Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  22 Dhu al-Hijjah 1444 Na: HTY- 1444 / 28
M.  Jumatatu, 10 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hadhramout Inahitaji Dola yenye Kusimamia Uislamu, Sio Kujitawala Yenyewe
(Imetafsiriwa)

Mwishoni mwa Juni 2023, Mkuu wa Baraza la Rais nchini Yemen, Rashad Al-Alimi, alitangaza rasmi kuidhinisha kujitawala wenyewe kwa Jimbo la Hadhramout na akaahidi kujumlisha uzoefu huu kwa majimbo yote. Katika hotuba ya televisheni iliyotangazwa huko Hadramout, alisema, "Tunakubaliana na gavana kwamba Hadhramout itajisimamia yenyewe kifedha, kiutawala, na kiusalama. Ikiwa uzoefu utafaulu, tutaupanua kwa majimbo mengine."

Kutoa mamlaka ya kujitawala wenyewe kwa Hadhramout si chochote zaidi ya suluhisho la kiviraka la Baraza la Rais. Ni maneno matupu na jaribio la kutuliza mihemko baada ya sauti ya dharau inayoongozwa na baadhi ya watu wanaodai kuwa viongozi wa kijamii katika Hadhramout kutokana na dhulma walizofanyiwa watu huko. Huku wananchi wa jimbo hilo wakiteseka sana, wakishuhudia uporaji wa rasilimali za nchi mbele ya macho yao na kustahamili njaa, umaskini, na mateso ya kimfumo katika huduma za umeme na maji, pazia limeinuliwa kwa miradi iliyogharimu zaidi ya riyal bilioni moja za Saudi kwa uchapishaji wa vitabu vya shule, kuanzisha shule za mfano, na kuimarisha ustahamilivu vijijini!

Mzozo mkali jimboni Hadhramout, mojawapo ya majimbo makubwa zaidi ya Yemen, kati ya Saudi Arabia, kibaraka wa Marekani, na Imarati, kibaraka wa Uingereza, haufichiki kwa mtu yeyote. Mwezi uliopita, kuundwa kwa Baraza la Kitaifa la Hadhramout kulitangazwa nchini Saudi Arabia, licha ya kwamba wengi wa wanachama wake ni wafuasi wa Uingereza. Baraza hili linalenga kukabiliana na Baraza la Mpito, linalofadhiliwa na Imarati. Katika kipindi chote cha mzozo huu, makundi mbalimbali yanaundwa, viongozi wanasaidiwa kwa safari na gharama kubwa, huku maslahi na matatizo ya wananchi yakitozingatiwa. Hadramout, pamoja na rasilimali zake nyingi za mafuta, madini, na samaki, haihitaji kujitawala yenyewe ili kuongeza migawanyiko na kuitenganisha na Yemen. Inahitaji dola yenye kujali inayokata mikono ya wezi badala ya kuwalinda, kukomesha dhulma ya kimpangilio, uporaji na ufisadi ambao umelikumba taifa hili kutokana na utabikishaji wa kanuni za kibepari, kupunguza adha kwa wananchi na kutekeleza mageuzi ya kina ili kushughulikia matatizo na mahitaji yao.

Watu wa Yemen, wakiwemo watu wa Hadhramout, na Waislamu kwa jumla, wanapata mateso ya aina mbalimbali kutokana na watawala vibaraka. Sera ya kusambaratisha iliyotabanniwa na Uingereza wakati fulani na Marekani wakati mwingine, kwa mujibu wa maslahi yao, inadhoofisha tu na kuugawanya Ummah. Wanajaribu kujionyesha kama suluhisho kwa kuwasambaratisha, lakini ni mithili ya mtu kumchorea mkate mwenye njaa! Iraq na Sudan ni mashahidi wa moto uliosababishwa na masuluhisho haya, pamoja na ukiukaji wao wa Sharia unaoweka umoja wa Ummah.

Dola ya Kiislamu pekee ndiyo yenye uwezo wa kutoa maisha ya staha kwa Waislamu wote, kuhifadhi mali zao na kuzigawanya kwa usawa, na kuwahakikishia haki zao bila mapendeleo au ubaguzi. Ni dola inayolea, kupeana, na kutoa, bila kupata faida kutokana na raia wake. Hulisha wenye njaa, huvisha walio uchi, na kuwatunza vijana na wazee. Uislamu pekee ndio wenye uwezo wa kumkomboa mwanadamu kutoka katika mfumo wa kibepari na mateso yake ambayo yanaathiri wanadamu wote. Kurudi kwa Uislamu, unaowakilishwa na dola yake, Khilafah, kwa njia ya Utume, inayopigiwa debe na Hizb ut Tahrir, kuko karibu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً] “na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51].

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ] “Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum: 4,5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu