Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 24 Muharram 1445 | Na: 1445/07 |
M. Ijumaa, 11 Agosti 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ulaya Kukimbizana na Wakati katika Kuzinyonya Rasilimali Muhimu za Tunisia
(Imetafsiriwa)
Chini ya mwezi mmoja baada ya Tunisia kutia saini mkataba wa maelewano juu ya Ushirikiano wa Kimkakati na Mpana na Muungano wa Ulaya, ilitangazwa kwa haraka kuwa ilipata zaidi ya euro milioni 300 kutoka kwa Tume ya Ulaya kusaidia ufadhili wa mradi wa uunganishi wa umeme kati ya Tunisia na Italia, haswa kati ya Menzel Tamim na Sicily. Mnamo Agosti 8, 2023, Kampuni ya Umeme na Gesi ya Tunisia (STEG) na mwendeshaji umeme wa Italia Terna zilitia saini makubaliano na Tume ya Ulaya kwa ruzuku ya jumla ya Euro milioni 307 kusaidia maendeleo ya miundombinu ya mradi huu. Kiasi hiki kinaongezwa na mchango wa Italia wa euro milioni 270 kwa mradi huo. Wakati huo huo, Tunisia alilazimika kukopa karibu euro milioni 250 kutoka Benki ya Dunia mnamo Juni 22, 2023, ili kuharakisha ujenzi wa kituo cha ubadilishaji umeme cha Tunisia. Zaidi ya hayo, Tunisia ilikopa euro milioni 300 kutoka Benki ya Ulaya kwa ujenzi na maendeleo ili kukarabati upya Kampuni ya Umeme ya Tunisia. Yote haya yanafanyika wakati nchi inakabiliwa na mgogoro mbaya wa kifedha na kiuchumi, ambao raia wake hubeba shida zake kupitia juhudi na riziki zao. Wanaulizwa kuwa na ustadi na uvumilivu zaidi katika kukabiliana na utendakazi duni wa serikali hii fisadi.
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Umeme na Gesi ya Tunisia, Hichem Elloumi, walisisitiza kwamba makubaliano haya yanawakilisha hatua ya kimkakati ya kuamsha daraja halisi la nishati kati ya Ulaya na Afrika Kaskazini.
Kuhusiana na suala hili, afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia ingependa kufafanua yafuatayo kwa rai jumla:
Kwanza: Hapo awali tulionya juu ya suala la kuunganisha Tunisia na Ulaya katika sekta ya nishati, tukisema kwamba ni njama mbaya. Haimaanishi chochote ila uporaji zaidi, udhibiti, utiifu, na udhalilishaji. Sasa tunaona kwamba serikali inasonga mbele katika kupata nishati kwa bwana wa Ulaya, bila kujali hata kidogo hatima ya watu waliozongwa na deni.
Pili: Pia tulisema kwamba lengo la kuunganisha Afrika Kaskazini na Ulaya katika sekta ya nishati ni kudhibiti vyanzo vya nishati mbadala na machimbuko yao. Kwa njia hii, Ulaya inakuwa mdhibiti wa vyanzo hivi baada ya kupora na kudhibiti mafuta ya kisukuku. Dori ya Tunisia itafungika katika kutoa ajira ya bei rahisi na kukuza miundombinu kwa Ulaya, huku watu wa Tunisia wakibeba gharama kubwa maradufu kupitia mikopo inayodhoofisha ambayo inazidisha mapungufu, umaskini, na utegemezi. Je! Utawala huu utaendelea na ukaidi wake na kufuata sera ya kutoroka kwa muda gani, ikifungia macho ukweli huu wa kisiasa unaong'aa?
Tatu: kumtii bwana wa Ulaya kunakofanywa na serikali mtawalia kunahujumu kauli zote kuhusu uhuru na kujitegemea. Dhati ni ubwana kamili juu ya viwanda muhimu (ikiwemo nishati) katika suala la uzalishaji na usambazaji, badala ya kuzifunga kwa kampuni za kibepari za kikoloni na kuibebesha nchi madeni kwa ajili ya wakoloni wa Ulaya. Wanaiona Tunisia tu kama hifadhi ya nishati, wakifaidika na mwanga wa jua na upepo wake leo kama walivyofanya na gesi na mafuta yake hapo zamani, huku wakiwafanya watawala wake watumishi wa maslahi yao na walinzi wa mipaka yao ya baharini.
Nne: Imeonekana wazi kuwa Tunisia itabaki chini ya macho ya Wazungu, sio tu kwa sababu ni chanzo cha nishati ya msingi na mbadala, lakini pia kwa sababu ndio nukta ya karibu zaidi ya kuiunganisha na bara kwa gharama ya chini zaidi. Kwa hivyo, hakuna njia kwa Tunisia kujiacha huru kutokana na mnyororo wa ukoloni na kukataa aina zote za kujinyenyekesha isipokuwa kupitia dola yenye hadhi na ya kifahari ambayo inatoa maamuzi, sera, na sheria juu ya msingi wa Uislamu. Ubwana ni wa Sharia, na mamlaka ni ya Ummah.
Kwa kumalizia, sisi, katika afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, tunatoa wito kwa watu wote wenye ikhlasi, haswa wale walio na nguvu, ushawishi, maarifa, na maoni, kubeba jukumu la kuunusuru Uislamu na Waislamu na kuikomboa nchi hii kutokana na utawala wa Magharibi na vyombo vyake vya ndani. Hili linaweza kupatikana kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itakomboa nchi na watu wake, ikiwarudishia Waislamu utajiri wao wa madini, vyanzo vya nishati, na mali zengine ambazo Mwenyezi Mungu amezifanya kuwa mali ya umma kwa Waislamu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ؛ فِي الْكَلَإِ وَالْمَاءِ وَالنَّارِ»
“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: malisho, maji na moto.”
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |