Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Marufuku ya Hijab ya Ubelgiji: Kutopendelea upande wowote kama Haki mpya ya Kimungu (Droit Divin)

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) imeidhinisha marufuku ya Ubelgiji ya kuvaa hijab shuleni, uamuzi ambao umezusha mijadala kuhusu uhuru wa kidini na usekula barani Ulaya. Mahakama ilipata kwamba marufuku hiyo, iliyokusudiwa kuhakikisha ‘kutopendelea upande wowote’ katika elimu ya umma, haikiuki Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu. Kesi hiyo ilianzishwa na mwanafunzi mmoja Muislamu ambaye alidai kuwa sera hiyo inakiuka haki zake za uhuru wa dini na elimu. Hata hivyo, ECHR iliamua kwamba marufuku hiyo ilihalalishwa na haja ya kudumisha ‘kutopendelea upande wowote,’ kama ilivyotarajiwa.

Soma zaidi...

Ash-Sham ndio Nyumba ya Khilafah

Tunaweza kusema kwamba kuwasili kwa Khilafah katika Bait ul Maqdis kuna dalili zaidi ya moja. Ya kwanza ni kwamba Bait ul Maqdis ni eneo la kihistoria, kisiasa na kijografia la ulimwengu wa kale. Ni kitovu cha dini zote na kitovu cha umakini wao. Yeyote anayeidhibiti atatawala ulimwengu wa zamani. Hii ina maana kwamba pale Khilafah itakaposimamishwa, basi Waislamu watatawala ulimwengu mzima licha ya Mayahudi na Wakristo kuwa dhidi yao. Pili ni malipo kwa watu wa Ash-Sham kwa yale yaliyowapata na maumivu, kuvunjika, subira na uvumilivu waliyopitia kwa miongo mingi.

Soma zaidi...

Barakoa Zimepomoka: Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Palestina haitakombolewa kwa kujifunza kuhusu historia yake. Kususia, kutengwa na vikwazo havitaikomboa Palestina. Palestina haitakombolewa kwa msaada wa chakula. Palestina itakombolewa wakati wana shupavu wa Umma katika majeshi ya Waislamu watakapowaasi watawala wasaliti, wakavunja minyororo yao na kuandamana kuelekea Al Quds.

Soma zaidi...

Zama za Mitandao ya Kijamii: Ufichuaji wa Uongo

Kuibuka kwa mitandao ya kijamii, watu wamejikuta wakiweza kuunganika na walioko maeneo mengine ya dunia. Hili liliyapa faida makampuni na serikali hadi ilipotumika dhidi yao. Wakati mauwaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina yalipoanza, watu wa Gaza waliweza kuunganika kwenye majukwaa kama ya TikTok na kuchapisha picha na video juu ya hali ya sasa.

Soma zaidi...

Katika Historia nzima ya Kijeshi ya Kiislamu, Makamanda wa Kijeshi wa Kiislamu Waligeuza Mawimbi ya Vita katika Hali Mbaya. Wako wapi Warithi wa Waheshimiwa wa Leo?

Mtume wetu (saw) ndiye kielelezo pekee kwa maafisa wetu wa kijeshi katika kubadili wimbi la vita. Pindi idadi kubwa ya Waislamu ilipozidiwa na shambulizi la kushtukiza la adui katika Vita vya Hunain, Waislamu waliangukia chini ya shambulizi hilo katika wakati dhaifu na wakavunja muundo. Wimbi la vita lilibadilika kwa muda mfupi na kushindwa kulianza kuonekana.

Soma zaidi...

Kuporomoka kwa Lazima Kulikokaribia

Mfalme Abdullah II wa Jordan hivi majuzi alitembelea Ikulu ya White House kupokea maelekezo kuhusu dori yake katika mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza. Biden alikuwa makini kuushirikisha utawala wa Jordan katika mipango yake ya kusuluhisha usitishaji vita kati ya umbile la Kizayuni na Hamas.

Soma zaidi...

Mauaji ya Halaiki ya Kimya nchini Congo: Kimya cha Magharibi na Usaidizi kwa Jina la Faida

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nyumbani kwa usambazaji mkubwa zaidi wa cobalt, chuma muhimu kinachotumika katika utengenezaji wa betri za lithiam-ion kwa ajili ya simu, tablets na magari ya umeme. Mnamo 2022, akiba ya cobalt ya Congo ilikadiriwa kuwa karibu tani milioni nne za metric, ambazo ziko mashariki mwa nchi, huku akiba ya kimataifa ikiwa ni tani milioni 8.3.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu