Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  12 Sha'aban 1440 Na: 1440/20
M.  Alhamisi, 18 Aprili 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mamlaka ya Tunisia Imeamua Kuihusisha Mahakama ya Kijeshi
(Imetafsiriwa)

Kwa mara ya pili wiki hii, Mamlaka ya Tunisia kimakusudi imeamua kuihusisha mahakama ya kijeshi katika kuishtaki Hizb ut Tahrir katika mashtaka mawili. La kwanza lilikuwa ni shtaka la Ustadh Abdel Raouf Amiri, mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, mnamo 15/04/2019 (lililo akhirishwa). La pili ni shtaka la Mounir Amara, afisa wa Hizb katika Wilaya ya Tunisia, na shtaka lake litafanywa katika Mahakama ya rufaa ya kijeshi nchini Tunisia mnamo Ijumaa, 19/04/2019, ikijua fika kwamba uamuzi msingi katika kesi ya Ustadh Munir Amara haukuwa kusikiliza kesi. 

Ni muhimu kutaja kuwa mashtaka ya kijeshi ya chama hiki yalikuwa kwa sababu ya taarifa kwa vyombo vya habari zilizo chapishwa ili kufichua uhalifu wa kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi ulio tekelezwa na Mamlaka hii, na utumizi wa vikosi vya usalama na jeshi kulinda ujumbe kutoka umbile la Kiyahudi na utumizi wa vitengo vya kijeshi kuyazunguka maeneo ya utajiri kama hifadhi kwa kampuni za kikoloni kutokana na mapinduzi ya vijana wa Tunisia waliotaka kuikomboa nchi yao na utajiri wao kutokana na ufujaji wa kampuni hizo.

Mashtaka haya ya kijeshi ni upanuzi wa mahakama ya kijeshi na taasisi ya jeshi, iliyo dhibitiwa na mamlaka ya Tunisia (iliyo na hamu ya usawazishaji wa mahusiano) ili kupambana na rai na kauli zenye ikhlasi. Ni muundo hatari ambao haukutekelezwa na hata Ben Ali aliye ng'atuliwa, na juu ya hayo, ni uhalifu zaidi juu ya uhalifu wa usawazishaji mahusiano.

Hivyo basi, tunatoa wito kwa waandishi habari wenye ikhlasi na waheshimiwa kuchukua majukumu kamili katika ufuatiliziaji wa kadhia hizi za kijeshi, sio tu kwa sababu zinahusiana na Hizb ut Tahrir, lakini kwa sababu zinahusiana na usalama wa nchi na njama za watawala wa Tunisia dhidi ya nchi hii na nia yao ni kuvilazimisha vyombo vya usalama na jeshi kuwatumikia maadui wa nchi hii…

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu