Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  21 Jumada II 1445 Na: HTS 1445 / 17
M.  Jumatano, 03 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je! Ukoloni wa Kimarekani Umeweza Kunasa Sura ya Ukoloni wa Kiingereza, Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko, kwa Mara Nyingine Tena?!

(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne 2/1/2024, vyombo vya habari vilichapisha maandishi ya tangazo la mwisho la mazungumzo ya uratibu kati ya Vikosi vya Kirai vya Kidemokrasia "Taqadum" (sura mpya ya Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko) na Vikosi vya Msaada wa Haraka, ambayo yalifanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na yalitiwa saini na Waziri Mkuu wa zamani Hamdok, mkuu wa uongozi wa "Taqadum", na Mohamed Hamdan Dagalo Hemedti, kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Pande hizo mbili zilikubaliana kuwa "rasimu ya ramani ya utendakazi na tangazo la kanuni zinaunda msingi mpya wa mchakato wa kisiasa ambao unamaliza vita na kuasisi serikali ya Sudan..."

Mkutano huo kati ya "Taqadum", sura mpya ya Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko, na Vikosi vya Msaada wa Haraka, na kufanya makubaliano nayo, inamaanisha kuwa Marekani imefanikiwa kuunganisha vibaraka wa Ulaya na Uingereza (Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko) na kuwaingiza katika uhalifu wa RSF, na unyanyasaji ilioufanya dhidi ya raia, pamoja na mauaji, vitisho, uhamishaji, ukiukaji wa heshima, na wizi wa pesa na mali. Kilichoviingiza Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko ndani ya mtego huu sio chengine ila ni kuvinjari kwao na haraka yao ya kurudi madarakani. Hawakujifunza kutokana na mtego huo ambao hapo awali ulikuwa umewekwa kwao katika Hati ya Katiba, ambao walitumbukia ndani yake mwaka wa 2019 na Baraza la Jeshi na nyuma yake Marekani, wakati muhula wa kwanza wa Urais wa Baraza la Enzi ulipewa jeshi , na muhula wa pili ungekuwa kwa raia baada ya miezi 21. Kabla ya kumalizika kwa muhula wa jeshi kama mkuu wa Baraza la Enzi, mapinduzi ya Al-Burhan yalifanyika mnamo Oktoba 2021, kwa msaada wa Hemedti.

Halafu kukawa na udanganyifu wa muundo wa makubaliano mnamo 15/12/2022, ambayo ikiwa hatimaye yangetiwa saini, ambayo ilipangwa kuwa Aprili 2023, nguvu halisi ingejitokeza kwa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko, ambayo Marekani haiwezi kuruhusu, na hivyo ukaja mchezo wa kuigiza wa mzozo kati ya majenerali hao wawili, Al-Burhan na Hemedti, ambayo ilisababisha vita hivi vilivyolaaniwa ambavyo vilisababisha uharibifu kamili, na kueneza ufisadi katika nchi nzima.

Marekani imefanikiwa kuviburuza Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko ndani ya kinamasi kilichotulia cha RSF, na badala ya kuwaleta karibu na madaraka, itawatenga kabisa nao kutokana na ushawishi wa hasira ya watu wa Sudan kwa uhalifu unaofanywa na RSF.

Enyi watu wa Sudan, Enyi ambao Mwenyezi Mungu amewakirimu na wahyi Mtukufu: Mnawezaje kukubali kung’atwa kutoka kwa shimo moja la ukoloni mara mbili, au hata mara kadhaa, wakati Mtume (saw) amesema: «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi kutoka katika shimo moja mara mbili.”

Vibaraka ni kama mabwana zao, hawajali mambo ya watu au usalama wao. Wanajali tu kukaa kwenye viti (vya utawala) na mabwana zao wakiwaendesha. Msidanganyike kwa maneno ya unafiki na udanganyifu kutoka hapa na pale kwamba wanajali Sudan na watu wake. Udhalilishaji wa miaka sitini na nane ya utawala wa kikoloni kupitia vibaraka wao umetosha kwetu. Hebu naturudi kwa Mwenyezi Mungu kwa toba, na kutawalisha na sheria yake chini ya kivuli cha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume; ambayo itahifadhi umoja wa Sudan na nchi zengine za Kiislamu, kung’oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka nchi yetu, na kuasisi maisha yetu kwa msingi wa Uislamu mtukufu.

Wanyoofu miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi lazima waache upuuzi huu na kuregesha mamlaka yaliyoporwa kutoka kwa Ummah; ambayo majenerali wawili hao wanayapigania katika kuutumikia ukoloni wa Kimarekani! Jukumu kuurudishia tena Umma mamlaka yake yaliyonyakuliwa, kuufanya uwe marekebisho ya njia yake, na huduma kwa imani yake kupitia kusimamisha dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; Ndio njia pekee kulingana na Sharia ya kuzitabikisha nidhamu za Uislamu, kung’oa ushawishi wa makafiri, na kujikomboa kutokana na makucha ya ukoloni.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu