Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kufichua Njia Zote Zisizo Sahihi na Zenye Kutuweka Mbali na Suala la Palestina

(Imetafsiriwa)

Suala la Palestina ni jaribio. Kama wewe upo wazi kuhusu kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) ametuagiza na Mtume Wake (saw) amekifanya kivitendo katika hali kama hiyo, basi unaweza kuchuja vishawishi vyote bandia, vya wenye kulipwa, na waoga ambao hawalinganii katika njia ya sawa kutatua suala hili. Badala yake, wanakuja na aina zote za nadharia na mapendekezo lakini hawako tayari kutamka kile kinachohitajika. Zifuatazo ni njia maarufu zaidi sisizo sahihi zinazotuweka mbali na zinazopendekezwa kuwa ni suluhisho kwa suala la Palestina.

1. Kuongea kinadharia kuhusiana na matokeo ya karibuni:

Wataalamu wengi wa kinadharia wameshughulika hivi leo wakizungumza kuhusu nani atanufaika na matukio haya ya karibuni, nani yuko nyuma yake, kwa nini yanatokea wakati huu, na kadhalika. Sikiliza. Kuwa mwenye kusikiliza hoja! Hata kama hili lilikuwa ni lenye kufaa, lingeweza kuwa ni jambo la mwisho tunalolazimika kulitafuta. Hadi hivi sasa kuna masuala ya kutosha ambayo majibu yake yapo wazi na yanahitaji kuzungumzwa. Tafauti gani itapatikana kuhusiana na nani aliyekula njama na aliyepanga, wakati matokeo yake ni mamoja, nayo ni mauwaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Palestina?

2. Kuwakumbusha wengine namna gani ardhi hii imetukuzwa:

Wale wanaoshughulika mchana na usiku kuzungumzia kuhusu namna gani tatizo hili limechimbuka na Mitume wangapi wamepatikana katika Ardhi hii Tukufu, Nina wauliza, kwani madaktari wanakupatia mafunzo yasiokwisha kuhusu maradhi na historia yake wakati unachokihitaji ni upasuaji?

3. Kukusanya michango:

Kwa wale walio na fikra ya kukusanya na kutuma michango kwa ndugu zetu Wapalestina. Hatukufanya haya kwa muda wa kutosha hadi sasa? Je, imesaidia? Haikuwa ni kukusanya fedha kwa wale ambao wako hai hivi sasa ili mara wanapo uliwa, makaburi yao na majeneza yaweze kutayarishwa?

4. Kususia bidhaa za ‘Israel’:

Halikuwa hili ni suluhisho la kiashirio tu na kwamba sio tatuo halisi? Hatukuwa sisi tukijaribu kufifiliza hatia yetu ya kutofanya kitu sahihi kwa kadhia kama hizi? Utajizuia tu kununua bidhaa kutoka kwa muuzaji ambaye ameikalia nyumba yako na kuuwa familia yako?

5. Kuwekeza kwenye biashara za Wapalestina:

Je, uko makini kweli? Je, ni uwekezaji ndio wanaohitajia? Kila eneo lao la asili walilonalo linawachwa kwa kuvamiwa na wewe unawataka watu kuwekeza katika biashara zao? Biashara gani wataendesha wakati hakuna majengo tena yaliobaki? Biashara gani inayoweza kuendeshwa katika eneo la jela ya wazi?

6. Kupigana vita vya Mitandaoni:

Kama hilo litakuridhisha, endelea nalo, lakini unajua kuwa mitandao utakayotumia kama eneo la mapambano inamilikiwa na wao na hawatochelewa kukuengua jukwaani, kukuzuia na kusitisha akaunti yako. Zaidi ya hapo, je ni kweli unafikiri Palestina itakombolewa kwa makala za Facebook, ku-like video za Instagram, na kusambaza WhatsApp?

7. Kuacha madhambi:

Ndio bila shaka tunahitaji kuacha madhambi na kuleta Toba, lakini dhambi ambayo lazima tuiwache hivi sasa ni dhambi ya kutotoa sauti zetu. Dhambi ya kutowalingania wale walioko mamlakani walio na nguvu kwenda kuwasaidia ndugu zetu wa Palestina.

8. Kufanya dua kwa ikhlasi:

Ndio fanya dua, usiku na mchana, lakini utabakia unaleta dua tu wakati unahitaji digrii, wakati unahitaji kazi, unapohitaji kuoa, au utafanya zaidi ya dua kwa kutoka na kutenda yote yanayohitajiwa?

9. Kubisha hodi kwenye milango ya OIC:

OIC imekipata kipi katika miaka 75 iliyopita? Nini ukweli wa OIC? Je, hiyo sio sehemu ya tatizo hilo hilo tunalojaribu kulitatua? Je, kuna yeyote mwenye akili timamu anayetarajia watawala hawa walionyamaza kimya juu ya mamia ya maovu yanayotekelezwa kila mahala katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa watafanya jambo chanya?

10. Kubisha hodi kwenye milango ya UN:

UN yenyewe ndio taasisi ambayo imekuwa ikifanya juhudi za kuihalalisha Israel. UN ndio inayohakikisha kuwa Waislamu ambao kwa asili yao kutokana na Hadith kwamba ni kitu kimoja, kuwa wamebaki wamegawanyika, basi kwa vipi tutaitegemea kutatua mzozo huu?

11. Usaidizi wa kidiplomasia, kimaadili na kisiasa:

Hili lina maana gani? Ndio kwa namna hii unaweza kutatua matatizo yako? Ndio kwa namna hii dunia inatatua matatizo yake? Au ni kupitia njia za kimatendo?

12. Kwamba Waislamu ni dhaifu:

Je, ni kweli? Aliye dhaifu zaidi miongoni mwetu, bila ya kuwa na jeshi rasmi, bila kuwa na jeshi la anga, wenye idadi ndogo ya milioni chache ya watu, na yenye mipaka iliyozungukwa, karibuni tu imeweza kuwashinda mataifa makuu mawili. Yeyote anaye eneza hadithi hizi dhaifu licha ya kuwa kwetu na jeshi kubwa, ndege kadhaa za mashambulizi, manuwari za kivita, na silaha za nyuklia ni muongo aliye muoga, licha ya nafasi yake aliyo nayo.

Basi usiwe na shaka akilini mwako kuwa jambo hili linalazimisha uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu. Ni jukumu letu kuwakumbusha juu ya jukumu hili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Abdul Baseer Kazi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu