Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hakuna Mapumziko Baada ya Leo

Mwanzoni mwa ujumbe huu kulimaanisha jitihada zisizochoka kwa ajili ya Dini hii. Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha kuhusiana na Sayyidna Muhammad (saw),

[يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ* قُمْ فَأَنذِرْ]

“Ewe uliyejigubika! Simama na uonye! [74:1-2]. Kwa aya hii, wahyi ulikuwa ni Ujumbe. “Simama na uonye!” ikimaanisha kujitayarisha kusonga mbele kwa juhudi na kuwaonya watu. Hivyo kwa aya hii, Muhammad (saw) amekuwa RasulAllah (Mtume wa Mwenyezi Mungu) (saw), kama alivyopata Nubuwwah (Unabii) kwa Wahyi wa mwanzo. Yeye (saw), peke yake, lazima sasa abebe ujumbe huu kwa watu ambao hawakuusikia kabla na wakawa wamezama kwenye ujinga. Wakati Mama wa Waumini, Khadija bint Khuwaylid (ra), alipoona mzigo wa mumewe ukiwa na majukumu makubwa ya kuufikisha Ujumbe wa Uislamu, alijitahidi kumliwaza kwa kumwambia اِرتحْ" " “pumzika kwa uzuri.” Hata hivyo, huku akitambua kiundani jukumu kubwa kabisa lililo mbele yake, alisema (saw),

«لا راحةَ بعدَ اليومَ يا خديجة»

“Hakuna mapumziko baada ya leo ewe Khadija.”

Amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa hakika, amesema ukweli. Mtume (saw) alisimama kama alivyo agizwa, kwa miguu yake na kujiweka kwa ajili ya jukumu jipya. Hakukuwa na mapumziko kwake, mpendwa wetu. Imeamuliwa na Bwana wa Ulimwengu (swt) kwamba atawajibika kuubeba mzigo huu mzito wa mizigo yote. Usingizi, utulivu, kivuli mwanana wakati wa joto au ujoto wa kitanda wakati wa baridi imekuwa sasa ni vitu vigeni katika maisha yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisimama haraka kwa ajili ya mazito yanayomsubiri. Jukumu kubwa limemuelemea aliye mzuri zaidi ya viumbe wote, likimsukuma kwenye usumbufu wa maisha ili kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu liwe juu. Mtume wa Mwenyezi Mungu  (saw) alisonga mbele kwa msimamo kamili wa kuondokana na ubinafsi, kutotulia na hakupumzika katika kubeba mzigo wa Amana kubwa kabisa. Yeye (saw) alibeba mzigo wa kuwaongoza wanaadamu na uzito mkubwa sana wa juhudi ya zaidi ya miaka ishirini, hakuna kilichomshughulisha kuondokana na ujumbe huu.

Hakuna mapumziko katika wakati ambapo watu wenye umri wa zaidi ya miaka arubaini hufikiria kupanga mambo ya shughuli zao na familia zao. Wakati wengine wakipumzika na wake zao, Mtume (saw) anamuacha Mama wa Waumini, Khadija (ra), ili kukumbana na mazito na kukataa (kwa wanaolinganiwa) anapoyalingania makabila kwa ujumbe wa Uislamu. Wakati wengine wakipata afueni ya ucheshi wa kufurahisha watoto wao, Mtume (saw) akitumia masaa mengi kujadili na kufundisha kikundi cha Waislamu wapya ili waweze kuyayuka na Uislamu. Hakuna mapumziko katika umri wa miaka hamsini, wakati watu wakilenga juu ya kuoa na njia za kutafuta maisha ya watoto wao, kwani Mwenyezi Mungu (swt) ameuchagua Uislamu uweze kusimamishwa kama dola na hivyo hakuna mapumziko kwake (saw) akiwa ni mtawala, mlinganizi wa mataifa kwenye Uislamu na Faatih (Mfunguaji) wa miji. Na hakuna mapumziko kwenye miaka ya zaidi ya sitini, wakati watu wanastaafu na kushughulikia mashamba na mipango ya maisha kwa wajukuu wao, Yeye (saw) akisimama kidete kuwahubiria watu.

Kwa hakika, tunashuhudia haya hata wakati wa kifo chake kilipokaribia. Kumbuka siku zake za mwisho, Enyi ndugu zanguni, wakati watu wengine wamejikubalisha kupumzika pamoja na vipenzi wao, kuwaenzi wenza wao katika kipindi cha mwisho cha maisha yao, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akipambana kwa umadhubuti mkubwa wa maumbile yake kwa umri wake mkubwa, mwili mgonjwa na unaochakaa. Jumatatu ya tarehe ishirini na tisa Safar mwaka wa kumi na moja Hijria, alihudhuria mazishi katika Al-Baqii’. Wakati anarudi alihisi maumivu ya kichwa na joto la mwili kupanda sana kiasi joto lake kuhisiwa hadi juu ya ukanda wa kichwa. Siku ya jumatano, siku tano kabla kifo chake joto la mwili wake lilipanda zaidi kutokana na ukali wa maradhi yake. Mtume (saw) alidhoofika na kusumbuliwa na maumivu. Hata katika hali hiyo, hakukuwa na mapumziko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mtume (saw) aliamrisha,

«صُبُّوا عَلَيَّ سَبْعَ قِرَبٍ مِنْ سَبْعِ آبَارٍ شَتَّى حَتَّى أَخْرُجَ إِلَى النَّاسِ فَأَعْهَدَ إِلَيْهِمْ»

“Nimiminieni Qirab saba (viroba vya ngozi) vya maji kutoka visima saba tofauti ili niweze kuwatokea watu na kuzungumza nao.” Kisha walimkalisha kwenye chombo na kummiminia maji hadi akasema,

 «حَسْبُكُمْ، حَسْبُكُمْ»

“Inatosha, inatosha.” Akajihisi anajimudu kwenda msikitini. Akaingia hali amejizonga kichwa, akakaa juu ya mimbari na kuwahutubia watu waliokusanyika wakimzunguka. Akasema,

«لَعَنَ اللَّهُ الْيَهُودَ اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ»

“Mwenyezi Mungu amewalaani mayahudi kwa kuyafanya makaburi ya Mitume wao misikiti.” Kisha Mtume (saw) akasema,

«لَا تَتَّخِذُوا قَبْرِي وَثَنًا يُعْبَدُ»

“Msilifanye kaburi langu kuwa kama sanamu la kuabudiwa.” Kisha akajitoa kwa watu na kuwataka kulipa kisasi kwa jambo lolote ambalo huenda limewakwaza, akisema,

«فمَن كُنْتُ جلَدْتُ له ظَهرًا فهذا ظَهري فلْيستقِدْ منه ومَن كُنْتُ شتَمْتُ له عِرضًا فهذا عِرضي فلْيستقِدْ منه»

“Yeyote ambaye nimempiga mgongo wake basi huu mgongo wangu na alipize juu yangu. Na yeyote ambaye nimemvunjia heshima yake basi nami heshima yangu hii, naye alipize kisasi.”

Kumbuka, Enyi ndugu zanguni, maelezo ya Hind bin Abi Halah, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuwa na huzuni sana, akifikiria daima. Alikuwa hana mapumziko (yaani ya muda mrefu).” Hakukuwa na mapumziko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Ilikuwa ni jambo lililo machoni mwake, akifikiria kuhusu masuala ya Ummah, daima akitafuta kwa ajili ya kilicho bora zaidi. Ilikuwa ni katika kasi na hima yake kwa ajili ya harakati yake, bila mapumziko kwa ajili ya kumaliza kazi nzuri na kuonja ladha ya Ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt). Ilikuwa ni katika nguvu ya ibada yake binafsi, wakati miguu yake ikivimba kutokana na Qiyam ul-Layl na alipoulizwa kuhusu hili, alisema,

«أَفَلَا أَكُونُ عَبْدًا شَكُورًا»

“Basi nisiwe mja mwenye shukurani?” Na ilikuwa ni katika umakini wake na uchangamfu wa hotuba yake, akiwalingania wengine kutokana na usingizi wao, kuwahuisha waliochoka na kufanya wasipumzike wale waliotosheka kwa kuhangaikia zaidi na zaidi.

Nishati kwa ajili ya harakati hii na udharura wake ni kutoka kwenye Mwangaza ambao hauzimiki, uliokamilika, ulioepukana na ghushi, Nur (mwangaza) wa Wahyi na ahadi ambazo zinajumuisha radhi za Mwenyezi Mungu Ar-Rahmaan, Ar-Rahiim, Pepo Yake na uhakika wa mapumziko yasio na mlingano katika maisha yasio ujua mwisho, wala kifo, wala maumivu, wala ugonjwa, wala mitihani na dhiki. Angalieni aya nzuri ndugu zanguni wapendwa, tafakari juu yake ili kutu ziondoke kutoka nyoyoni mwetu na ziangaze vyema. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

. [أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ]

“Mnadhani mtaingia Peponi, bila kukujieni kama yaliowajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu” [Surah Al-Baqarah 2:214]. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ]

“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanaosubiri.” [Surah Al-Baqarah 2:155]. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُور[

“Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na bila shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutokana na walio pewa Kitabu kabla yenu na wale walioshiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.”  [Surah Aali ‘Imraan 3:186]

Hivyo, sio shani kuwa mtu kama huyu, kipenzi cha vipenzi wote, Mtume (saw), aliyefunuliwa Wahyi kwa Dini hii na ahadi zilizomo, kumulika nguvu isiochoka kwa wote waliomzunguka, ikiwasha mioyo yao na akili kwa namna ya kipekee, ufuatiliaji ulio thabiti wa radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Kumbuka, kufanya bidii kwa ajili ya Uislamu kuwa ni dola. Kumbuka, Mus’ab (ra) akiyawacha maisha ya anasa na mapenzi ya mama aliye tajiri akifanya juhudi ya kuibeba Dini na kutunukiwa heshima ya kusimamisha Uislamu kuwa ni dola. Kumbuka jitihada za kuieneza dini. Kumbuka, Handhwala (ra), shahidi aliyeacha raha kwa mke wake mpya kwa ajili ya Jihad na ambaye amepata heshima ya mwili wake kuoshwa na Malaika kwa matayarisho kwa ajili ya Pepo. Na kumbuka kuhifadhiwa kwa dola hiyo. Mkumbuke Ammar bin Yasir (ra), akiwa katika umri wa miaka tisini na tatu, ndio ndugu zanguni ni tisini na tatu, akiwaacha wajukuu zake na huenda watoto wake pia, akitembea kwa hatua ndefu kuelekea kwenye vita vya Siffiin, akiangaza njia kwa wengine katika kipindi cha Fitna. Hakuna mapumziko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), au kwa Maswahaba wake (ra), isipokuwa makaazi ya Milele ya Firdaus!

Enyi ndugu! Enyi wenye kutamani usuhuba mwema wa RasuluAllah (saw) katika Maisha Yajayo, Maisha yasiyo na mwisho! Enyi wenye kutaka kuwa wa mbele katika wa mbele! Enyi wenye kutaka kunyanyuliwa kuwa mashahidi! Bebeni Dini hii bila kuchoka, ili mustahiki usuhuba huo na zawadi hiyo. Unganisheni usiku wenu na mchana wenu, msiache kupita hata dakika seuze saa, laleni kwa kutosheleza mahitaji tu, geuzeni macho yenu mbali na anasa za maisha ili muweze kumkabili Mola wenu kwa nyuso za tabasamu. Jitahidini ili juhudi zenu ziongezewe na rasilimali za vitu, jitahidini ili Mwenyezi Mungu (swt) awe radhi nasi, na azizidishe juhudi hizo kwa malipo na matokeo mema. Hakuna mapumziko kwetu, hakuna mapumziko kwetu, hadi mapumziko ya milele Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 31 Disemba 2020 20:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu