Jumanne, 14 Rajab 1446 | 2025/01/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mkono Mrefu wa Serikali Zinazotawala Katika Nchi za Waislamu ili Kuzifisidi na Kuzitia Usekula Familia!

(Imetafsiriwa)

Tunapozungumzia kuhusu familia, tunazungumzia kuhusu kiini kinachounda jamii, na hivyo basi, ufisadi wowote au dosari yoyote inayoathiri kiini hiki itaonekana katika jamii na dola nzima, achilia mbali kuzungumzia kuhusu mchakato wa mpangilio wa ufisadi wa kiini hiki, na vipi ikiwa ufisadi huu utafanywa chini ya masikio ya dola na macho yake, bali, ina mkono mrefu ndani yake, unaohisika katika nchi za Waislamu. Serikali zinazotawala hazikuacha juhudi yoyote katika kutia usekula na ufisadi ndani ya familia na mujtamaa wa Waislamu ili kuwaridhisha mabwana zao, Amerika na Ulaya, na ili kufikia hili wametumia viwango vikubwa vya pesa, na kufanya kazi kutekeleza hili kupitia mbinu kadha wa kadha, miongoni mwazo ni:

1.Utungaji na uingizaji kanuni na sheria kutoka ng’ambo zinazo kiuka vipengee vya Uislamu katika sehemu ile inayoitwa “Hadhi ya Kibinafsi”: baada ya kuvunjwa Khilafah na kutoweka kwa Uislamu kama nidhamu ya utawala, vipengee vingi vilitoweka pamoja nayo kutoka katika uhalisia wa maisha, na Waislamu wakasalia pasi na sheria zozote zinazo tekelezwa kutoka katika dini yao wenyewe isipokuwa katika nyanja za ibada na kanuni za “Hadhi ya Kibinafsi”. Lakini maadui wa Uislamu hawakuruhusu hata hizi pia kubakia, kwa hivyo walijaribu kuzitenganisha na maisha ya Waislamu. Kwa hivyo, waliunda vibaraka wao katika biladi za Kiislamu ili kutunga nidhamu ya kanuni na sheria kinyume na Uislamu na nidhamu yake ya kijamii, na kutabanni mtazamo wa Kimagharibi. Nchini Tunisia, kwa mfano, Bourguiba alitunga Kanuni ya Hadhi ya Kibinafsi mnamo 1956, ambayo alipotoka kutoka katika hukmu za kisheria na kudai kirongo kuwa haikukiuka sheria ya Kiislamu na kwamba imevuliwa kutoka katika roho yake na vipengee vyake japokuwa wingi wa kanuni zake imejengwa kutokana na sheria ya Ufaransa, na inajumuisha msururu wa kanuni ambazo ziko kinyume na hukmu za kisheria za kukatikiwa. Ambazo mifano yake ni mingi kama vile: kupuuza tofauti ya dini kama jambo linalokiuka ndoa kwa mujibu wa kanuni ya kimataifa ya haki za kibinadamu, inayosema kuwa “Wanaume na wanawake walio na umri uliotimu, pasi na mipaka yoyote ya kirangi, taifa au dini, wana haki ya kuoana na kuunda familia”, na kama ilivyo marufuku ya ndoa ya wake wengi na adhabu kwa mume aliye na wake wengi kwa mujibu wa sura ya 18, kama vile ukiukaji wa hukmu ya Kiislamu iliyo tabanniwa. Na kisha wakaja wajukuu baada yake na kukamilisha mchezo wa ufisadi katika uwanja wa kijamii, na wakapambana na hukmu za Allah, utungaji wa kanuni kinyume na vipengee wazi vya Uislamu, ambapo kanuni mpya zilitungwa katika enzi ya El-Sebsi zinazo ruhusu ndoa ya mwanamke wa Kiislamu kwa mwanamume asiye Muislamu. Hivi majuzi, Raisi wa Tume ya Uhuru wa Kibinafsi na Usawa, katika Afisi ya Raisi wa Jamhuri ya Tunisia, Bouchra Belhaj Hamida, alitangaza kuwa kamati imeanza kupendekeza kanuni itakayo jumuisha kumtaja mume pamoja na mke kama viongozi wa kisheria wa familia, kufutilia mbali mahari katika mkataba wa ndoa, ambapo aliikadiria kama matusi kwa wanawake, pamoja na kadhia ya usawa baina ya wanaume na wanawake katika urithi ambayo ndiyo inayobebwa kwa sasa.   

Nchini Misri na Saudi Arabia, wanataka kuwekwa umri maalumu wa ndoa. Pia nchini Saudi Arabia, marekebisho yamefanywa kwa nidhamu ya usimamizi wa wanaume “Wilayah” juu ya wanawake, na mifano katika muktadha huu ni mingi, lakina hakuna nafasi ya kuitaja.

2.Amali na matukio ya kujiburudisha (sekta ya burudani): mipango ya burudani imekuwa miongoni mwa mbinu maarufu za kuingiza usekula na ufisadi katika familia za Waislamu. Haya yanajiri, chini ya kisingizio cha kuondoa shinikizo za maisha, kusaidia na kukuza vipaji, pamoja na kuzungumzia kuhusu kupata mapato ya kiuchumi na faida za kimada kwa ajili ya watu kutokana na miradi hii. Miradi na amali za ufisadi zinazo gongana na maadili ya Kiislamu na kupigia debe maadili ya Kimagharibi na kuyaingiza katika nchi za Waislamu. Wanatafuta njia ya kueneza uovu na uchafu miongoni mwa Waislamu, inayojumuisha mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake na kufichua Awrah na maovu mengine chini ya guo la mamboleo na uwazi. 

Saudi Arabia, kwa mfano, inayoshuhudia mpangilio wa kampeni ya kuibebesha umagharibi na usekula inayotekelezwa moja kwa moja na dola hiyo ili kuifurahisha Amerika, imetangaza mpango katika nyanja ya mabadiliko ya kiuchumi ya Kisaudi, ambao miongoni mwa nguzo zake ni sekta ya “Utamaduni na Burudani” na uwekezaji katika sekta ya utalii. Hivyo basi, kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa, “Ruwaza ya Kitaifa” inalenga kuongeza maradufu matumizi ya familia katika utamaduni na burudani ndani ya Ufalme huo kuanzia asilimia 2.9 hadi asilimia 6. Katika muktadha huu, Mamlaka ya Burudani ilianzishwa kuambatana na Ruwaza ya 2030 iliyo wasilishwa na Mohammed bin Salman ili kuhalalisha na kuidhinisha kisheria vitendo vyote vya ufisadi na muozo nchini Saudi Arabia. Kwa hayo, Haramu imekuwa Halali kupitia mashekhe wa Kisaudi baada ya miaka mingi ya ukandamizaji na upungufu, hususan kuhusiana na wanawake, na uovu (Munkar) ukawa wema (Ma’ruf) kupitia Mamlaka ya Burudani chini ya mwito wa uwazi. Kwa hivyo, iliandaa maonyesho, sherehe, na matamasha ya kisanii na muziki, na kusimamia kuanzishwa kwa sinema, ufunguzi wa Jumba la Opera, kuandaa mitindo ya wanawake, kuwaruhusu wanawake kuhudhuria mechi za mpira, na kufanya matamasha ya mchanganyiko wa wanaume na wanawake. 

Hafla na vipindi vingi pia zinaandaliwa katika biladi za Waislamu kwa usaidizi na udhinishwaji wa Dola hiyo ingawa haziandaliwi moja kwa moja nayo, kama vile vipindi vya vipaji (kucheza, kuimba na kuigiza) ambavyo vinapeperushwa na vyombo vya habari, pamoja na amali zilizoandaliwa na mashirika na taasisi zisizo za kiserikali.

3.Nidhamu ya kielimu na mtaala: fahamu ya familia na uhusiano kati ya wanachama wake imekumbwa na yale yaliyozikumba fahamu nyenginezo na fikra za ufisadi na kujaribu kuwatia usekula chini ya sera za kielimu ambayo haikujengwa juu ya Uislamu, na inatafuta kuiangamiza thaqafa ya Kiislamu katika nyoyo za watoto wa Kiislamu. Hii inaonekana waziwazi katika mabadiliko ya kudumu yanayofanywa na serikali tawala juu ya mtaala wa elimu kwa kuitikia maagizo ya mabwana zao, ambapo tunaamini kuwa marekebisho haya yanaangazia fahamu za haki za wanawake na usawa wao na wanaume, ambapo ni anwani pana ambapo hivi karibuni imebeba pamoja nayo miito kama utambuzi wa kibinafsi wa wanawake, kujimakinisha kibinafsi katika jamii na kuondoa udhibiti wa wanaume. Natija yake, elimu na utafutaji ajira zikawa ni kipaumbele kuliko ndoa na kuanzisha familia kwa wasichana wengi. Ndoa za mapema zilipigwa vita katika marekebisho haya ndani ya mipaka hii. Vilevile, miongoni mwa mada zilizohutubiwa zilikuwa ni afya ya uzazi kwa wanawake, haja ya mpango wa uzazi na kupunguza ukubwa wa familia na idadi ya wanafamilia. Ndani ya mpaka huu, tunawaona wakizigawanya familia kwa vigawanyo vya familia ya karibu (ndogo) familia pana (kubwa), wakizisifu familia za karibu na kuzikashifu familia pana, na kuzikadiria familia kubwa kama familia za “kitamaduni” huku familia zenye wanafamilia wachache kama “za kisasa”. Hii huonyeshwa katika sura wanazoziweka kwa ajili ya familia, hususan katika viwango msingi, ikilinganishwa na picha mbili, moja yapo ikiwa ni ya kale (picha ya familia pana) na nyengine ni ya kisasa (picha ya familia ndogo).   

Baya zaidi, walibadilisha picha za kina mama na kina nyanya waliojifinika katika picha wanazo ziweka kwa ajili ya familia, pamoja na picha nyenginezo zinazo onyesha wanawake wakiwa hawakujifinika wakiwa na nguo za kimagharibi na mapambo, kama ilivyo katika mabadiliko ya hivi karibuni katika mtaala wa shule mnamo 2016 nchini Jordan na Palestina, pamoja na picha za wanaume ambao ndevu zao zimenyolewa zilizobadilisha picha za wanaume wenye ndevu. Katika njia hii iliyo fungamanishwa na akili za watoto hawa kuwa familia halisi ni familia ndogo, na kwamba kuyaona makosa haramu na kufichua uchi (Awrah) katika familia yao ni jambo la kawaida; bali, ni kuendelea kwa miji! 

Katika muktadha wa watoto, haki za watoto na uhuru wa kuchagua vitendo vyake yamesisitizwa, na hata kama wazazi wanataka kuwazuia watoto wao kutokana na kufanya jambo, au ikiwa watakumbwa na ghasia kutoka kwao, wanaweza kuishia polisi au mashirika ya haki za kibinadamu. Huu ni mwaliko kwa watoto kuwaasi wazazi wao, na ni kupigania haki hadi katika usimamizi (Qawamah) na uchungaji kutoka katika mtizamo wa kisheria

4.Usaidizi na kusahilisha kazi ya mashirika ya kieneo na ya kimataifa ya haki za kibinadamu na wanawake yanayotafuta kuifisidi familia za Waislamu, yanayotekeleza shughuli zao chini ya guo la haki za wanawake na watoto kwa hivyo yanapenya katika mashule na vyuo vikuu, yakipenyeza fikra za sumu miongoni mwa wanafunzi wake, na kuandaa hafla angamivu na amali zenye madhara kwa familia na mujtamaa. Yanaingia majumbani na kupigia debe mipango ya uzazi ili kuiwekea mipaka familia chini ya mwito wa afya na usalama wa wanawake, kuipiga vita familia ya wake wengi na ndoa ya mapema, na kupambana na fahamu ya ulezi chini ya bendera ya haki za wanawake, kutambulika kibinafsi na uhuru wa maamuzi, kuzuia udhibiti na utawala wa wanaume juu yake. 

5.Kuidhinisha na kukubali mikataba ya kimataifa inayolenga nidhamu ya kijamii katika Uislamu, ikiwemo kadhia ya ndoa na familia, kama mkataba wa CEDAW, ambao masharti yake yanalingani uhuru wa kuanzisha mahusiano haramu baina ya vijana wa kiume na wa kike chini ya kisingizio cha uhuru wa kibinafsi. Pia unalingania usawa kamili baina ya wanaume na wanawake, kuondolewa kwa ndoa kwa mujibu wa vipengee vya sheria ya Kiislamu na kutabanni ndoa za kiserikali, kuondolewa kwa usimamizi (Wilayah) wa baba juu ya watoto wake, hususan wa kike, na mambo mengine yanayo kiuka vipengee vya Uislamu.

 Hizi ni baadhi ya njia na mbinu zinazotumiwa na serikali zinazo tawala katika nchi za Waislamu ili kuifisidi familia za Waislamu katika jaribio la kuzitia usekula; hivyo basi, kutia usekula katika biladi za Waislamu kwa jumla. Hili lahitaji msimamo makinifu kwa kila Muislamu mwenye ikhlasi na makini katika Dini yake na Ummah kutibua njama hizi na maovu haya. Na inawahitaji kufanya kazi kwa ikhlasi na kwa nguvu kuileta dola inayotutawala kwa kitabu cha Mola wetu, kusimamia mambo yetu, na kuhifadhi mujtamaa na familia zetu. Dola hii ni Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo ni ahadi ya Mola wetu Ta’ala, na bishara njema ya Mtume wetu (saw). 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bara’ah Manasrah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:14

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu