Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Magharibi Haiwezi Tena Kuficha Kufeli Kwake Wazi Katika Kuwalinda Wanawake

(Imetafsiriwa)

Mnamo Mei 7, 2023, msichana wa miaka 15 nchini Amerika alipatikana amekufa kwenye jaa baada ya kutoweka kwa siku tatu. Ingawa mauaji ya vijana si jambo geni nchini Amerika, kisa hiki kilinigusa kwa njia tofauti. Miundo mbalimbali ambayo inakusudiwa kumlinda Gracie na wasichana wengine kama yeye ilifeli; kuangazia matatizo yaliyopo katika kila ngazi katika jamii huria ya kisekula. (Chanzo)

Pindi habari zilipozuka kwamba msichana mdogo amepotea katika mji mdogo, bila shaka zilianzisha shughuli nyingi kwenye mitandao ya kijamii na katika jamii huku polisi, marafiki, familia na wanajamii wakianza kumtafuta. Haikuchukua muda mrefu kabla ya muda wa kutoweka kwake kujulikana na maswali mengi yalikuja akilini, “Msichana wa miaka 15 anapoteaje kwa siku 2 kabla ya familia yake kuwasiliana na watekelezaji wa sheria?”; “Wazazi wake walimruhusuje kwenda nyumbani kwa mwanamume wa miaka 29?”; “Kwanza kwa nini mhukumiwa wa uhalifu wa ngono, ambaye uhalifu wake ulikuwa unyanyasaji wa kingono kwa mtoto mdogo, kumiliki na kutengeneza ponografia ya watoto barabarani?” Ndipo maelezo yakaanza kujitokeza na kila tabaka likaangaza mwanga mkali wa jinsi tulivyo katika mazingira hatari katika jamii ambayo haifanyi kuchunga mambo ya raia wake kuwa jambo kuu. Nambari ya moja, msichana huyu alitoka katika nyumba iliyovunjika. Hakuwa na baba yake kumtunza na mama yake hakuwa makini, kama inavyo dhihirika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, “Nilichohitaji kufanya ni ku Google jina lake. Ingenichukua sekunde mbili. Sikufikiria kufanya hivyo. Inaniuma kwamba nilichohitaji kufanya ni ku Google jina lake na ningemwona yeye ni nani.” Kwa hiyo, alijua kwamba binti yake alikuwa na mtu huyu, ambaye hata hakumjua!

Tabaka zinazopaswa kuwepo ili kuwalinda watoto na wanawake katika jamii hazipo katika jamii ambapo wanadamu wanafanywa kuwa wa juu katika hukumu. Kwanza, kitengo cha familia kimevunjika. Kina baba mara nyingi hawapo pichani, wakiwaacha wanawake kulea watoto wao wenyewe, na kuishi na fedha zisizotosheleza mahitaji ya kila siku. Nyumba za mzazi asiye na mwenza pia huwaacha watoto wakiwa katika hatari ya kuathiriwa na uhusiano wa wazazi wao na wenza ambao hauhusiani nao, na pia, kuishi katika mazingira ambayo husukuma pombe, dawa za kulevya, na uasherati kuanzia kwa umri mdogo kupitia njia za burudani na mitandao ya kijamii. Hakuna uwajibikaji kutoka kwa wazazi kwa watoto wao.

Kisha, tuna kufeli kwa mfumo wa mahakama katika kumlinda Gracie. Badala ya kutunga sheria kwa ajili ya ulinzi wa raia wake, sheria zinatungwa kwa matakwa na matamanio ya mwanadamu. Kwa miaka mingi, Timothy Doll alikuwa tishio kwa wasichana wachanga katika jamii na alipokea tu kofi kwenye mkono kutoka kwa mfumo wa mahakama kwa kifungo cha nje, na kumruhusu kurudi kwenye njia yake ya kuwanyanyasa wasichana bila uoga, au kujali!

Hatimaye, kufeli kwa jamii kwa jumla. Kuanzia kwa familia kubwa, majirani, wanajamii, walimu, hakuna mtu aliyekuwepo kumtunza Gracie. Ili kuhakikisha kwamba alikuwa salama na si katika mikono ya hatari. Hiyo ni kwa sababu ubinafsi ndio nembo kuu ya jamii ya kisekula. Hakuna uwajibikaji kuwatunza na kuwalinda wengine chini ya mfumo huria, wa kibepari. Thamani pekee aliyonayo mtu ni uhuru wa kufanya chochote anachotaka!

Kinaya katika hadithi hii ya kusikitisha ni kwamba mambo yale yale ambayo Wamagharibi wanawashambulia Waislamu na shariah ya Kiislamu kwayo ndiyo mambo ambayo yangemlinda Gracie na wasichana wengine na wanawake kama yeye. Kazi ya Khalifa ni kuhakikisha kwamba mambo ya raia wa Dola yanachungwa. Anapaswa kuhakikisha kwa amri ya Muumba na kupitia zana za mfumo wa kiuchumi kwamba raia wote wana chakula, mavazi, na paa juu ya vichwa vyao. Uovu, kama vile pombe, dawa za kulevya, uchi, mchanganyiko huru wa wake na waume, n.k. ni marufuku kabisa katika jamii. Hili linalinda maumbile yasiyo na hatia ya watoto wadogo, linaweka raia wa dola salama dhidi ya kuanguka katika msururu wa uraibu na uhalifu, na kukuza mahusiano mzuri kati ya mume na mke.

Uislamu ndio Dini pekee iliyobainisha waziwazi dori na majukumu ya baba na mama, ili kila mmoja atimize wajibu wake na washirikiane kuwalea watoto wao kwa mapenzi, huruma na ucha Mungu (swt). Hivyo basi, ni muhimu mno kwa dola kupandikiza fahamu hizi kwa raia wake.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍۢ وَبِمَآ أَنفَقُوا۟ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ]

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa.” [Surah An-Nisa:34].

Mtume Muhammed (saw) amesema,

« كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ »

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na ataulizwa juu ya raia wake. Kiongozi aliye juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake. Mwanaume ni mchungaji wa familia yake na ataulizwa juu yao. Mwanamke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe na watoto wake na ataulizwa juu yao.” (Bukhārī 6719, Muslim 1829)

Fahamu ya Kiislamu ya qawaamah (usimamizi wa mwanamume juu ya mwanamke) ni fahamu moja ambayo inawafanya Wamagharibi kuchoshwa zaidi na chuki yao mbaya dhidi ya Uislamu. Ingawa wanapindisha maana yake kusukuma ajenda ya ufeministi ya, “hatuhitaji wanaume”, ni wazi mthili ya mchana kwamba kuwa na baba (au Mahram) katika dori ya ulezi kutakuwa ni kinga kwake dhidi ya kuwa windo la wanaume wasio na maadili, umaskini, mfadhaiko, na wasiwasi.

Mujtamaa wa Kiislamu nao pia ni ule ambao umejengwa juu ya udugu na udada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Kutoka kwa Abu Hamza Anas bin Malik (r) - Mtume (saw) amesema:

«لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لأَخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ» “Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye yale anayojipendelea nafsi yake.” (Bukhari na Muslim). Na Mtume (saw) amesema:

«مَنْ رَأَى مُنْكَرًا فَاسْتَطَاعَ أَنْ يُغَيِّرَهُ بِيَدِهِ فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ. فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ. فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ بِلِسَانِهِ، فَبِقَلْبِهِ. وَذَلِكَ أَضْعَفُ الإِيمَانِ»

“Atakayeona miongoni mwenu uovu, basi na aubadilishe kwa mkono wake (kwa kuchukua hatua); na ikiwa hawezi, basi kwa ulimi wake (kwa kutamka); na ikiwa hawezi, basi kwa moyo wake (kwa kuhisi kuwa ni makosa) - na huo ndio udhaifu wa imani.” (Imepokewa na Muslim, 49)

Fahamu hii inarekebisha mawazo ya mtu binafsi na badala yake inayabadilisha kwa hisia ya uwajibikaji kwa wale wanaoishi pambizoni mwako; karibu na mbali. Kwa hiyo, ikiwa mtu atamwona mwingine anafanya dhambi, au katika ukingo wa kufanya hivyo, watawazuia kama ilivyoelekezwa katika Hadith hapo juu. Katika hali ya uhalifu unaofanywa, mfumo wa mahakama una adhabu za wazi na kali kwa kila aina ya ufisadi kiasi kwamba raia wanahisi ni jambo lisilofikirika kabisa kujihusisha na tabia ya aina hii.

[إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَنْ يُقَتَّلُوا]

“Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.” [Al-Maidah: 33].

Kwa maana nyengine, katika jamii inayotawaliwa na Shariah, mwanamume hawezi kamwe kujisikia raha kumtumia mwanamke kwa sababu anajua atawajibishwa na jamii na mfumo wa mahakama, ambao hauchukulii usalama wa mwanamke kiwepesi.

Kwa hakika ni wazi kwamba usalama na ulinzi kwa wanawake utatokea tu baada ya kusimamishwa tena Khilafah na kushikamana na Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni wazi pia kwamba kama Waislamu tunaoishi nchi za Magharibi, tuna wajibu wa kuwasilisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kama suluhisho pekee la kuwalinda watoto wetu kutokana na jinai hizo mbaya na za kikatili na jinai nyingine zote dhidi ya wanadamu ambazo zinawakumba Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa usawa.

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ ۗ وَلَوْ ءَامَنَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ لَكَانَ خَيْرًۭا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” [Aal-i Imran:110].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu