- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vipi Khilafah Italinda Uislamu na Ummah wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Tangu Makafiri walipovunja Khilafah Ottomaniya kwa mikono ya Mustafa Kamal, vibaraka Waingereza tangu kubuniwa kwao miaka 94 miladia iliyopita, Ummah wa Kiislamu haujaona zuri lolote isipokuwa kuwa nyuma ya mataifa, ukiishi chini ya hali halisi iliyojaa machungu na fedheha, udhaifu na utumwa. Unaishi chini ya muongozo wa kikafiri na wanaopigia debe ukafiri. Na unaendelea kula makombo kutoka katika meza za dunia huku ukiendelea kulizwa na mataifa yote kutoka Mashariki na Magharibi. Kupoteza cheo chetu ambacho dunia ilikuwa inakiogopa na kupoteza Palestina, Iraq na mengineyo na kutawala kwa Ukafiri juu Waislamu kila mahali kama ilivyo Palestina, Syria, Mashariki Turkistan, Myanmar na nchi nyingine za Waislamu na kuenea kwa umasikini, njaa, ukosefu wa ajira, kudidimia kwa thamani, maadili na kubakia nyuma kisayansi na kiuchumi… yote ni natija ya kukosekana kwa Khilafah.
Kufikiria na thaqafa ya Kimagharibi kuanzia demokrasia, urasilimali, usekula na uhuru; unadhibiti nyanja zote za maisha na nidhamu za serikali, utungaji sheria, uchumi na utajiri, mtaala wa elimu na vyombo vya habari na mwenendo wa maisha. Kwa maana nyingine, nchi za Waislamu ziko chini ya ukoloni Umagharibi katika kila aina zake, kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijeshi ndani ya nchi nyingi.
Machungu ya Ummah wa Waislamu yanayotokana na hali duni yasingelikuwepo lau kungelikuwepo na nguvu ya kuyasitisha au kuyapinga. Nguvu hii inayotishia inaweza kuwa kubwa, ya dhati na yenye nguvu inayotoka ndani ya Ummah; nidhamu yenye nguvu ambayo itakayositisha ukandamizaji na maonevu kwa kuikata mikono na kuyaondosha mamlaka yenye kufanya hivyo. Na nidhamu hii inatokana na itikadi ya Kiislamu ambayo imekuja kwa wahyi ambao tunaamrishwa kuifuata. Kuiwacha inatizamwa kuwa ni udikteta na kurudia nyingine katika kuhukumu ni Ukafiri, kukiuka na ukosefu wa haki. Kuhusiana na udikteta tunaamrishwa tuukufuru ima ni wa kihukumu zinazo husiana na mwanadamu kama mtu binafsi, kama hukm za swala, saumu au zinazo husiana na Ummah kama kikundi ambazo zinatekelezwa kupitia dola mfano nidhamu ya kuadhibu, muamalat, mahakama, uchumi, kijamii, elimu, sera za ndani na nje, makubaliano, vita, kuamrisha mema na kukataza maovu na mengineyo. Yote haya yanaweza kujumuishwa chini ya nidhamu ya dola ya Kiislamu, Khilafah. Hivyo basi, ni kimaumbile kusema kuwa kusimamisha dola hii ni kusimamisha hukm za Uislamu katika ardhi; ni mama wa faradhi zote na ni jukumu nambari moja la kufanya kazi kuisimamisha.
Lakini fikra kuhusu Khilafah ni ngeni na watu wamefahamu kuwa "kurudia Uislamu" ni kurudia katika ibada na akhlaqi za kibinafsi. Fikra za ujamaa, utaifa na uzalendo zilikuwa zenye mvuto sana wakati wa nyuma. Ilidaiwa kuwa Uislamu uko nyuma na ni ndoto isiyoweza kuwa kweli. Lakini shukrani ni kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kufaulu ni Kwake kutokana na kazi ya mukhlisina ndani ya Ummah Wake, Khilafah na umoja wa Ummah chini ya mamlaka ya mtawala anayetawala kwa sheria za Mwenyezi Mungu imekuwa ndio mwito wa Waislamu katika ardhi hii na, licha ya kutofautiana katika njia na baadhi wamepotea njia kutoka ya sawa. Hivyo basi, Khilafah ni moja ya malengo makubwa ya Uislamu na sura kubwa ya umoja na ushikamano unaoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وٰحِدَةً وَأَنَاْ رَبُّكُمْ فَٱتَّقُونِ)
“Na kwa yakini huu Ummah wenu ni Ummah mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.” [Al-Mu’minun: 52]
Kinachoonyesha kiu ya Ummah kutaka Uislamu ni kwamba kila mahali ambapo Waislamu wanatakiwa kupendekeza au kuchagua baina ya ambacho ni cha "Kiislamu" na chengine, katika umoja, miungano au taasisi au nyinginezo mshindi ni ile ya "Kiislamu." Yaliyotokea Tunisia, Misri, Jordan na kwengineko ni ushahidi wa hayo. Wanaoneysha muamko wa Kiislamu ambao unawafanya makafiri Wamagharibi kutetema kwa uoga wa kurudi kwa Uislamu katika ulingo wa mzozo wa kimataifa. Ulianza kupambana na Waislamu kama "wenye misimamo mikali, magaidi na wenye siasa kali."
Ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kuona kwamba sura ya Khilafah inaonekana zaidi kuliko hapo awali. Idadi kubwa wanataka na wanafanya kazi kurudisha utukufu wao wa zamani. Wanamuota Omar al-Farouq, Omar bin Abdul-Aziz, Salah ud-Din al-Ayyubi, Saqr Quraish, Harun ar-Rashid... nk. Wanatamani izza, hadhi, haki na nguvu mpaka warudi wawe Ummah bora uliotolewa kwa watu.
Dola hii ya Kiislamu iliyoahidiwa –Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume – ni dola ya kimfumo ambayo katiba yake imetokana na itikadi ya Kiislamu na Waislamu wamepewa amana ya kuifikisha itikadi hii kwa watu na mataifa yote.
Lau tutaangalia yale ambayo dola ya Khilafah inaweza kufanyia Uislamu na Ummah wa Kiislamu, tutaona ndani ya nyanja zote za maisha:
Utawala kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu utarudi, na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake (saw) utarudi kuwa ndio marudio ya Ummah kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):
(وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ)
“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’ida: 49].
Imamu, mtawala muadilifu atarudi na kundi litaungana baada ya kugawanywa na Ummah utarudi kuwa Ummah mmoja na mwili mmoja baada ya wakoloni kuugawanya na kuufanya kuwa vijidola vingi na makabila mengi. Mtume (saw) asema:
«إِنَّمَا يَأْكُلُ الذِّئْبُ مِنَ الْغَنَمِ الْقَاصِيَةَ» “...Hakika mbwa mwitu humla mnyama aliyepotea.”
Twasema kuwa ni wangapi waliopotea wameliwa tokea kuvunjwa kwa Khilafah; Palestina, Iraq, Kashmir na Mashariki Turkistan wote wamepotea na orodha inaendelea. Wote watakuwa dola moja bila mipaka wala vizuizi na fungamano la kiitikadi litakuwa ndio msingi na kuondosha mafungamano ya uzalendo, utaifa na mafungamano yanayo dorora. Uwiano wa jamii, watu na dola utazidi.
Kwa kurudi kwa Khilafah, ni kurudi kwa usalama na amani na nguvu za Waislamu na cheo chake cha kuogopewa ndani ya mioyo ya maadui zao. Cheo hichi cha kuogopewa kilipotea kwa kupotea Khilafah. Mwenyezi Mungu alikiondosha cheo cha kuogopwa kutoka katika mioyo ya maadui zetu kwa mujibu wa maneno ya Mtume (saw):
«وَلَيَنْـزِعَنَّ اللهُ مِنْ قُلُوبِ أَعْدَائِكُمُ الْمَهَابَةَ مِنْكُمْ» “na Mwenyezi Mungu ataondosha uoga kutoka katika vifua vya maadui zenu wasiwaogope.”
Moja kati yao, hususan watawala wamekuwa kama watumwa. Anaposhambuliwa kimaneno au kimwili na bwana wake, hawezi kufanya lolote na cheo cha kuogopwa na kutishiwa na adui kutarudi, Mtume (saw) anasema:
«نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ» “Mwenyezi Mungu amenipa ushindi kwa kuwaogopesha maadui zangu kwa urefu wa safari ya mwezi mmoja.” na
«الإِسْلامُ يَعْلُو وَلا يُعْلَى عَلَيْهِ» “Uislamu daima uko juu na hautakiwi kupitwa.”
Imamu, ni ngao ambayo nyuma yake tunapigana itarudi, ambaye atatangaza Jihadi kueneza Uislamu duniani kote. Na atayaunganisha majeshi kuikomboa ardhi tukufu ya Palestina na kuirudisha katika moyo wa Uislamu na dola ya Kiislamu, ardhi ya Isra na Mi'raj, ardhi ya Mahsher and Mansher (kujumuika na kufufuliwa).
Umbile la Kiyahudi lisingelikuwepo katika ardhi ya Palestina lau Khilafah ingelikuwepo. Sote tunajua cheo cha Khilafah wakati wa Ottomaniya na kukataa kwao kuipoteza hata kama ilikuwa katika hali dhaifu. Imamu ataulinda Uislamu na Waislamu kila mahali na kujibu uadui na ukosefu wa haki na kuokoa maisha, pesa na majumba yao.
Utajiri wa Ummah wa Kiislamu, rasilimali na pesa zake zitarudishwa, ambazo zimeporwa na Makafiri na vibaraka wao mbele ya macho na masikio ya Waislamu. Uchumi wake utaimarika. Biashara, viwanda na ukulima, mahusiano ya kibiashara tofauti tofauti ndani na nje yatarudi. Khalifah atatumia rasilimali katika kusimamia mambo ya Ummah na maslahi yake ili watu waweze kuishi kwa hali nzuri, ustawi, baraka na furaha. Ibn Khaldun alitaja katika utangulizi wake kwamba yale yaliyopelekwa katika Bait ul-Mal (hazina) ya Waislamu ndani ya Baghdad wakati wa Khilafah ya Abbasiya ya al-Ma'mun ni sawa na dola bilioni 70 na tani 1,700 za dhahabu leo. Itakuwaje leo lau Waislamu wangelikuwa na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na Mwenyezi Mungu (swt) akawabariki na Khalifah mchamungu. Kutabakia nyumba ya Muislamu masikini?! Mwenyezi Mungu amuhurumie Khalifah muadilifu Umar bin Abdul Aziz ambaye chini ya Khilafah yake Waislamu hawakupata hata mtu mmoja anayestahiki Zaka.
Hukm za nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu zitatekelezwa na mabenki ya riba, ukiritimba, ukosefu wa ajira, mapendeleo na watu wa kati na kati wataondoka na kila mmoja aliye na haki ya kufanya kazi au kustahiki cheo atachukua.
Uislamu na Ummah wa Kiislamu utarudi tena katika ushindi wake na izza yake na kuchukua sehemu yake ya mbele ya kisayansi. Elimu itakuwepo katika kila ngazi na haitofungwa kwa matajiri na wenye nguvu. Dola itakuwa na uwezo wa kisayansi na kiteknolojia unaohitajika kwa viwanda vizito, vita vya kisasa na nyanja nyingine za maisha zitakazotumiwa katika ulinganizi wa Uislamu. Yote haya yatawezekana pale tu kutakapo kuwepo na Sultan (kiongozi) mchamungu, anayejali maslahi ya Ummah wake na haya ni kupitia kumiliki viwango vya juu vya kiteknolojia na wanasayansi wabunifu. Panapokuwa na dola ya Khilafah inayodhamini ubunifu, wasomi Waislamu ambao wamehamia Magharibi watarudi. Upeo wa kisayansi na kijeshi utarudi kama ilivyokuwa zamani pale Waislamu walipoweza kushinda upeo wa kisayansi na kijeshi wa Roma na Fursi. Baada ya hilo Waislamu waliweza kuchimbua rasilimali katika ardhi hizo na kuvumbua sheria za kisayansi zinazo watawala na kufaulu kufikia viwango vya juu vya kiutabibu, uhandisi, falaki, maeneo na mengineyo. Ulaya ilituma wanafunzi wake kupokea sayansi kutoka kwa Waislamu.
Hukm za Mwenyezi Mungu na sheria za kuadhibu zitatekelezwa tena. Yeyote atakayekiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu ataadhibiwa. Makosa yanayo ficha fikra sahihi za Kiislamu yataondoka; kwani yametokana na Wamagharibi na wandani wao ambao wamebeba fikra zilizo oza za hadhara ya kisekula ya kirasilimali. Na muundo wa familia na wanawake utarudi katika sehemu yake iliyowekwa na Uislamu, ambayo iliondoshwa na maadui wa Uislamu waliovutiwa na thaqafa ya Kimagharibi na kumpotosha mwanamke kuwa ana haki ambazo Uislamu umemnyima, na kwamba eti amefaulu kupata yale ambayo Uislamu umemnyima, ilhali uhalisia ni kinyume chake; kudorora na majanga yanayomkumba mwanamke yanasababishwa na kukaa mbali na hukm za Uislamu na kubeba mtizamo wa Kimagharibi katika kutafuta haki zake.
Khilafah Rashida italinda hadhi ya Ummah na kuwalinda wanawake na italiongoza jeshi lake. Hivi ndivyo alivyo fanya Mtume (saw) pale ambapo mwanamume Myahudi alipo shambulia vazi la mwanamke Muislamu na ndivyo alivyo fanya Khalifah al-Mu'tasim. Khilafah Rashida ndiyo inayo linda familia na jamii kutokana na makosa na ufisadi na kutekeleza nidhamu ya kijamii na kuondosha uchafu na mchanganyiko. Itaondosha uovu na ukiukaji wa sheria za Mwenyezi Mungu na haki za watu. Khilafah itadhibiti vyombo vya habari na kuviongoza kwa maslahi ya Ummah, itafunga channeli na vipindi vya kifisadi na ufisadi na kufuatilia kwa karibu mitandao ya angavuni ili kuondosha mitandao mibaya kutoka kwa watu. Madhambi na sababu za ufisadi ni natija ya moja kwa moja ya kukosekana kwa umbile la kisiasa linalo tekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu. Izza na ulinzi wa wanawake ni Khilafah, Khilafah ndio mlinzi. Vita vya Wamagharibi dhidi ya vazi la kiShari'ah na sheria za nidhamu ya kijamii ni vita dhidi ya Uislamu.
Baada ya yote haya, na kukosekana kwa muda mrefu kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika maisha yetu kwa kukosekana kwa dola ya Uislamu iliyo dhaminiwa na Khalifah wa Waislamu na mamlaka yao. Kwani haujafikia wakati ambapo Waislamu warudie kile ambacho kitawapa izza na chanzo cha nguvu zao na umoja wao. Baada ya kuona kwa macho yao namna madhambi yalivyo wapelekea kutaabika? Ni kuachana kwao na Dini na kuitelekeza katiba yao na hukm za kiShari'ah. Mwenyezi Mungu (swt), Msema Mkweli, asema:
(وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى * قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا * قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنسَى )
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhalika leo unasahauliwa.” [Ta-Ha: 124-126]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muslima Ash-Shami (Umm Suhaib)