: Humkuumbwa kwa ajili ya kuwalinda madhalimu, wala kupigana kwa manufaa ya chama fulani. Nafasi yenu haitokani na maagizo yaliyoundwa ili kudumisha utiifu wa kipofu katika kumuasi Muumba. Bali, nafasi yenu ni kutetea matukufu na ibada tukufu na heshima, na kufanya kazi ya kusimamisha tena maisha kamili ya Kiislamu, kwa kuwaunga mkono wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itapangua machafuko haya kwa hukmu za Mola Mlezi wa Walimwengu wote, katika nchi za Waislamu, na hata katika ulimwengu mzima.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu