Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  17 Muharram 1445 Na: 1445/06
M.  Ijumaa, 04 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia Iliongoza Ujumbe kwenda kwa Wizara ya Uchumi na Mipango
(Imetafsiriwa)

Asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 4/8/2023, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, ukijumuisha Mkuu wa Afisi ya Kisiasa, Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Ustadh Yassin bin Yahya, na Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Ustadh Habib Al-Madini, uliomba mahojiano na Waziri wa Uchumi na Mipango, Ustadh Samir Said, kufuatia kile alichokitamka katika kikao cha mashauriano ya Bunge kilichofanyika mnamo Ijumaa tarehe 28/7/2023 kuwa kuna kukosekana kwa usawa wa uchumi mkuu nchini Tunisia, ambayo inalazimu kwenda kwenye "mageuzi" kwa sababu yamekuwa ya lazima na lazima yawe ya kina, na kuongeza kuwa serikali imeanza kutekeleza mageuzi haya na kuyafanyia kazi muda mfupi uliopita.

Waziri Saied alisema, "Mfuko wa Fedha wa Kimataifa umesalia kuwa chaguo la kwanza na la kukinaisha kwa Tunisia hadi muda huu, na hakuna njia badali ya hilo, akitoa wito kwa wale ambao wana chaguo badali kulifichua na kulitangaza na kulijadili. Ikiwa litakinaisha, basi atakuwa wa kwanza kubadili mawazo yake,” kulingana na usemi wake.

Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri alisema, baada ya kwenda kwa Wizara ya Uchumi na Mipango, “Kauli ya waziri inastahili kuzingatiwa kutoka upande wetu. Hizb ut Tahrir ni mwanzilishi katika kupendekeza masuluhisho ya kina. Waziri mmoja wa zamani alikuwa tayari ameshatoa kauli kama hiyohiyo, akipendekeza kwamba hatuna suluhu zaidi ya kuamiliana na IMF, na tulimuandikia barua na kumweleza kuwa kuna njia nje ya mzunguko wa mfumo wa kibepari ambao ndani yake tabaka la kisiasa katika nchi yetu limeshindwa, miaka mia moja iliyopita, kwa kuitikia maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa.” Ustadh Al-Amiri alisisitiza na kusema: “Mfuko wa Fedha wa Kimataifa hivi sasa uko mbioni kumaliza kile kilichosalia cha ubwana wa nchi yetu ambao unahusiana haswa na uchumi wake.”

Aidha alieleza kuwa ujumbe huo ulikwenda kwa Waziri wa Uchumi na Mipango, ukiambatana na taarifa kutoka kwa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, kwa madhumuni hayo, na kijitabu kiitwacho “Suluhu 10 za Kiuchumi za Kiislamu zinazotuzuia kukopa kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Matawi yake,” kutokana na shauku ya hizb kuwasilisha uwezo wa hukmu za Shariah katika kutatua mgogoro wa kiuchumi, na kwa hakika matatizo yetu yote, kwani ni hukmu zinazochipuza kutokana na itikadi yetu sisi kama Waislamu, na ziko nje ya mduara wa masuluhisho ya viraka ya kibepari yaliyofilisika ambayo yametekelezwa kwa muda mrefu katika nchi zetu, na kuongeza tu umakinishaji wa utawala wa kikoloni.

Wakati tukisubiri kikao na Waziri, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia tunasisitiza umakini wa hizb katika kutoa masuluhisho ya Sharia ili kuiondoa nchi hii kutoka katika migogoro inayofuatana ambayo wakati wake umefika wa kusuluhishwa kimsingi kupitia utekelezwaji Uislamu pamoja na hukmu zake na masuluhisho katika nyanja zote za maisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu