Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  25 Safar 1445 Na: 02 / 1445 H
M.  Jumapili, 10 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ushawishi wenye Sumu wa Marekani na Athari Zake Mbaya
(Imetafsiriwa)

Mnamo Agosti 27, 2023, uongozi wa yale yanayojulikana kama SDF (Majeshi ya Kidemokrasia ya Syria), pia yanayojulikana kama QSD, yalimkamata kiongozi wa baraza la jeshi la Deir Ez-Zor baada ya kumvutia, pamoja na baadhi ya makamanda wake, kwenye mkutano mmoja katika kambi ya Waziri huko Al-Hasakah. Kitendo hiki cha udanganyifu kilifanywa na Mazloum Abdi, na baraza la jeshi la Deir Ez-Zor lilikuwa moja ya vitengo vya Kiarabu ambavyo vilikuwa sehemu ya SDF.

Kabla ya tukio hili, kutokubaliana kulitokea kati ya makundi mawili, ambako kulitatuliwa kupitia upatanishi wa majeshi ya Marekani.

Kufuatia kukamatwa kwa Ahmed al-Khubayl, anayejulikana pia kama Abu Khawla, kiongozi wa baraza la jeshi la Deir Ez-Zor, kabila lake lilihamasishwa kudai kuachiliwa kwake. Wito wa kutaka hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Wakurdi walio ndani ya safu za SDF ulipaza sauti zaidi, na maombi yalifanywa kwa Waarabu walio ndani ya SDF kujiuzulu. Hata hivyo, miito hii ilipokea machache.

Ni dhahiri kwamba mkorogo wa Marekani na uingiliaji kati wake wenye sumu ndio sababu ya shida hizi zote. Matokeo ya vitendo hivi ni hatari sio tu kwa umoja wa watu lakini pia kwa utulivu wa eneo. Eneo hili linatamani amani na umoja, likiwa huru kutokana na uingiliaji kati na ajenda za kigeni.

Watoto wa maeneo yaliyokombolewa kaskazini na kaskazini magharibi, wanaosimamiwa na Uturuki, wamejibu kile kinachotokea katika maeneo yanayodhibitiwa na SDF (Majeshi ya Kidemokrasia ya Syria), ambayo yanasimamiwa moja kwa moja na Marekani.

Katika siku za hivi karibuni, tumeshuhudia mwisho wa matukio haya na kurudi kwa vikosi vya SDF kwenda maeneo ya mashariki mwa Mto Furat. Lakini, kile kilichotokea ni hatua ya kwanza katika mpango wa Marekani wa kukuza mgawanyiko kati ya Waarabu na Wakurdi na kuwaangazia viongozi wa Kiarabu wanaohusiana nao, wenye uwezo wa kutekeleza njama zao za kisiasa.

Kama ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir ambayo inabaki kuwa chama kinachoongoza ambacho hakiwadanganyi watu wake, na imekuwa na uzoefu na kujulikana na nyinyi katika miaka yote ya Mapinduzi, hatujasaza juhudi yoyote katika kutoa ushauri na kufichua hatari na njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham. Hivyo basi, ni wajibu kwetu kuwashauri watu wetu na kutoa mwanga juu ya ukweli fulani, tukitumaini kuwa utatumika kama funzo kwa siku zijazo, inshallah.

1- Ni nipi kilichotokea katika majimbo ya Furat Mashariki chini ya macho na masikio ya vikosi vya Marekani? Wao ndio waliowapa nguvu viongozi na watu wa vyama vya kujitenga vya Kikurdi, pamoja na PKK, na wengine katika jimbo hilo lenye idadi ya Waarabu, kuwafanya washirika katika vita vyao dhidi ya 'ugaidi' na kuwawezesha kudhulumu na kukandamiza watu.

Lau ingetaka kukomesha utawala na ukandamizaji wao, ingeweza kufanya hivyo. Lakini, ni Marekani yenyewe ndiyo iliyoruhusu hili kutokea, ikiruhusu mapigano ya hivi karibuni kufanywa ndani ya masikio na macho yake. Hili limeongeza uhasama na chuki kati ya Waarabu na Wakurdi, kwani linaanza kuchora mipaka ya umwagaji damu, likitaka kutenganisha watoto wa taifa moja.

2- Vyama vya Kikurdi vya kujitenga vilivyo madarakani haviwakilishi ndugu zetu wa Kikurdi. Vyama hivi vimejiweka katika huduma ya Marekani na mataifa mengine ya ulaji njama dhidi ya Ummah. Ni ala duni mikononi mwa nchi hizi, zilizodanganywa kwa miaka mingi na bado zinatumika kama silaha hatari dhidi ya vipote vya Wakurdi na Waarabu. Suala sio, kama ambavyo Marekani ingependa iwe, mapigano kati ya Wakurdi na Waarabu; Badala yake, ni mapambano kati ya waliokandamizwa na wenye kukandamiza, kwa msaada wa Marekani kwa malengo maovu.

3- Imedhihirika wazi kwamba uongozi wa Baraza la Kijeshi la Deir ez-Zor umejitenga na uungwaji mkono wa wananchi, sawa na viongozi wengine ndani ya mfumo wa makundi. Wametumia nyadhifa zao, ambazo zilijengwa juu ya damu ya mashahidi na mihanga ya wanamapinduzi, kwa ukandamizaji, utawala, na uvamizi dhidi ya watu wa mapinduzi. Viongozi hawa walipewa dhamana ya kubeba mwenge wa mapinduzi, kuindoa dhulma kutoka kwa watu wao, na kufikia malengo ya uasi wao. Lakini, badala yake, wamekuwa ni ala duni mikononi mwa mataifa yanayo kula njama dhidi ya watu wao wenyewe. Wametoa kwa hamu utiifu kamili kwa mabwana zao, na hivyo kupoteza huruma, uungwaji mkono, na umoja wa watu katika nyakati magumu.

4- Baadhi ya viongozi wa kikabila ambao wamechukua hatua dhidi ya vikosi vya SDF wameanza kutafuta suluhu kutoka kwa Marekani na vikosi vya muungano, na kusahau kwamba Marekani ni mfadhili wa utawala wa uhalifu na muungaji mkono wa mashirika ya Kikurdi yaliyojitenga. Ni nyuma ya njama zote zilizopangwa dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham, ikiwa ni pamoja na suluhisho lake la kisiasa lenye sumu na azimio hatari la kimataifa nambari 2254, ambalo linalenga kukandamiza mapinduzi ya Syria na watoto wake wanyoofu. Je, mapinduzi yatashinda vipi wakati yanatafuta suluhu na uungwaji mkono na wale wanaokula njama dhidi yake mchana na usiku?

5- Harakati za kweli za watu na wito wa dhati wa kuomba msaada ambao umeenea katika maeneo yote yaliyokombolewa ni matendo yenye baraka, yanayoonyesha asili ya kina ya mapinduzi ndani ya nyoyo za watoto wake. Inaonyesha kuwa mapinduzi bado yanawaka ndani yao, licha ya njama za kishetani na njama kubwa zinazofanywa na mataifa yenye uadui na ala zao duni dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham na watu wake waaminifu.

Hata hivyo, miito hii ya wananchi isiyo na mpangilio imethibitisha hitaji la dharura la kuwepo kwa uongozi wa kisiasa wa dhati na makini unaoweza kuzuia juhudi hizi kutoka katika malengo yao na kukwamisha mipango ya wale wanaotaka kunyonya mienendo ya wananchi kwa mipango ya njama zao. Ni muhimu kuziimarisha harakati hizi za dhati kwa mwamko wa kisiasa, kuzifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee na kuinusuru Dini Yake na wanaodhulumiwa miongoni mwa waja Wake.

Zaidi ya hayo, mujahidina lazima waasisi uongozi wa kijeshi wa dhati na wenye uzoefu, wenye jukumu la kupanga juhudi zao na kupanga mipango ifaayo kwa ajili ya vita vya maamuzi na vyenye athari. Hii inahakikisha kwamba hakuna mtu anayewaongoza watu katika vita vya pembeni ambavyo vinamaliza juhudi za wanyoofu na kupanda ukataji tamaa katika nyoyo zao, na kuwapelekea kukubali suluhisho lolote la njama lililowekwa juu ya Mapinduzi ya Ash-Sham. Hili ni sawa na vile watawala wasaliti walikuwa wakifanya kwa kuonyesha kutokuwa na uwezo wa majeshi yao kukabiliana na umbile nyakuzi la Kiyahudi.

Amali za kijeshi zinahitaji mipango na mpangilio sahihi, na lazima ziimarishwe na ufahamu wa uongozi wa kisiasa. Yote haya ni muhimu ili kufikia misingi thabiti ya mapinduzi ya Ash-Sham, ya kwanza kabisa miongoni mwao ikiwa ni kupinduliwa kwa utawala wa kihalifu, katiba yake, nguzo zake zote, nembo zake, na kusimamisha utawala wa Kiislamu juu ya magofu yake.

6- Imethibitika pasi na shaka, kwamba sababu ya kurudi nyuma na kukata tamaa kulikoyapata Mapinduzi ya Ash-Sham baada ya kuanzishwa kwake kwa baraka na udhibiti wake juu ya zaidi ya 80% ya ardhi ya Syria ni kwamba yalikubali msaada na pesa chafu za kisiasa kutoka nje. Hili liliufunga uongozi kwa wafuasi, ambao ulitupora uamuzi wa mapinduzi, ukageuza mkondo wake, na kuyaweka kwenye hila za maadui zetu.

Hakuna wokovu kwetu kutokana na hali yetu ya sasa isipokuwa kwa kukata mikono ya wafuasi, kukataa masuluhisho ya wenye chuki, na kushikamana na kamba yenye nguvu ya Mwenyezi Mungu peke yake. Tunapaswa kuweka tumaini letu Kwake kuinusuru Dini Yake na kuliheshimu Neno Lake kupitia kutabanni mradi mtukufu wa Kiislamu wa kutabikisha mfumo na sheria Zake chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hebu natumwamini Mwenyezi Mungu ili atujaalie kufaulu, hebu na tumnusuru Mwenyezi Mungu ambaye mikononi mwake Peke Yake umo ushindi, ili Mwenyezi Mungu atujaalie ushindi na atutimizie ahadi yake kama alivyosema Yeye, Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surat Muhammad:7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu