- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Palestina baina ya Njia ya Sharia ya Mabadiliko na Masuluhisho ya Kivipande
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote njema ni za Mwenyezi Mungu aliye mteremshia mja wake Kitabu na wala hakukipinda, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyefikisha amana na akathibitisha hoja, na akatuacha baada yake juu ya dalili nyeupe. Uwongofu ulio bora kabisa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu haabudiwi kwa chochote isipokuwa kwa kile anachokitaka, wala hakurubiwi Kwake isipokuwa kwa Alichohalalisha.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake:
[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ]
“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Isra 17:1].
Palestina na Ash-Asham kwa jumla ni ardhi iliyobarikiwa kwa andiko la Qur’an Tukufu. Imetajwa ndani ya Qur'an na kuregelewa katika muktadha wa aya kadhaa, zikiwemo zile zinazoashiria baraka na utakatifu wake, na zengine zinazohusiana na hadithi za manabii watukufu kama vile Nabii Issa, amani iwe juu yake, au ilitajwa kuwa ni ardhi ya mkusanyiko, au kinachoashiria kuwa Waislamu watairithi, kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas, na ikatajwa katika tafsiri ya Al-Shawkani, Ibn Razi, na wengineo. Na Qur’an inapoifanya ardhi kuwa yenye baraka na kuwarithisha Waislamu, basi ni kadhia ya umma wa Qur’an, na wala haijuzu kulizungumzia bila ya muktadha huo. Hatuzungumzii suala la Palestina kwa sababu ni ardhi ya Waarabu, au tunabishana juu yake kwa kujinasibisha na Wakanaani, kwa mfano. Haijuzu kuitetea kwa sababu ni ardhi ya Waarabu, kwani hii ni mantiki potofu inayogongana na asili ya itikadi ambayo ni ya wanadamu wote, na inalinganisha sawa kati ya Mwarabu, Mturuki na Afghan wanapokutana chini ya bendera ya Mungu mmoja.
Mtazamaji wa mapendekezo yanayohusiana na ardhi iliyobarikiwa ya Palestina huona ndani yake upotoshaji mkubwa wa vijana, na majaribio ya nguvu ya kuwapotosha vijana wanyofu wenye shauku ya jihad na ukombozi kutoka kwa dira sahihi ambayo kwa hakika inaongoza kwenye ukombozi wa nchi hii. Na ikiwa tutafumbia macho uratibu wa usalama kati ya Mamlaka ya Palestina na umbile nyakuzi la Kiyahudi, na uhalalishaji mahusiano unaofanywa na tawala za uharibifu katika nchi za Kiislamu, kwa siri na dhahiri, kuna juhudi kubwa na hatua zinazofanywa kwa bahati mbaya na wale walioichukua kadhia hiyo kuwa yao wenyewe. Haicheleweshi ushindi, bali inakiuka Sharia na inazuia mradi halisi wa ukombozi na inaongeza juhudi za madhalimu katika vita vyao dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa.
Vyombo vya habari vinavyolisha fikra za wazalendo na wataifa vinapigia debe uzalendo na kupuliza tarumbeta hii usiku na mchana vinabeba mzigo wa kila kijana aliyetoka na ari yake kwa ajili ya nchi hii na kusahau kuwa ardhi hii ni imani isiyo na mipaka iliyochorwa na ukoloni.
Wanasiasa wanaoonya juu ya vita vya kidini chini ya kisingizio cha hofu kwa watu na mustakabali wao kwa kweli wanatumikia uvamizi huo, ambao umekuwa ukifanya kazi kwa miaka mingi kubadilisha mzozo huo kutoka kuwa ni mzozo wa kiitikadi hadi mzozo wa "Israel na Palestina", kuhakikisha uzimuaji wa mamilioni ya majeshi na raia Waislamu wanaotamani kusujudu karibu na Msikiti wa Al-Aqsa.
Na wanaharakati waliostahamili dhulma ya kukaliwa kwa mabavu na mateso ya madhalimu, na kulingania jina la Palestina duniani, na masaa marefu yanahesabiwa kwao katika mapambano yao kwa ajili ya Palestina, iwe kwenye mtandao au wanaposafiri ng’ambo na kuzungumza katika semina, mikutano ya waandishi wa habari na matangazo ya redio kuhusu Palestina, lakini kwa bahati mbaya wamebeba ndani yao Palestina iliyochakachuliwa na kudogoshwa. Palestina kwa kiwango cha wale walioikalia kimabavu kwa mara ya kwanza na kuiondoa kwenye ramani ya dola ya Khilafah, Sykes-Picot Palestina, ikiwa na mipaka iliyovunjwa vunjwa kutoka kwa upanuzi wake wa asili, Ash-Sham na kukumbatia kwake asili ya Umma wa Kiislamu, kwa hiyo wakabeba mtazamo wa kupotoka na finyo wa Palestina. Kwa bahati mbaya, masuluhisho na nadharia zao pia zilipotoshwa na hazikuibuka ili kukabiliana na ukubwa wa suala hili na ukubwa wa suluhisho msingi ambalo, kwa hakika, ndilo suluhisho pekee linalomkinaisha Muislamu yeyote anayeregea kwenye imani yake, ukombozi wa kina wa ardhi yote ya Palestina, na kuirudisha kwa ummah kama sehemu ya Ash-Sham na dola ya Kiislamu.
Kwa wote hao: Mwenyezi Mungu Mtukufu huabudiwa atakavyo Yeye, na Uislamu ni fikra na njia ya lazima kwa hilo, na Mwenyezi Mungu amesema:
[فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ]
“Basi, simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa” [Hud 11:112], si kama munavyopenda. Yeyote anayetaka kuikomboa Palestina kwa kuwa ni Palestina, vipi mutashughulika na Chechnya, Burma, au Kashmir, je hizi si nchi za Kiislamu zilizokombolewa kwa kumwaga damu?! Ardhi hii ni ya Mwenyezi Mungu, na kukombolewa kwake ni wajibu ili sheria ya Mwenyezi Mungu isimamishwe ndani yake. Hakuna njia bila ya Dini ya Mwenyezi Mungu kutimiza kadhia hii na kadhia nyengine za Waislamu.
Kila pendekezo lisilokuwa la ukombozi wa nchi nzima ni kuutukuza ukaliaji kimabavu, na kila mwito unaoelekezwa kwa asiyekuwa Ummah kwa majeshi yake yote na taswira yake ni wito uliofichwa kwa kujua au kwa ujinga wa mmiliki wake. Hatuna maregeo yoyote isipokuwa Qur’an ya Mola wetu Mlezi, Utukufu ni Wake Yeye, na Sunnah za Mtume wetu (saw) na hatuna ushindi wowote isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, sio kutoka kwa Umoja wa Mataifa, wala kutoka kwa Jumuiya ya Dola za Kiarabu, wala kutoka Amerika, wala Urusi, wala China. Bali, ni kwa ajili ya Ummah peke yake pamoja na wanachuoni wake, wanasiasa, na maafisa waaminifu, makamanda katika majeshi, wanaharakati, na washawishi kutoka katika koo na wengineo. Kwao peke yao tunawageukia na kuwashikilia kwenye jukumu walilopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu; kufanya kazi kwa nguvu zao zote kuiokoa Masrah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa Mayahudi.
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَى قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.” [Al-Anfal 8:72]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bayan Jamal
Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:
#Time4Khilafah |
#EstablishKhilafah |
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#KhilafahBringsRealChange |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
أقيموا_الخلافة# |
كيف_تقام_الخلافة# |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |