Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Michezo ya Runinga: Kiwanda Kinacho Sambaza Uovu wake Juu ya Familia na Jamii!

(Imetafsiriwa)

Michezo ya runinga imekuwa maarufu miongoni mwa watu wa umri wote walio na tofauti katika kupenda kwao. Idhaa za michezo ziko makini kupeperusha michezo tofauti tofauti mfano filamu za kawaida, filamu za kisasa, filamu za utafiti pamoja na michezo ya kuendelea katika runinga kuanzia ya kijamii hadi ya vichekesho, mapenzi na ngono, michezo ya kitoto na vipindi vya mfululizo kiasi kwamba kila vioo vya runinga vilivyo na vipindi hivyo vimekuwa marafiki wa kila mwanachama wa familia kwa kutegemea anachopenda na kutamani. Hasa nyakati hizi za maendeleo ya kiteknolojia, runinga za mfululizo na vipindi haviko tu katika runinga bali pia vinapatikana katika angavu.

Hii michezo na vipindi vya mfululizo-hususani vilivyo tafsiriwa-havikosi fikra ngeni na maadili juu ya thaqafa ya Kiislamu ambayo yanagonga na maadili ya Kiislamu na mizizi ya misingi yake na inalenga kujenga fikra jumla ndani ya ardhi za Waislamu ili ziwiane na fikra na fahamu za Kimagharibi na kuchukua zile zilizo oza ili ziweze kupigiwa debe ndani ya jamii zetu kama za kimaumbile na kawaida na kwamba inafuatiwa na Sera ya vyombo vya Habari ndani ya ardhi za Waislamu, ikilenga familia na jamii ndani ya ardhi za Waislamu.

Twaona kwamba katika hizi filamu za mfululizo kwa mfano zinashajiisha mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake, na kuufanya kuwa ndiyo maisha na hitajio la zama hizi, na tunapata kuwa inashajiisha tamaduni ya kuwa uchi na uzinifu ndani ya wanawake Waislamu, wakilifanya hilo kama kuenda sawa na mtindo na kuwa wazi kwa ulimwengu. Pia tunapata kuwa wanapigia debe mahusiano ya Haramu kati ya wanaume na wanawake wadogo, wakiwafanya wakubali na kuvutiwa na “mapenzi”. Fauka ya hayo, tunapata ishara ya kuanikwa kwa Munkar na vitendo vilivyo katazwa mfano kuoneshwa kunywa pombe kama kitu cha kawaida, pamoja na miito ya uhuru kamili na uhuru uso vikwazo na vidhibiti vya hukmu (Shari’ah), ikijumuisha sherehe na mila za kishirikina na kuabudu masanamu ambazo zinapenyeza hizi filamu na vipindi vya mfululizo hususan vya Kihindi.

Athari ya hizi filamu na vipindi vya mfululizo haikufungika tu katika fikra na fahamu zake lakini zimejitokeza katika tabia za kula na mavazi pamoja na mahusiano kati ya wanachama wa jamii na familia, lakusikitisha ni kuwa mashujaa wa sinema hizi wamekuwa ndiyo wakuigwa na baadhi ya watoto Waislamu, kujifananisha nao katika mavazi, kunyoa, matembezi na tabia, na hata majina yao wakiwataja watoto wao!!

Tukiangalia hali za wanawake ndani ya michezo hii, tunawaona wakiwasilishwa kwetu katika sura zifuatazo: ima akiwa hana uwezo na ni mwenye kukandamizwa na hana udhibiti juu ya chochote na hana thamani katika jamii, katika muktadha huu jukumu kuu la wanawake kuwa mama na mke nyumbani linapigwa vita na kuoneshwa sababu za kupata shida kwake. Mwanamke anaoneshwa kama aliye kandamizwa na kutaabika kwa sababu ni mwanamke aliye kifungoni ndani ya nyumba yake. Hana kazi isipokuwa kuangalia nyumba yake na kulea watoto wake, na hivyo basi, imepandikizwa katika akili za wanawake kuwa suluhisho la matatizo yao lipo katika kuleta uasi dhidi ya jukumu hilo na kazi zilizomo ndani yake. Katika picha ya pili, amewasilishwa kama mwenye uwezo wa kushindana na wanaume na kusimamia mambo yake na kujitosheleza mahitaji yake na kufanya maamuzi yake kibinafsi, kwa kuwa yuko huru katika vitendo vyake, na anafanya anavyotaka bila mipaka. Hakuna vidhibiti juu ya mzunguko wake na kila kinachoweka kikwazo kwa uhuru wake anakiweka nyuma yake.

Yeyote anayefuatilia michezo ya runinga ataona kwamba wanatengeneza hadithi za mapenzi na ngono kama muongozo jumla, wakizipeana katika njia ambayo ni kinyume na uhalisia na kuwasilisha picha za uongo ambazo hupelekea katika kuunda ruwaza ya makosa kwa wale wanaotaka kuoana kwa maisha ya ndoa, ambapo mtizamo wa maisha ya ndoa ni wa kukamilika na uliojaa mapenzi bila kujali majukumu ya ndoa, na kwamba maisha yana uzito na mashaka. Mume katika filamu na vipindi hivi ni mtanashati, mtu wa kisasa, kijana na tajiri anayemletea zawadi mkewe ima ni au si siku adhwimu, na mke naye anaoneshwa kama mrembo, mwenye mvuto, asiyekuwa na shughuli bali kuhudhuria sherehe, vilabu na kusafiri na mumewe kama ambaye mwanamke huyu hana majukumu au kazi za kifamilia, na kama ambaye mume huyu hajui gharama yoyote, jukumu lolote na hana usimamizi wa watoto. Natija yake ni kuwa vijana hawa muda si mrefu wanakuja kugongana na uhalisia, majukumu na kazi zilizowekwa juu yao na kufungua mlango wa matatizo na mizozo ya ndoa ambayo hatima yake ni kuelekea katika talaka. Huu ni kwa mtizamo huu.

Kwa upande mwingine, wanaume na wanawake wadogo wanatafuta vigezo maalumu katika wale wanaotaka kuoa kwa mtizamo wa uwezo wa kimuonekano na kimada unaowasilishwa na sinema hizi. Huu ndio utangulizi wa kufeli kwa maisha ya ndoa kwa sababu kila mmoja anatizama muonekano bila kujali msingi, na kila mmoja anatafuta yule atakayeishi naye “hadithi ya mapenzi” kama alivyoona katika sinema, na sio kutafuta mtu kwa mujibu wa Dini na akhlaq, mtu ambaye utaishi naye kwa mapenzi, kuhurumiana na utulivu, kama alivyosimulia Allah (swt) ndani ya kitabu Chake katika Surat Ar-Rum, aya 21:

وَمِنْ آَيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآَيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿

“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa watu wanao fikiri”

Njia hii ya kufikiria haikufungwa tu kwa wale wanaotaka kufunga ndoa, bali hata kwa wale wanandoa. Wafuatiliaji wa michezo hii hususan wanawake huyapata maisha yao ni ya upweke na kushughulishwa na maisha yaliyowasilishwa katika michezo hiyo ambayo inapelekea katika mizozo na matatizo ya ndoa ndani ya majumba.

Hii ni sehemu tu ya fikra za sumu na chuki zinazopeperushwa na michezo ya runinga miongoni mwa watoto Waislamu, ambayo inalenga kufisidi Ummah kwa kupeana fahamu za Kimagharibi na kuzibadilisha fahamu za Kiislamu kuhusiana na mahusiano tofauti tofauti, mfano kati ya mahusiano ya wanaume na wanawake kwa kuzizungumzia mada ambazo zimetokana na Wamagharibi na watawala wao mfano mada kuhusu “ugaidi,” na kuwasilisha maisha ya Kimagharibi kama maisha ya kivyake ya kufuatwa. Wanaounda, kuziongoza na kuzipiga picha hizi sinema katika maeneo mazuri na yenye kuvutia mno na majengo yenye kuvutia na yaliyo ghali, mitindo na miziki yenye mvuto, pamoja na kuchezea hisia zote za uzuri wa mwanadamu ili kuweza kuathiri watazamaji, hususan watu wachanga.

Hivyo basi, lazima tuwe makini na vyombo vya habari na vinavyopeperusha, ima ni michezo au mengineyo, kwa makini na uangalifu ni lazima tusiwawache watoto wetu wakiume na wakike Waislamu watumike kama chombo katika mikono yao au chambo rahisi katika midomo yao. Hivyo basi, tunatoa mwito kwa wazazi kushirikiana katika kuzisimamia familia zao na kuwalinda kutokana na vyote vinavyo fisidi na kuwapa sum Allah (swt) asema ndani ya Surat At-Tahreem, aya 6,

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴿

“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.”

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bara’a Manasra

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:56

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu