Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakavyo Sitisha Ukoloni ndani ya Ardhi za Waislamu 

Leo kuna zaidi ya dola hamsini za Waislamu, zote zikidai kuwa Uislamu ndio dini yao na chimbuko la utambulisho wao. Dola zote hizi daima ziko katika mchakato wa kujenga na kujenga upya matumaini ya kufaulu katika malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Wamagharibi. Malengo haya yanakwenda kinyume na dini ambayo wengi wanatangaza kujifunga kwayo kama dini ya dola.

• Matatizo ya kimwili na kimali yametokana na kujitenga na kufanya ibada na kumepelekea maumivu ya kimwili, kiakili na kihisia kwa takribani wafuasi bilioni 1.8 wa Uislamu na hawatoweza kuondokana na hili mpaka pale ambapo tatizo linalo sababisha hayo ambalo ni kujisalimisha kwa mabwana wakoloni limeondoshwa kabisa.

• Dola za Waislamu ni wahanga wa ukoloni mambo leo ambao una nguvu lakini hauna majukumu, kwa kuwa ni aina mbaya ya ukoloni. Dola ya Khilafah itahakikisha kuwa hakuna serikali, mashirika, taasisi au wacheza dori kutoka nje wana uwezo wowote kuingilia kati kisiasa, kiuchumi, kijeshi au kielimu katika usimamizi wa mambo ya serikali. Itasitisha uchakachuaji wa uchumi wetu ili kuhudumia maslahi ya serikali za Kimagharibi na mashirika ya kigeni. Itakataa mikopo ya IMF na sera zake ambazo ndio chanzo cha kupunguza matumizi ya serikali katika afya, elimu na aina zote za ustawi na kupunguza thamani ya pesa za Waislamu zikilinganishwa na dolari ya Marekani. Dola ya Khilafah itatekeleza nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu ambayo haitotoa tu suluhisho la umaskini na kuganda kiuchumi katika ardhi za Waislamu bali pia itakuwa ni chanzo cha kulingania nidhamu ya Kiislamu kwa nchi za Ulimwengu wa Tatu ambazo zimetiwa kitanzi kutokana na sera kandamizaji za kirasilimali na mikopo ya riba. Pesa za Waislamu zitadhaminiwa kwa dhahabu na fedha kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt). Hii itamaanisha kuwa fikra ya akiba ya sarafu itaanguka.

• Siasa ni kiungo muhimu katika kusimamisha serikali ya Kiislamu. Kuweko na hisia ya Kiislamu katika siasa ndani ya dola za kikoloni na zisizokuwa za kikoloni zimekuwa kikwazo kwa usekula kutochukua mamlaka kamili. Kuweko kwa makundi ya Kiislamu ni ushahidi tosha kuwa ndani ya mioyo watu wanajua kuwa suluhisho la matatizo yao lipo katika Uislamu. Qur'an na Sunnah ndio itakuwa chanzo cha sheria na chama chochote kitakachokuwa kinalingania chochote kinyume na Uislamu kitakataliwa na kushtakiwa.

Dola ya Khilafah itakuwa na dori ya kufichua sura mbaya ya ulafi wa siasa za kirasilimali ambayo umeipelekea dunia kuwa katika uwendawazimu uliopo sasa ambapo thamani ya maisha inapimwa kwa kutumia pesa na rangi. Nidhamu hii ya kidhalimu ya kisiasa inawatumia watu kama nguru wa kufanyiwa majaribio ya kimatibabu, kijamii au kiuchumi; itaondoshwa katika ardhi zote za Waislamu na hii itakuwa ni mfano mzuri kwa nchi nyingine na njia ya da'wah.

 “Baadhi ya mbinu muhimu za kisiasa ni kufichua uhalifu wa dola nyingine, kuonyesha hatari ya siasa zao, kufichua madhara ya njama zao na kuvunjilia mbali utambulisho wao.” (Kifungu 185, Kielelezo cha Katiba ya Hizb ut Tahrir kwa serikali ya Khilafah)

• Athari nyingine ya ukoloni ni utumwa wa kiakili katika watu. Huku fikra zao zikijaribiwa, uwezo wao ukifedheheshwa, elimu yao ikibandikizwa kuwa haina maana na ushujaa wao ukitajwa kuwa ni uhayawani na kuficha machungu yao eti ni kuiga kwa utiifu. Kurudi kwa Khilafah itakuwa ishara tosha kuwa akili imeanza kubadilika na mengine yatafanywa kutokana na mazingira yatakavyo kuwa yameandaliwa na Dola. Badala ya kukandamizwa, Waislamu watahisi kuthaminiwa na watacheza dori muhimu pasina kurudi nyuma katika itikadi yao. Serikali ya Khilafah itaandaa nidhamu ya elimu ambayo itatibu maradhi ya kukosa utulivu katika akili na kujenga kizazi cha Waislamu wa kweli. Serikali itang'oa ukoloni wa Kimagharibi katika kuingilia kati mtaala wa elimu ndani ya ardhi za Waislamu ambazo zimelenga kupandikiza fikra na utiifu wa Kimagharibi katika akili za vijana Waislamu na kuwafanya kuwa masekula na matamanio na hisio zao ni kwa mujibu wa uhuru. Lakini, Khilafah itatekeleza nidhamu ya kijamii ambayo imejengwa kutokana na Uislamu safi na inayolenga  kujenga utambulisho (Shaksiyya) wa Kiislamu na akili bunifu na za uongozi katika kila nyanja ya maisha na masomo. Itaandaa kizazi ambacho kwa mara nyingine kitatoa kwa ulimwengu akili kama za Abd-al-Rahman al Sufi (aliyevumbua nidhamu ya nyota mbali zaidi ya Milky Way), Ibn Firnas (mtu wa kwanza kuruka angani), Fatima al Fihri (mwanamke wa kwanza kuzindua chuo kikuu), Al Zahrawi (mjuzi wa upasuaji). Hawa ni baadhi tu ya majina kutoka katika historia iliyojaa Waislamu waliofaulu na sababu ya kufaulu kwao ni kutokana na akili iliyojengwa na elimu ya Kiislamu.

 “Lengo la sera ya elimu ni kuunda utambulisho wa Kiislamu kifkra na kitabia. Hivyo basi, masomo yote katika mtaala lazima yachaguliwe kwa msingi wa sera hii.” (Kifungu 171, Kielelezo cha Katiba ya Hizb ut Tahrir kwa serikali ya Khilafah)

• Sera ya Kigeni ya Khilafah itakuwa Da'wah na Jihadi, Waislamu watalindwa na kueneza Uislamu. Ukoloni ndani ya ardhi za Waislamu ulianza tokea Muingereza na nchi za Ulaya zilipoingia katika ardhi za Waislamu na kupora rasilimali zao na kuua watu wao na wanaendelea kupora na kuua

Khilafah itaondosha kambi za kijeshi, majeshi na majasusi wa kigeni kutoka katika ardhi yake na haitokubali kattu mmoja wa wanajeshi wake kutumika kama kibaraka ili kupigana kwa maslahi ya serikali za kigeni. Serikali ya Khilafah pia itasitisha mateso ya Waislamu katika nchi zisizokuwa za Kiislamu. Badala ya kuiomba Umoja wa Mataifa, Khilafah itaunganisha jeshi lake na kuwakomboa watu wa Rakhine, Kashmir, Palestina, Mashariki ya Turkistan na Syria. Viongozi Waislamu madhalimu kama Rais Sisi wa Misri na Muhammad Bin Salman wa Saudi Arabia lazima wahesabiwe kwa makosa ya kumwaga damu za Waislamu. Serikali zote za Waislamu  zitajumuishwa kuwa chini ya dola moja ambayo ina nguvu na uwezo wa kuathiri hali ya kimataifa. Umoja na mamlaka pamoja na nguvu za kweli zitaifanya Khilafah kuwa kubwa kisiasa, kiuchumi na kijeshi na kuogopwa na makafiri wote. Chini ya Khilafah, Waislamu hawatopata tu ulinzi na usalama bali pia watajua maana ya kweli ya Jihadi. Jeshi lililoandaliwa kwa thaqafa ya Kiislamu ndio litakuwa uti wa mgongo wa serikali.

 “Ni lazima jeshi lipewe elimu ya kijeshi ya ustawi wa juu inayowezekana, na kunyanyuliwa ustawi wake wa kifikra kadri iwezekanavyo; na kila mtu katika jeshi kupewa thaqafa ya Kiislamu inayomuwezesha kuwa na busara ya kijumla kuhusu Uislamu.” (Kifungu 67, Kielelezo cha Katiba ya Hizb ut Tahrir kwa serikali ya Khilafah)

Enyi kaka na dada, sote tumechokana na mabaki yaliyo oza ya ukoloni. Wakati umetima wa kuyaondosha pamoja na wale wanaudhamini mfumo huu ulio oza. Umejaza dunia kwa machungu na mahangaiko na tiba iko katika kuikumbatia nguvu waliyopewa Waislamu na Mwenyezi Mungu (swt) –Kutekeleza nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt) katika mgongo wa ardhi hii.

 (وَقُلْ جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا)

“Na sema: "Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!" [Al-Isra: 81]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:49

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu