Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mama, Mke, na Mke Nyumbani: Malipo ya Utumwa wa Uzaaji Watoto!
Hivi Ndivyo Namna Usekula Ulivyo Yafisidi Maisha ya Wanawake!

(Imetafsiriwa)

Nini maana ya mwanamke kuwa mama, mke na mke nyumbani kwa mujibu wa itikadi inayokataa maadili yote ya utu, akhlaqi, au ya kiroho kwa sababu inaona kuwa manufaa ndio kipimo cha vitendo na kwamba manufaa ndio mizani na kinacho pimwa? Itikadi hii huona kuwa wanadamu huthaminiwa kwa mujibu wa uzalishaji wao ndani ya mujtamaa na kwa kiwango cha mapato yao ya kimada! Hivyo basi, mke nyumbani si mmoja wa watu wanaozalisha kwa sababu hukmu inayo pimiwa watu ni: “Ikiwa mtu atafanya kazi atafanikiwa”. Lakini mama na mke nyumbani wako nje ya mpangilio huu mpya wa kimataifa kwa sababu hawafanyi kazi ya kulipwa, na kwa sababu wamefungika na mume, watoto na familia kama ilivyotajwa katika waraka wa Beijing.   

Ikiwa mwanamke anafanya kazi bila ya malipo au ujira; anafanya kazi kwa bidii na kuchoka na kujitolea wakati wake, afya na juhudi pasi na mapato ya kimada, inazingatiwa kuwa ni ujinga na kubakia nyuma ikiwa ni kwa ridhaa yake, au huonekana kuwa ukandamizaji na kukiuka haki zake ikiwa ni kwa kulazimishwa.

Hii ndiyo sababu wanawake kama kina mama, wake na wake nyumbani huorodheshwa ima kama wasiojitendea haki au kukandamizwa; ima walichagua kwa khiyari kuishi na jukumu duni la kiasili, kujiweka mbali na ushirikiano wa ujenzi na uimarishaji wa jamii zao, na kujimakinisha na kujenga uhuru wao. Na kwa kuwategemea wanaume kuwapa masrufu yao na uangalizi wao, wamekuwa mzigo kwa familia na wasiokuwa na maana. Uorodheshaji huu umewatia mtegoni wanawake katika machaguo yao, na kuwaweka katika hisabu na maswali endapo watalalamika au kudai haki zao zozote. Kwa vyovyote vile, sheria haiwalindi wajinga na wale waliojipuuza! Na kabla ya hilo, inawaanika wanawake kukejeliwa na hata kuchukiwa na wanawake wengine! Na huenda wakatelekezwa na waume zao ikiwa watabeba imani kuwa maisha ya ndoa ni ushirikiano katika dori na majukumu, na sio kuwa kila mmoja ana majukumu yake maalumu; kwa hiyo anakataa kuwa mtoaji masrufu wa pekee, na mwanamke awe mwenye kufaidika na mpatilizaji! 

Kigawanyo cha pili hupokea maliwazo na uungwaji mkono kwa sababu mwanamke hakuchagua kujiweka katika sanduku hilo, bali ndoa, familia na watoto ni uovu usioepukika. Na hii ndiyo kadari nyeusi inayo wasubiri wanawake wenye kufeli, ambao hawakufanikiwa kimasomo! Mwanamke anapokea maoni haya yanayo muonesha yeye kama mwathiriwa, na rai kuwa lau angekuwa na kazi maishani, ni bora zaidi kuliko kufungwa katika kuta za nyumba, akisafisha, akipika na kulea watoto wake, na kwamba kazi yake ndani ya nyumba yake ni kumdunisha na kumnyima haki zake. Swali la – “Kazi yako ni nini?” – linamtia hofu na kero, na aghalabu hujibu kwa haya na aibu: “Kwa bahati mbaya niko nyumbani!”

Wanawake ambao ni mfano wa kuridhika, heshima, cheo, kusafiri na walio ngangari. Ni wale wanaofanya kazi ili kujidhihirisha na kupambana na mipaka ya ghariza zao, na hawakubali kuwa bila ya ajira au kutengwa na dori yao kufungika tu kama “mashini ya kutengeza watoto” na kuangalia nyumba, na kushindana na wanaume wakati mwengine katika kazi nzito na ngumu. Wao huziepuka dori msingi zilizotayarishwa kwa ajili yao, na kuvunja vizuizi vya kuwategemea wanaume. Mwanamke huyu huenda akaolewa na kuzaa, lakini hasikizi uzushi juu ya mama na mke na ulezi wa watoto, bali anatia juhudi na nguvu zake maradufu kwa gharama yake na familia na watoto wake, ili asipoteze Medali ya Heshima inayopokewa na serikali, taasisi, vyombo vya habari na mashirika ya utetezi wa wanawake kwa kuwa mwanamke ngangari aliye na uwezo wa kukabiliana na changamoto hizi!! Lakini swali linabakia: Ni nani aliyeziweka changamoto hizi na masharti haya yasiyompa utu kamili isipokuwa anapo jinyongoa zaidi na kupuuza majukumu yake ya kighariza chini ya kisingizio cha kujinadi kibinafsi? Je, lengo nyuma yake ni kupata maslahi ya wanawake au maslahi ya warasilimali walafi?

Maoni yote haya yaliafikiana na maendeleo ya kiviwanda katika nchi za Kimagharibi, zilizoona haja ya wanawake kushiriki katika kazi nje ya nyumba na wanaume ili kuongeza uzalishaji. Na kwa kuwa nguvu kazi ni lazima iwe rahisi, wanawake ndiyo chaguo bora. Hata leo, mwanya wa ujira kati ya wanaume na wanawake unaweza kuonekana miongoni mwa wale wanaofanya kazi hizo hizo kama wanaume licha ya wito wa usawa na madai ya kuondoa tofauti na ubaguzi baina ya wanaume na wanawake! Huu ni usekula katika mikataba yake mibaya na michafu zaidi; huwanyanyasa wanawake kwa gharama ya cheo chao cha mama, familia na mazingira ya kimaumbile kupitia kunadi madai ya kirongo ili kuwadanganya wanawake!

Usekula ulikiuka ghariza ya mwanamke na kuvuruga maisha yake siku ile ulipo hujumu dori ya mama na kuifunga katika kuzaa pekee. Dori hiyo iliachiwa mayaya na wafanyikazi wa nyumbani. Dori ya kuchunga watoto kwa sasa sio tena ya mama pekee. Hata fikra ya mama anayezaa ilitupiliwa mbali na kubadilishwa kwa mama badali anaye kodisha uzao wake, ikimpa mama asili fursa ya kufanya kazi na kujionesha na kudumisha swiha na mwili wake!! Kwa hivyo fungamano pekee baina ya mama na mwanawe, uzio wa kitovu, lina badali ya kimada aliyopewa na serikali za kirasilimali eneo la Magharibi kwa njia rasmi na ya halali; na hivyo, kufuta ghariza ya kike kikamilifu, na kukiuka moja wapo ya msingi mikuu: kuwa mama mbebaji mtoto tumboni mwake!! Hii ilimfanya mtetezi wa wanawake kuwa na ujasiri na kulilaumu umbile la kike. Simon De Beauvoir aliandika katika kitabu chake kwa jina ‘The Slavery of Childbearing, “Kuzaa huufunga uhuru wa wanawake, kihakika ni utumwa ambao ni lazima upigwe vita, na mzizi wa ukandamizaji wanawake ni majukumu yao kuwa wajawazito, uchungaji na ulezi wa watoto!”

Wamagharibi wameamua kudhoofisha kinga ya jamii ya Kiislamu kupitia uenezaji wa neno “ukombozi wa wanawake” kumaanisha kuwa mwanamke ni mtumwa ambaye ni sharti akombolewe na kwamba amepotea na anahitaji kuokolewa. Kikwazo pekee cha ukombozi wake ni wale wanaoupigia debe! Shambulizi dhidi ya fahamu ya “mama, mke na mke nyumbani” ni kali hadi neno mke likawa linasifia hali ya kijamii kinyume na maana ya kindani iliyobebwa na wanawake wa Kiislamu kuhusu mume, uhusiano wake naye, fahamu ya utiifu na uhusiano mwema, heshima, ukaribu na huruma. Fahamu hizi msingi, ambazo zimefafanuliwa katika nususi za kisheria, zinawasilishwa kwa njia chafu katika runinga, na hukumbwa na chuki na istihizai, au kupitia baadhi ya wahubiri na darasa za kidini katika runinga na idhaa, kuongeza chumvi sifa hizo ili kutuonyesha kuwa mke mwema ni kiumbe cha kindoto na sio mwanadamu wa kawaida.

Filamu, musalsala, hadithi na riwaya zimeunda sura mpya kwa mwanamke wa Kiislamu kuhusu ndoa kama fungamano la kimasharti lililojengwa juu ya usawa wa haki na majukumu, kuheshimu uhuru, haki ya upinzani, ubadilishanaji majukumu ya kifamilia, uhuru wa kifedha na fahamu nyenginezo fisidifu zilizo potoka kutokana na ufahamu wa kisheria juu ya ndoa na mume. Na kuigeuza uwanja wa mzozo katika ushindani uliozushwa ambao ndani yake mwanamke ni lazima athibitishe thamani na ubwana wake; vyenginevyo, ataishia kuwa kama mke anayemsubiri mumewe jioni amletee unga aoke!  

Serikali katika biladi zetu za Kiislamu zimetilia nguvu fahamu hizo potofu kupitia kupitisha kanuni kinyume na ufahamu wa kisheria. Kanuni kama hizo zinaamrishwa kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Dunia na taasisi zenye nguvu zinazofanya makongamano na warsha, yanayotoa maamuzi kuwa wanawake wa Kiislamu wamekandamizwa majumbani mwao chini ya usimamizi wa waume zao na kulingania kuachana na mila na destruri zinazotilia nguvu fikra hii. Makubaliano ya CEDAW hukadiria kuwa aina za ubaguzi dhidi ya wanawake huanza kwa kuzifunga dori zao kwa cheo cha mama, ndoa na ulezi, na hivyo basi, vifungu vilivyotiwa saini na biladi nyingi za kiarabu vimekuwa vya kuondoa aina za unyanyasaji kwa kuifanya ndoa ya mapema kuwa uhalifu, kupeana haki ya uavyaji mimba na talaka … na hivi majuzi ni nchini Tunisia, ambapo ni haki kwa wanawake wa Kiislamu kuolewa na mwanamume kafiri!!   

Hadhi ya mke nyumbani imetelekezwa na kuchukiwa, na hata katika kadi za vitambulisho rasmi katika nchi nyingi, sehemu ya taaluma inajazwa kama “asiye na ajira”. Imeshuka hata kumwita “asiye na taaluma” katika baadhi ya nchi zinazodai kuwa viongozi wa haki za wanawake!! Lakusikitisha, dori ya mke nyumbani imekejeliwa na kutoheshimiwa sana katika biladi zetu za Kiislamu. Kazi imekuwa ni lazima na sio kwa mujibu wa haja ya wanawake kwake au haja ya jamii kwa kazi yake. Zaidi ya hayo, kazi hiyo haistahili maumbile ya wanawake. Janga kubwa ni kuwa kazi imekuwa ni shinikizo la kiuchumi linaloikamua nguvu ya mwanamke na kutumia masharti ya kimada yanayo dorora, kumnyima dori yake asili kama mama mchungaji wa watoto wake, mke mchungaji wa mumewe na mke nyumbani mchungaji wa nyumba yake pasi na kufikiria kuhusu udharura wa utafutaji riziki na kuhakikisha maisha ya sawa ambayo mume ameshindwa kupeana, au sahihi zaidi ni dola kushindwa kupeana!

Matokeo yake yakawa ni majanga; kutelekezwa kwa familia kukaenea ndani ya familia nyingi, na matatizo ya kindoa yakawa mengi kutokana na majukumu mazito na shinikizo za kimwili na kisaikolojia zinazo wazunguka wanandoa. Viwango vya utundu miongoni mwa watoto vimeongezeka kwa kutoweka kwa walezi wao katika ufuatiliziaji na uangalizi. Familia nyingi zimevunjika na viwango vya talaka, viwango vya useja na kuzembea katika kuoa na kuvunjika kwa mkataba vimeongezeka!!

Kwa kuwa taasisi ya familia ni msururu wa duara zilizounganika pamoja, imeundwa na kulindwa na sheria ya Allah. Wamagharibi wametambua umuhimu wa dori ya wanawake katika taasisi hii na hivyo kuwalenga kama kina mama, wake na wake nyumbani katika jaribio la kuzalisha sura ya wanawake wa Kimagharibi katika muundo tatanishi mno!

Lakini ni jambo lisiloweza kukataliwa kuwa orodha ya vipaumbele vya wanawake wa Kiislamu imegeuka juu chini. Dori ya mama, mke na mke nyumbani sio tena misheni yao ya kwanza. Dori kubwa na ujira wa mama kwa Allah (swt) imepotea isipokuwa yeye (mama) atekeleze dori yake vyema, amche Allah na ajali na kuwajibika katika nyumba yake.

Uislamu umedhamini maisha thabiti na ya utulivu kwa wanawake kama wanadamu, ukizingatia ghariza yao na kuwapa majukumu katika njia inayo kwenda sambamba na mazingira na maumbile yao. Inabakia kusemwa kuwa utekelezaji wa hukmu hizi za kiwahyi ni jukumu la kisheria kwa wanaume na wanawake na hukmu hizi ni lazima zitekelezwe na dola inayounda mazingira muafaka kwa wanaume, wanawake na familia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Nisreen Budhafri

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu