Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah Anaongoza katika "Ni Nani anacheza ngumu dhidi ya Waislamu!"

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 28 Septemba 2022, Serikali ya India ya BJP ilipiga marufuku shirika la India la Popular Front na mashirika mengine 8 yanayohusiana yaliyosajiliwa kwa miaka 5. Serikali ilidai kuwa imepiga marufuku PFI na makundi washirika wake kwa madai ya kufanya "shughuli zisizo halali" ambazo "zinaathiri uadilifu, uhuru na usalama wa nchi". Imetaja madai ya kundi hilo kuwa na uhusiano na makundi ya Kiislamu yaliyopigwa marufuku – Harakati ya Wanafunzi wa Kiislamu ya India (SIMI) na Jamat-ul-Mujahideen Bangladesh (JMB) - pamoja na Dola ya Kiislamu ya Iraq na Syria (ISIS). Zaidi ya hayo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (MHA) ilisema, "PFI na washirika wake au wanachama au  viongozi wanafanya kazi kwa wazwazi kama asasi ya kijamii na kiuchumi, kielimu na kisiasa lakini, wamekuwa wakifuata ajenda ya siri ya kutia itikadi kali sehemu fulani ya mujtamaa wakifanya kazi kuhujumu fahamu ya demokrasia”. (Chanzo: BBC)

Marufuku hiyo na kukamatwa kwa wakati mmoja kwa zaidi ya watu 275 katika majimbo 15, kulikofanywa kabla ya marufuku, ilishuhudia ushirikiano wa hali ya juu wa Serikali ya Muungano wa BJP na Shirika la Kitaifa la Uchunguzi (NIA) katika kituo hicho na serikali kadhaa za Majimbo (baadhi zikidai hata kuwa dhidi ya BJP), Idara za Polisi za Serikali na Mahakama, na katika visa vingine hata wanajeshi, kutekeleza uvamizi wa usiku wa manane. Waliokamatwa walishtakiwa kwa sheria kali zinazohusiana na Sheria ya Kuzuia Shughuli Kinyume cha Sheria (UAPA). Maandamano ya wanaharakati wa PFI dhidi ya kukamatwa kwa watu hao yalishuhudia kukamatwa zaidi na kusajiliwa kwa zaidi ya kesi 1400 katika muda wa wiki 1. Vitendo visivyo na kifani vya MHA vilisababisha ukashifu kutoka kwa viongozi, wanasiasa na waandishi wa habari kote nchini (Waislamu na wasiokuwa Waislamu) waliuona hata ukamataji huo kama "uliokuwa wa kidemokrasia" na huku wengine wakiunga mkono serikali.

India inashuhudia dhana ya "nani mtiifu zaidi (kwa Hindutva) kuliko mfalme"!. Muhula uliopita wa BJP (2014-2019) ulishuhudia mashambulizi ya kikatili dhidi ya Waislamu yaliyofanywa na mashirika mbalimbali yaliyojifisha guo kama vile Kupinga Uongofu, Kupinga Ulaji Nyama ya Ng'ombe, Kupinga Adhana na mengineyo. Muhula wa sasa (tangu 2019) umeshuhudia kushambuliwa kwa Waislamu na taasisi za serikali zenyewe. Huku muhula wa sasa ukikamilika muda wake, inaonekana kwamba viongozi mbalimbali wa BJP wanajaribu kuonyesha ni nani mkali dhidi ya Waislamu kwa matumaini ya kuwa mgombeaji mwingine wa wadhifa wa Waziri Mkuu. Tunaona haya katika jimbo la Uttar Pradesh kwa Waziri Mkuu (CM) Yogi Adityanath akivunja nyumba za wanaharakati na kuzuia swala katika maeneo ya umma. Tunaona haya katika jimbo la Assam kwa CM Dkt Himanta Biswa Sarma akivunja majengo ya madarassa kwa madai ya uwongo ya "viungo vya ugaidi". Tunaona hili katika jimbo la Karnataka kwa CM Basavaraj Bommai akikataza Hijab katika taasisi za elimu. Na sasa, Waziri wa Mambo ya Ndani Amit Shah akitupa kofia yake uwanjani kwa kuwafungia wanaharakati kwa mamia, akijaribu kuonyesha ni nani anayeweza kuwa mkali zaidi. Mwenendo huu wa kutisha ni sawa na matukio ya Ujerumani ya Nazi ambapo majenerali wa kijeshi walitunukiwa nishani kwa kuongeza mbinu za kuwaangamiza watu wao wenyewe!

Miezi michache iliyopita Waziri Mkuu (PM) Narendra Modi na Jaji Mkuu wa India (CJI) N V Ramana walishiriki jukwaa la umma ambapo PM aliitaka CJI kuharakisha kesi mahakamani. Labda, inafaa zaidi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Modi kuzingatia ushauri wa Waziri Mkuu kwa kutofunga watu bila ya ulazima. Kulingana na data za Takwimu za Magereza za 2021 za India, kati ya jumla ya wafungwa 554,034 katika magereza ya India, ni 122,852 pekee (23%) ndio wafungwa kamili na 427,165 (77%) wako chini ya kesi na maelfu wachache wanatumikia zaidi ya miaka 5 hadi 10 chini ya- kesi bila ya hatia. Zaidi ya 85% ya walio chini ya kesi ni Waislamu na Madalit wanaotoka katika hali zisizo bahatika kiuchumi. Licha ya India kudai kuwa ni demokrasia kubwa zaidi na yenye vipaji tele, 35% ya nyadhifa za Mahakama zimeachwa wazi. Si ajabu kwamba zaidi ya kesi milioni 40 zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali nchini kote. Mwendo wa kesi unaweza kuchukua muda wowote kati ya mwaka 1 hadi 7 kuanzia kwa mahakama za Vikao vya Wilaya hadi Mahakama Kuu za Jimbo hadi Mahakama za Upeo. Kwa kuzingatia demografia ya kiuchumi ya walio chini ya mashtaka, wana changamoto kubwa za kutumia gharama kubwa za kisheria za mara 5, mara 25, mara 100 za mishahara yao ya wastani ya kila mwezi katika Vikao, Mahakama Kuu na Mahakama ya Upeo mtawalia, ikiwa watabahatika kufanya hivyo. Ufisadi wa Mahakama na Uzembe ni nguvu hasi zaidi inayozidisha uchungu wa mfungwa, familia zao na jamii. Inashangaza kwamba ripoti ya kina ya PSI-2021 ambayo ina zaidi ya kurasa 500 inashindwa kuonyesha data inayohusiana na UAPA ambayo sasa ina sifa mbaya sana nchini. Kwa kuzingatia hali halisi ya kutisha ya mahakama za India, mtu anashangaa mantiki ya mbinu ya serikali kufafanua zaidi ya milioni 250 ya watu wake wenyewe badala ya kuongeza natija na uwezo wao. Idadi ya Waislamu wa India iko mbali na kuwa wachache, badala yake iko imara ikilinganishwa na idadi ya watu wa Urusi au Marekani.

Tangu Septemba 11, 2001 imekuwa ndio hali, hasa katika "ulimwengu wa kidemokrasia", ambapo Muislamu yeyote anaweza kudaiwa "kuhusishwa" na makundi (kama vile ISIS au SIMI) au watu binafsi na mamlaka na watu kuridhika na mashtaka na hukumu za vyombo vya habari. Ushahidi wa kuzushwa wa "ugaidi" unaodaiwa na NIA mara nyingi si chochote zaidi ya Vitabu, Stakabadhi, Kalamu/Hard drives au SIM kadi. Sheria kali za UAPA zilizowekwa zaidi kwa Waislamu na Madalit tayari ni ubaguzi kwa ufafanuzi wa kanuni za haki zilizo makinishwa vyema. Wakosoaji wa UAPA wametaja mara kwa mara tofauti hizi ambapo, mtu binafsi anahesabiwa kuwa na hatia na mzigo wa uthibitisho wa kutokuwa na hatia ni kwa mshtakiwa, dhamana inanyimwa kama kawaida na inatolewa kwa ubaguzi, viongozi wa serikali hawawezi kuhesabiwa na mchakato wa mahakama bila kibali cha awali kutoka MHA na zaidi. Serikali inaendelea kuwafungia waandamanaji na wanaharakati, licha ya ukweli kwamba chini ya 3% ya kesi za UAPA husababisha kuhukumiwa huku zikishindwa kuchunguzwa na mahakama. Moja ya madai ambayo MHA ilitoa dhidi ya waliokamatwa ni kwamba walikuwa wanachama wa SIMI. Hali ikiwa ndio kesi, mnamo Machi 2021, mahakama ya Wilaya katika jimbo la Gujarat iliwaachilia huru wanaharakati Waislamu 126 ambao walikamatwa mwaka wa 2001 kama wanachama wa SIMI, mara tu baada ya Waziri Mkuu wa BJP Vajpayee kupiga marufuku SIMI mwaka 2001. Waliokamatwa wengi wao wakiwa ni Waandishi, Walimu, Wanachuoni na viongozi wa Dini walikamatwa walipokuwa wanahudhuria semina ya 8 iliyoandaliwa na Bodi ya Elimu ya Walio Wachache ya India juu ya mada "Vifungu vya Kikatiba kwa Haki za Kielimu za Walio Wachache." Walikamatwa na kuzuiliwa kwa miaka 2 gerezani chini ya sheria za UAPA na kuachiliwa kwa kukosekana ushahidi thabiti baada ya kesi kusikilizwa kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20 ambapo ilivuruga sana maisha yao ya kawaida na riziki zao.

Hakika, MHA na mamlaka yake yaliyopitiliza inaweza kufanya maajabu ambapo kuna haja kubwa ya mabadiliko kama vile kutokomeza uhalifu, ubakaji, dawa za kulevya na ufisadi ambapo India iko juu kuliko nchi nyingi za Asia na Ulaya. Mji mkuu wa India Delhi ulikuwa na uhalifu mara 4 zaidi ya wastani wa nchi hiyo wa 385 kwa kila 100,000 mnamo mwaka wa 2019. Uhalifu dhidi ya wanawake uliongezeka kutoka 54 kwa kila 100,000 mnamo mwaka wa 2015 hadi 62 (kwa kila 100k) mnamo mwaka wa 2019. Afisi ya Kitaifa ya Kurekodi Uhalifu imefichua kuwa uhalifu dhidi ya mwanamke unafanywa kila baada ya dakika 3, mwanamke anabakwa kila baada ya dakika 29, kifo cha mahari hutokea kila baada ya dakika 77, na kesi moja ya ukatili unaofanywa na mume au jamaa wa mume hutokea kila dakika 9. Mnamo mwaka 2021 zaidi ya watoto 121,351 walitoweka huku wanawake wakiwa wengi wao wakiwa wahasiriwa wa biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu wakiishia kwenye madanguro. Silaha haramu zinazosambazwa nchini India ni takriban nusu ya zile haramu zinazosambazwa duniani (zaidi ya milioni 75). Kufikia 2018 India ilikuwa na takriban watu milioni 40 wanaotumia dawa haramu na hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila mwaka, huku bandari nyingi zikibinafsishwa mikononi mwa Adani, mfanyibiashara tajiri wa Gujarat. Mnamo 2021, India ilishika nafasi ya 2 kote duniani kote katika uhalifu wa mtandaoni ikiwa na zaidi ya 52k na inaokua kwa karibu 5% kila mwaka katika miaka michache iliyopita. Faharisi ya ufisadi ya India ilisimamia katika 78 kati ya nchi 180.

Waislamu nchini India na ulimwenguni watatambua kwamba ni dhahiri sana kuona matokeo ya kukosekana Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu. Vitendo kama vile vya serikali ya kidemokrasia ya India havifanywi kwa nia ya kulinda demokrasia kama wanavyodai. Bali ni chuki tupu kwa Uislamu na Waislamu. Licha ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wa India kwa Waislamu na watu wake yenyewe, Amerika au Ulaya hazina nia ya kuizuia, ikionyesha wazi kwamba Umoja wa Mataifa au vyombo vingine kama hivyo vinaombwa pale tu inapokidhi maslahi ya dola ya kikoloni. Badala yake wanaipongeza India kwa kandarasi na viti vya mabaraza/makongamano. Khilafah, tofauti na Umoja wa Mataifa, hakika itasimamia ustawi wa wana wa Adam (as) kwani hakika ni kivuli cha Mwenyezi Mungu duniani. Khilafah inalazimika kutumia njia zote - za kidiplomasia, kiuchumi na kijeshi ili kuhakikisha maisha ya watu na mali haziliwi na mbwa mwitu wa Taghut. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) asema

(وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ)

 “Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji!” [Surah Al-Baqarah: 11].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Riadh Ibn Ibrahim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu