Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Qatar Inahamasisha Mashini yake Yenye Nguvu ya Vyombo vya Habari Kuwanyamazisha Wanaokashifu Matumizi Makubwa kwa Kombe la Dunia kwa Kudai Kupatiliza Faida ya Fursa hii Kulingania Uislamu
(Imetafsiriwa)

Mara tu habari za matumizi makubwa ya Qatari kwa maandalizi ya Kombe la Dunia kuenea, ambayo yalifikia dolari bilioni 220 (mara 19 ya kima ambacho Urusi ilitumia kwenye Kombe la Dunia lililopita mnamo 2018), makala mingi yalionekana kujaribu kuhalalisha matumizi haya na kuonyesha juhudi za Qatar za kuitumia hafla hii ya michezo na hitaji lake kubwa kueneza Hadith za Mtume (saw), kupaza sauti ya adhan ya swala na kumleta Mlinganizi Zakir Naik nk.

Bila shaka sisi hatupingi dhidi ya upatilizaji wa hafla yoyote kulingania kwa Mwenyezi Mungu. Tunaweza tu kuunga mkono juhudi zozote za kueneza Dini ya Mwenyezi Mungu, hasa ikiwa hii italinganishwa na yale yanayotokea katika nchi za Hijaz ya vita vya wazi dhidi ya Uislamu na kuenea kwa maovu na uchafu.

Hata hivyo, uamuzi wetu juu ya mambo lazima ujengwe juu ya viwango vilivyo wazi na vya kudumu, na mtu yeyote mwenye hekima hapaswi kufagiliwa mbali chini ya ushawishi wa uhalisia au ushawishi wa matamanio. Tunahukumu uhalali wa mambo sio kwa msingi wa uhalisia wake, au kwa msingi wa kuyalinganisha na yale ambayo ni mabaya zaidi kuliko hayo, au kwa kuzingatia mapenzi yetu kwa kandanda, au kwa kuzingatia kuvutiwa na mitindo inayong'aa.

Kwa bahati mbaya, uhalisia ulio mbali na Uislamu ulilazimishwa juu yetu, na kuenea kwa mazingira ya udhalilifu kulishusha upeo wa matarajio. Zaidi ya hayo, kukosekana kwa dhana sahihi ya jinsi maisha yanavyopaswa kuwa katika jamii ya Kiislamu kulitufanya tujivunie mambo ambayo hayatakiwi kujadiliwa hata kidogo, na ambayo yanapaswa kuchukuliwa kuwa ukweli.

Miongoni mwa mambo ambayo wanaojivunia mafanikio ya Qatari wanayakuza ni simulizi ya kupiga marufuku pombe na nembo za LGBTQ katika viwanja vya michezo na maeneo yake. Nashangaa jinsi jambo hili linavyokuzwa kuwa ni mafanikio makubwa, huku nikijua kwamba habari hiyo ina ushahidi wa kutoweza kwake?! Je, pombe na ushoga vimeharamishwa katika viwanja vya michezo na mazingira yake pekee, na kuruhusiwa nje yake?! Je, Uislamu uliharamisha maovu haya katika eneo fulani pekee?! Je, kuharamisha yaliyoharamishwa katika sehumu ndogo na kuruhusiwa kwake nje yake kumekuwa ni mafanikio yasiyo na kifani yanayostahiki kusifiwa na kutajwa?

Kuruhusu kuwepo kwa msikiti karibu na viwanja vya disko, wakati swala inaingia katikati ya ngoma, na kukubali kuwepo kwa mwanamke mwenye staha karibu na mwanamke mwenye tabarruj (mwenye kuonyesha mapambo yake kwa wasio mahrim); Haya yote hayazingatiwi kuwa ni ulinganizi kwa Uislamu, bali ni ulinganizi wa wazi wa usekula, na kuwaruhusu waovu kufanya uasherati na mtu wa dini kutekeleza ibada yake, kwa sharti kwamba dola ibaki inatawaliwa na sheri ya mwanadamu. Ama ulinganizi wa Uislamu, kama alivyotufundisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw) ni kuwasilisha muundo wa Kiislamu ulio safi na usio na doa kwa yale yaliyoharamishwa.

Kuwekwa kwa soka kama hafla ya kimataifa na kuipa sifa hii kubwa yenyewe ni njama dhidi ya Uislamu, hata kama pombe imepigwa marufuku kabisa na sio tu katika uwanja wa michezo na maeneo yake. Ina maana gani kwa watu kushughulishwa na mpira ambao wachezaji hupeana pasi uwanjani?! Ina maana gani kwa watu kujishughulisha na jambo lisilokuwa na maana kabisa, hata kama Qatar au nchi nyingine yoyote ya Kiarabu itashinda Kombe la Dunia lenyewe, na sio tu kuwa mratibu wake pekee? Je, italeta tofauti gani kwa maisha ya watu? Je, nchi zilizoandaa hafla hii zilipata faida gani? Je, nchi zilizoshinda Kombe la Dunia zilipata faida gani? Ina maana gani kwa Waislamu kujishughulisha na upuuzi huu wakati ambapo damu yao inamwagika, rasilimali zao zinaporwa, na matukufu yao yanakiukwa?

Vipi mtu mwenye akili timamu atahalalisha kujifurahisha katika wakati ambapo Mayahudi wananajisi sehemu takatifu zaidi za Waislamu na kuua wazuri wao?! Mtu mwenye akili timamu anawezaje kuhalalisha kujifurahisha na anasa wakati mamilioni ya Waislamu wanakosa kipande cha mkate au kipande cha bati la kuwakinga na joto la jua au mvua ya angani?! Vipi mtu mwenye akili timamu atahalalisha kujifurahisha huku jela za madhalimu zimejaa wanachuoni, watu wema na Mujahidina (wapiganaji)?! Vipaumbele vyenu viko wapi enyi Waislamu?! Munavipangaje?! Ni mahitaji gani yanakuja kwanza?! Munatanguliza vipi? Simaanishi starehe, bali starehe za anasa, juu ya vipaumbele vya juu?! Hii ni hekim na maono gani?

Kusema kwamba Qatar imeandaa hafla hii ili kulingania kwa Mwenyezi Mungu bila shaka kunagongana na uhalisia na ni ujinga. Qatar kamwe haijawahi kubeba hamu ya Uislamu, lakini tangu kuanzishwa kwake imekuwa koloni la Uingereza, na tangu miaka ya tisiini ya karne iliyopita imegeuka kuwa pango la njama za Uingereza, hasa baada ya kuzinduliwa kwa Al-Jazeera.

Kwa bahati mbaya, kumbukumbu za watu ni fupi sana, na akili zao zinatekwa haraka!

• Je, tumesahau kwamba Qatar ni mwenyeji wa kambi ya Kimarekani ya Al-Udeid inayotumiwa kuwashambulia Waislamu Iraq, Syria na Afghanistan?

• Je, tumesahau dori ovu iliyofanywa na Qatar, kwa utambuzi wa maafisa wake wakuu zaidi, katika kupenyeza makundi ya Syria na kuwapotosha kutokana na mkondo wa mapinduzi?

• Je, tumesahau dori ya Qatar, pamoja na utambuzi wa maafisa wake wakuu zaidi, kuishinikiza Hamas na kuisukuma kwenda sambamba na Mamlaka ya Palestina ya Abbas kwenye njia ya uhalalishaji mahusiano (na Mayahudi)?

• Je, tumesahau kwamba Al-Jazeera ilikuwa ya kwanza katika kuhalalisha mahusiano na vyombo vya habari na Mayahudi, na bado ingali inaendelea na njia hiyo hiyo leo, licha ya kuomboleza kwake juu ya Shireen Abu Akleh?

• Kwa nini haikutajwa kufunguliwa kwa nchi kwa ajili ya watalii wa Kiyahudi ambao watakuja Qatar kuhudhuria mechi kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka kwa umbile vamizi la Palestina? Ikiwa kweli lengo ni kulingania kwa Mwenyezi Mungu, basi Abd al-Rahman al-Sumait, Mlinganizi wa Kuwait, Mwenyezi Mungu amrehemu, ambaye ni mtu asiye na ulinzi, anakadiria idadi ya wale waliosilimu mikononi mwake barani Afrika pekee ni milioni saba, na hakutumia hata ushuri moja ya kile Qatar imetumia! Na hakujiwekea urembo huu wa kirongo.

Haya ni kuhusu da’wah ambayo hufanywa na watu binafsi. Ama kuhusu dola, alichotufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni kwamba njia ya dola ya Kiislamu kubeba da’wah ni kutabikisha hukmu za sharia ndani ya dola na kuibeba nje kupitia da’wah na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuzifungua nchi na kuutekeleza Uislamu kwa watu wake, ili wauone Uislamu kivitendo duniani. Hii itakuwa ndio sababu ya wao kuingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa Qatar haiwezi kubeba Uislamu kinje, hii ndio hali katika kuutekeleza nyumbani.

Leo, watu wanajivunia kwamba Qatar inazionyesha Hadith za Mtume hadharani na kupaza wito wa swala (adhan) kwa sauti nzuri, na wanayaona haya kuwa ni mafanikio makubwa kwa manufaa ya Uislamu! Vipi kama ingetabikisha Hadith hizi na hukmu nyenginezo za Shariah kivitendo; hali ingekuwaje?

Tatizo la Qatar ni kwamba siku Uingereza ilipoiasisi, iliifanya kuwa nchi ndogo sana katika eneo na idadi ndogo ya watu (kilomita za mraba 11570, watu 300,000, 10% ya jumla ya wakaazi wa imarati), ikilinganishwa na nchi jirani, kama eneo la Saudi Arabia ni mara 185, eneo la Iran ni mara 142, na eneo la Iraq mara 37. Inaonekana kwamba jambo hili lilizua mipagao miwili miongoni mwa watawala wa Qatar:

1- Mpagao wa kuendelea kubaki madarakani, kwani wanajua kuwa wao ni zao la ukoloni na hawana mvuto. Kuondoa kifiniko cha ukoloni kutoka kwao kunawafanya kushikilia madaraka kwa siku chache tu. Kwa hiyo, wanatafuta kila njia ya kuendeleza radhi ya Magharibi kwao, na wanajitolea kutumikia miradi ya kikoloni kwa kujitolea, labda wanajishindia kujadidishwa kwa mikataba yao ya kazi. Ni wazi kuwa pesa nyingi zilizotumika kuandaa Kombe la Dunia zilienda kwa kampuni za Kimagharibi na haswa Uingereza.

2- Mpagao wa hofu kwamba moja ya nchi zinazowazunguka itawameza. Wanajua kwamba udhaifu wa eneo la nchi hii, uwezo wake dhaifu wa kibinadamu, na umbile la jografia yake hufanya usalama wake kuwa tete, hata kama inalihami jeshi lake kwa vifaa vyenye nguvu zaidi. Wanakumbuka vizuri jinsi Iraq ilivyoivamia Kuwait, ambayo ni zaidi ya Qatar katika eneo na idadi ya watu kwa mara 1.5 kwa masaa tu, hivyo wanatumia kiasi kikubwa cha fedha ili kuwa na sifa duniani na kiti cha "heshima" chini ya jua, wakidhani kwamba sifa yao inaweza kuwa ulinzi kwao na kizuizi dhidi ya kushambuliwa.

Lakini hawajui kwamba hata watumie kiasi gani, hayatawapa:

• Kinga kutoka kwa mkoloni, na tuliona kwamba Magharibi haikuhamasisha mwanajeshi hata mmoja kuitetea Ukraine, ambayo inashirikiana nayo katika dini, kabila na historia; ilitosheka na kutuma silaha na kusema, “Nenda wewe na watu wako, mkapigane, sisi tumeketi hapa.”

• Kinga dhidi ya Dola ya Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, ambayo itafagia eneo hilo na kuviondoa viti hivi vilivyochakaa kwa kasi ya kupepesa jicho.

Mwishowe, nasema kwamba Waislamu hawakuumbwa kwa ajili ya starehe na kujifurahisha, hata kama inajuzu. Ndio, inajuzu kujipumzisha kwa aina fulani ya mchezo na furaha, lakini hilo sio lengo la asili, na sio kwa gharama ya mambo mazito, na halijumuishi yaliyoharamishwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Abdullah

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Afya Yetu ni Utajiri Wetu Vifo vya Wahamiaji »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu