Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Raia wa Kiulimwengu – Ajenda ya Kimagharibi

Athari za ukoloni na ukoloni mamboleo kwenye mfumo wa elimu katika nchi za Waislamu zimekuwa wazi kwa Umma wa Kiislamu. Karne ya 21 imeona kuendelea kuingiliwa katika mitaala ya elimu ya nchi za Kiislamu na Magharibi, kupitia kushawishi wataalamu wa kifikra na sera ya serikali. Nakala hii itaangalia fahamu ya uraia katika Mtaala mpya wa Kitaifa (SNC) wa Masomo ya Kijamii kwa Darasa la 4 na 5 nchini Pakistan. Fahamu ya Kimagharibi ya uraia tayari iko katika mtaala wa masomo ya kiwango cha kawaida (O-Level) ambao unafundishwa nchini Pakistan, kwani Viwango vya kawaida (O-Levels) ni kulingana na vipimo vya kisekula vya Uingereza.

Ina ajenda hatari ya kukuza fahamu ya uraia kulingana na ajenda ya UN ili kueneza fahamu za mfumo wa Kimagharibi. Mfumo wa Kimagharibi wa urasilimali umeenea kote ulimwenguni kupitia zana nyingi. UN ni mojawapo ya zana madhubuti ambayo hueneza fikra zake kupitia mifumo ya elimu katika nchi za Waislamu. Kutabanniwa kwa mifumo ya elimu inayotegemea Magharibi kumefafanua upya fikra za vizazi vya Waislamu kupitia kuwaanika  katika thaqafa ya kigeni inayowasilishwa kuwa bora kifikra, kithaqafa na kihadhara. Masomo kama vile Kiingereza, Sayansi, Historia na Masomo ya Kijamii hurahisisha lengo hili. Mkakati huu umesababisha fahamu zingine, kama demokrasia na dola ya kitaifa kuhalalishwa na kufanywa kuwa za kiulimwengu.

Ni kawaida kwa mfumo wowote kuwasilisha ulimwengu imani, fikra na nidhamu zake. Mfumo wa Kiislamu pia unataka kutawala ulimwengu kwa kuwasilisha imani, fikra na nidhamu zake. Walakini, mbinu, njia na mitindo ya kufikia malengo haya hutofautiana sana. Magharibi inatafuta kulazimisha mfumo wake wa kiulimwengu kwa manufaa ya warasilimali, huku Uislamu huweka mfumo wa kiulimwengu kwa msingi wa uadilifu. Magharibi ilitumia nusu ya kwanza ya karne ya 20 kukuza fahamu ya dola za kitaifa. UN iliundwa kurahisisha uundaji huu mpya wa mfumo wa kiulimwengu. Khilafah ya Uthmani ilivunjwa na watu anuwai, ambao waliishi chini ya utawala wa Uislamu kwa karne nyingi, walilazimika kuhamia nchi zingine kwa jina la kujitawala wenyewe, utaifa na dola za kitaifa. Ubwana kwa dola  ya taifa uliingizwa katika mfumo mpya wa kiulimwengu. Wazo la dola yoyote kupanua mipaka yake kupitia ufunguzi lilifanywa kuwa haramu kupitia 'sheria ya kimataifa'. Hili lilikuwa shambulizi la moja kwa moja kwa sera ya kigeni ya mfumo wa Kiislamu. Kwa hivyo, usawazishaji mahusiano wa dola za kitaifa ulikamilishwa. Fauka ya hayo, fahamu ya demokrasia kama nidhamu ya utawala ilienezwa kama nidhamu bora na yenye maendeleo zaidi. Walakini, mgongano wa fahamu hii dhaifu ulionekana wazi. Magharibi iliunda watawala vibaraka chini ya pazia ya wafalme na madikteta, na kuasisi uhusiano nao ili kuendeleza malengo yao. Kwa hivyo kiuhalisia, fahamu ya demokrasia siku zote imekuwa si chochote zaidi ya alama iliyowekwa na Magharibi kuhukumu maendeleo ya taifa lolote.

Baada ya Vita vya pili vya Dunia na kwa kuundwa kwa UN, uraia ulifafanuliwa kuwa unategemea utaifa na sio imani. Fahamu ya Ummah ilitokomezwa na Waislamu wakawa watiifu kwa bendera iliyowasilishwa kwao na mabwana wao wa kikoloni chini ya udanganyifu wa Uhuru. Mwishoni mwa karne ya 20, mfumo wa Kimagharibi ulieneza sana fahamu ya Utandawazi. Ajenda ya kweli ya fahamu hii imefichwa na kwa mangati ya ulimwengu wenye utulivu na umoja. Utandawazi una fasili nyingi: "Utandawazi inajumuisha uunganishaji wa uchumi wa kitaifa katika uchumi wa Kimataifa kupitia biashara, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (wa mashirika na kampuni za kimataifa), mtiririko wa mtaji wa muda mfupi, mtiririko wa kimataifa wa wafanyikazi na ubinadamu kwa jumla, na mtiririko wa teknolojia" (Bhagwati, 2006) na "Utandawazi ni ujumuishaji unaokua wa uchumi na jamii kote ulimwenguni" (Collier na Dollar, 2001).

Inadaiwa kwamba neno 'utandawazi' halielezei aina yoyote ya jamii na inasemekana kuwa ni mchakato wa upanuzi wa upeo wa kimataifa na ujumuishaji. Walakini, kwa uchunguzi wa karibu, ni mfumo wa Kimagharibi ndio ambao umepanuka kutoka Kaskazini hadi Kusini; hakukuwa na uhamishaji wa mawazo, maadili au nidhamu kutoka Kusini kwenda Kaskazini. Utandawazi umekuwa mchakato ambao mfumo wa Kimagharibi umeendeleza imani yake ya usekula, mawazo yake ya uhuru, maadili yake ya haki za binadamu na nidhamu yake ya demokrasia kote ulimwenguni. Thaqafa maarufu iliyoenezwa ulimwenguni ni ushuhuda wa ukweli huu. Huu ndio mfumo wa Kimagharibi ambao unataka kukuza fahamu ya raia ya kiulimwengu ambayo inajumuisha maadili yake. Mtu yeyote ambaye haitii hii ni mwenye msimamo mkali au asiyekuwa mvumilivu. Kwa hivyo, mfumo wa Kimagharibi umeunda hadithi kuhusu raia mzuri  ni yupi kwa msingi wa tabanni ya maadili yake.

Mtaala mpya wa Masomo ya Kijamii huanza kwa mada ya uraia kwa kuangazia 'Raia wa Kiulimwengu' na hufafanua fahamu kuu zifuatazo: Raia; wa kiulimwengu na wa kidijiti; haki na majukumu; utofauti; uvumilivu; usimamizi wa amani na migogoro; adabu za kawaida (ukurasa 25). Maneno haya yanaonekana kana kwamba hayana madhara, lakini yote yana maana za kimfumo ambazo zinarahisisha kutawala kwa mfumo wa Kimagharibi. Maana hizi zinajadiliwa hapa chini.

Mada ya 1 - Uraia: Kiwango cha 1 - Tambua haki na majukumu ya raia na sababu kwa nini zinaweza kubadilika kwa kubadilika kwa muda.

Katika jamii yoyote fahamu za uraia zinapaswa kufafanuliwa kutoka kwa imani ya jamii hiyo. Katika jamii ya kidemokrasia, haki na majukumu ya raia hufafanuliwa na sheria iliyoundwa na Bunge au Baraza la Wawakilishi (Congress). Hizi zimebadilika kwa karne nyingi, kwa sababu hiyo ndiyo hali ya sheria zilizotengenezwa na mwanadamu. Katika miaka ya 1960, raia nchini Uingereza hawakuruhusiwa kushiriki ushoga. Ndani ya miaka 50, sio tu kwamba sheria imebadilishwa ili kutoa nafasi kwa kitendo hiki, bali imeelezewa kama haki ya kimsingi. Sheria zaidi iliruhusu ndoa na kutabanni haki za mashoga. Kwa hivyo, mabadiliko ya maumbile ya sheria za Magharibi ni dhahiri. SNC inakuza nidhamu ya demokrasia na maendeleo ya kihistoria ya demokrasia yatapatikana ndani ya vitabu. Inatukuzwa kama mfumo unaobadilika ambao unaleta uboreshaji kwa jamii. SNC inafafanua raia mzuri kama yule anayefuata na kukuza demokrasia kama muundo bora wa serikali na anaamini maadili ya usekula, uhuru na demokrasia ambayo yote ni nguzo za mfumo wa Kimagharibi.

SNC haitaji kuhusu nidhamu ya utawala ya Waislamu, Khilafah, ambayo kwayo ubwana ni wa Mwenyezi Mungu (swt) na sheria hazibadiliki kwa wakati na mahali. Msingi wa utawala ni Quran na Sunnah, huku Ijtihad ikiruhusiwa juu ya mambo mapya kwa msingi wa Usoul. Sheria hizi hazibadiliki kwa wakati na mahali. Fahamu ya raia kulingana na Uislamu ni yule anayeishi chini ya mamlaka ya Khilafah ya Kiislamu. Raia ndani ya Khilafah wanaweza kuwa Waislamu au wasiokuwa Waislamu. Wanaweza kuwa juu ya kabila lolote. Raia wasiokuwa Waislamu wanajulikana kama Ahli-Dhimma, Watu wa Mkataba. Wanaahidi kutii sheria za serikali na badali yake serikali inalinda maisha yao, mali, imani, akili na heshima. Historia ya Kiislamu imejaa mifano inayothibitisha kuwa Khilafah ndio serikali pekee ya kweli iliyolinda haki za raia wake. Hakuna mfumo mwingine ambao umeweza kufanya hivyo. Mafanikio ya mfumo wa Kiislamu yanatokana na fahamu ya Taqwa inayobebwa na watawala wa Kiislamu, ambao wanaelewa jukumu lao la kulinda Ahli-Dhimmah. Mwenendo huo unatoka kwa Sunnah iliyoteremshwa kwa wahyi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Ni wajib juu yetu kutoa kuwapa watu wa Dhimma ulinzi ule unaopewa Waislamu, hii ni kutokana na maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw),

«أَلا مَنْ قَتَلَ نَفْسًا مُعَاهِدًا لَهُ ذِمَّةُ اللَّهِ وَذِمَّةُ رَسُولِهِ فَقَدْ أَخْفَرَ بِذِمَّةِ اللَّهِ، فَلا يُرَحْ رَائِحَةَ الْجَنَّةِ، وَإِنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ سَبْعِينَ خَرِيفًا»

“Hakika, yeyote anayeuwa nafsi iliyowekea ahadi ya kulindwa (Mu'ahid), ambayo ina dhimma ya Mwenyezi Mungu na dhimma ya Mtume Wake (saw), basi amekiuka dhimma ya Mwenyezi Mungu, hivyo hatasikia harufu ya Pepo; na hakika harufu yake inahisika umbali wa vuli sabiini”, imepokewa na Al-Tirmidhi. Na Al-Bukhari ameipokea kwa lafdhi,

«مَنْ قَتَلَ مُعَاهَدًا لَمْ يَرِحْ رَائِحَةَ الْجَنَّةِ وَإِنَّ رِيحَهَا تُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ أَرْبَعِينَ عَامًا»

“Yeyote atakayemuua Mu'ahid (mtu aliyepewa hifadhi na Waislamu kwa mkataba) hatasikia harufu ya Pepo na hakika harufu yake inapatikana umbali wa (mwendo wa) miaka arubaini.”

Watu wa Dhimmah wanafurahia haki sawa na zile zinazofurahiwa na Waislamu katika suala la kusimamia mambo yao na kukimu maisha yao. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«أَطْعِمُوا الْجَائِعَ ، وَعُودُوا الْمَرِيضَ ، وَفُكُّوا الْعَانِيَ»

"Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru aliye kifungoni (kwa kulipa fidia yake)," imepokewa na Al-Bukhari kupitia Abu Musa. Na kutoka kwa riwaya kama ilivyopokewa na Abu Dawud katika Sunan yake,

«عَلَى أَنْ لاَ تُهْدَمَ لَهُمْ بَيْعَةٌ، وَلاَ يُخْرَجَ لَهُمْ قَسٌّ، وَلاَ يُفْتَنُوا عَنْ دِينِهِمْ مَا لَمْ يُحْدِثُوا حَدَثًا أَوْ يَأْكُلُوا الرِّبَا»

“Kwamba makanisa yao hayatavunjwa, wala makasisi wao hawatatolewa, wala hawatafitinishwa na dini yao (kutolewa kwa nguvu katika imani yao) maadamu hawatazusha tukio au kula riba.”

Mtume (saw) alikuwa akiwatembelea wagonjwa, kama ilivyo nakiliwa na Al-Bukhari kutoka kwa riwaya ya Anas (ra),

«كَانَ غُلاَمٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَعُودُهُ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ فَقَالَ لَهُ ‏‏ أَسْلِمْ ‏‏‏.‏ فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهْوَ عِنْدَهُ فَقَالَ لَهُ أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ فَأَسْلَمَ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ يَقُولُ ‏‏ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنَ النَّارِ»‏

"Kijana mmoja Myahudi alikuwa akimhudumia Mtume (saw) basi akawa mgonjwa, Mtume (saw) akaja akamtembelea, akakaa mbele ya kichwa chake kisha akamwambia silimu. Kijana akamtazama babake ambaye alikuwa naye babake akamwambia mtii Abul-Qasim. Basi kijana akasilimu, Mtume (saw) akatoka huku akisema shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye amemwokoa (kijana) na Moto." Hii inaashiria kuwa inaruhusiwa kuwazuru, kuwa na adabu na urafiki nao.

Al-Bukhari alimepokea kutoka kwa Amru Bin Maymun kutoka kwa Umar Bin Al-Khattab (ra) ambaye alimshauri wakati wa kifo chake "Nami namuamrisha Khalifah baada yangu hili na hili, na namuamrisha kwamba kupitia dhimma ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw), atimize dhimma yao, apigane nyuma yao na asiwalazimishe kufanya kazi zaidi ya uwezo wao.”

Wanachuoni wa zamani wa Uisilamu kwa hivyo walifafanua haki za Waislamu kwa dhimmi. Mwachuoni maarufu wa fiqh ya Malik, Shihab al-Din al-Qarafi anasema: Dhimma ya ulinzi inatuwekea majukumu fulani kwa ahl al-dhimmah. Wao ni majirani zetu, chini ya makao yetu na ulinzi wetu kwa dhamana ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake (saw), na dini ya Uislamu. Yeyote anayekiuka majukumu haya dhidi ya yeyote kati yao kwa neno la matusi, kwa kusingizia hadhi yake, au kwa kumdhuru au kusaidia katika hilo, amekiuka dhamana ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake (saw) na dini ya Uislamu.

Mada 1 - Uraia: Kiwango cha 1- Haki za Binadamu- Tambua haki msingi za binadamu kama ilivyoelezwa na UN.

Kiwango hiki kiko wazi sambamba na ajenda za UN kama inavyoonekana kutoka katika kifungu cha 18 cha Azimio la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNDHR) kinachosema: Kila mtu ana haki ya uhuru wa fikra, dhamiri na dini; haki hii ni pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake, na uhuru, awe peke yake au katika jamii na wengine na hadharani au faraghani, kudhihirisha dini au imani yake katika kufundisha, kutekeleza, kuabudu na kuzingatia.

Haki za binadamu zilizojadiliwa katika UNDHR haziwezi kuwa kipimo kwa Waislamu. Uislamu umeelezea haki kulingana na imani yake wenyewe. Mara tu Muislamu akisha asisi imani ya kifikra, fikra zake, maadili na mihemko yake hufafanuliwa na vipimo vya Uislamu, na hivyo anakuwa na shakhsiyya ya kipekee ya Kiislamu. Uislamu hauruhusu kuhojiwa fikra zake msingi, na mjadala au tofauti ya maoni yamefungwa kwa mambo yaliyo chini ya kigawanyo cha Mubah, yaani kuruhusiwa. Uislamu unalinda haki za raia wake katika kutekeleza imani yao na pia unamlazimisha Khalifah kulinda haki zote zilizopeanwa na Shariah.

Mada ya 1 - Uraia: Kiwango cha 1 - Utofauti na Uvumilivu - Elewa kuwa watu wote wana haki sawa, bila kujali tofauti za kidini na za kikabila, na jifunze kuheshimu tofauti za kibinafsi katika maoni.

Tofauti na uvumilivu huzingatiwa kama msingi wa jamii za kidemokrasia. Uvumilivu na haki ya kufuata mfumo au dini yoyote huchukua umuhimu mkubwa. Nchi za Magharibi hujiona kama mifano ya kuigwa kwa demokrasia na uhuru. Walakini, mgongano wa mawazo haya duni ya kibinadamu umefichuliwa na kutovumiliwa kwa alama za Kiislamu barani Ulaya. Kupigwa marufuku kwa burqa, pazia la uso na minara katika nchi za Ulaya ni mifano ya kutovumiliwa kwa dini na tamaduni zisizo za Magharibi. Vyombo vya habari vya Magharibi vimejaa matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu na vinaunda mazingira ya kutovumiliana kutokana nayo kuna ongezeko la uhalifu wa ghasia dhidi ya Waislamu. Viongozi mashuhuri wa Magharibi na wanasiasa hawazuii chuki zao kwa Uislamu; badala yake, wanachukua fursa yoyote kuudhalilisha mfumo wa Kiislamu, na hivyo kusababisha chuki na kutovumiliana. Kupigwa marufuku kwa mavazi ya Kiislamu kunataka kuwaowanisha Waislamu ndani ya maadili ya Magharibi na kwa hivyo fahamu ya utofauti ni uongo mwingine ambao Magharibi inaipigia, lakini haiitekelezi.

Uislamu unatambua kwamba imani za watu haziwezi kubadilishwa kwa nguvu. Uislamu ulitoa usalama kwa raia wake wote bila kujali imani au kabila. Uislamu unawaruhusu raia wake wasio Waislamu kutekeleza imani zao ndani ya nyumba zao; Walakini, imani yao haiwezi kuenezwa katika jamii. Kabla ya Uislamu, milki ambazo zingeteka mataifa zingewanyanyasa watu na kuwalazimisha wafuate njia yao ya maisha. Mfumo wa Kimagharibi pia ni maarufu kwa mauwaji ya kimbari ya idadi ya wanati wa Amerika na Waaborigini wa Australia. Ni mfumo wa Kimagharibi ndio ambao haukukubali utofauti. Wamishonari wa Kikristo walitumwa Afrika, Asia, Latin Amerika na Amerika Kusini ili kuwalazimisha watu wabadilike kuwa Wakristo. Simulizi ya Magharibi kwamba inazalisha jamii tofauti na yenye uvumilivu ni uongo ambao umefichuliwa katika harakati za hivi karibuni za Maisha ya Weusi nchini Amerika. Baada ya miaka 300 ya demokrasia Amerika haitoi haki sawa kwa raia wake.

Hatari iliyofichika kwa Umma wa Kiislamu katika suala la 'utofauti na uvumilivu' imeundwa kushambulia Aqeedah ya Uislamu. RasulAllah (saw) alionya kuwa watu watapotoka kutoka kwa Aqeedah ya kweli ya Uislamu. Wakati wa Khilafah ya Abbasiya, wakati Mu'tazila walipopotoka katika imani za kimsingi, wanachuoni waliinuka ili kupambana nao na kuwazuia kuwapotosha Waislamu. Wale waliotunga Hadith walikabiliwa na enzi za Muhaditheen ambao waliulinda Uislamu kupitia uboreshaji wa sayansi ya hadith (Ulum ul Hadith). Wakati wa miaka 1300 ya utawala wa Kiislamu, Aqeedah na nidhamu za Uislamu zililindwa na Ummah, wasomi na watawala. Shariah inalinda imani ya Kiislamu kwa kumzuia Mwislamu kuritadi. Wanaoritadi wanakabiliwa vikali na adhabu ya kifo ya hudud inatekelezwa isipokuwa wakitubu. Kwa hivyo utukufu wa Aqeedah ya Kiislamu unadumishwa. Uislamu unaruhusu tofauti ya maoni katika matawi ya Fiqh katika maandiko ambayo yana maana isiyo ya kukatikiwa (dhanni dalalah) na machimbuko yasiyo ya kukatikiwa (dhanni thuboot) pekee. Uislamu hauruhusu mtu yeyote kubadilisha imani ya Uislamu. Uislamu pia unakataza Waislamu kubadilisha Dini yao na kuacha hukmu za kukatikiwa (qati ahkam).

Mada 1 - Uraia: Kiwango cha 1 - Eleza umuhimu wa uhuru wa kusema.

Uhuru wa kusema ni uongo mwingine ambao umefichuliwa haswa tangu 9/11. Mtu yeyote anayehoji juu ya vita dhidi ya ugaidi hupewa jina baya kama mfuasi wa misimamo mikali. Mamia ya watu huko Magharibi wamekamatwa na kuwekwa kizuizini kwa uhuru wao wa kusema na maoni ambayo yanakwenda kinyume na maelezo ya serikali za Magharibi. Kuzungumza dhidi ya mauwaji ya mayahudi wa Ulaya, na kuhoji ukweli wake na pia kujadili umbile la Kiyahudi hupewa vibandiko kama wapinga-mayahudi na huwaweka watetezi wa maoni haya gerezani. Hii inathibitisha kuwa hakuna jamii inayoweza kuruhusu raia wake kusema bure bila vizuizi. Uhuru wa kusema pia ni alama ambayo Magharibi hutumia kuhukumu maendeleo. Uislamu unadhibiti maneno na matendo ya Waislamu na kuyafunga kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) anachoona kinakubalika. SNC itafungua mlango kwa watu wenye mawazo ya kisekula kuanza kupinga kanuni msingi za Uislamu na kwa hivyo kukikanganya kizazi kijacho kuhusu fahamu za Kiislamu. Hii tayari imedhihirika katika shule na vyuo vikuu, ambapo mgawanyiko kati ya wasekula na wanafunzi wanaoupenda Uislamu umeonekana.

Mada ya 1 - Uraia: Kiwango cha 1 - Usimamizi wa Amani na migogoro - Elewa umuhimu wa majadiliano na mazungumzo kama zana za kutatua migogoro nyumbani na shuleni.

Nchini Pakistan Umoja wa Mataifa wa Nadharia (MUN) ni kiungo maarufu cha kalenda ya shule haswa katika shule za kibinafsi. Wanafunzi wanahimizwa kujadili juu ya maswala yenye utata katika mtindo wa UN. Miongozo ya mjadala ina kanuni 2 - moja ni kwamba maagizo ya kidini hayawezi kuwa sehemu ya hoja na ya pili ni kwamba lazima utetee wazo hata ikiwa haliamini. fahamu za msingi zinakuza kwamba hakuna haki na kosa msingi - kila mtu anaweza kuamini kile anachokipenda na kwa hivyo anaweza kusema anachotaka. Kwa hivyo, uhuru wa maoni na kusema unaonekana kama thamani ya kiulimwengu bila ya kizuizi. Walakini, kama tunavyojua kuwa migongano ndani ya mfumo wa Kimagharibi inamaanisha kuwa daima watapata takhsisi kwa sheria zao wenyewe. Kwa mfano, kuzungumza juu ya Jihad kuwa ndio sera ya kigeni ya dola ya Kiislamu inaweza kupelekea kukamatwa huko Magharibi. Kwa hivyo, SNC inatafuta kueneza kwamba Magharibi ina zana bora za kukuza amani na itajaribu kueneza fahamu hii ulimwenguni. Michakato ya mazungumzo na amani imekuwa sifa ya sera ya kigeni ya Magharibi na kuonekana kama njia bora ya kuleta amani. Usawazishaji mahusiano na uvamizi wa Kiyahudi na maridhiano ya Afghanistan na Amerika ni mifano ya kuonyesha jinsi ilivyo muhimu kupinga fahamu hii ya usimamizi wa mizozo kwani ni chombo cha sera za kigeni za Kimagharibi. Uislamu una miongozo yake mwenyewe juu ya amani, lakini hairuhusu Waislamu kudhulumiwa katika mchakato huo. Mwenyezi Mungu (swt) ameamuru,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Surah al-Baqarah 2:191]. Hivyo basi usimamizi wa amani na mizozo katika Uislamu utafafanuliwa kupitia Uislamu na sio mawazo potofu ya UN.

Mada ya 1 - Uraia: Kawango cha 1 - Maadili ya kawaida - Tambua na utekeleze adabu za kawaida katika ulimwengu uliostaarabika wa leo.

Magharibi inajivunia kuwa imestaarabika. Swali linapaswa kuulizwa, imestaarabika vipi na uchafu na uzinzi ni jambo la kawaida? Imestaarabika vipi wakati raia wake wana njaa na hawana ulinzi? Imestaarabika vipi wakati inatumia silaha zilizopigwa marufuku katika vita? Imestaarabika vipi wakati inavunja sheria zake wenyewe na kuyashambulia mataifa mengine na kusababisha vita vya miaka na uharibifu kamili wa miji, na maumbile? SNC inataka kuiweka hadhara ya Kimagharibi kama kiwango kinachopaswa kufikiwa. Inatafuta kueneza kiulimwengu imani na fikra za Kimagharibi.

Uchambuzi huu mfupi wa sehemu za mtaala wa Masomo ya Kijamii unaonyesha kuwa watoto wa Pakistan wanapewa kitambulisho kipya. Hiki ndicho kitambulisho cha Raia wa Kiulimwenguni. Kitambulisho hiki kimewekwa juu ya fahamu dhaifu na nyepesi za Kimagharibi kama ilivyojadiliwa hapo juu na itasababisha Waislamu ambao wanaeneza mawazo potofu ya Kimagharibi na hivyo kupotosha Ummah kutokana na maregeleo ya mfumo wa Kiislamu. Mtaala wa elimu katika nchi za Waislamu unapaswa kuonyesha imani na maadili ya Uislamu. Wanafunzi wanapaswa kuzama katika maadili yake na kujivunia urithi wao, na wanafunzi wanapaswa kufundishwa fahamu za uraia kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu. Uislamu unafafanua raia wa Kiislamu wa serikali ya Kiislamu kama yule ambaye ana imani thabiti katika Aqeedah ya Kiislamu, anaonyesha shakhsiya ya Kiislamu na anataka kulinda mfumo wa Kiislamu. Raia wa Kiislamu huwahesabu watawala, analinda maadili ya Kiislamu katika jamii kupitia kuamrisha mema na kukataza maovu. Raia huyu wa Kiislamu anaelewa kuwa lazima amlinde Ahli-Dhimma kama ibada kwa Mwenyezi Mungu (swt). Raia wa Kiislamu anaelewa kuwa lazima asaidie upanuzi wa dola ya Kiislamu ili kuchukua mfumo sahihi kwa ulimwengu na kuwainua wanadamu kutoka kwenye giza la mfumo wa Magharibi. Ni muhimu kuipinga SNC na kuitisha kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah, ambayo itahakikisha mtaala wa elimu kwa msingi wa Aqeedah ya Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Maryam Ansari – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 19:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu