Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Maandamano ya Iran Yanaweza Kufanikiwa?

(Imetafsiriwa)

Maandamano nchini Iran sasa yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Iran tangu kifo cha Mahsa Amini mikononi mwa polisi wa maadili wa Iran, alipokamatwa kwa kukiuka kanuni za mavazi za nchi hiyo. Maandamano hayo yaliyotokea ni makubwa zaidi utawala huo wa watu wa dini kuwahi kukabiliana nayo kwa muda mrefu. Utawala huo wa watu wa dini umekuwa madarakani tangu Mapinduzi ya 1979, lakini miongo kadhaa ya ufisadi, uzembe na usimamizi mbovu wa kiuchumi utawala huo leo ni dhaifu kuliko ulivyowahi kuwa. Ingawa hakuna uwezekano wa serikali hiyo kupinduliwa, hakuna uwezekano pia kuwa inaweza kubakia hali katika muundo wake wa sasa bila kubadilika.

Wakati Shah alipopinduliwa mnamo 1979 simulizi ya utawala wa watu wa dini ilikuwa ni kufanyika kwa mapinduzi ya Kiislamu, ambayo yalikuwa dhidi ya Marekani, yote yalifanywa pamoja na Ayatollah Ruhollah Khomeini mwenye fikra huru, akiwa na malengo makubwa ya kuigeuza Iran kuwa dola ya kikanda. Licha ya mapinduzi hayo kuchukuliwa kuwa ya Kiislamu, makundi yaliyohusika zaidi yalikuwa yasiyo ya Kiislamu na yalijumuisha wakomunisti, wasomi, watu wa mrengo wa kushoto, vyama vya wafanyikazi na wengine wengi ambao hawakuwa wakitafuta mapinduzi ya Kiislamu. Akiwa madarakani Khomeini alijikita katika kukabiliana na vitisho vyote vinavyoweza kujitokeza kwa utawala huo mpya, jambo ambalo lilimpelekea kuyageuka makundi yote yaliyomsaidia kuingia madarakani. Khomeini alikuwa hofu sana hivi kwamba aliunda Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwani hakuliamini jeshi.

Utawala huo wa watu wa dini uliunda nguzo nyingi na taasisi za serikali kudumisha kushikilia kwao madaraka. Waliunda mfumo wa kisiasa ambao umewaruhusu kuitawala Iran na siasa zake tangu wakati huo. Kileleni mwa mfumo huu ni mtu mwenye nguvu zaidi, kiongozi mkuu, wadhifa ambao hadi sasa umeshikiliwa na watu wawili pekee. Wa kwanza alikuwa mwanzilishi wa jamhuri hiyo ya Kiislamu, Ayatollah Khomeini, ambaye alishikilia wadhifa huo kuanzia mwaka 1979 hadi kifo chake mwaka 1989. Alirithiwa na msaidizi wake mkuu na rais wa zamani wa awamu mbili, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo kwa miongo mitatu iliyopita na kwa sasa bado yuko mamlakani. Kiongozi mkuu hachaguliwi kwa kura ya umma bali na Bunge la Wataalamu, ambalo ni kundi la viongozi wakuu wa kidini. Ana mamlaka makubwa na huteua uongozi wa taasisi zenye nguvu zaidi za kisiasa za nchi hiyo, ikiwemo utangazaji wa serikali, Wanajeshi, Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Baraza la Walinzi.

Utawala huo wa watu wa dini mithili ya utawala wa kinasaba wa Pahlavi kabla yake ulianzisha mfumo wa serikali kuu kwani ni 50% -60% pekee ya idadi ya watu wa Iran ndio Wafursi. Iran imegawanywa katika idadi kubwa ya makabila na utawala huo wa watu wa dini kama vile utawala kabla yake hudumisha hali ya usalama sio tu kudumisha utawala wake lakini pia kuwatawala watu walio wachache ambao wanaweza kuwa tishio. Kaskazini-Magharibi mwa Iran wanaishi kabila la Wakurdi na Waazheri ambao hawajioni kama Wafursi. Waazheri wana mavuguvugu ya kujitenga katika mkoa wa Ardabil na wanataka kujiunga na Azerbaijan. Kifo cha Mahsa Amini, ambaye alikuwa Mkurdi, kilisababisha eneo hili kufanya maandamano makubwa zaidi dhidi ya utawala huo. Wakurdi na Waazheri kwa muda mrefu wamekuwa wakitendewa vibaya na serikali kwani hawawaamini. Kusini-Magharibi ni eneo la kimkakati zaidi la Iran la Khuzestan ambalo linashikilia rasilimali zake za kawi. Hapa ndipo Waarabu walipokaa kwa muda mrefu, ambao wamechukua tofauti kwamba eneo hilo liliitwa Ahwaz na hii ilibadilishwa na serikali kuwa Khuzestan ili kuifanya iwe Kifursi. Utawala huo kwa muda mrefu umenyonya utajiri wa nishati wa maeneo hayo na kuacha fujo kubwa katika suala la umaskini na ukosefu wa ajira katika eneo hilo. Katika mipaka ya Mashariki ya Iran kwa muda mrefu kumekuwa na masuala kwenye mpaka wa Afghanistan na mkoa wa Sistan-Baluchistan, ambao idadi kikubwa ni Wasunni na daima umekuwa ukiyumba  kwani watu wa huko wamehangaika na umaskini, huku utawala ukiwaona kama jamii inayoshukiwa. Iran ni taifa kubwa lenye nyanda na milima inayoweza kukaliwa na watu iliyozungukwa na maeneo ya vijijini na mijini ya Uajemi. Haya basi yamezungukwa na idadi kubwa ya makabila ya wachache na kwa pamoja wanalingana na idadi ya Wafursi.

Utawala wa watu wa dini umekabiliwa na maasi na maandamano mengi katika kipindi chote cha utawala wake wa miongo minne. Tunachokiona nchini Iran leo ni sura ya hivi punde zaidi ya hili. Mwanasosholojia mashuhuri wa Iran Mohammad Fazeli kutoka chuo kikuu cha Tehran alisema kuwa maandamano hayo si matokeo ya matukio ya hivi karibuni tu, bali ni zao la zaidi ya miaka 40 ya utawala mbaya nchini Iran. Fazeli alisema kuwa kuna matatizo mengi ambayo hayajatatuliwa ambayo yamekuwa yakiongezeka katika miongo minne iliyopita, bila ya jaribio lolote la serikali kuyashughulikia. Alisema, "Rais Raisi anaposema atachunguza kifo cha Mahsa Amini, watu hawawezi kumwamini kwa sababu kesi kama hizo hapo awali hazijatatuliwa." Wakati huo huo, kukosekana kwa matumaini ya siku za usoni baada ya miongo kadhaa ya mfumko mkubwa wa bei, ukuaji uliodumaa wa uchumi, kuzorota kwa mfumo wa utawala na mambo mengine mengi yamesababisha hasira dhidi ya utawala wa Iran, na Wairan wengi hawana tena hofu ya kuandamana na kuzungumza wazi dhidi ya utawala uliofeli wa watu wa dini.

Kilichowageuza wengi dhidi ya utawala wa watu wa dini ni ukweli kwamba baada ya miongo minne umeharibu uchumi, umefukarisha wananchi na unaendelea kuwakandamiza. Pato la Taifa la Iran lilipungua kwa 70% kutoka $599 bilioni mwaka 2012 hadi $191 bilioni leo! Viwango vya maisha nchini Iran leo vimefikia kiwango cha chini kabisa kwa zaidi ya karne moja. Bei zinaendelea kupanda, na kufanya bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa, zisiweze kumudu Wairan wengi.

Nchini Iran mabadiliko ya kihistoria yamekuja kwa njia mbili. Ime serikali ya kigeni inavamia au kuunga mkono kikundi ndani ya Iran, hii ndio ilifanyika wakati Urusi na Uingereza ziliivamia Iran mwanzoni mwa WW1 na WW2 ili kuhakikisha inaweza kutumia rasilimali za nishati za Iran kwa juhudi za vita. Mnamo mwaka wa 1979 Wafursi na watu walio wachache na watu kutoka matabaka tofauti ya jamii walikusanyika ili kumpindua Shah. Leo watu walio wachache nchini Iran watahitaji uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Wafursi ikiwa wanataka kuung’oa utawala huo. Harakati za upinzani kwa sasa zinafanya maandamano makubwa lakini zimegawanyika kwani hazina kiongozi mkuu na hazijahamasisha maeneo ya vijijini ambayo ndio ngome ya watu hao wa dini.

Hatua kwa hatua Iran inabadilika kutoka kwa dola ya kitheokrasi inayotawaliwa na watu wa dini hadi kuwa na serikali ya IRGC wanayojiona kuwa walezi wa mapinduzi ya 1979. Huku watu wa dini wakipoteza uaminifu, hakuna uwezekano baada ya kifo cha Khamenei, IRGC itahitaji kiongozi mkuu ili waendelee kubaki madarakani hivyo huenda kuwe na kiongozi mkuu mwenye uwezo mdogo kama nembo tu. Serikali ya kiimla inayoongozwa na kiongozi wa kijeshi huenda iwe ndio mustakabali wa Iran. Kama ile ile ya Iran mwanzoni mwa karne ya 20 wakati Kanali Reza Khan, alipokuwa waziri mkuu mwaka 1921, alimpindua Ahmad Shah mwaka 1925 na kuanzisha Utawala wa Nasaba wa Pahlavi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu