Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sa’ad bin Muadh, Mkuu wa Ansar (ra)…

Ni nani Sa’ad wa Ummah Huu hivi leo?!

(Imetafsiriwa)

Kuwataja watu wakubwa wa historia ya Uislamu, sio kama kutaja habari za kale zozote za “mashujaa” wa kihistoria. Tafauti baina ya historia ya Waislamu watukufu na “mashujaa” wa historia ni kuwa usomaji wa habari za Waislamu watukufu ni kwa sababu ya kufuata mifano yao. Tunafuata nyayo zao, na kuchukua mafunzo kutoka kwenye matendo yao ya kishujaa. Kumbuka kuwa hawakufanya hayo matendo ya kishujaa kwa sababu walikuwa “hekaya za zamani.” Bali walifanya hayo kwa sababu walifahamu Uislamu kuwa ni aqida na hukmu za Shariah. Walitekeleza hukmu hizi kwa ukamilifu, na hivyo walijitafautisha. Walikuwa miongoni mwa wenye ushupavu na ambao nususi za wahyi ziliwatukuza. Miongoni mwa mashujaa hao ni swahaba mtukufu, Sa’ad bin Muadh, mkuu wa Ansar (ra).

Yeye (ra) ni miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajir na Ansar, na waliowafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” [Surah At-Tauba 9:100]

Swahaba huyu mtukufu (ra) anastahiki heshima hii na hadhi hiyo, kwa tendo lililo bora. Ilikuwa ni tendo kubwa la kijasiri ambalo viongozi wa Kikureshi, Waarabu na viongozi wengine walikataa kufanya. Ni tendo kuu la Nusrah kwa Uislamu na Mtume wake (saw). Kwa hivi, watu wenye nguvu hivi leo lazima watambue kuwa dola ya Kiislamu ilisimamishwa mara baada ya Sa’ad kutoa Nusrah kwa Muhammad (saw). Lazima wafahamu kuwa hadhi ya yule anayesimamisha Uislamu hivi leo atakuwa kama yule aliyetoa Nusrah kwa Mtume (saw).

Cheo chake insha Allah, ni kama cheo cha Sa’ad bin Muadh (ra), ambapo kuhusiana naye Mtume (saw) amesema,

«اهْتَزَّ العَرْشُ لِمَوْتِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ» “Arshi ilitetemeka kwa mauti ya Sa’ad bin Muadh.” [al-Bukhari and Muslim]. Adh-Dhahabi (rh) amesema, هذا متواتر أشهد بأن رسول الله صلى الله عليه وسلم قاله “Hii ni mutawaatir. Nashuhudia kuwa Mtume (saw) ni hakika amesema hilo.” [al-‘Uluw li’l-‘Aliy al-Ghaffaar]. Adh-Dhahabi ameielezea hii kwa urefu katika kitabu chake al-Fawaa’id, kutoka kwa Abu Sa‘iid al-Khudri (ra) ambaye amesema, “Mtume (saw) amesema,

«اهْتَزَّ الْعَرْشُ لِمَوْتِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ ، مِنْ فَرَحِ الرَّبِّ عَزَّ وَجَلَّ» “Arshi ilitetemeka kwa mauti ya Sa‘ad ibn Mu‘adh, kwa sababu ya furaha ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.” Katika as-Sunnah ya ‘Abdullah ibn al-Imam Ahmad, imesemwa, عَنِ الْحَسَنِ قَالَ لَقَدِ اهْتَزَّ عَرْشُ الرَّحْمَنِ جَلَّ وَعَزَّ بِجِنَازَةِ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ فَفَسَّرَهُ الْحَسَنُ فَرَحًا بروحهُ “Imepokewa kwamba al-Hasan amesema, imetikisika Arshi ya Ar-Rahman Aliyetukuka kwa maziko ya Sa’ad ibn Muadh (ra). Al-Hassan amefasiri kuwa ni furaha kwa roho yake.”

Inampasa kila kamanda wa Kiislamu kusoma kuhusu Sa’ad (ra) na kuzingatia. Ni Sa’ad (ra) aliyesimama siku ya Badr, siku ya al-Furqan, na kumwambia Mtume (saw), “لقد آمنا بك وصدقناك... وشهدنا أن ما جئت به هو الحق، وأعطيناك على ذلك عهودنا ومواثيقنا على السمع والطاعة لك، فامض يا رسول الله لما أردت فنحن معك، فوالذي بعثك بالحق لو استعرضت بنا البحر فخضته لخضناه معك ما تخلف منا رجل واحد، وما نكره أن تلقى بنا عدونا غداً، إنا لَصبرٌ في الحرب، صُدقٌ عند اللقاء، لعل الله يريك منا ما تقر له عينك، فسر على بركة الله “Tumekuamini na kukusadiki juu ya ulichokuja nacho kuwa ni haki, na juu ya hilo tumekupa ahadi na ithibati yetu juu ya kukusikiza na kukutii. Basi amua ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; na sisi tupo pamoja nawe. Naapa kwa yule aliyekuleta kwa haki lau ukituamrisha kuchupa baharini nasi tutachupa pamoja nawe, na hatokuhalifu yeyote kati yetu. Hatutochukia kukutana na adui yetu kesho, sisi ni wenye Subira katika vita, wakweli katika mapambano. Mwenyezi Mungu akuonyeshe kutoka kwetu kile kitakachotuliza macho yako, basi na tutegemee baraka za Mwenyezi Mungu na usaidizi wake.”

Hili ndio jambo ambalo watu wenye Nguvu na Nusra kutoka kwa makamanda na maafisa kwenye jeshi la Waislamu lazima walitambue, kuhusu msimamo wa watu, katika kuamua majaliwa ya Ummah. Hii ni kuwa wanatumia maisha yao kama alivyokuwa Sa’ad, katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt). Hakika, Sa’ad alifahamu kwa usahihi maisha ya dunia. Kwa hivyo, yeye (ra) alitekeleza jukumu la kutoa Nusrah kwa Uislamu na Mtume wake (saw) katika kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu juu ya ardhi. Kifo chake kilikuwa kama bwana harusi aliyepambwa kwenye bustani za Peponi. Huyu ndiye Sa’ad ambaye watu walimwambia Mtume (saw), ما حملنا يا رسول الله ميتاً أخفَّ علينا منه “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hatukuwahi kubeba maiti nyepesi kama hii”. Juu ya jambo hili Mtume (saw) akasema,

«مَا يَمْنَعُهُ أَنْ يَخِفَّ وَقَدْ هَبَطَ مِنَ المَلاَئِكَةِ كَذَا وَكَذَا، لَمْ يَهْبِطُوا قَطُّ قَبْلَ يَوْمِهِم، قَدْ حَمَلُوْهُ مَعَكُم»

“Hakuna kilichofanya mwili wake kuwa mwepesi isipokuwa kuna Malaika kadha na kadha wameshuka na kumbeba pamoja nanyi ambao hawakuwahi kushuka kabla ya siku hiyo.”   [imenukuliwa kutoka Tabaqat, ya ibn Sa’ad.]

Huyo ndiye Sa’ad (ra) ambaye alipokufa Jibril (as) alikuja kwa Mtume (saw) na kusema, من هذا العبد الصالح الذي مات؟ فتحت له أبواب السماء وتحرك له العرش “Ni nani huyu mja mwema aliyekufa? Milango ya mbingu imefunguka na Arshi imetikisika kwa ajili yake.” Mtume (saw) akasema,

«هَذَا الْعَبْدُ الصَّالِحُ الَّذِي تَحَرَّكَ لَهُ الْعَرْشُ، وَفُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ، وَشَهِدَهُ سَبْعُونَ أَلْفاً مِنَ الْمَلَائِكَةَ لَمْ يَهْبِطُوا إِلَى الْأَرْضِ قَبْلَ ذَلِكَ، وَلَقَدْ ضُمَّ ضَمَّةً ثُمَّ أُفْرِجُ عَنْهُ»

“Mja huyu mwema ambaye Arshi imetingishika kwa ajili yake na milango ya mbingu imefunguka, na wakashuhudia Malaika sabiini alfu ambao hawakuwahi kushuka ardhini kabla yake, hakika amezikwa na wakaondoka.” [Hii imepokewa na Haakim na kusahihishwa na al-Dhahabi. Imam Ahmad ameitaja kuwa yenye isnad hasan.]

Hakika, hadhi hii imetayarishwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa yule aliyetoa Nusra kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), wakati alipoisimamisha Dola ya Kiislamu. Hadhi hii ni sawa na huenda, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, ikawa ni kubwa zaidi kwa wale wanaotoa Nusra kwa Waislamu katika zama hizi. Ni wakati ambapo Uislamu haupo katika maisha yao, na huku nguvu ya ukafiri na ukatili ikiwazonga, maadui wanajikusanya dhidi yao na mifumo yote na amri zinawagonga kwa kuwafikiana. Hivyo, yule aliyefuzu miongoni mwa Watu Wenye nguvu na Kinga ni yule aliyeitumia fursa hii, ambayo imejitokeza baada ya karne kumi na nne kwa mara ya pili. Mwenye kufuzu anahangaikia kuipata zawadi hii na hadhi ya yule aliyeipatiliza fursa kwa mara ya mwanzo, kiongozi wetu, Sa’ad bin Muadh (ra).

Ama kwa yule aliyenyimwa miongoni mwa Watu wenye Nguvu na Kinga, ni yule aliyeiuza Akhera yake kwa Dunia, au Akhera kwa Dunia ya mwengine. Huyu anahangaikia medali, vyeo na nafasi kubwa kubwa katika jeshi la Waislamu. Hawekezi haya katika kuunusuru Uislamu na Waislamu, na kusimamisha hukmu za Sharia za Mola wa walimwengu wote hapa duniani. Badala yake anayafanya haya ili kupata fungu kubwa zaidi la starehe za dunia, na majivuno ya muda mfupi. Anasahau kuwa medali na vyeo havitomkinga na ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt), wala kwa chochote chengine kutokana na moto wa Jahannam, kama atashindwa kutoa Nusra kwa Dini hii.

Afisa mwenye kumiliki nguvu na kinga lazima atambue kuwa Sa’ad bin Muadh (ra) alikuwa ni binadamu kama sisi. Alikuwa na ghariza za kibinadamu ambazo sisi pia tunazo. Alikuwa na misukumo ya ghariza ya kumiliki, ya kizazi na ya kuishi, ambazo dhihirisho lake ni mapenzi ya pesa, hadhi, watoto na wanawake… Hata hivyo, kwa sababu imani yake ilikuwa safi na ya wazi, alikuwa na hakika kuwa starehe za dunia hii ni starehe za kupita tu. Alikuwa na hakika kuwa starehe za Akhera ni za kudumu na hazikatiki, na hizo ndio starehe halisi. Wenye kumiliki Nguvu na Kinga hivi leo lazima watambue kuwa Swahaba Sa’ad (ra) sio katika wasiofanikiwa katika historia ambapo lazima isijirejee. Kama alivyokuwa Saad (ra), wao pia wanaweza kufanya matendo yake mazuri, kwa kuwa Nusra yao ni kama Nusra yake. Kutajwa kwao leo ni sawa na tamko la wahyi la jana, kwa Sa’ad (ra).

Kutoka kwa Asim bin Qatada, imepokewa kuwa, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alilala, na Malaika alimjia – au Jibril alisema – wakati alipoamka, na kusema, من رجل من أمتك مات الليلة، استبشر بموته أهل السماء “Ni mtu gani kutoka Ummah wako aliyefariki usiku huu, ambaye maisha ya baada ya kifo chake yanafurahiwa na walioko mbinguni? Alisema, «لا أَعْلَمُ إِلا أَنَّ سَعْداً أَمْسَى دَنِفاً (مريضاً). مَا فَعَلَ سَعْدٌ؟» “Sijui, isipokuwa ni kwamba Sa’ad alipatwa na maradhi, Sa’ad amefanya nini?” Walisema, يا رسول الله، قد قبض، وجاءه قومه فاحتملوه إلى ديارهم “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), roho yake imeshachukuliwa. Watu wake wamekuja kumchukua na kwenda naye majumbani mwao.” Mtume (saw) aliswali swala ya asubuhi na kwenda pamoja na watu. Watu walitembea kwa haraka, hadi viatu vyao kuwavuka, na majoho yao kuwavuka. Mtu mmoja akasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), watu wamechoka.” Mtume (saw) alisema,

«إِنِّي أَخْشَى أَنْ تَسْبِقَنَا إِلَيْهِ الْمَلَائِكَةُ كَمَا سَبَقَتْنَا إِلَى حَنْظَلَةَ» “Ninahofia Malaika watatutangulia kama walivyotutangulia kwa Handhwalah (ra).” Alikuwa akirejea, «هَنِيئاً لَك أَبَا عَمْرٍو! هَنِيئاً لَك أَبَا عَمْرٍو» “Hongera ewe Abu Umar! Hongera ewe Abu Umar!”

Enyi Mnaomiliki Nguvu na Kinga miongoni mwa Maafisa wa majeshi ya Kiislamu! Hiki ndicho kipindi ambapo azma imetambulika, na matukufu yamenakiliwa. Hiki ndicho kipindi ambapo hamtapoteza kitu katika kutoa Nusra kwa Dini hii. Hivyo msipoteze fursa hii. Tekelezeni maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa tamko thabit, “Tupo kwa ajili yako, Ewe Mwenyezi Mungu, tupo kwa ajili yako”. Hivi leo, Ummah wa Kiislamu unakulilieni, basi itikieni kwa kusema, “Sisi ndio faraja yenu, enyi Ummah wetu, sisi ndio tulizo lenu.” Leo, Hizb ut Tahrir imenyosha mikono yake kwenu ili mlimalize jukumu lenu pamoja nayo, basi itikieni kwa kauli, “Sisi ndio Sa’ad wenu, Hizb ut Tahrir, sisi ndio Sa’ad.” Muitikieni yule anayekuitieni kwenye maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt)… Hamtaki kuwa katika njia ya Sa’ad wawili, Sa’ad bin Muadh na Sa’ad bin Ubadah, As’ad na Usayd?! Hamtaki kituo chenu kuwa kama kituo chao, na kupanda kufikia kituo chao, kupata starehe za kudumu kama zao?!

Enyi Mnaomiliki Nguvu na Kinga miongoni mwa Maafisa wa majeshi ya Waislamu! Msimamo wa kiongozi wa Ansar, Sa’ad bin Muadh (ra), ulijaza furaha nyoyoni mwa Waislamu. Jina lake halitajwi, isipokuwa ndimi zinakuwa na furaha kwa kumuombea Dua. Haijasikika Arshi ya Aliyetukuka ikitingishika kwa kifo chake, isipokuwa macho yakibubujikwa na machozi ya furaha kwa ajili yake, kukiwa na shauku kubwa ya kuyapata mfano wa hayo. Je kuna njia nyengine ya kurejea kwa Mola wetu (swt)?! Utukufu wa watu upo kwenye misimamo yao, kwa hali yoyote iwayo, kukiwa na msisitizo wa kuyafikia, licha ya kila aina ya changamoto iliyopo… Mnaishi katika wakati ambao, wito sawa na ule wa Muhajirun kwa Ansar unatolewa kwa mara nyengine. Kwa hiyo, kuweni Ansar wetu hivi leo. Nyanyueni utukufu wa Dini yetu. Nyanyueni utukufu wa Ummah wetu.

Tunajua kwa yote haya, kama mjuavyo. Mahala penu stahiki ni juu ya viwanja vya mapambano. Basi viko wapi viwanja vya mapambano ya utukufu ambavyo watawala hawa wamefungua kwa ajili yenu?! Viko wapi vita vya heshima ambavyo wamepigana pamoja nanyi?! Viko wapi vita vya kishujaa, ambavyo majina yenu na matendo mazuri yamehifadhiwa?! Viko wapi vita ambavyo nyinyi mnatambulika navyo, na kutambulika nanyi? Tunajua, kama mjuavyo, kuwa nyinyi si tu waajiriwa. Jukumu lenu sio tu utulivu na kuhifadhi maisha. Nyinyi ni ufunguo wa milango ya muendelezo katika utawala na uwezeshaji katika mamlaka. Nyinyi ni jukwaa la Umma kwa ajili ya Jihad dhidi ya maadui wa Dini. Ummah unahitaji kukuoneni mkiwa kama Musa bin Nasir, Uqba bin Nafi’, Muhammad bin Qasim na Tariq bin Ziyad.

Mnafahamu, Enyi Watu wa Nusra Yetu, kuwa watawala hawa wanataka kushinda kwa ushawishi wao, na kubakia katika udhalimu wao. Wanakutakeni kusimama pamoja nao na kulinda uongo wao. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) anakutakeni kuchukua mamlaka kutoka kwa watu hawa. Mwenyezi Mungu (swt) anakutakeni kuwapatia mamlaka ya utawala watu wa Da’wah, kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume, ili watawale kwa yale yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametushushia. Watawala hawa wanajuwa kuwa miongoni mwenu kuna wanyenyekevu wanaoheshimu Dini yao. Wanajua kuwa miongoni mwenu kuna wenye hasira nao, kwa sababu ya miamala yao ya aibu na maafikiano. Wanajua kuwa miongoni mwenu kuna ambao hisia zao zinatingishika kwa kile ambacho Ummah unakabiliana nacho chini ya mikono ya maadui zao, pamoja na wale wanaopatwa na maumivu wanayoyahisi Waislamu…

Kwa hiyo, wanakutisheni, wanakutengeni, wanakuchunguzeni, wanakubaneni, wanakubadilisheni vyeo vyenu na kukuhojini. Wanampandisha cheo afisa mwenye fikra ya uovu, huku wakikataa kumpandisha cheo afisa mwenye kuheshimika, aliyetengenea. Wanafanya hayo kufadhaisha uwezo wenu katika kuleta mabadiliko, wakati Mwenyezi Mungu (swt) anakutakeni kuwatwaa watawala, kuwachapa migongo yao, kuwang’oa, na kuuepusha Ummah kutokana na uovu wao. Mwenyezi Mungu (swt) anakutakeni kuwa wenye nguvu dhidi ya watawala waovu, wenye huruma kwa Waislamu, na walinzi wa Dini hii. Huu sio muda wa kusitasita, wala sio muda wa kuchelewa chelewa. Huu ni muda wa haki kwa Ummah na Nusrah kwa Dini hii. Kama hamtotoa kipaumbele kwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) juu ya masuala ya uovu, hali ngumu itabakia kwa Dini yenu na Ummah wenu. Na mambo yatageuka dhidi yenu Akhera, kwa kupuuza kwenu.

Hivyo je Sa’ad (ra) angeweza kukubali kile ambacho Mayahudi wanafanya kwa Waislamu Palestina? Au Marekani ilivyofanya Iraq na Afghanistan, pamoja na uadui wake wa uvamizi dhidi ya Waislamu kila mahali? Au kile Urusi ilichofanya Chechnya na Syria, India katika Kashmir, na China katika Turkestan Mashariki?! Basi kwa vipi, vizazi vya Sa’ad vinayakubali haya yote? Hatuwageukii waovu miongoni mwa wanaomiliki nguvu miongoni mwenu, ambao ni sawa na watawala. Tunawageukia walio wakweli miongoni mwenu. Hatutaki Nusrah isipokuwa kutoka kwa walio na mfano wenu. Kwa hiyo, hamna sababu ya kukataa. Hamna sababu ya kubakia kimya na kutulia tu. Kama hamtochukua hatua ya kutoa Nusrah kwa Dini yetu, basi nani atachukua hatua hiyo?

Kubadilisha watawala wa leo, ili kusimamisha hukmu kwa yote yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ni suala muhimu zaidi ya maagizo yote katika Dini. Mabadiliko haya ya kivitendo yapo chini ya mabega ya wenye kumiliki nguvu, kabla ya wengine wote. Njia zimeandaliwa kwa ajili yenu, ili mahitaji ya Ummah yawe ni kubadilisha watawala. Njia zimeandaliwa kwa ajili yenu, kiasi kwamba watawala wanahofia kisasi cha wananchi juu yao. Njia zimeandaliwa, kiasi kwamba upanga wa wavamizi wa Marekani na Ulaya umevunjika chini ya fuawe ya mujahidina, huku makamanda wa Kiyahudi wameanza kugundua hofu yao ya kuibuka kwa Salahuddin hivi sasa.

Njia zimefunguliwa na zinawasubiri wale watakaopita kuelekea kwenye Haki. Toeni Nusra yenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ya Khilafah ya pili kwa njia ya Utume inakusubirini. Kuweni Ansar wa leo mtakaotoa Nusra ya kurejea kwake. Kuweni akina Sa’ad wa Ummah huu hivi leo. Sa’ad yupo miongoni mwenu, basi na ajitokeze. Ummah una hamu ya kumuona miongoni mwenu. Unamsubiri Sa’ad kuchukua mamlaka, juu ya Haki, kuiweka ikiwa ni amana kwa watu wanyenyekevu wa Da’wah, ili wasimamishe Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, kuhukumu kwa Haki. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[مَنْ كَانَ يَظُنُّ أَنْ لَنْ يَنْصُرَهُ اللَّهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى السَّمَاءِ ثُمَّ لِيَقْطَعْ فَلْيَنْظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُ مَا يَغِيظُ]

“Anayedhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera na afunge kamba kwenye dari kisha aikate. Atazame je hila yake itaondoa hayo yaliyo mkasirisha?.” [Surah Al-Hajj 22:15]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu