Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Uamuzi wa Houthi wa Kuziainisha Marekani na Uingereza kama Maadui wa Yemen

Mehdi Al-Mashat, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa, alitoa uamuzi mnamo Jumatatu, 19/02/2024, kuziainisha Marekani na Uingereza kuwa nchi mbili zenye uadui dhidi ya Yemen. Uamuzi huo ulikuja baada ya kupitishwa kwa sheria katika Bunge la Wawakilishi jijini Sana'a, na muda mfupi baada ya kuainishwaji wa Mahouthi kama "kundi maalum lililoundwa la kigaidi la kimataifa."

Soma zaidi...

Nini Kinachotofautisha Uteuzi wa bin Mubarak kutoka kwa bin Abdul Malik katika Serikali ya Aden?!

Mnamo tarehe 6/2/2024, uamuzi ulitolewa na Baraza la Rais mjini Aden kumteua Ahmed Awad bin Mubarak kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Aden, akimrithi Maeen Abdul Malik. Uteuzi wa Ahmed bin Mubarak umekuja baada ya Baraza la Rais kufeli katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kuafikiana juu ya idadi ya wagombea wa nafasi ya uwaziri.

Soma zaidi...

China Haijatia Madoa Mikono yake kwa Damu ya Waislamu huko Palestina, Lakini Imejaa Madoa na Damu ya Waislamu wa Uighur

Gazeti la Al-Thawra, lililotolewa jijini Sanaa mnamo Jumanne, Januari 29, 2024, lilikuwa na kichwa cha habari kutoka kwenye jukwaa "China huko Arabia: Meli za China zakwepa haki ya Yemen kwa sababu China haikutia madoa mikono yake kwa damu ya Wapalestina na haikushiriki katika uharibifu uliotokea kwa Yemen."

Soma zaidi...

Kwa Tangazo la Misaada ya Kigeni kama Silaha Dhidi ya Sanaa Je, Serikali ya Wokovu Imegeukia Misaada ya Kigeni kwa Sababu ya Uhaba wa Machaguo au Hakuna Chaguo Jengine?!

Gazeti la Kila Siku la Al-Thawra, lililotolewa mjini Sanaa mnamo Ijumaa, Februari 2, 2024, lilizingatia majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Hussein Al-Azzi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kupitia tweet yake kwenye jukwaa la X. Alisema: “Waingereza kudokeza kutumia misaada kama silaha dhidi ya watu wa Yemen ni aibu,” Naibu Waziri aliongeza katika tweet yake kwamba “dokezo hili halitawazuia watu wa Yemen kuendelea na uungaji mkono wao wa haki wa msaada wa kibinadamu kwa raia mjini Gaza.”

Soma zaidi...

Taarifa Zafichua sehemu ya Malengo ya Marekani katika Vita katika Bahari Nyekundu

Mnamo Jumatano, Januari 17, 2024, shirika la Bloomberg la Marekani lilifichua kushindwa kwa Washington kufikia mkakati wake unaolenga kuifunga Bahari Nyekundu kwa urambazaji. Shirika hilo lilitaja kuwa takriban meli 114 na meli za mafuta zilivuka Bab el Mandeb mnamo Jumatano iliyopita, siku tano baada ya uvamizi wa majini uliofanywa na vikosi vya kijeshi vya Marekani na Uingereza katika Bahari Nyekundu.

Soma zaidi...

Vitendo vya Mahouthi Vinatekelezwa kwa Ufadhili na Idhini ya Utawala wa Marekani!

Tovuti ya Al-Omama iliripoti katika habari zake chipuka mnamo Jumatano, Novemba 29, 2023, taarifa ya msemaji wa eneo wa Wizara ya Kigeni ya Marekani, Samuel Warburg, chini ya kichwa: "Wizara ya Kigeni ya Marekani: Washington Haina nia ya kuweka Vikwazo Vipya juu ya Mahouthi kwa Sababu Moja Pekee. "

Soma zaidi...

Katikati ya Mvutano wa Nchi za Kikoloni juu ya Ushawishi nchini Yemen ni Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume Pekee ndiyo Itakayomaliza Mateso ya Watu wa Yemen

Mnamo siku ya Jumatano, maandamano maarufu yalianza kwa siku ya pili mfululizo katika Jimbo la Aden. Waandamanaji walifunga barabara katika vitongoji vya Mansoura na Sheikh Othman. Maandamano hayo yalijumuisha majimbo jirani ya Lahj na Abyan, juu ya hali mbaya ya maisha na kuongezeka kwa bei za juu, pamoja na kukosekana kwa huduma msingi kama vile umeme, maji, na huduma za afya, ambazo zimeyasibu Majimbo hayo kusini mwa Yemen kwa miaka mingi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu