Jumatatu, 04 Sha'aban 1446 | 2025/02/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Rajab 1446 Na: HTS 1446 / 43
M.  Jumatatu, 27 Januari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hotuba ya Kisiasa katika Soko Kuu la Port Sudan
Hatari ya Kubadilisha Hukmu za Uislamu
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa leo, tarehe 27 Rajab 1446 H, sawia na tarehe 27 Januari 2025 M, katika Soko Kuu la Port Sudan chini ya kichwa: “Kubadilisha Hukmu za Mwenyezi Mungu ni Hatari Kubwa na Madhara Makubwa.”

Ustadh Yaqub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza kuhusu ufaradhi wa kusimamisha hukmu za Mwenyezi Mungu na kutabikisha Shariah Yake ndani ya dola na jamii. Alitahadharisha juu ya hatari kubwa inayoletwa na kubadilisha hukmu yoyote kati ya hizi, akisisitiza kwamba umma zilizotangulia, zilipochukua badilisha maamrisho ya Mwenyezi Mungu, zilikumbwa na balaa, uharibifu, na adhabu kali.

Alibainisha kwamba tangu Khilafah ya Kiislamu—dola ya Uislamu na Waislamu—ilipoondolewa miaka 104 iliyopita (Rajab 1342 H – Rajab 1446 H), hukmu za Sharia zimebadilishwa. Kwa hivyo, Waislamu waliachwa na serikali bandia, za kiutendaji ambazo hazina ubwana na zinashindwa kushughulikia matatizo. Badala yake, serikali hizi zinatekeleza mifumo ya dola za kikoloni, kama vile demokrasia, usekula, na utawala wa kiraia na kijeshi, pamoja na mifumo mingine iliyoundwa na mwanadamu.

Amesisitiza zaidi kwamba wajibu wa Waislamu hivi leo ni kusimamisha dola yao wenyewe, Khilafah Rashida, inayotabikisha Sharia na kubadilisha hali ya sasa kuwa bora zaidi.

Wakati wa sehemu ya maingiliano, kulikuwa na watu wengi waliojitokeza, na wahudhuriaji walifuatilia hotuba hiyo kwa hamu kubwa. Amali hiyo ilipata uungwaji mkono mkubwa, huku mhudhuriaji mmoja akieleza kushajiishwa, akisema kwamba yeye hufuatilia hotuba hizi mara kwa mara na aliwahi kuhudhuria amali kama hii katika mji wa Al-Qadarif na sasa huko Port Sudan, alipongeza juhudi hizi katika kuelimisha Umma na kuutaka usimamishe Dini yake kwa kuhuisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu