Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mawasiliano ya Kieletroniki Yalivyo Vunja Majumba Yaliyokuwa Makini na Kuwatenganisha Watu!

(Imetafsiriwa)

Japokuwa mawasiliano ya kieletroniki ya habari yamefupisha masafa, yamekuwa njia fupi ya kupelekea talaka na mizozo ya ndoa. Na japo ilitumika kuwaunganisha wapendanao na wasiokuwepo baada ya kusubiri kwa muda mrefu, inawatenganisha wanachama wa familia na kuwasaidia kuwavunja kabisa, hakika ni jambo la utata mno!

Namna mitandao ya kieletroniki ya mawasiliano ilivyogeuka na kuwa laana baada ya kuwa baraka?!

Vyombo vya Habari vimebadilisha tabia na muundo wa matangamano baina ya watu, na chini ya mapinduzi ya kiteknolojia, watu wengi walianza kuugua upweke, kutengwa na jamii na msongo wa mawazo. Majumba zamani yaliyokuwa hai kwa gumzo la familia sasa yako kimya kama ambaye ni matupu hawamo, na ziara kwa ndugu na majirani siku adhwimu na likizo zimebadilishwa na jumbe na picha. Na kelele zilikuwa zikijaa ndani ya majumba ya mababu/nyanya kutokana na kujumuika kwa watoto na wajukuu, ile nishati, mizunguko na urafiki haupo tena. Kila mmoja anakuja akiwa amebeba kifaa chake na baada ya kujuliana hali, kila mmoja hujiweka kipembeni mwa nyumba, huku kiwiliwili chake chaishi na familia, lakini roho na akili yake haipo!

Kutokana na kusambaa kwa mitandao ya kijamii, majumba yamekuwa bila mipaka na stara imeondoshwa kutoka katika maisha ya watu na familia. Siri za majumba mengi zimekuwa wazi kwa kila mtu na kila hatua ya maisha yao ya siri yamepeperushwa, ikisababisha matatizo mengi ya kifamilia, mfano talaka na mizozo ya ndoa pamoja na wivu, kijicho na vita kati ya watu katika jamii.

Kwa mujibu wa utafiti na ripoti, mitandao ya kijamii hususani Facebook na WhatsAapp ndiyo vyanzo msingi vya kuwepo kwa viwango vya juu vya talaka. Hatuwezi kuweka takwimu zote hapa lakini wacha tutaje tu baadhi ya ushahidi unaoonesha ukubwa wa tatizo hili ili kuzinduana. Ndani ya Palestina, mahakama za Sharia zimesema kuwa nusu ya kesi za talaka zinatokea kabla sherehe ya ndoa, na wajuzi wanatoa sababu kadhaa kwa hili; kwamba ya juu zaidi ni mawasiliano ya kimitandao. Kwa mujibu wa takwimu zilizopeperushwa mnamo 2016, miaka mitatu iliyopita imeshuhudia kuzidi kwa idadi ya talaka ndani ya Jordan, inayozidi kila mwaka kwa zaidi ya kesi 1000 kutoka zile za mwaka wa awali, tukizingatia kuwa njia za mawasiliano ya kisasa, Facebook, WhatsApp, ndiyo sababu kuu za kuzidi kwa kesi za talaka. Tafiti zaashiria kuwa mitandao ya mawasiliano ilisababisha asilimia 50 za kesi za talaka UAE. Kitengo cha Muongozo wa Familia ndani ya UAE inakadiria kuwa mizozo ya ndoa ilizidi kwa zaidi ya kesi 5000 mnamo 2015 ambazo kuanzia asilimia 50 hadi 60 zinahusiana na mitandao ya kieletroniki na 1000 kati ya hizo ziliishia na talaka.

Takwimu na ushahidi huu wa kushtusha unaonesha namna hii mitandao na aplikesheni za simu za mkono zinavyosababisha mizozo ya ndoa kwa wale ambao wanairuhusu imiliki maisha yao; kwa upande mwingine kwa kumtenganisha mtu na familia yake na kumfanya asitekeleze majukumu yake juu yao hususani ikiwa mtu huyo ametekwa na matumizi yake na kuchukua muda mwingi nayo sawa na au kupitiliza muda mzazi anaotumia na watoto wake, au wanandoa wanaotumia ambayo ni ya kushtusha kwa hali nyanja zote mbili. Kutekwa huku kunawafanya wazazi kufeli katika utendaji wao wa kazi juu ya watoto wao katika elimu, kuwaongoza, kuwapa upendo na mapenzi yanayostahili na kuwasikiza wao na matatizo yao ambayo inapelekea kwa watoto kuchukua muelekeo hatari na kuwafanya waanze kuwa na tabia mbaya, kando na thaqafa iso madhubuti na fahamu za makosa ambazo watoto wanasoma kama natija ya kutumia muda wao mwingi katika mitandao hii na ilhali wazazi wao hawajui kuihusu.

Kwa wanandoa, kutekwa huku kunapelekea kutelekeza na mawasiliano mabaya kati ya wanandoa na kufeli kufanya kazi zao kuelekea upande mwingine, na wakati mwingine mmoja kati ya wanandoa hao hupata ndani ya vyombo hivyo vya habari kama sehemu ya kujificha ili asitumie wakati wake na mwenzie kwa sababu baadhi ya matatizo baina yao yanapanua pengo na kuzidisha mizani ya matatizo.

Kwa upande mwingine, mitandao hii na aplikesheni zake zimewezesha mawasiliano na kuzalisha mahusiano na kubadilishana kwa jumbe na picha kati ya wanaume na wanawake ambayo imepelekea –kukosekana kwa uchajiMungu na kumuogopa Allah (swt) –kumepelekea viwango vikubwa vya usaliti, ambayo ni moja ya sababu ya viwango vikubwa vya talaka kama ilivyodhibitishwa na rekodi za Mahakama ambazo ziko juu kutokana na kesi za talaka kwa sababu ya usaliti.

Urahisi huu wa mawasiliano umesababisha wanandoa wengi kupoteza uaminifu kati yao, ambacho ni moja kati ya misingi muhimu ya mahusiano mazuri ya ndoa, ikiwasababishia baadhi yao kuishi katika hali ya kushuku na kutoamini upande mwingine. Inaweza kumsukuma mmoja wa wanandoa kufuatilizia na kuchunguza yote yanayomfikia mwenzake kupitia mitandao hii na aplikesheni zake na kufuatilia wanaotuma.

Mazungumzo kuhusu suala hili ni marefu na yakusikitisha, lakini twamalizia kwa kusema kuwa mawasiliano ya kieletroniki yameunda urongo na kupanua pengo ndani ya mahusiano ya kifamilia kati ya dunia mbili: moja ambayo ni ya kweli, na nyingine ambayo si kweli, inayoathiri vibaya mahusiano ya kifamilia na kuzidisha pengo kati ya wanachama wa familia. Hivyo basi, jotojoto na ukaribu wa wanachama wa familia umekosekana licha ya kuwepo kiwiliwili, ambapo wanashikilia simu zao bila kujali wamekaa na nani; hivyo basi watu walisambaza misemo mfano: “Njia za mawasiliano zilisitisha mawasiliano.” Natija ni kuwa na sura mbili ambapo mahusiano ya kweli yamepungua na mahusiano ya tarakilishi yamezidi kwa hiyo urafiki na mahusiano yamepanuka kieletroniki lakini yamepungua mashinani na hisia za kinafiki na za uongo zimeibuka miongoni mwa wanachama wa familia moja, na hata miongoni mwa wanachama wa jamii jumla

Miongoni mwa natija zake ni kukosekana kwa utulivu katika majumba na kusitisha kwa mkataba ambao Allah (swt) ameelezea ndani ya Kitabu Chake wazi, Alisema:

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أفضى بَعْضُكُمْ إلى بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقاً غَلِيظاً﴿

“Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?” [An-Nisa: 21]

Ndugu na dada ni muhimu kuyafanya mawasiliano ya kieletroniki kama Baraka inayotuunganisha na kutuleta karibu, na sio laana inayo vunja majumba yaliyokuwa makini na kuwatenganisha watu wake.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bara’ah Manasrah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:57

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu