- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Viongozi Viziwi, Mabubu, Vipofu wa Ulimwengu wa Kiislamu wanaipa Marekani na Dola ya Kiyahudi Ruhusa ya Kutekeleza Mauwaji ya Halaiki kwa Wapalestina
(Imetafsiriwa)
Katika kipindi cha wiki chache zilizopita na ndani ya masaa 48 yaliyopita, dola ya Kiyahudi imeivamia Gaza kwa kiwango kisicho cha kawaida ambacho hakijashuhudiwa katika kumbukumbu za sasa. Kigugumizi kilichoushika uongozi wa ulimwengu wa Kiislamu kimevunja rekodi zote za kukosa uaminifu na usaliti. Kwa kila mauwaji ya Mpalestina anayeuawa na dola ya Kiyahudi, uongozi wa ulimwengu wa Kiislamu hutamka maneno matupu yanayotolewa kutoka kwenye nyoyo chafu ambapo inawatia nguvu Mayahudi kuwauwa Waislamu zaidi.
Badala ya kuzuia umwagikaji damu za Wapalestina, Mfalme Abdullah wa Jordan ameshughulishwa zaidi katika suala la “hakuna kuingia wakimbizi [wa Kipalestina] Jordan”. Aliposukumwa na uzito wa hali ya mambo, Abdullah alielezea, “kuendelea kwa vita vya Gaza kutapelekea kuripuka kwa hali ya mambo” na kisha aliendelea kutumia vikosi vyake vya usalama katika kila fursa kukandamiza kikatili msimamo wa Jordan na watu wa Gaza. Raisi Sisi wa Misri kama alivyo Abdullah ni mwenye wasiwasi sana kuhusu naqba mpya, yaani, dola ya Kiyahudi kuwasukuma Wapalestina kutoka Gaza “kuhamia…Misri”. Hata wakati vikosi vya jeshi la Al Sisi vilipoonyesha utayari wao kuingilia Gaza, Al Sisi ameharakisha kushusha fursa yao ya ushindi kwa kuliambia jeshi “msivuke mipaka na kuwa na njozi kuhusiana na nguvu zenu”.
Kisha kuna Erdogan aliyewaambia waandamanaji hivi karibuni kuhusiana na mashambulizi ya chuki ndani ya Gaza, “tutakutangazeni duniani kuwa ni wahalifu wa kivita”. Matamshi haya yalitosha kwa dola ya Kiyahudi kumuita balozi wake na kutathmini upya mahusiano yake na Uturuki. Wakati huo huo kwa upande wa Erdogan hakukuwa na matokeo ya ulipizaji kisasi wa kidiplomasia na Uturuki imepuuza shida za wakaazi wa Gaza na imeendelea na uhusiano wake wa kinafiki na dola ya Kiyahudi. Ama kwa Waziri wa Fedha wa Saudia Al Jadaan ametoa umuhimu mdogo kuhusiana na umwagikaji damu wa Wapalestina wasio na hatia katika Gaza na ametaka kuelekeza kwenye “kutoongezeka” na kuanza tena juhudi za usawazishaji wa mahusiano na dola ya Kiyahudi mara baada ya vita kumalizika.
Hayo ndio matendo maovu ya watawala, na usaliti wao kwa Gaza unaonekana wazi. Wapo kuwaridhisha na kuipa uhai dola ya Kiyahudi, huku wakizima matumaini ya watu wa Gaza. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,
[وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَكْرُ أُوْلَئِكَ هُوَ يَبُورُ]
“Na wanaopanga vitimbi vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya hao vitaondoka patupu” [Faatir: 35:10].
Kwa watawala, matumizi pekee ya nguvu yamehifadhiwa kuwafunga na kuwazuia Ummah kuikomboa Gaza kutoka kwa utawala wa kidhalimu wa Kiyahudi. Na wanapokumbushwa kuhusu mrundikano mkubwa wa silaha na ukubwa wa bajeti za kijeshi, watawala kwa makusudi wana hafifisha uwezo wa nguvu zao za kijeshi na kukuza nguvu za dola ya Kiyahudi. Huu ni upotoshaji mkubwa wa ukweli na kila mwenye hata kiasi kidogo tu cha hisia huweza kuona kuwa ulimwengu wa Kiislamu una uwezo na utayari wa kuishinda kirahisi dola ya Kiyahudi na kuikomboa Palestina kabisa. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,
[فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ إِنَّهُ لاَ يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ]
“Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anaemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikanusha ishara zake? Hakika hawafanikiwi wakosefu”. [Yunus: 10:17].
Jambo la chini zaidi ambalo ulimwengu wa Kiislamu unaweza kufanya kwa watu wa Gaza ni kutekeleza mpango wa nukta 10 ambao hautohakikisha tu ukombozi wa Palestina lakini pia utapunguza uingiliaji wa Wamagharibi katika ardhi za Waislamu:
1. Kuvunja mara moja mikataba yote ya amani na dola ya Kiyahudi na kukata mahusiano yote ya kidiplomasia. Kuwafukuza wawakilishi wote wa dola ya Kiyahudi kutoka ardhi za Waislamu na kushikilia rasilimali zao zote. Kwa hivyo Misri, Jordan, Bahrain, Imarati, Uturuki, Morocco, Sudan, na nchi nyenginezo za Waislamu zimalize mikataba yote ya amani, kumaliza mahusiano ya kidiplomasia na mashirikiano yasiokuwa rasmi.
2. Kusimamisha aina zote za ushirikiano wa kiintelijensia, kuzifikia njia za mapitio ya maji na anga. Misri lazima ishikilie kwa haraka ushirikiano wa intelijensia wa Wapalestina na dola ya Kiyahudi. Jordan imalize usaidizi wake wa kuwa daraja la anga linalosambaza silaha na risasi kwa IDF (jeshi la Israel) linalomwaga damu za Wapalestina.
3. Nchi za Waislamu zimalize aina zote za ushirikiano na dola ya Kiyahudi. Hii inajumuisha aina zote za ushirikiano wa kibiashara na kitamaduni. Kwa mfano, Uturuki ni mshirika mkuu wa tatu wa kibiashara wa dola ya Kiyahudi wakati Imarati inaendesha zaidi ya safari 140 za anga kwa wiki kukuza ushirikiano wa kitamaduni. Aina hizi za usaidizi kwa dola ya Kiyahudi usitishwe kwa haraka.
4. Kazakhstan, Nigeria, na Azerbaijan zinaisambazia dola ya Kiyahudi zaidi ya asilimia 50 ya mafuta ghafi kukidhi mahitaji yake ya nishati. Usambazaji huu usimame mara moja kwa dola ya Kiyahudi na mikataba yote ya mafuta isimamishwe.
5. Vikosi vya majini vya Uturuki, Misri na Lebanon viweke zuwio kwa bidhaa zote (za kijeshi na zisizo za kijeshi) zisiingie katika bandari za dola ya Kiyahudi Mashariki mwa bahari ya Mediterania. Pia, vikosi hivi vizuwie machimbo ya gesi baharini na kukata usambazaji kwa dola ya Kiyahudi. Vikosi vya Misri, Saudi Arabia na Jordan viweke zuwio mfano wa hilo katika Ghuba ya Aqaba na kuinyima dola ya Kiyahudi aina zote za bidhaa muhimu.
6. Syria na Lebanon zifungue mipaka yao bila kufungwa na kuruhusu majeshi ya Uturuki, Iran, Iraq kuyapeleka kwenye mipaka ya kaskazini mwa dola ya Kiyahudi. Hivyo hivyo, majeshi ya Misri, Saudi Arabia, Jordan, na nyenginezo ziizingire dola ya Kiyahudi, na wakati muwafaka ukifika ziikomboe Palestina.
7. Pakistan ihamasishe na ipeleke silaha zake za kimbinu za nyuklia katika batalioni za majeshi ya Waislamu na iweke tayari silaha zake za kimkakati za nyuklia ili kutia hofu dola ya Kiyahudi isifikirie hata kidogo kutumia silaha za nyuklia.
8. Mataifa ya Ghuba ambayo yamewekeza zaidi katika rasilimali kwa dolari za Kimarekani wazigeuze mara moja kuwa sarafu na kugeuza matumizi kwenye rasilimali zisizo za dolari. Pia, mafuta yote, gesi na madini ya thamani yanayosafirishwa kwenye masoko ya kimataifa yatenganishwe na dolari.
9. Ulimwengu wa Kiislamu uitishe kikao cha haraka pamoja na Urusi na China na kuwashawishi kutumia fursa na kuidai Ukraine na Taiwan. Hii inakusudiwa kuzusha jinamizi la usalama kwa Marekani, na itabidi kuchagua baina ya kuisaidia dola ya Kiyahudi, kuihifadhi Ulaya, au kuzilinda nchi za Asia ya Pasifiki.
10. Ulimwengu wa Kiislamu hautoendelea kuitambua sheria ya kimataifa, ambayo Wamagharibi wanaichukua wapendavyo. Sheria ya kimataifa ni unafiki uliotoka kwa dola chache kubwa za Magharibi kuzidhibiti rasilimali za Ummah, kutekeleza mauwaji ya halaiki kwa Waislamu na kuendeleza migawanyiko katika ulimwengu wa Kiislamu.
Licha ya urahisi wa utekelezaji wa matendo haya, watawala wa ulimwengu wa Kiislamu hawatochoka kubuni sababu za ovyo zinazokusudiwa kuchelewesha utekelezaji wa nukta hizi. Hivyo ni juu ya Ummah kuwakwepa watawala hawa waoga na kuyataka majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu moja kwa moja kuikomboa Palestina. Kama majeshi yatasitasita na kutokuwa na uhakika, basi Ummah uunganishe safu zao kwa kuiregesha tena dola ya Khilafah Rashida, ambayo itakuwa ni yenye ushindi katika kuikomboa Palestina kama kupepesa jicho tu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,
[إِن يَنصُرْكُمُ اللّهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]
“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani basi baada yake yeye atayekunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aali Imran 3:160].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Islam Mujahid – Wilayah Pakistan