Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ijtihadi Zinazohusiana na Mabadiliko - Sehemu ya 2

Jihadi – Ni Njia ya Kusimamisha Khilafah?

Baada ya Waislamu kuihisi hali mbaya waliokuwa wakiishi, utambuzi wa baadhi yao ukaanza kupata nguvu kuelekea kwenye kubadilisha ukweli huu. Maono ya muamko juu ya msingi wa Uislamu yameanza kutambaa miongoni mwao na matokeo yake vyama vya kisiasa na vikundi vimeanza kuundwa kwa lengo la kuleta mabadiliko. Hata hivyo, vimeanza kuelekea kwenye njia tofauti na kukiuka nyingi ya njia za Hukmu za Kisheria. Tofauti hii na migongano imetokana na Ijtihadi za kimakosa walizozifikia. Baadhi yao waliona kuwa jamii ni jamii ya Kiislamu ambayo ina makosa. Kwa hivyo inahitaji marekebisho na sio mabadiliko (uhuishaji). Wao, kwa hiyo, wakaanza kufanya matendo ya kurekebisha kama kutoa usaidizi na misaada kwa masikini, mayatima na wale wenye mahitaji, kujenga maskuli, hospitali, kulingania urekebishaji wa tabia za watu, kulingania watu katika ibadati na kushikamana na Sunnah, kuandika na kuchapisha vitabu vya Kiislamu na thaqafa za Kiislamu na kuwahubiria na kuwaongoza watu kwenye haki. Wamekosea na wamewafanya wengine kukosea wakiwaweka mbali na njia ya sawa (ya mabadiliko). Katika makala iliopita tumeonyesha ufafanuzi unaohusiana na matendo yaliopangwa na Sharia kwa dola, chama na watu binafsi. Pia tumefafanua kuhusiana na matendo hayo hapo juu kuwa ni matokeo ya Ijtihadi za kimakosa, zisizo na mahusiano na suala nyeti la Waislamu, na hatimaye hawatoweza kufikia lengo ambalo Waislamu lazima walifanyie kazi ili kulifikia, yaani, kusimamisha Khilafah na kurejesha kuhukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Katika makala haya, tutajadili matendo ya kunyanyua silaha dhidi ya watawala wa Ulimwengu wa Kiislamu kuwa kama njia ya kurejesha Khilafah.

Baadhi ya makundi katika Ummah wameona kwamba uhalisia ni kuwa maisha ya Waislamu hivi sasa baada ya kuanguka kwa Khilafah sio ya Kiislamu na kuwa watawala waliopo hawatawali kwa Kiislamu. Kwa sababu hiyo, wanaona kuwa ni wajibu kushika silaha dhidi yao, kupigana nao na kuwauwa pindi wakishikilia kuendelea kuwa hivyo. Hii itafuatiwa na kuwaweka watawala watakaotekeleza Uislamu na hivyo tatizo litaondoka. Wale wanaochukua msimamo huu hutegemea dalili zao juu ya Hadithi sahihi zikiwemo:

Hadithi iliopokewa kutoka kwa Ubada bin Saamit (ra):

«بَايَعْنَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى السَّمْعِ وَالطَّاعَةِ فِي عُسْرِنَا وَيُسْرِنَا وَمَنْشَطِنَا وَمَكَارِهِنَا وَعَلَى أَنْ لاَ نُنَازِعَ الأَمْرَ أَهْلَهُ وَعَلَى أَنْ نَقُولَ بِالْعَدْلِ أَيْنَ كُنَّا لاَ نَخَافُ فِي اللَّهِ لَوْمَةَ لاَئِمٍ»

“Tulimpa bay’ah Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) juu ya usikivu na utiifu katika hali ya uzito na wepesi, na kwa tunayoyapenda na tunayoyachukia, na tusizozane na mtu (mtawala) juu ya jambo la usimamizi, na kwamba tuseme haki popote tutakapokuwa, tusiogope kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu” (Bukhari).

Na Hadithi ya Ummu Salamah (ra) aliyesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّهُ يُسْتَعْمَلُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ فَتَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ فَمَنْ كَرِهَ فَقَدْ بَرِئَ وَمَنْ أَنْكَرَ فَقَدْ سَلِمَ وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ ‏‏ ‏.‏ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلاَ نُقَاتِلُهُمْ قَالَ ‏ لاَ مَا صَلَّوْا»

“Viongozi watachaguliwa juu yenu, na mtawaona wakitenda mema na maovu. Yule anayechukia matendo yao maovu basi amejiweka mbali na lawama. Na anayepinga basi amesalimika. Lakini anayeridhia matendo yao maovu na akawafuata (amejiingiza kwenye maangamivu). Watu wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi je, tupigane nao? akasema: Hapana, muda wa kuwa wanaswali,” (Muslim na Abu Dawud).

Hii ina maana kwamba: Muda wa kuwa wanatekeleza Hukmu za Uislamu miongoni mwenu ambapo Swala ni sehemu yake. Hii inafahamika kutokana na upande wa kutaja sehemu ikikusudiwa yote nayo ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

 [فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ]

“Basi na amkomboe (shingo) mtumwa” [An-Nisaa 4:92].

Kwa kutaja shingo ambayo ni sehemu ya mtumwa, lakini mtumwa ndiye aliyekusudiwa. Kwa hivyo inachukuliwa kutokana na hadithi hizi mbili na hadithi nyengine mfano wake kuwa watawala wa Waislamu hivi leo wanaotekeleza hukumu za kikafiri juu yao lazima wapingane na kupambana nao. Vivyo hivyo huwa wanauliwa pindi wakiendelea kuonyesha ukafiri wa wazi ambapo kunapatikana dalili ya wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hii ni kwa sababu wao huwa sio waumini kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ]

“Na wasio hukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri” [Al-Ma’idah 5:44].

Wale waliofuata njia hii kwa lengo la kurejesha maisha ya Kiislamu wamekosa ufahamu kamili wa tofauti baina ya uhalisia ambao tunaishi nao hivi leo na uhalisia ambao Hadithi zimekuja kushughulikia na kutumika. Kile tunachokishuhudia leo kuhusu ukafiri wa wazi haukuanza katika wakati wetu na tumejikuta sisi tukiishi ndani yake kwa kipindi kirefu. Tumezaliwa ndani ya Nchi za Kikafiri (Dar al Kufr), na bado tunaishi ndani yake na tumekuwa tukiishi maisha yasiyo ya Kiislamu katika nchi hizi. Nchi hizi na maisha haya hayajabadilika kwa yeyote kati yetu kinyume na wale waliokuwepo wakati Dola ya Khilafah ilipovunjwa na makafiri na Mustafa Kamal ambapo ilifuatiwa na kuwekwa kwa watawala katika ardhi za Waislamu ili wahukumu kwa mfumo wa Kikafiri. Wakati huo, ilikuwa ni wajibu juu ya Waislamu walioshuhudia uovu huo wa kutisha kuchukua silaha dhidi ya wale wanaochochea uovu huu na kumuuwa kila anayesimama kushupalia dhidi ya njia ya kutekeleza Uislamu.

Kwa hivyo, Hadithi ambazo zimeegemea dalili zao juu yake zinaonyesha kuwa wale wanaoelekezwa kunyanyua silaha na kuwapiga vita watawala ambao wanadhihirisha au kuonyesha Ukafiri wa Wazi (Kufr Bawah) ni, wale Waislamu wanaoshuhudia mabadiliko ya Dar ul-Islam kwenda Dar ul-Kufr. Hii ni kwa sababu Sultan (Mtawala) na Amani (usalama) ni kwa Waislamu na ni kwa hao Waislamu waliotoa Bay’ah kwa Khalifah ili wawatawale kwa Uislamu. Kama mwengine atakuja na kuzozania mamlaka ya Khalifah huyu na kuchukuwa utawala kutoka kwake bila ya haki ili awatawale Waislamu kwa yale asiyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt); pindi hili likitokea, basi itakuwa ni wajibu kwao kumleta kwenye Uislamu au vyenginevyo atauliwa na kurejeshwa Khalifah wao au kufanyike baya’h kwa mwengine awatawale kwa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Hii ni kwa sababu maelezo ya Hadithi ya mwanzo yapo hivi: ‘Isipokuwa mkiona Ukafiri wa Wazi (Kufr Bawah)’ na hii ina maana kuwa (kabla ulikuwa) hujaona Ukafiri wa Wazi kutoka kwa mtawala na baadaye ukaona kutoka kwake au katika kipindi chake. Kwa hiyo, kauli hii inamuelekea yule aliyeshuhudia mabadiliko kutoka kwenye Uislamu kwenda kwenye Ukafiri na haitumiki kwa Waislamu wa wakati wetu ambao hawajashuhudia mabadiliko haya kutokea.

Hii ni kwa upande mmoja na kwa upande mwengine; uhalisia ambao tunaishi, ambao ndio wenye kuhitajika kubadilishwa, sio maeneo ya Kiislamu au maisha ya Kiislamu. Hii ni kwa kuwa matakwa ya maeneo ya Kiislamu hayapo katika eneo lolote miongoni mwa maeneo au ardhi za Waislamu. Masharti ni utekelezaji wa sheria za Uislamu katika nyanja zote za maisha na usalama wa ardhi uwe katika usalama wa Waislamu.

Namna hiyo hiyo inapatikana katika Hadithi ya pili iliotajwa juu inayoeleza: ‘Basi je, tuwapige vita? Akasema (saw): Hapana muda wa kuwa wanaswali’. Maana yake ni kuwa msiwapige vita watawala muda wa kuwa wanatekeleza Sharia za Mwenyezi Mungu. Ikiwa wataacha na kutekeleza chengine kisichokuwa Uislamu basi hapo lazima wapigwe vita. Hii vile vile inawaelekeza wale wanaoshuhudia watawala waliokuwa wakiutekeleza Uislamu.

Kwa namna hiyo, uhalisia ambao Waislamu wanaishi hivi leo tokea kuanza kwa karne ya ishirini, ambayo unahitajika kubadilishwa, unashabihiana na uhalisia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) alipojikuta ndani ya Makkah kutokea muda aliopelekwa na risala kuhusiana na Manat ya Hukmu (Uhalisia ambao Hukumu zinatekelezwa). Kwa hali hiyo, ni muhimu kwa wabebaji Da’wah wanaofanya kazi kuleta mabadiliko kufahamu kwa upana uhalisia huu. Hii ni ili waweze kuchunguza na kutafiti dalili na Hukmu za Sharia zinazotumika juu ya uhalisia huu na hivyo waweze kujifunga na njia za Kisharia katika kufanya kazi ya kuleta mabadiliko. Ili wafanye kazi katika jamii kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyofanya alipokuwa Makkah.

Kwa kuhitimisha, uhalisia wa Waislamu wanaoishi hivi leo, ambao unahitajika kubadilishwa, unashabihiana na uhalisia ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amejikuta akiishi nao ndani ya Makkah tokea muda aliopelekewa ujumbe. Kwa namna hiyo ni muhimu kwa wabebaji Da’wah wanaofanya kazi ya kuleta mabadiliko kutambua kikamilifu uhalisia huu. Hii ni ili waweze kuchunguza na kutafiti dalili na Hukmu za Kisharia zinazotumika kwenye uhalisia huu na ili waweze kujifunga na njia ya Kisharia katika utendaji wenye lengo la kuleta mabadiliko. Ni kwa kutenda ndani ya jamii kama ambavyo Mtume (saw) alivyotenda akiwa Makkah, kwa mujibu wa hatua zilizochukuliwa na Mtume (saw) kama ifuatavyo: Nuqta-ul-Ibtidaa’ (Nukta Kianzio) ambayo ni hatua ya kujifunza thaqafa. Hii inafuatiwa na Nuqtat-ul-Intilaaq (Nukta ya kusonga mbele) ambayo inapelekea kwenye hatua ya Tafaa’ul (maingiliano). Hii tena inafuatiwa na Nuqtat-ul-Irtikaaz (nukta ya Nusra) ambayo hupelekea hatua ya kupata utawala.

Sio siri kwa Waislamu kuwa Hizb ut Tahrir ni kiongozi ambaye hawadanganyi watu wake, na inafanya kazi kufikia lengo lake la kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Inafanya kazi mchana na usiku kufikia lengo lake kwa imani thabiti isioyumba kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) ya ushindi kwa Ummah huu, mamlaka na khilafah haitofeli, na itakuja katika kipindi alichokiweka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakuna shaka kuwa ushindi una sababu moja, ambayo ni kuwa unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

[وَمَا ٱلنَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَكِيمِ]

“Na msaada hautoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikma” [Surah Aal-Imran 3:126].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Hameed bin Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu