Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  9 Dhu al-Hijjah 1444 Na: HTY- 1444 / 27
M.  Jumanne, 27 Juni 2023

 Pongezi za Idd ul-Adha Iliyobarikiwa 1444 H
(Imetafsiriwa)

Inatupa furaha kubwa katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen kutoa pongezi kwa Ummah mzima wa Kiislamu na kwa wabebaji Dawah wanachama, wa Hizb ut Tahrir, wanaume na wanawake, hasa Amiri wa hizb, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah; pongezi na baraka bora na za dhati kwa mnasaba wa Idd ul-Adha iliyobarakiwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie wote ibada na matendo mema katika siku hizi zilizobarikiwa.

Enyi Waislamu:

Kila mwaka mahujaji husafiri kwenda kwenye Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu (swt) kutekeleza ibada ya Hijja katika ngazi moja, ambapo umoja wa Waislamu unadhihirika katika ibada, hisia, hali na malengo, katika mandhari kubwa ambayo maadui wa Waislamu kutoka katika nchi za kikafiri na watumishi wao kutoka kwa watawala wa Waislamu, wanaiogopa. Kwa kuwa hakuna kasumba ya majimbo wala ubaguzi wa rangi au upendeleo wa rangi, jinsia au tabaka, na hakuna mipaka; Mola ni mmoja, Dini ni moja, Qiblah ni kimoja, Ummah ni mmoja, na lengo ni moja.

Umma wa Kiislamu ni Ummah mmoja, Dini yake ni moja, Aqidah (itikadi) yake ni moja, Mola wake ni mmoja na Nabii wake ni mmoja, lakini kilichopungukiwa ni dola moja yenye mtawala mmoja chini ya kivuli cha bendera moja. Katika kila msimu wa Hijja Waislamu hujiuliza: kwa nini umoja huo mkubwa katika Hijja na ibada zake haupatikani katika umoja wa kisiasa uliokuwepo? Ambao Waislamu wamekuwa wakiufurahia kwa karibu karne kumi na nne? Lakini leo hii wanalaani kukaliwa kimabavu mara elfu na kulaani mipaka mara milioni, kwani inawakumbusha makubaliano yaliyolaaniwa ya Sykes-Picot ambayo yaliigawanya dola moja ya Waislamu vipande vipande viitwavyo nchi au falme na utawala wa kisheikh, na wanatamani sana siku watakaposafiri baina ya nchi za Kiislamu kwa uhuru wa hali ya juu, na wanatamani sana siku watakapohiji pamoja na Amir ul Muuminin (Amiri wa Waumini).

Hija ni ibada, ni nguzo ya tano ya Uislamu, lakini kutokana na ufisadi wa tawala na wanaoisimamia, ibada hii imegeuka kuwa biashara. Kila mwaka tatizo la gharama kubwa za Hijja linaongezeka, ambalo limekuwa ni tatizo na kizungumkuti kinachomsumbua kila mtu, hasa wale wenye kipato kidogo, wale wanaotaka kufanya ibada hii tukufu, hivyo wanakusanya pesa kwa shida sana, na wanaweza hata kuuza baadhi ya mali zao ili kuweza kuifanya. Kwa hivyo, msimamo wa dhati lazima uchukuliwe mbele ya wakiritimba na wafisadi. Ulafi na ukiritimba huo hautatatuliwa isipokuwa kwa dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, inayotekeleza mipaka ya Mwenyezi Mungu (swt), na ibada zake zifanywe kwa kumtii Mwenyezi Mungu (swt), sio kuchuma pesa.

Idd hii imewasili katika mazingira magumu ambayo Ummah mzima wa Kiislamu unakabiliana nayo. Yemen, ambayo ilikuwa na furaha chini ya utawala wa Uislamu, imegubikwa na masaibu kila upande, mchana na usiku, kwa sababu ya watawala vibaraka ndani na nje ya nchi ambao hawathamini matukufu ya Mwenyezi Mungu (swt). Hawatawali kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, bali wanatawala kwa mfumo wa kisekula wa kijamhuri uliolazimishwa juu yao na adui yao!! Njia pekee ya kutoka katika maafa na migogoro hii inayoubana na kuuponda Ummah ni kuufanyia kazi utawala wa Kiislamu chini ya Dola ya Khilafah Rashida inayounganisha Ummah na kusimamisha utawala wa Uislamu. Sisi katika Hizb ut-Tahrir tunatoa wito kwa Umma wa Kiislamu ufanye kazi nasi ili kusimamisha faradhi hii kubwa, taji la faradhi, na tunaiweka mikononi mwenu rasimu ya katiba tuliyoitayarisha kwa ajili ya dola hii itakayosimamishwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, ili kwa sikio la kufahamu lifahamu kutoka kwa viongozi wanaotafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na kutoka kwa maafisa wa jeshi, washawishi, na kila mmoja katika watoto wa Ummah huu, ili tuitekeleze kivitendo:

Kiarabu: https://www.hizb-ut-tahrir.info/ar/index.php/resources/hizb-resources/21203.html

Kiingereza: https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/literature/hizb-resources/2122.html

Ewe Mwenyezi Mungu, uharakishe ushindi na afueni; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu