Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uharibifu Mkubwa dhidi ya Familia (Sehemu ya 1):

Urasilimali Unamfedhehesha Mama

Neno uharibifu hivi sasa nimaarufu linajadiliwa katika muktadha wa uchumi wa kidijitali kwamba ni kukosa umakinifu kwa biashara duniani kwani njia za kibiashara za zamani zimepitwa na wakati. Lakini maana ya uharibifu katika makala haya ni hasa fujo na machafuko yanayo athiri mamilioni ya familia kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na limekuwa janga la kibinadamu ambalo limesababishwa pakubwa na msukumo wa harakati za kuwawezesha wanawake. Katika hali yake ya usasa, ukombozi wa wanawake ukioanishwa na nidhamu ya kiuchumi ya kisekula, ambayo kumezaliwa zama mpya zenye uharibifu wa umama ambao hauathiri tu wanawake Waislamu bali pia unawanasa kina mama ndani ya nchi zisizokuwa za Waislamu hususan Magharibi na Asia-Pacific.

Sehemu ya kwanza ya makala hii itatathmini namna huu uharibifu unavyosababishwa na uhamiaji wa ukombozi wa wanawake unaochochewa na nidhamu ya kiuchumi ya kisekula katika kuwapatiliza kina mama, hivyo basi imekuwa na dori ya moja kwa moja katika kuwatelekeza mamilioni ya watoto na kuzidi kwa idadi ya talaka. Kisha katika sehemu ya pili, tutatathmini namna uhuru, moja ya sehemu ya misingi ya usekula urasilimali ulivyo sababisha kupungua kwa idadi ya familia na hata kupelekea kuhatarisha maendeleo.

Uhamiaji wa ukombozi wa wanawake: Ukoloni mkubwa juu ya Umama

Tangu kuzinduliwa kwake, urasilimali kiuhakika daima unawadharau wanawake na unawaangalia kama wafanyikazi duni au njia za uzalishaji. Kilele cha dori ya wanawake ipo tu katika kuwanasibisha na lugha ya kiuchumi – nako ni kuzalisha mada na faida katika biashara za kirasilimali. Maslahi maovu ya urasilimali katika siku zake za mwanzo yalikuwa yamefunikwa na fikra za ukombozi wa wanawake na pazia ya miito ya kuwawezesha wanawake ili ionekane tamu.

Lakini katika zama hizi za uharibifu, uso wa kweli wa Urasilimali unafichuka kwa kasi. Ulafi wake umewafanya kina mama kupatilizwa pakubwa hususan wale walioko katika eneo la Asia-Pacific kama soko la mwisho katika matumaini ya Urasilimali unaofariki. Eneo hili linakumbwa na uhamiaji wa ukombozi wa wanawake ambao umesababishwa na matarajio ya kirasilimali yasiyokwisha ya ukuaji wa uchumi. Matarajio haya yameangaziwa wazi katika hotuba ya Hillary Clinton katika Wanawake wa APEC na Jukwaa la Uchumi, 29 Juni 2012 ambapo alisema,Wanawake sasa wanawakilisha asilimia 40 ya wafanyikazi duniani, asilimia 43 ya wafanyikazi wa kilimo duniani, na ni zaidi ya nusu ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani. Kwa hiyo inaingia akilini: Kwa kudhibiti uwezo wa kiuchumi kwa wanawake ni kwa kila nchi kama kuwacha pesa mezani. Haingii akilini hususan wakati ambapo tunajizatiti kujikuza ili kutoka katika janga la kiuchumi.”

Matamshi ya Clinton yanafichua wazi dhamira ya kweli ya nchi za kirasilimali ambazo zinamoyo wa kuwatoa kafara wanawake kwa sababu wanawatizama kama wafanyikazi tu na injini ya ukuwaji wa uchumi. SIO kama kina mama wa kizazi kijacho na heshima inayostahiki kulindwa. Urasilimali kwa makusudi unawafedhehesha kina mama ni wafanyikazi tu, hata wakiwango cha chini. Kwa mujibu wa ripoti ya ILO 2013, wanawake milioni 43 wameajiriwa kama mayaya, wapishi, wasimamizi wa nyumba na vijakazi. Ilidhihirisha ongezeko kubwa la idadi ya milioni 19 ya wanawake walioajiriwa kama wafanyikazi wa nyumbani kwa zaidi ya takribani ya miaka 18 iliyopita. Umasikini na ukosefu wa ufanisi kwa mamilioni ya wanawake ndani ya nchi zao kumewalazimisha kuwacha nyumba zao na watoto wao ili kwenda kutafuta maisha. Wengi wa wafanyikazi wa nyumbani wanatoka katika nchi za ulimwengu wa tatu zikijumuisha ulimwengu wa Waislamu. Wengi wakitoka Asia Pacific (milioni 21.4), wakifuatiwa na Latin Amerika na kisha Caribbean ikiwa na milioni 19.6. Ni utekelezwaji wa urasilimali duniano na mpangilio wake wa kifedha wa riba na nidhamu yake ya masoko huru pamoja na misingi yake ya uhuru ambayo imesababisha utajiri kurundikana katika mikono ya wachache na natija yake ni kusababisha uhamiaji wa ukombozi wa wanawake kwa sura ya wafanyikazi wa nyumbani na kuwapelekea kunyanyaswa.

Makumi ya Mamilioni ya Watoto wanawachwa nyuma

Fikra ya sumu ya ukombozi wa wanawake kwa ushirikiano na ulafi wa urasilimali daima hautilii maanani athari yake juu ya watoto, familia na jamii kwa ujumla. Athari hii kubwa imetolewa ilani na Vannesa Tobin, naibu mkurugenzi wa New York wa Umoja wa Mataifa wa Mfuko wa Watoto (UNICEF) ambaye alisema kwamba tafiti kadhaa zimeonyesha kwamba gharama za kijamii zinazotokamana na uhamiaji wa wafanyikazi zinashinda zile za manufaa ya kiuchumi, huku mahusiano na mabadiliko ya kifamilia yakiathiriwa kwanza. Tobin alisema kwamba kuzidi kwa uhamiaji wa "ukombozi wa wanawake" umezidisha matatizo kwa kuwa inamaanisha “kubadilisha upya dori ya kiuchumi ya wanawake katika mujtama na ndani ya familia.” (2008, Kongamano la Kimataifa Kuhusu Jinsia, Uhamiaji na Maendeleo)

Uharibifu wa umama, kwa kuongezea na kutikiswa kwa taasisi ya ndoa daima imezalisha uwepo wa kizazi kisichokuwa na msingi, chenye matatizo na kilichotelekezwa na ikiwa ni natija ya taifa ambalo linawaajiri kina mama kama injini za ukuwaji wa uchumi. Tume ya Indonesia ya Ulinzi wa Watoto (2016) ilichapisha taarifa kuhusu mamilioni ya watoto wachanga waliotelekezwaa na mama zao ili kwenda kufanya kazi ng'ambo. Wapo watoto wa Indonesia milioni 11.2 waliokosa malezi ya wazazi na mapenzi kutoka kwa mama zao, ilhali taarifa za UNICEF (2008) zinaashiria kwamba takribani watoto milioni 6 ndani ya Filipino wametelekezwa kwa kuwa mama zao wamekuwa wafanyikazi wahamiaji. Watoto waliotelekezwa pia wanakabiliwa na matatizo wanapo hamia ng'ambo na mama zao ambao ni wafanyikazi wahamiaji. Ndani ya Sabah – Malaysia – inakadiriwa kwamba kulikuwepo na takribani watoto elfu 50 kutoka kwa wafanyikazi wahamiaji wa Indonesia ambao hawapati haki nzuri za elimu. Ndani ya Hong Kong, pia nako kunalo suala la "watoto ambao hawakusajiliwa" waliozaliwa kutokana na mamia ya maelfu ya wafanyikazi wahamiaji wa Indonesia na Filipino.

Uhamiaji wa kiuchumi umewatenganisha mamilioni ya watoto kutoka kwa mama zao nalo pia linatokea ndani ya Uchina. Kwa mujibu wa Muungano wa Wanawake Wote wa Uchina na UNICEF (2016) wapo watoto milioni 61 ndani ya Uchina waliochini ya umri wa miaka 17 ambao wamewachwa katika maeneo ya vijijini huku mzazi mmoja au wote wakihama kutafuta kazi. Zaidi ya watoto wanaume na wasichana milioni 30 wengine wakiwa na umri wa miaka minne wanaishi katika shule za mabweni za serikali katika vijiji mbali na wazazi wao na mara nyingi mbali na nyanya/babu zao au walinzi wao. Watoto hawa waliotelekezwa ndani ya Uchina wanakabiliwa na matatizo mengi kama usafirishaji wa watoto, vurugu za kijinsia, kujiua, uhalifu na maradhi mengine ya kimujtama kama yalivyofanyiwa utafiti na Li Yifei (2015), Profesa kutoka Chuo cha Beijing Normal. Hii ndiyo athari ya uharibifu wa umama ndani ya mujtama wa kisekula ambao uko mbali na nuru na muongozo wa Uislamu. Kumbuka Mwenyezi Mungu (swt) asema"

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى﴿

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (Ta Ha, 20:124)

Kuwawezesha wanawake kukubwa ndani ya Uislamu ni kuwajenga katika dori yao kama walinzi wa mujtama na walimu wa kizazi kijacho, SIO kama kikosi cha wafanyikazi. Katika Kielelezo cha Katiba cha Hizb ut Tahrir (Muqaddimah Dustur), katika kipengee kinachohusiana na Nidhamu ya Kijamii ya Uislamu ("Nizam al-ijtima'i"), kinasema, “jukumu msingi la mwanamke katika Uislamu ni kama mama kwa watoto wake na msimamizi wa nyumba ya mumewe. Mwanamke ni heshima inayostahiki kulindwa."

Mfano wa Uislamu uko kinyume na Urasilimali. Uislamu haswa unahifadhi mahusiano mazuri baina ya jukumu la umama la wanawake na ubora wa kizazi kijacho kwa kuhakikisha kuwa maumbile ya umama yanabakia kwa ukamilifu ndani ya jamii na kuhakikisha kudumu kuzaliwa kwa kizazi bora kupitia uungwaji mkono na nidhamu za elimu, kijamii na kiuchumi za mfumo wa Kiislamu, illhali wakati huo huo zikiwadhamini wanawake kupata haki za kielimu, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Uislamu unaamrisha kwamba wanawake lazima wadhaminiwe matumizi kutoka kwa jamaa zao wanaume, na lau watakuwa hawana jamaa yeyote mwanamume, basi dola itahakikisha kuwa inawakidhia mahitaji yao ya kifedha.

Mjadala kuhusiana na kuendelea kwa athari za uharibifu juu ya umama katika familia na mtizamo wa Uislamu juu ya ujenzi wa familia madhubuti utatathminiwa katika sehemu ya pili ya makala hii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:58

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu