Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 12 Jumada II 1444 | Na: HTY- 1444 / 09 |
M. Alhamisi, 05 Januari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maeneo ya Mabomu ya Ardhini katika Pwani ya Magharibi Yamegeuka kuwa Viwanja vya Vifo kwa Watu wa Yemen
(Imetafsiriwa)
Watu wa Yemen wameteseka kutokana na hali ya utegaji wa mabomu ya ardhini tangu kuzuka kwa mizozo ya kisiasa na kijeshi katika miaka ya 1960 na vikiwemo vita vya maeneo ya kati na matukio ya 1994 na kuendelea. Tangu kuanza kwa mzozo wa hivi karibuni wa kimataifa wa Yemen, mabomu ya ardhini yametegwa katika mikoa ya Taiz, Saada, Hodeidah, Ma'rib, Abyan, Lahij, Al-Dhale, Al-Jawf, Al-Bayda, Sana'a, Shabwa na mikoa mingine. Idadi kubwa ya mabomu yaliyotegwa ardhini yametegwa kiholela na hivyo kusababisha ugumu wa kuyapata, pamoja na kukosekana kwa ramani zinazoeleweka, aina ya mabomu yaliyotegwa na kukosekana kwa kada wenye sifa stahiki wa kuyashughulikia ili kuyafukua kwa muda mfupi. Miongoni mwa changamoto za kiufundi ni ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kugundua vifaa hivi na vilipuzi. Pia, kusombwa na mafuriko kwa baadhi ya mabomu ya ardhini kutoka eneo moja hadi jengine inatatiza uhakiki wa maeneo ambayo yamesambaa.
Hatari ya mabomu nchini Yemen inatokana na kuenea kwa wingi wa mabomu yaliyotegwa ardhini, ambayo yamegharimu maisha ya watoto wengi, wanawake na wazee, na kusababisha ulemavu wa kudumu na hasara ya kiuchumi kwa watu binafsi na jamii. Ni dhahiri kwamba utegaji wa mabomu ya ardhini umejikita ima katika vijiji, ardhi za kilimo, au ndani ya majumba, shule, misikiti, na maeneo ya malisho, na hii inaweza kuwa kwa madhumuni ya kijeshi, lakini ilikuwa ni kuwatisha watu wakati huo huo. Hii inaashiria kwamba vita havikosi njia za kinyama za uharibifu kwa aina mbalimbali za silaha zinazoua watu. Mabomu ya ardhini ni mojawapo ya silaha hizo zinazotumiwa na Mahouthi, hasa katika pwani ya magharibi ya Hodeidah na pia huko Shabwa. Haipiti wiki moja bila wahasiriwa wa mabomu yaliyotegwa ardhini huko. Katika miaka sita iliyopita, raia 1,929 waliuawa, na vituo vya umma 2,872 viliangamizwa au kuharibiwa. Takwimu za hivi punde za Mradi wa MASAM wa Saudia wa kibali cha mabomu ya ardhini cha Mahouthi nchini Yemen zinaonyesha kuwa, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018 hadi Aprili 2022, kituo hicho kilisafisha na kuharibu mabomu 322,789, vilipuzi na makombora.
Inashangaza sana kwa yule anayetega mabomu ardhini na hata baharini ambayo yanapoteza maisha ya watu wa imani yake na nchi yake, wanaokwenda kutafuta riziki, kisha anaomba msaada wa kuyaondoa! Sana'a ilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa wa msaada unaohitajika kwa timu za kutengua mabomu ambazo zilisaidiwa kwa magari ya magurudumu manne, na kisha kutumia magari hayo katika vita. Pia, Mkataba wa Ottawa wa kutengua mabomu ulitiwa saini na serikali ya Aden, ili kutoa msaada kwa Yemen katika uwanja wa utenguwaji mabomu ardhini kwa muda wa miaka 5.
Vitendo vya kikatili vinavyofanywa na pande zinazozozana za ndani dhidi ya watu wa Yemen, vinaashiria kuwa pande hizo hazijali watu wa Yemen na usalama wao. Kama ambavyo hawajali njaa, baridi na joto. Wanajali tu maslahi yao binafsi na maslahi ya dola kubwa zinazoipigania Yemen kwa damu, viungo vya maiti na pesa za watu wake. Ni dola ya haki na uadilifu pekee ndiyo itakayosimamisha mauaji na maangamivu nchini Yemen na watu wake; dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu aharakishe kusimama kwake, na awaongoze watu wa Yemen kuifanyia kazi kwa utambuzi na ikhlasi.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |