Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 12 Jumada I 1441 | Na: HTS 1441 / 24 |
M. Jumanne, 07 Januari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wajumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Walikutana na Naibu Katibu wa Kwanza wa Wizara ya Habari na Utamaduni
(Imetafsiriwa)
Wajumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walikutana na Ustadh Ar-Rashid Saeed Yaqoub, Naibu Katibu wa Kwanza wa Wizara ya Habari na Utamaduni, na aliyepewa jukumu la mkurugenzi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Redio na Runinga katika afisini mwake mnamo Jumatatu 06/01/2020. Wajumbe walikuwa wakiongozwa na Ustadh Nasir Ridha – Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, akiandamana na wanachama wawili wa kamati, Sheikh Abdul Qadir Abdul Rahman na Mhandisi Muhammad Mustafa. Wajumbe hao walisisitiza kuwa Uislamu una suluhisho kwa maswala moto nchini, na kutoa mfano wa mapigano na uhasimu ambao unatokea kati ya makabila, japokuwa makabila haya yana muongozo mmoja, ambao ni Uislamu, unaokataza kuua roho, na kukataza ubaguzi wa rangi na migawanyiko ya kimikoa.
Wajumbe pia wameonyesha kuwa nidhamu ya ardhi ya Hawakir ni nidhamu inayogongana na Uislamu, kwa sababu umiliki wa ardhi katika Uislamu haupewi makabila, lakini badala yake hupewa watu binafsi, ima ni kwa ajili ya nyumba au kilimo, na malisho ni ya watu wote, na kuwa suluhisho hizi zinatekelezwa tu katika serikali ya Kiislamu ambayo hutumia vyombo vyote vya habari kufundisha watu kanuni za Uislamu na fahamu kama hizo ambazo tumezitaja.
Mkutano huo pia ulijadili hali ya vyombo vya habari, na kwa muktadha huu, Ar-Rashid aliwauliza wajumbe kuwasilisha ruwaza ya Hizb ut Tahrir ya Khilafah kupitia runinga, akiashiria kuwa ina nafasi ya asilimia 40 ya vipindi vya Kiislamu, na mlango wa vyombo vya habari uko wazi, na kuwa yeye – akimaanisha Ar-Rashid – anataka kuendelea kuwasiliana na chama kuhakikisha kuwa anasikiza maoni na mawazo yake moja kwa moja kutoka kwake, akithibitisha kuwa anakijiua chama na uwepo wake ulimwenguni kote.
Mwisho, Ar-Rashid Saeed aliwashukuru wajumbe wa chama kwa ziara hiyo. Kwa upande mwingine, wajumbe pia walimshukuru yeye kwa mapokezi yake mazuri na kuwasikiliza.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |