Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kubadilisha Uovu Mmoja kwa Mwingine:

Umoja wa Mataifa Kamwe Hautawalinda Waislamu

Mauwaji ya halaiki ya Srebrenica yalikuwa ni janga la kuogofya katika historia ya wanadamu. Mauwaji hayo ya halaiki yalifanyika katika miji ambayo Baraza la Usalama liliitambua kama maeneo salama, lakini kisha likakataa kuidhinisha vikosi vya kutosha kuyalinda. Matokeo yake, zaidi ya wavulana na wanaume wanati wa Bosnia 8,000 walichinjwa katika kipindi cha wiki moja ya unyama, ambapo yangezuiwa. 

Mwezi huu unakamilisha kumbukumbu yake ya 25.

Miaka 25 tangu damu ya kaka zetu na dada zetu wa Kiislamu ilipo mwagwa, katika tukio ambalo Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wake walipuuzia waziwazi tishio kwa Wabosnia, kama walivyo puuzia tishio kwa Waislamu wa Rwanda mwaka mmoja kabla.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hii ilikuwa ni, "ishara haribifu" alioashiria kufeli kwa Umoja wa Mataifa. Wanasema kuwa walianza kulichukulia 'Jukumu la Kulinda' kwa uangalifu zaidi baada ya mambo ya kutisha kutokea katika miaka ya tisiini.

Hivyo basi, ni kwa nini Waislamu kote duniani wangali wanateseka? Ni kwa nini Waislamu Kashmir, Rohingya, China na Palestina wangali wanakabiliwa na mauwaji ya kimbari? Ni kwa nini Waislamu nchini Yemen na Syria wangali wanauwawa katika mvutano wa kung'ang'ania mamlaka?

Umoja wa Matiafa una nyudhuru nyingi kwa mauwaji yanayo fanyika katika maeneo haya; ukosefu wa utulivu wa kisiasa, migawanyiko miongoni mwa Nchi Wanachama, uhaba wa rasilimali.

Nyudhuru hizi zimesababisha hali ambapo Waislamu kote duniani wanachinjwa na kuuwawa, ambapo wanakosa usaidizi msingi na wanaishi katika dhurufu mbaya.

Licha ya uhalisia huu, wanasema kwa ujasiri kuwa "Ulimwengu unatutazama sisi hapa katika Umoja wa Mataifa na katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na unatutarajia tudumishe haki hiyo na kukidhi matamanio hayo. Hili ni jukumu letu la pamoja leo. Na ndio namna ambayo tunaweza kutoa vyema heshima kuu kwa waathiriwa wa Srebrenica." (Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson mnamo 2015) 

Wanasema kuwa kutoa heshima kuu kwa waathiriwa wa Srebrenica kupitia kutuma majeshi ya kuweka amani ambao kwa sasa wanacheza dori katika kuimarisha juhudi za kuzuia, kutekeleza jukumu la kuwalinda wale walio hatarini na kutekeleza haki ya watu wote ya kuishi kwa "amani na hadhi." Kuwalinda wananchi katika nchi ndio "kipaumbele".

Kufikia nukta hii, pamoja na orodha ya rekodi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani na hadhi yetu, tunahitaji kuangalia uhalisia wa wanajeshi wa kuweka amani na 'ulinzi' wao.

Wanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa na dori yao:

Wanajeshi wa kuweka amani au "kofia za samawati" hupelekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Huku shirika hili likiwa halina jeshi la kudumu au polisi wake binafsi, Nchi Wanachama huombwa kuchangia wanajeshi au polisi wanaohitajika kwa kila operesheni. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, "Pindi majeshi ya kuweka amani yanapo tumika chini ya Umoja wa Mataifa huunganishwa kwa kujitolea kudumisha au kuregesha amani na usalama wa ulimwengu. Wanashirikiana katika kusudio moja la kuwalinda walio madhaifu zaidi na kutoa usaidizi kwa nchi zilizo katika kipindi cha mpito kutoka katika mzozo hadi katika amani."

Kidhahiri, wanatarajiwa "kushikamana na viwango vya juu kabisa vya suluki na kuhudumu kwa njia ya utaalamu na nidhamu" pindi wanapoitwa "kudumisha amani na usalama, kusahilisha mchakato wa kisiasa, kulinda raia, kusaidia katika kupokonya silaha, kuwamakinisha na kuleta uwiano mpya wa waliokuwa wapiganaji; kusaidia maandalizi ya uchaguzi, kulinda na kuboresha haki za kibinadamu na kusaidia katika kuregesha utawala wa sheria."

Wanajeshi wa kuleta amani wao ndio hutekeleza mauwaji:

"Wanajeshi wa kuleta amani mara kwa mara sasa hupewa majukumu mazito ya kulinda raia. Aghlabu huwa wanaidhinishwa kutumia mbinu zote zinazostahiki katika kulinda watu." (Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson mnamo 2015)

Licha ya hili, bado wangali husimama kando huku raia wakishambuliwa. Kama ilivyo onyeshwa katika uchunguzi wa 2014 ambao umegundua kwamba kati ya matukio 570 yaliyo ripotiwa, wanajeshi wa kuweka amani "hawakuripoti kujibu matukio 406 (asilimia 80) ambapo raia walishambuliwa." Matokeo yake, raia walishambuliwa, kujeruhiwa, kudhulumiwa kimapenzi, kutekwa nyara na kukosa makao, miongoni mwa mengineo. 

Lakini kitu cha kuchukiza ni kwamba sio tu wanapuuzia vitisho kwa raia ambao wanapaswa kuwalinda, wao wenyewe ni tishio.

Miongoni mwa vichwa vya habari kuhusu wanajeshi wa kuweka amani vinajumuisha:

“Wanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa baba za watoto, kisha kuwatelekeza, mamia ya watoto nchini Haiti, ripoti inasema”

Wanachama wa jeshi la kuweka amani la Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanadaiwa kugeuka kuwa wawindaji wa ngono, wakikhini wajibu wao wa kulinda

Huu ndio ukweli unao chukiza, na kuogofya zaidi kwa ukweli kwamba sio haya sio matukio ya kipekee. Kuna msururu wa unyanyasaji na dhulma za kimapenzi unaofanywa na vikosi vya kijeshi na raia wanaoshiriki katika misheni za kuweka amani, ambao hauwezi kupuuziwa. Kuwekuwepo na ripoti nyingi za maafisa wa Umoja wa Mataifa kutekeleza uhalifu mbaya na utovu wa nidhamu wa kimapenzi, kuanzia ubakaji hadi ukahaba wa lazima wa wanawake na wasichana wadogo nchini Bosnia, Burundi, Cambodia, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea, Haiti, Kosovo, Liberia, Sierra Leone, na Sudan. Kuna ripoti kwamba wanajeshi wa kuweka amani wanawanyanyasa kimapenzi wanawake na wasichana.

Haya sio matukio ya zamani au ya kipekee. Ni sehemu ya tatizo rasmi lililopo leo.

Kama ilivyo onyeshwa katika ripoti ya CNN, maafisa wa Umoja wa Mataifa waliwalazimisha "wanawake na watoto kushiriki ngono kwa badali ya chakula, wamelangua wanawake katika misheni za Umoja wa Mataifa na kuwabaka rasmi, na wametekeleza vitendo vyenginevyo vya kinyama vya ghasia za kimapenzi". Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, walibadilisha chakula au pesa (katika baadhi ya visa, kwa uchache wa mayai mawili au dolari 4 za Kiamerika) kwa unyanyasaji wa kimapenzi wa wasichana wadogo kati ya umri wa miaka 12 na 14.

Uchunguzi wa hivi karibuni wa shirika la Associated Press (AP) umefichua kwamba katika kipindi cha miaka 10, "Umoja wa Mataifa umepokea takriban madai 2,000 ya unyanyasaji na dhulma za kimapenzi dhidi ya wanajeshi wake wa kuweka amani". Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa 'wametuhumiwa rasmi kuwadhulumu au kuwanyanyasa kimapenzi raia wa eneo hilo 42, wengi wao wakiwa wasichana wenye umri mdogo. Ni shtaka moja la jinai pekee ndio limesajiliwa.' (Washington Post)

"Tangu 2015, kuwekuwepo na madai 83 ya unyanyasaji na dhulma za kimapenzi nchini humo. Madai hayo yanawahusu baadhi ya wanajeshi 177 wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa na manusura 255. Hadi leo, ni watu watano pekee kati ya waliotuhumiwa ndio wamefungwa jela". (Al Jazeera)

Nchini Haiti, majeshi ya kuweka amani ya Umoja wa Mataifa yalitumwa Haiti kuregesha utulivu. Badala yake walileta kipindupindu eneo hilo, wakiwauwa na kuwaambukiza maelfu ya raia, na kuwadhulumu kimapenzi wanawake na wasichana. Kwa mujibu wa shirika la Human Rights Watch, "Kwanza wanawake hao walikuwa ni masikini na sasa hali zao zimekuwa hata mbaya zaidi. Kati ya wanajamii 2,500 waliohojiwa na watafiti kuhusu kuishi mijini na wanajeshi wa kuweka amani, asilimia 10 waliibua – pasi na kushinikizwa - kadhia ya watoto ambao baba zao ni wanajeshi hao".

Sasa mnamo 2019, Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa "wamepokea madai 38 ya unyanyasaji na dhulma za kimapenzi (SEA) unaohusisha maafisa wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo raia na wanajeshi wasiovalia sare katika operesheni za kuweka amani, pamoja na wale kutoka kwa mashirika, hazina na miradi".  

Matokeo? Hakuna ulinzi

Umoja wa Mataifa unasema kuwa wametabanni masharti makali zaidi kwa vikosi vyao vya kuweka amani. Makatibu Wakuu wametangaza kujitolea kwao kwa "sera ya kutovumilia hata kidogo" unyanyasaji na dhulma za kimapenzi, kuamrisha na kuandika ripoti nyingi kuhusu swala hili.

Wanazilaumu nchi wanachama kwa kutochukua hatua. Kama inavyo onyesha ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, "Napenda kutaja kuwa Umoja wa Mataifa wenyewe hauna mamlaka ya kuyaleta mashtaka dhidi ya madai au washukiwa wa uhalifu uliotekelezwa dhidi ya wanajeshi wake wa kuweka amani, wala hauna mamlaka ya kuwashtaki.  Shirika hili linategemea Nchi Wanachama kutimiza wajibu wao chini ya vyombo husika vya kisheria vya kimataifa vilivyo tajwa chini ili kutekeleza mamlaka yao ya kuchunguza uhalifu kama huo na baadaye kuwashtaki watendaji uhalifu huo kwa mujibu wa sheria zao za kitaifa." 

Nchi wanachama upande wao, wanaulaumu Umoja wa Mataifa, na kuusukuma kuchukua hatua kali zaidi.

Kile ambacho hawasemi ni kwamba wameruhusu mauwaji kama haya kufanyika kwa kuwa wamewapa wanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa kinga. Kuna sheria za kihakika zinazo walinda wanajeshi wa kuweka amani, zinazounda hali ya halisi inayo waruhusu kuwanyanyasa na kuwadhulumu wanawake na wasichana.

Huku Umoja wa Mataifa ukikataa hili, ukisema kuwa "hakuna kinga kwa dhulma za kimapenzi.", Wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa wana kinga kutokana na mamlaka ya mahakama katika nchi yoyote ulimwenguni, ikiwemo mataifa yao wenyewe. Matokea yake, hawawezi kushtakiwa isipokuwa Katibu Mkuu aondoshe kinga hiyo. Kivitendo, hili halitokei. Na ingawa, vikosi vilivyo tolewa nan chi wanachama wa Umoja wa Mataifa vinaweza kushtakiwa na nchi zao, hili ni nadra sana kutokea. 

While the UN denies this, saying that “there is no immunity for sexual abuse.”, United Nations staff have immunity from the jurisdiction of courts in any country in the world, including their own nations. As a result, they can’t be prosecuted unless the Secretary General waives that immunity. In practice, this doesn’t happen. And even though, troops provided by U.N. member states can be prosecuted by their home country, this rarely happens. (Chanzo: Ripoti ya CNN)

Badala ya kuwapa haki wahanga na kuwalinda, kama ulivyo ahidi, Umoja wa Mataifa unawaficha na kuwalinda majeshi ya kuweka amani.

"Majibu ya hamaki ya Umoja wa Mataifa daima ni kwa lengo la kuficha, kushughulika kindani, ili kulifanya tatizo litoweke" Beatrice Lindstrom, wakili wa Taasisi ya Haki na Demokrasia nchini Haiti (IJDH). (Chanzo: Al Jazeera)

"Umoja wa Mataifa kwa haraka imeripoti madai ya nchi zenye kuchangia vikosi ya kuepuka kutangazwa hadharani na kuwapa muda wa kuzificha." (Chanzo: Al Jazeera)

Katika hali ambazo ni nadra ambapo mashtaka yanatokea, adhabu huwa si kali kuliko katika nchi za nyumbani. Kama ilivyo onyeshwa pindi "vikosi vya Uruguay vilipombaka rasmi na kumdhulumu mtoto mmoja nchini Haiti. Katika kesi hiyo, vikosi hivyo vilitumikia kifungo cha miezi mitatu katika magereza ya taifa lao kwa kosa la 'ghasia za kibinafsi'." (Chanzo: Ripoti ya CNN)

Hivyo basi iko wapi haki? Uko wapi ulinzi? Mauwaji ya halaiki ya Srebrenica huenda yakawa yameshutumiwa na ahadi huenda zikiwa zimewekwa ili kuhakikisha hayatokei tena, lakini je, hali za watu ziko bora chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa?

ushahidi waonyesha kuwa majeshi ya kuweka amani yamesababisha tu hali ambayo watu wamebadilisha uovu mmoja kwa mwingine.

Umoja wa Mataifa hauwezi kuaminiwa kutatua matatizo yetu, bali jibu haliko katika shirika badali… liko katika mfumo badali.

Tunahitaji kukubali kuwa kuufanyia marekebisho Umoja wa Mataifa au hata kuufutilia mbali na kuubadilisha kwa shirika jengine hakutabadilisha chochote. Kwa sababu tatizo liko katika mfumo huru wa kirasilimali.

Ni mfumo unaoruhusu unyanyasaji.

Unawalinda wanyanyasaji, kwa gharama ya wahanga.

Umoja wa Mataifa hauwezi kuaminiwa au hata kutarajiwa kuleta mabadiliko au kulinda watu kama ulivyo ahidi. Shirika badali haliwezi kuaminiwa au kutarajiwa vilevile.

Mtume (saw) amesema:«يَا عِبَادِي إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا فَلَا تَظَالَمُوا» “Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamishwa dhulma katika nafsi yangu na nimeijaalia kuwa haramu baina yenu, basi msidhulumiane.” (Bukhari)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#Srebrenica25YearsOn       #Srebrenitsa25Yıl    #SrebrenicaMiaka25Baadaye          سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu