Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kujitolea Kwetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) Huja Kabla ya Kujitolea Kwetu kwa Familia na Kazi

Katika zama zetu, kujitolea kwa maswala ya kifamilia, uzazi, masomo, taaluma, au biashara huja kabla ya kujitolea kwa majukumu yetu ya Kiislamu kwa jamii ya Kiislamu (jamaa’ah) na Dini. Mapungufu kama hayo ni ya gharama kubwa wakati ambapo ukandamizaji juu ya Umma wa Kiislamu umefikia kiwango cha juu kabisa. Inaonekana kana kwamba watawala wa Waislamu wanafanya mipango kandamizi kwa niaba ya wakoloni, bila hata kujaribu kuhalalisha misimamo yao. Jitihada kuu zilizochukuliwa dhidi ya Ummah, rasilimali zake, Dini yake na ardhi zake hazitokei tena moja baada ya nyingine. Mipango kadhaa inaendelea sambamba katika wakati wowote ule. Hakika, ni juu ya kila Muislamu kutoa hisa yake kamili kwa kazi ya kurudisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Kwa hivyo haipaswi kwa raia, ambaye ni wajibu kwake kubeba ulinganizi wa Uislamu, kupuuza jukumu lake, akitoa majukumu ya kifamilia kama kisingizio. Haipaswi kwa afisa wa jeshi, ambaye ni jukumu lake kutoa Nussrah kusimamisha tena Uislamu kama dola, anashindwa katika jukumu lake kwa sababu amejitolea katika taaluma yake yenye kumhitaji mno.

Kwa kweli, mtu huegemea kwa familia yake na taaluma yake kwa maumbile yake. Uegemeaji huo hutoka kwa katiba ya kihisia (ghariza) ya mwanadamu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameiumba. Mwanadamu ana hisia (ghariza) ya kuendeleza kizazi, kwa hivyo anahisi huruma kwa kizazi chake na huruma kwa wazazi wake. Mwanadamu ana hisia ya kuendeleza maisha, kwa hivyo anahisi hisia ya uwajibikaji kwa masomo yake, kazi au biashara. Ana msukumo wa kustawi na kutimiza ahadi zake. Hii ndio asili ya mzozo ambao mwanadamu huhisi wakati wowote akiulizwa kujitolea katika sababu zilizo zaidi ya mahitaji yake ya kibinafsi ya kazi. Katika ulimwengu wa Magharibi, uliokosa mwongozo, kuna mazungumzo mengi juu ya usawa katika maisha ya kazi, wakati bora na wakati wa kupumzika kwa jamii kwa ujumla. Mzozo huu hauwezi kusuluhishwa kwani mfumo wa maisha wa Kimagharibi umetungwa na mwanadamu, una kasoro na mapungufu. Masuluhisho yaliyotengenezwa na wanadamu hayatatui mzozo huo ipasavyo, kutoa utulivu. Kwa hivyo, watu wanaathiriwa sana na hatia, majuto, wasiwasi, mafadhaiko na msongo wa mawazo, huku wakitapia mahitaji yao, wakishindwa kuweka usawa.

Lakini, Waislamu wamebarikiwa na mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ambaye alimuumba mwanadamu na hisia zake. Ujuzi na Hekima Yake hazina mapungufu yoyote. Alhamdulillah kwa Uislamu ambao ndio mwongozo kamili. Ni Uislamu ndio huamua usawa katika maisha na kipaumbele katika majukumu. Ni Dini hii moja ndiyo ambayo inaunganisha imara yale yaliyokuja kabla na yaliyofuata, na maisha haya. Kwa kufanya hivyo, unatoa mwangaza dhaifu ambao wale walioathiriwa na usekula wanautafuta. Aliyeangazwa ni yule anayeunganisha maisha haya na yale yaliyokuja kabla na yanayofuata baada ya maisha haya. Zaidi ya hayo, Uislamu haukuacha mwelekeo wa mambo ya kifamilia, na biashara kwa hamu ya kihisia pekee. Badala yake, Uislamu uliunda mwelekeo kulingana na ufahamu ilio wazi wa nafasi yake sahihi maishani, kuhusiana na Uislamu na Jihad. Mwenyezi Mungu (swt) asema,                                                 

كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّى يَأْتِيَ اللَّهُ بِأَمْرِهِ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ)

“Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.” [Surah At-Tawbah 9:24]. Kwa hivyo kulingana na aya tukufu, mapenzi kwa baba, wana, kaka, wenzi wa ndoa, jamaa, nyumba, na biashara hayapaswi kuja mbele ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Mapenzo haya kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) ni Wajibu (Fard). Mapenzi ni uegemeo (mayl) ambao huunda tabia ya nafsiyyah ya mwanadamu. Mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) ni aina ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyaunganisha na fahamu ya Shari'ah, na hivyo kuyafanya yawe ya Wajibu. Al-Azhari amesema, "Mapenzi ya mja kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake yanamaanisha kuwatii na kufuata amri yao." Al-Baydaawi amesema, "Mapenzi ni utashi wa kutii." Ibn 'Arafah amesema, "Mapenzi katika lugha ya Waarabu yanamaanisha matakwa ya kitu kwa unyoofu." Az-Zajjaaj alisema, "Mapenzi ya mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kuwatii na kukubali kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) amekiamuru na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amekileta." Kwa hivyo uegemeo huu unafinyangwa na Uislamu. Hamu kihisia ya familia na taaluma imezidiwa na hamu ya kumwabudu Mwenyezi Mungu (swt) na kutekeleza majukumu katika Uislamu.

Uislamu uliweka majukumu ya lazima (faraa'id) kwa wazazi, watoto, familia, na biashara. Uislamu ulimsifu yule ambaye amejitolea kudumisha uhusiano na familia. Uislamu unapongeza kufanya kazi kwa uangalifu kutimiza mikataba ya uajiri na biashara kadri awezavyo. Lakini, Umma wa Kiislamu hauhusiki na mambo haya peke yake. Ni Ummah wa kipekee wa Kiislamu ambao umepewa jukumu la kuwaongoza wanadamu wote kwenye nuru ya Uislamu. Hakuna Mtume baada ya RasulAllah (saw), kwa hivyo ni juu ya Ummah kutekeleza ulinganizi wa Uislamu. Umma wa Kiislamu ni Ummah bora zaidi ulioletwa kwa wanadamu, kwa sababu unaamrisha mema na unakataza maovu. Ni Ummah wa Kiislamu ndio unaosimamisha Uislamu kama mfumo wa maisha kama mfano kwa wanadamu wote. Ni Ummah wa Kiislamu ndio unaoulingania ulimwengu ili kuukumbatia Uislamu kupitia Dawah yenye nguvu.

Kwa kuongezea,pindi watu wanapoegemea katika Uislamu baada ya kupokea Dawah, ni Umma wa Kiislamu ndio ambao huwaondoa watawala wao kwa Jihad ya vikosi vyake vya jeshi. Hii ni ili Uislamu uweze kutekelezwa kivitendo juu yao. Muislamu haishii tu katika maswala ya familia na biashara peke yake. Maono yake yanaendelea mbali zaidi ya mambo haya, yanapanuliwa na hamu ya utekelezaji wa Uislamu, Dawah na Jihad. Ni maono haya yenye nguvu ndiyo ambayo yanamruhusu kujitolea muda kutoka kwa familia yake na biashara, ili wakati wa ujana wake na kilele cha juhudi zake zitolewe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Muislamu anaipa kipaumbele kazi ya kusimamisha tena Uislamu kama mfumo wa maisha, kuimarisha Dawah na kurudisha Jihad kama mpango ulioandaliwa na wa kiulimwengu.

Katika karne zake zote, hadhara ya Kiislamu ilileta haiba ambazo zilikuwa ni magari ya mabadiliko katika jamii na ulimwengu. Ilimfanya kila Muislamu kuijali jamii ya Kiislamu na Dini yake, ikimlazimisha kuweka mbali matamanio na matakwa ya kibinafsi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, katika zama tukufu za Maswahaba (ra) na baada yake, Uislamu uliwaleta wale ambao walifanikiwa kazi isio na kifani ya kuendeleza dhamira ya Uislamu. Uislamu uliwaleta wafanyabiashara raia ambao wanaamrisha mema na wanakataza maovu, wakifanya mabadiliko ya zama zao na zama za wale wanaokuja. Inadhihirisha kuwa jenerali wa jeshi anatambua kwamba jukumu lake sio tu kupigana na maadui, bali pia kubeba Dawah ya Uislamu kwao, kabla ya mapigano. basi natuzingatieni na kutafakari hali zote mbili, ili tufaidike katika zama zetu.

Raia nawazingatie mfano wa mfanyabiashara na Aalim (mwanachuoni), Imam Abu Hanifah (rh). Abu Hanifa (rh) alikuwa mfanyabiashara stadi na alikuwa na biashara yenye faida. Riziki yake ilikuwa katika hali ambayo yeye mwenyewe aliwapa wanafunzi wake kile kinachoitwa sasa "ufadhili wa masomo," akisimamia masurufu yao wa kifedha, ili waweze kujitolea kujifunza Dini kutoka kwake. Zaidi ya biashara yake, hata hivyo, Imam Abu Hanifah alifaulu katika uwanja wa elimu ya Uislamu na mafundisho yake. Imam Abu Hanifah alikuwa amejitolea sana katika harakati tukufu ya kutafuta elimu. Imetajwa katika "Utangulizi wa Marginalia wa Ibn Abidin"

رأى الإمام أبو حنيفة غلامًا يلعب بالطين ، فقال له: يا غلام ، إياك والسقوط في الطين, فقال الغلام للإمام إياك أنت من السقوط ، لأن سقوط العالِم سقوط العالَم)

“Imam Abu Hanifa alimuona kijana mmoja anacheza na tope, basi akamwambia: Ewe kijana, tahadhari usianguke kwenye tope, kijana akamwambia Imam: tahadhari wewe usianguke, kwani kuanguka kwa Aalim (mwanachuoni) ni kuanguka kwa ulimwengu."

Ibn Abideen kisha akasimulia,

فكان أبو حنيفة لا يفتي بعد سماع هذه الكلمة إلا بعد مدارسة المسألة شهرًا كاملاً مع تلامذته

“(Imam) Abu Hanifah hakutoa fatwa baada ya kusikia maneno haya, ila baada ya kuyasoma maswala haya kwa muda wa mwezi mmoja kamili pamoja na wanafunzi wake.”

Mbali na kufundisha wanafunzi wake, Imam Abu Hanifah (rh) alikuwa akizingatia wajibu wake wa kuamrisha mema na kukataza maovu, akihakikisha watawala hawakengeuki kutoka katika Uislamu. Imam Abu Hanifah alimwonya mwanafunzi wake, Abu Yusuf,

كن من السلطان كما أنت من النار، تنتفع بها وتتباعد عنها، ولا تدنُ منها؛ فإنك تحترق وتتأذى منها؛ فإن السلطان لا يرى لأحد ما يرى لنفسه

"Kuwa na mtawala kama jinsi unavyokuwa na moto, unanufaika nao na unajitenga mbali nao, wala huukaribii; kwani utakuchoma na kukuumiza; hakika Sultan haoni kwa wengine lile alionalo yeye mwenyew.” Imam Abu Hanifa ameeleza,

 إذا رأيتم العالم يرتاد أبواب السلاطين فاتهموه في دينه “Pindi mumuonapo Aalim (mwanachuoni) kila mara yuko milangoni mwa watawala, basi ituhumuni dini yake.”

Hakika msimamo wa busara wa Imam Abu Hanifah wa kuepuka kuwa karibu na watawala ni uko sambamba na hadithi iliyosimuliwa na Tabaraani, ambapo RasulAllah (saw) alisema,

«إيَّاكُمْ وَأبْوَابَ السُّلْطَانِ، فَإنَّهُ قَدْ أصْبَحَ صَعْبَاً هَبُوطَاً»

“Tahadharini na milango ya watawala, kwani hakika kushuka ni vigumu mno.” Kwa kuongezea, mtawala katika zama za Imam Abu Hanifah alikuwa chini ya uhasibu wake mkali, katika zama ambazo Khilafah alikuwepo na hukmu zilikuwa ni za Uislamu. Vipi basi sasa wakati ambapo Khilafah imevunjwa na hukmu za kikafiri zinatawala Ardhi za Waislamu? Je! Wale ambao wamejizatiti kufuata Fiqh ya Imam mtukufu Abu Hanifah wanapaswa kuwaje leo? Wanawezaje kukaa kimya wakati watawala wanaangamiza uchumi kupitia riba, wakitangaza vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw)? Wanawezaje kukaa kimya wakati Kashmir iliyokaliwa ikililia msaada, lakini hakuna uhamasishaji wa vikosi vya jeshi kuhakikisha ukombozi wake kupitia Jihad? Je! hifadhi ya masikiti itakuwaje fidia kwa hifadhi ya Dini kama mfumo kamili wa maisha?

Afisa wa jeshi wa Kiislamu wa leo naamzingatie Khalid ibn al-Walid (ra), ambaye anaheshimiwa na majenerali kote ulimwenguni kwa umahiri wake na ubunifu katika mkakati na mbinu za kijeshi. Pamoja na kujitolea kwake kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), alikuwa na ujuzi katika Dawah kwa Uislamu. Wakati wa vita vya Yarmuk, mmoja wa makamanda wa Kirumi aliyeitwa Georgius alisonga mbele kutoka kwa safu ya wanajeshi, akiuliza kukutana na Khalid ibn al-Walid (ra). Khalid (ra) alikwenda kumlaki na walisongea karibu sana hivi kwamba shingo za farasi wao zilikutana. Georgius aliuliza, “Ewe Khalid! Unalingania kwa kitu gani?” Khalid (ra) alijibu, "Kwa kushuhudia kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad (saw) ni mja na Mtume Wake, na kukubali kila kitu alichokileta kutoka kwa Mwenyezi Mungu." Georgius kisha akauliza, "Je! Vipi kuhusu wale ambao hawakubali hili?" Khalid (ra) alijibu, "Basi watalipa Jizyah na tutawalinda." Georgius kisha akauliza,"Je! Ikiwa hawatatoa?" Khalid (ra) alijibu, "Basi tutatangaza vita dhidi yao na tupigane nao."

Jenerali mtukufu wa jeshi, Khalid (ra) aliweka wazi utambuzi wake juu ya wajibu wa jenerali wa Kiislamu kuhusu Dawah na Jihad. Ikiwa watu wa ardhi wataukubali Uislamu, Uislamu hutekelezwa juu yao. Ikiwa watu wa ardhi watakubali kulipa Jizyah, Uislamu hutekelezwa kwao huku wakibaki kama raia wasio Waislamu, wakilindwa na serikali. Ikiwa watakataa, jeshi la Khilafah linapambana na jeshi lao mpaka Khilafah iweze kutekeleza Uislamu juu yao, kuwawezesha kuingia kwao katika Uislamu kwa kuona utekelezaji wake. Kama natija ya thaqafa ya jeshi la Kiislamu, maarifa ya Khalid (ra) yaliongezeka zaidi ya hukmu juu ya Jihad peke yake. Kisha yeye (ra) akafanya mazungumzo ya kina na Georgius juu ya Uislamu wenyewe, na baada ya hapo Georgius akasilimu na kisha akamuuliza Khalid, "Nifundishe Uislamu." Kwa hivyo, Khalid(ra) alimpeleka hemani kwake, akamimina gunia la maji juu yake na kisha akamwongoza katika kutekeleza rakaa mbili za swala. Khalid (ra) na Georgius waliendelea kupigana na Warumi hadi Georgius akapokea kifo cha shahada. Kwa hivyo hapa tunaona kuwa Khalid (ra) hakuwa tu Upanga wa Mwenyezi Mungu (swt), alikuwa ni mlinganizi mwenye ujuzi katika Uislamu. Yeye (ra) hakuhitaji kumpeleka georgius kwa mwanachuoni kuhusiana na hukmu za Jihad, Aqeedah ya Uislamu au utekelezaji wa Uislamu. Khalid (ra) mwenyewe alikuwa na elimu muhimu katika mambo haya msingi.

Basi nawazingatie wana wenye fahari wa Khalid (ra) mfano wa Khalid (ra) kama unavyopaswa kuzingatiwa. Nawazingatie katika wakati ambapo Msikiti Al-Aqsa na Kashmir iliyokaliwa ziko chini ya uvamizi, huku Dawah na Jihad zikisimamishwa. Nawazingatie katika wakati ambapo uhusiano na majenerali wa Magharibi sio wa kuwalingania kwenye Uislamu au kuwakabili kwenye uwanja wa vita, bali ni wa ushirikiano, muungano na hatua ya pamoja. Je! Utaalamu katika kupigana utafidia vipi dhambi na kutelekezwa huko? Vipi?! Imam Ahmad na Abu Dawud (hii ni riwaya ya Abu Dawud) walipokea kwamba Ibn Umar alisema, "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema,

«إِذَا تَبَايَعْتُمْ بِالْعِينَةِ وَأَخَذْتُمْ بِأَذْنَابِ الْبَقَرِ وَرَضِيتُمْ بِالزَّرْعِ، وَتَرَكْتُمُ الْجِهَادَ سَلَّطَ اللهُ عَلَيْكُمْ ذُلًّا لَا يَنْزِعُهُ حَتَّى تَرْجِعُوا إِلَى دِينِكُم»

“Mtakapofanya biashara kwa 'Iynah (aina ya Riba), na mkachukua mikia ya ng'ombe (kulima ardhi) na mkaridhika na mazao yake, na mkaiwacha Jihad, Mwenyezi Mungu atawasaliti juu yenu kwa udhalilifu ambao hautauondoa mpaka mregee katika Dini yenu.”

Kwa hivyo, kila mmoja wetu azingatie, ima ni mfanyabiashara, afisa wa jeshi, mfanyikazi wa kampuni, mwanachuoni, mwandishi wa habari au mwanafunzi, mizani kati ya familia na biashara, kwa upande mmoja, na kujitahidi kuuregesha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, kubeba Dawah kwa wanadamu wote na Jihad kwa upande mwingine. Tuwe wakweli katika mapenzi yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), tukijitolea nafsi zetu kwa ajili ya Dini yetu. Hakika, alfajiri ya Uislamu inaonekana, kwa hivyo tujitahidi kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab ibn Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 12 Oktoba 2020 14:11

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu