Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  15 Jumada I 1444 Na: HTY- 1444 / 08
M.  Ijumaa, 09 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahouthi Wanasubutu dhidi ya Sheria za Mwenyezi Mungu kwa Kuifanya iwe chini ya Uzoefu wa Kiarabu na Kimataifa!!!
(Imetafsiriwa)

Washiriki katika mjadala wa jopo, ulioandaliwa na Wizara ya Sheria na Chama cha Biashara na Viwanda katika mji mkuu, Sana'a, juu ya rasimu ya sheria ya kuzuia miamala ya riba iliyoandaliwa na Wizara ya Sheria, walipendekeza rasimu hiyo ipelekwe kwenye kamati ya kisheria, kiuchumi na Sharia kwa ajili ya uchunguzi kwa kuzingatia uzoefu wa Kiarabu na kimataifa. Haya yalikuja katika hitimisho la kipindi cha Jumatatu, Disemba 5, 2022, mbele ya Mufti Mkuu wa Yemen, Shams al-Din Sharaf al-Din, Waziri wa Haki Nabil Al-Azani, Waziri wa Masuala ya Kisheria Ismail Al- Mahaqari, Waziri wa Bunge na Masuala ya Baraza la Shura Ali Abu Haliqa, na Mshauri wa Baraza Kuu la Kisiasa Abdulaziz al-Baghdadi.

Miongoni mwa yale washiriki waliyoyaeleza ni umuhimu wa kutilia maanani maoni ya Benki Kuu ya Yemen kabla ya kuchukua hatua zozote kuhusu benki na mfumo wa benki, kwani ndiyo mamlaka ya kwanza yenye uwezo kwa mujibu wa sheria kutunga, kutabanni na kutekeleza sera ya fedha, kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha, na kutenda kwa mujibu wa matokeo ya warsha hiyo, ambayo iliandaliwa na Benki Kuu ya Yemen katika mwezi wa Ramadhan iliyopita kuhusiana na suala hili, katika kumbukumbu ya wazi ya kuifanya maregeo benki kuu kwa msingi wa mfumo wa kibepari wa Kimagharibi, ambao nao umeegemezwa juu ya msingi wa nadharia ya utilitarianism (upigiaji debe mambo yenye kukuuza raha na kuridhika) na itikadi ya kutenganisha dini na maisha, wakati kanuni ni kwamba maregeo katika miamala yetu ni kwa yale Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliyoyaletwa kutoka kwa Mola wake Mlezi, Mwenye nguvu na Mtukufu, na kuyakubali na kuyatekeleza katika uhalisia wa maisha yetu bila ya kusitasita au kutoa udhuru.

Ni ajabu iliyoje! Je, washiriki hawatambui kuwa nchi zote za Kiislamu ikiwemo Yemen hazitawaliwi na Uislamu, hivyo wakasonga mbele kujadili matawi na kusahau msingi, au hii ndiyo kazi yao ya kupandikiza majivu machoni na kucheka videvu?! Juu ya hili, kusubutu kwa washiriki katika duara hilo la majadiliano dhidi ya hukmu za Mwenyezi Mungu kumefikia hatua ya kukosa heshima. Na hayo ni kwa wao kuzitiisha hukmu za Shariah kwenye kura ya maoni juu yake. Je, waiharamishe riba au waendelea kuamiliana nayo jinsi inavyoendelea kwa mujibu wa sheria za Kafiri Magharibi zinazotekelezwa nchini Yemen na hata duniani?! Badala ya kusema, “Tumesikia na tunatii,” kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye anasema katika Kitabu chake cha Hekima:

[وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالاً مُبِيناً]

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab:36].

Kisha wanafanya duara za majadiliano na wale waliojaza ndani ya nyoyo zao thaqafa ya Kafiri Magharibi mkoloni na wakafanya kuamiliana na yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kutawale miongoni mwa Umma wa Uislamu kutokana na kutokuwepo mamlaka ya Uislamu, ambayo, Mwenyezi Mungu akipenda, yatarudi tena, kuijaza ardhi haki na rehema, kama ilivyojazwa ugandamizaji, dhulma na taabu. Je, washiriki hao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha riba kwa njia ya wazi na isiyo na utata na upokezaji wa kukatikiwa na maana ya kukatikiwa?! Ambapo Mwenyezi Mungu amesema katika Wahyi usiobadilika:

[وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا]

Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. [Al-Baqarah:275]. Na Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ * فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِه]

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. * Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake!” [Al-Baqarah: 278-9].

Hata kama washiriki katika duara ya majadiliano walitoa sheria inayoharamisha riba, wote ni wenye dhambi, kwa sababu wajibu wa hukumu ulitoka kwao na sio matokeo ya kunyenyekea au kumfuata Mwenyezi Mungu, kama ambavyo Uislamu ni lazima utekelezwe kikamilifu katika nyanja zote za maisha na kutokiuka hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) kwa mujibu wa matakwa na maslahi, vyenginevyo maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yanawahusu wao:

  [أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَنْ يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنْكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَى أَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ]

Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda.” [Al-Baqarah: 85].

Kwa hivyo, Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa Umma wa Uislamu, wakiwemo watu wa Yemen, kutabikisha Uislamu kwa upana na kwa ukamilifu katika mambo yote ya maisha, na imetayarisha mradi kamili kwa ajili ya hilo, ikiwemo kipengee cha kiuchumi, kwani imetoa kitabu, Mfumo wa Kiuchumi katika Uislamu, ambacho kinarutubisha kipengee hiki, kwamba utekelezaji wake utafanyika tu chini ya kivuli cha Dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwa hiyo ni muhimu kufanya kazi ili kuisimamisha, na wajibu wowote ambao hauwezi kutekelezeka bila kwayo, huwa ni wajibu pia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu