Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah Imeundwa Kudumisha Haki kwa Ukamilifu na Kutoa Ulinzi wa Kweli kwa Walimwengu

Enyi Ummah Mtukufu!

Kwa hakika nyinyi ni Ummah bora miongoni mwa wengine wote, ulioletwa kwa watu, kwa sababu mnashikamana kile ambacho Mwenyezi Mungu ameamrisha na mnakataza kile ambacho Mwenyezi Mungu amekikataza na mna muamini Mwenyezi Mungu (swt). Utukufu wenu, heshima yenu, umahiri wenu katika dunia hii na utawala mliowahi kuwa nao na nafasi ya juu zaidi mliowahi kuishikilia, ilikuwa ni kwa sababu ya Uislamu na ni Uislamu tu. Pindi mkibaki nyuma na kuipoteza nafasi hii, basi ni kwa sababu ya kukosekana kwa Uislamu kuwa ni mfumo kamili wa maisha katika mambo yenu. Uislamu ulibakia katika nyanja zake zote za kimaisha ya kimatendo wakati alipopatikana Khalifah aliye wakusanya Waislamu wakawa ni kitu kimoja chini ya Dola ya Khilafah na kutekeleza sheria alizoziteremsha Mwenyezi Mungu (swt) juu yao. Hivyo, inasimamia mambo ya Waislamu na wasio Waislamu duniani kote na ilikuwa ni ua la ulimwengu kwa takriban karne kumi na nne na mwangaza wenye kung'aa zaidi ambao wanaadamu hawakuutambua na hawatautambua. [1] 

Mwenyezi Mungu (swt) ameuelezea Ummah huu kuwa ni jamii bora na ya kipekee iliowahi kuumbwa. Uislamu una suluhisho kwa matatizo yote ya mwanaadamu. Lakini japokuwa Ummah wa Kiislamu una suluhisho kwa kila matatizo haya, ni wazi kuwa bila ya dola inayotekeleza suluhisho hizi na kuwa ipeleke suluhisho hizi kwa wanaadamu wote, hauna athari inayohisika kwa maisha ya Waislamu au kwa wengineo. Tukio lisilo sahaulika la mauwaji ya Srebrenica ya 1995, pamoja na mifano mingine mingi ya karibuni ya maafa ya Ummah tokea kuanguka kwa Khilafah, ni ushahidi wa kuwa Ummah hautapata amani ya kweli, haki na hifadhi kwa kutokuwepo kwa dola ya Khilafah.

Matukio ndani ya Srebrenica na maeneo ya karibu yaliotokea baina ya Julai 10 na 19, 1995 yanajulikana. Katika masiku haya machache, kiasi cha Waislamu wa Bosnia 8,000 waliuliwa na vikosi vya wa Serbia wa Kibosnia [2] baada ya vikosi vya UN kuwatelekeza Waislamu wasiokuwa na silaha. John Dalhuisen, Mkurugenzi wa Shirika la Amnesty kwa Ulaya na Asia ya Kati amesema katika Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka 2015: “Miongo miwili baada ya dunia kugeuza macho yake kwa uovu mkubwa zaidi uliofanyika katika ardhi ya Ulaya tokea 1945, familia za wahanga wa mauwaji ya Srebrenica bado zinasubiri haki itendeke. Srebrenica sio tu inasimama kama ukumbusho usio sahaulika wa uwezo wa wanaadamu wa maovu lakini pia wa kushindwa kwa jamii ya kimataifa kuzuia mauwaji kutokea katika mazingira ya wazi yenye kuonekana. Miaka ishirini baadaye, viongozi katika Bosnia na Herzegovina wanakataa kukiri wapi miili imezikwa, kwa maneno wazi na kwa majazi. Kila muda ukirefuka kwa mwenye hatia kuepuka adhabu na maiti kubaki makaburini, ndiko kurefuka kwa uchungu huu wa jeraha kutakereketa kuchochea migawanyiko hatari ya kikabila na ya kuendelea.” [3]   

Hadi hii leo, Ummah unaomboleza wapendwa wao na hakuna wa kubeba huzuni zao au hata wa kuwaadhibu wauwaji kutokana na mauwaji. Hii ni dhulma dhidi ya Ummah, japokuwa historia ya Uislamu inatuonyesha kinyume ya namna heshima ya Muislamu ilivyo lindwa. Kwa mfano, wakati Mtume (saw) alipo wahamasisha Waislamu wa Madina kuhami heshima ya mwanamke alieshushiwa hadhi na mtu wa Bani Qaynuqa. Kama Khalifah Mu’tasim Billah, aliye peleka jeshi kubwa dhidi ya ngome madhubuti ya Amuria ya Utawala wa Kirumi kwa sababu askari wa Kirumi alimvua mtandio mwanamke wa Kiislamu. Kama juhudi za maamuzi na kishujaa za Salahuddin Al Ayubi, aliye washinda Makruseda na kuwafukuza nje ya Jerusalem. Sababu ya kwa nini ulinzi kama huo ulipatikana wakati huo na sio sasa ni kwamba Mtume (saw) na Maswahaba walikuwa na Khilafah, iliyo undwa kudumisha Haki kwa Waislamu na kulinda heshima ya Ummah. Lakini hivi leo wanawake na watoto wamekuwa wakiangamizwa, kubakwa na kufukuzwa, wavulana wasio na kinga na wanaume wanatengwa kwa makusudi, wakiuliwa na kuzikwa – kwa sababu tu ya kuwa ni Waislamu wa Kibosnia na dunia ikifumba macho yake.

Uislamu haulinganishwi na mifumo iliyobuniwa na wanaadamu kwa sababu haiwezi kuwa ni mikamilifu kama mfumo ambao umeteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Wakati Amerika, Uingereza au Ulaya wanapovamia nchi safi na zenye mahitaji au kujiita zenyewe kuwa ni wafadhili, kufikia malengo ya sera zao za kigeni, kumekuwa na mateso, mauwaji, maangamizi na unyonyaji hadi sasa. Hata hivyo, lengo la vita kwa Khilafah halikuwa kuangamiza watu na kuwafanya kuwa dhalili bali ni kuwawezesha kuonja matunda ya kweli ya haki na ulinzi na kuondoa tawala fisadi.

Wasio Waislamu wamepata haki, utulivu na furaha chini ya utawala wa Kiislamu. Hata Mayahudi wa Uhispania, wakati wakisakwa na kuuliwa na Wakristo kipindi cha Mahakama ya Uhispania ya Kanisa Katoliki ya kukomesha uasi (Spanish Inquisition), walikimbilia kwenye kitovu cha dola ya Khilafah na kupokelewa huko. Mayahudi wakati huo hadi hivi sasa huzingatia kuwa Mayahudi chini ya utawala wa Kiislamu katika Uhispania kuwa ni Zama za ustawi na furaha. Hata watu wa India, ima aliye Muislamu au asiye Muislamu, pamoja na mamia ya wanahistoria, wanaelezea kipindi cha utawala wa Kiislamu nchini India kuwa ni Kipindi cha ustawi, neema na furaha. Wakati Waislamu wanapokomboa nchi, huanza kutawala kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) na raia wasio Waislamu hutendewa kwa mujibu wa sheria ambazo Mwenyezi Mungu ameteremsha na kuanza kutumika rasilimali kwao, kuwalinda na kuwahakikishia haki zao.

Mtume (saw) amesema:

«أَلاَ مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِدًا أَوِ انْتَقَصَهُ أَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئًا بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»‏‏

“Yule anayemdhulumu Mu’ahid (Kafiri aliye na mkataba na Waislamu), au kudhoofisha haki zake, au kumkalifisha zaidi ya uwezo wake au kuchukua chochote kwake bila idhini yake, basi Mimi nitakuwa mpinzani wake Siku ya Kiama.” (Abu Daud na Al Bayhaqi). Mtazamo huu wa Muislamu kwa masikini, na vile vile juu ya namna Uislamu unavyo watendea wasio Waislamu chini ya dola yake, ni sababu mojawapo ya kuwa wengi wameikubali Imani. Haki kamili na ulinzi zimeingiza uaminifu katika utawala wa Kiislamu katika nyoyo za wasio Waislamu.

Mwanachuoni maarufu wa madhehebu ya Maliki Imam al-Qurafi amenukuu kauli ya Ibn Hazm kutoka kitabu chake Maratib al-Ijmaa’: “Kama maadui katika vita wamekuja katika ardhi yetu (Dola ya Khilafah) wakimlenga dhimmi (raia asiye Muislamu), ni wajibu kwetu kutoka kupigana nao kwa nguvu zetu zote na silaha kwani wapo chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kama tukifanya upungufu wowote kwa hilii, tutakuwa tumeshindwa kwenye makubaliano yetu ya ulinzi.”

Hivyo, hakuna itikadi, hakuna mfumo, hakuna dini au njia yoyote ya maisha inayo weza kuhakikisha mahusiano kama hayo ya kiuadilifu pamoja na sehemu nyengine za ulimwengu. Hii ina maana mauwaji ya Srebrenica sio ya ajabu, bali ni matokeo ya kimaumbile ya ukatili wa leo wa dunia ya ushawishi wa kibepari. Haiwezi kutegemewa leo kwa serikali yoyote au taasisi inayo weza kulinda damu ya Ummah au hata kuhakikisha haki kwa wanaadamu. Uislamu pekee ndio mfumo ambao unasema “Raia wote wa Dola waamiliwe sawa bila kujali dini, kabila, rangi au jambo jengine lolote. Dola imekatazwa kuwabagua watu katika mambo yote, ima yawe ya utawala au ya kisheria, au kusimamia maslahi ya watu”. [4]

Hata hivyo, usimamishaji wa Khilafah ni wajibu juu ya Ummah na unawajibika kufanya kazi kwa ajili ya lengo hili. Dola hii ndio pekee yenye uwezo wa kuwaeleza wanaadamu wote kwa namna ya nguvu na ilio muwafaka watu wote waweze kuhifadhika kutokana na maafa katika dunia hii na Akhera na haki na usalama viweze kufikiwa.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Amanah Abed

#Srebrenica25YearsOn  #Srebrenitsa25Yıl #SrebrenicaMiaka25Baadaye    سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 21 Julai 2020 17:50

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu