Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ]

 “...ipate kushinda dini zote.”
(Imetafsiriwa)

Katika hotuba ya Jaafar bin Abi Talib, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, aliyoitoa mikononi mwa Najash: "كنّا قوما أهل جاهليّة نعبد الأصنام، ونأكل الميتة، ونأتي الفواحش، ونقطع الأرحام، ونسيء الجوار، يأكل القويّ منّا الضّعيف..."  “Sisi tulikuwa ni watu wa jahiliya tukiabudu masanamu, tukila mfu, tukifanya uasherati, tukikata kizazi, tukiwatendea uovu majirani, na mwenye nguvu akimdhulumu mnyonge...” Hayo ndiyo maadili ya ujinga ambayo watu waliishi nayo kabla ya Mwenyezi Mungu kumtuma Mtume wake (saw) kwa uongofu wa kuwatoa katika magiza hayo na kuwaondolea dhulma waliyoteseka kwa moto wake. Aliwalingania kwenye nuru ya Uislamu na hukmu zake adilifu ambazo Muumba wao aliwawekea sheria. Aliwalingania kwa لا إِلَهَ إِلا اللَّه  “hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu.”

Ujumbe wake (saw) ulikuwa ni ujumbe mpana na wa kukataza, ambao kwao Mwenyezi Mungu alitaka kubadilisha fahamu zote potovu za kimaadili, kijamii na kisiasa zilizotawala katika sehemu zote za dunia. Ujumbe ambao ulijumuisha hukmu zote zinazoshughulikia matatizo ya watu na kuyapatia masuluhisho yenye ufanisi, yenye uponyaji ambayo si ya uwongo wala yenye upungufu, kwani yanatoka kwa Mjuzi wa yote. Mtume (saw) hakuishia kwenye kubadilisha watu binafsi pekee, bali alitaka kuhujumu mifumo na maadili ndani ya jamii na kuweka mifumo inayochipuza kutokana na imani ya Kiislamu. Uislamu ulikuja na ujumbe mpana ambao haukufungika kwenye jamii, tabaka, zama, au mahali. Ni ujumbe kwa watu wote

[تَبَارَكَ الَّذِي نزلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيراً]

“Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.” [Al-Furqan 25:1].

Mwenyezi Mungu alimtukuza Mtume wake kwa kuufanya ujumbe wake kuwa ndio mwisho wa ujumbe wote, hivyo hakuwa mtume kwa kundi au watu fulani, bali alikuwa ni mtume kwa watu wote. Ujumbe wake haukufungika kwa wanyonge wa Makka, wala kwa familia yake huko, wala kwa wale walio jirani yake bali ulielekezwa kwa matabaka na makundi mbalimbali ya jamii na kwa wanadamu kwa jumla. Yeye (saw) akawalingania katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mmoja wa pekee, kufuata hukmu zake, na kuepuka kumshirikisha, na kuwaregelea wengine kwa hukmu.

Uislamu uliihamisha jamii ya kabla ya Uislamu kutoka katika ibada ya wanadamu kwa wanadamu hadi ibada kwa Mola wa wanadamu, kutoka katika kuishi chini ya hukmu zilizolazimishwa na wenye nguvu kwa wanyonge hadi kuishi chini ya hukmu adilifu zilizowekwa na Mola wa walimwengu wote. Ni ujumbe tofauti na wa kipekee wa kukataza ambao hakuna ujumbe au dini nyingine inayoshirikiana nao katika kuweka sheria halali zinazoongoza maisha ya binadamu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifanya kazi ya kueneza rehma hii katika mashariki na magharibi ya dunia, hivyo akatafuta usaidizi kutoka kwa makabila ili ulinganizi wake unusuriwe na kulindwa na mtu. Haya ndiyo Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi, na tabiina, waliyoyafahamu, kwa kuwa walifahamu makusudio ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu wa waja wake.

[وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونَ]

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” [Adh-Dhariyat 51:56]. Na utukufu wa dini hii na utofauti wake katika kutatua matatizo ya watu ukawa dhahiri kwao, na uwezo wake wa kufanya hivyo bila ya sheria nyengine zozote zilizowekwa na mwanadamu, na vipi mtu huyu ataweza kufanya hivyo na hali yeye ni kiumbe dhaifu na masikini?!

Uislamu ulikuja na kufanya mabadiliko makubwa ambayo kwayo uling'oa maadili yote ambayo jamii ya kabla ya Uislamu iliegemezwa juu yake na badala yake ukaweka maadili kutoka kwa Mwenye nguvu, Mwenye hekima, yaliyoteremshwa na hukmu za Shari'a ambazo Mwenyezi Mungu aliziteremsha ili waja washikamane nazo na wasijiepushe nazo, na ili wasipotee njia, na hivyo wakaiacha njia aliyo wateremshia. Yeye (saw) alifikisha ujumbe wake na akatimiza amana yake na akaukabidhi kwa ummah wake ili uwe kiongozi wa umma zote wenye kuwaongoza kufuata njia ya haki na ili pasiwepo wa kuabudiwa katika ulimwengu huu isipokuwa Mwenyezi Mungu na kusiwe na kanuni na sheria nyingine isipokuwa hukmu na sheria zake zitawale.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliuacha Ummah wake kuwa ndio umma bora zaidi mikononi mwake, ukiiongoza dunia na kuitawala, lakini maadui wa Uislamu waliuhadaa usiku na mchana na wakafanya kazi ya kuudhoofisha na kuuhujumu. Msiba mkubwa uliupata Umma, na ukaipindua dola yake, ambayo iliegemezwa katika kutabikisha, kuhifadhi na kueneza hukmu za Uislamu, kwani ndiyo amana ambayo Mtume wake alikuwa ameikabidhi kwake. Makafiri walichukua udhibiti wa umma wa Uislamu na kueneza fahamu potovu ndani yake ambazo zilidhoofisha ufahamu wake wa dini yake na wakaweka juu yake fahamu za ukafiri ambazo zilitenganisha dini yake na maisha yake, hivyo ukawa chini ya sheria zilizotungwa na mwanadamu ambazo ziliukengeusha kutoka katika kushikamana na hukmu za sheria yake, na ukarudi kwenye ujinga na ukakabidhi usimamizi wa mambo yake na uhai wake kwa mwengine asiyekuwa Mola wake.

Umma wa Kiislamu na wanadamu kwa jumla wakaregea kuishi katika Jahiliyya. Ibn Kathir anasema katika tafsiri yake: “Na akasema:

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوْقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah 5:50]. Mwenyezi Mungu Mtukufu anawashutumu wale wanaokengeuka kutoka katika hukmu madhubuti ya Mwenyezi Mungu inayojumuisha kheri yote, inayokataza maovu yote, na ni adilifu kuliko rai, matamanio na maazimio mengine, ambayo wanadamu wameyaweka bila ya msingi katika sheria ya Mwenyezi Mungu, kama walivyokuwa wakihukumu kwayo watu wa Jahiliyya kutokana na upotofu na ujinga, ambao wanaliuweka katika maoni na matamanio yao.

Jahiliyyah sio kipindi cha wakati kilichotangulia Uislamu, bali ni kuishi chini ya hukmu zisizokuwa hukmu za Muumba. Na Ummah hivi leo unaishi katika ujinga, unaishi chini ya hukmu yalizotungwa na mwanadamu zinazolamishwa juu yake na maadui zake. Sasa unaishi chini ya sheria zinazofanya kazi ya kuhifadhi maslahi ya mabepari wasiosita kuua maelfu ya watu wasio na hatia na hawajali kuhusu malalamiko ya wanyonge au maombi ya watoto na wanawake. Sio siri kwa mtu yeyote kile ambacho Umma wa Uislamu unateseka hasa na wanadamu kwa jumla kwa kuzingatia mifumo iliyobuniwa na mwanadamu ambayo imetawala na bado inaendelea kutawala. Na hizi hapa barakoa za tawala hizi zikianguka, moja baada ya nyingine, ili kufichua nyuso mbaya ambazo zimejificha kwa muda mrefu nyuma ya kauli mbiu zao za uwongo na madai ya uwongo, na mazimwi ya kibinadamu yanayotawala dunia na yanayowatesa na kuwadhulumu watu na hata kufurahi yamejitokeza wazi wazi.

Umma wa Kiislamu umekumbana na misukosuko mingi tangu ulipoacha amana yake, uhalisia wake ukageuka kuwa mchungu baada ya kuongoza na kutawala mataifa, ukawa mkia wake; watoto wake wananyanyaswa, matukufu yake yanakiukwa, na mali yake kuporwa! Uhalisia ambao haufichiki kwa Mjuzi, Mwenye khabari

[وَإِذَا قَضَى أَمْراً فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ]

“na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa!” [Al-Baqarah 2:117]. Yeye ndiye Muweza wa yote na ana yote. Anatazama uhalisia huu ambamo ufisadi umeenea na madhambi ni mengi, na Yeye ni mvumilivu na haifanyi ardhi kuwameza madhalimu, na wala Hatumi upepo mkali juu yao, wala mafuriko, wala ukelele, na haleti watu wengine.

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawbah 9:33]. Mwenyezi Mungu atafichua kikamilifu, yaani “…ataifanya ishinde juu ya dini zote.” Na imethubutu katika hadith Sahih kutoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwamba amesema: «إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِيَ الْأَرْضَ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا، وَسَيَبْلُغُ مُلْكُ أُمَّتِي مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا» “Mwenyezi Mungu alinikunjulia mimi ardhi mashariki yake na magharibi yake. Bila shaka utawala wa umma wangu utafika katika sehemu zote nilizokunjuliwa ndani yake.” Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu, na hakubali dini nyengine, na hukmu zake ndizo hukmu pekee zenye uwezo wa kuongoza maisha haya.

Hivi ndivyo anavyotaka Mwenyezi Mungu; Uislamu uwe wa kitofauti, wa kipekee na utawale, Ummah wote wa Uislamu na wanadamu wote lazima wajue kwamba ndiyo dini pekee ambayo kwa wanadamu muongofu na wenye mafanikio, na kwamba ndio pekee yenye uwezo wa kutatua matatizo yake, na kwamba hukmu na sheria zote zinazotungwa na wanadamu si chochote ila ni masuluhisho ya kutatanisha na yenye mapungufu ambayo karibuni zitapitwa na wakati na kutokuwa na uwezo.

Mwenyezi Mungu amemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, na Uislamu uwe ndio uongozi pekee unaoweza kurekebisha yale yaliyoharibiwa na mifumo ya kabla ya Uislamu ambayo ilimfanya Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika wa kutunga sheria na kuelekeza, na kuwafanya wanadamu kuwa ndio wenye kutunga hukmu na sheria badala ya hukmu za Muumba wa wanadamu. Mwenyezi Mungu aliutuma Uislamu kuwa Dini ya Mwenyezi Mungu anayoikubali kwa waja wake ili waishi maisha mazuri bila ya kuzingatia sheria nyengine.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[الم * أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ * وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ]

“Alif, Lam, Meem * Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? * Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.” [Al-‘Ankabut 29:1-3]. Mwenyezi Mungu aliweka Sunnah yake kuwachunguza waja wake walioamini na kuwapambanua wakweli. Mtihani ambao ndani yake ataupima uchamungu wao na subira yao katika kumwabudu Yeye na ikhlasi yao katika kuinusuru Dini yake na kunyanyua bendera yake.

[أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْاْ مِن قَبْلِكُم مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُواْ حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللهِ قَرِيبٌ]

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” [Al-Baqara 2:214]. Mitihani na misukosuko aliyopitia Mtume wetu (saw) na maswahaba zake, ili kuifikisha dini hii na kuieneza. Walijitolea muhanga nafsi zao na mali zao na hawakuwa bakhili na chochote ili kuinua neno la Dini hii; yeye (saw) alitoa muhanga mkubwa ili Dini hii ifike mashariki na magharibi mwa ardhi. Hakusitishwa na maonyo au vishawishi, na alistahamili majaribu yote ili kufikia amana hii. Abu Talib alikwenda kwa Abu Jahl na kaumu yake na akawahutubia, akisema: Muhammad ni mtukufu kiasi gani wakati ulimwengu umewekwa mbele yake, lakini anakataa na kusema:«يَا عَمُّ، وَاَللَّهِ لَوْ وَضَعُوا الشَّمْسَ فِي يَمِينِي، وَالْقَمَرَ فِي يَسَارِي عَلَى أَنْ أَتْرُكَ هَذَا الْأَمْرَ حَتَّى يُظْهِرَهُ اللَّهُ، أَوْ أَهْلِكَ فِيهِ، مَا تَرَكْتُهُ»Ewe Ami yangu, Wallahi, lau wangeliweka jua katika mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto, ili niache jambo hili mpaka Mwenyezi Mungu atakapolidhihirisha, au nife ndani yake, kamwe siwezi kuliacha.” Hii ndiyo njia ya kila Muislamu, na ni lazima aifuate mpaka Mwenyezi Mungu aufanye Uislamu ushinde dini zote au afe bila ya hilo. Na ni muhanga mkubwa iliyoje huu: ni ushuhuda wa kuiregesha dini hii tukufu katika maisha ya watu ili waishi kwa kuzingatia hukmu zake za adilifu.

Kuishi katika maisha haya aliyoyaumba Mwenyezi Mungu hakuwezi kuwa sawa isipokuwa kuongozwe na maamrisho ya Muumba wake, na maadamu amri hizi ziko mbali na kutenganishwa na maisha haya, mwanadamu ataregea kwenye mzunguko wa giza na ujinga, na kuishi katika dhiki, ambayo hakuna kitakachomnusuru isipokuwa kurudi kwa Uislamu na hukmu zake na utabikishaji wake chini ya kivuli cha dola inayouhifadhi na kuueneza kuwa ni rehma na mwongozo kwa walimwengu.

Ewe Mwenyezi Mungu, tutumie wala usitubadilishe, na utujaalie tuwe miongoni mwa wenye kushuhudia ushindi wako uliouahidi na kuwatia nguvu waja Wako waaminifu mpaka Uislamu uregee kuwa ni uwongofu na rehma inayozunguka maisha ya wanadamu na kuangaza njia yao.

Imeandikwa kwa Ajili Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeina As-Samit

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu