Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hongera kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wageni wa Mitandao Yake kwa Mnasaba wa Sikukuu ya Idd ul Fitr iliyobarikiwa ya Mwaka 1443 H sawia na 2022 M

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na jamaa zake na maswahaba wake na wafuasi wake:

Kwa Ummah wa Kiislamu Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu: كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ...﴿ “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. [Aal-i-Imran: 110].

Kwa Wabebaji Dawah wasafi na wema, ingawa hatumtakasi yeyote kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa wageni waheshimiwa wa mitandao,

Natoa pongezi zangu kwenu katika Idd ul Fitr, na namuomba Mwenyezi Mungu (swt) awatakabalie saumu na qiyam na amali zote njema, na atuepushe na Moto wa Jahannam katika mwezi huu uliobarikiwa. At-Tirmidhiy amepokea katika Sunnah yake kutoka kwa Abu Huraira kuhusu masiku ya Ramadhan, amesema: Mtume (saw) amesema:

«وَلِلَّهِ عُتَقَاءُ مِنَ النَّارِ وَذَلكَ كُلَّ لَيْلَةٍ» “Kuna wale ambao Mwenyezi Mungu huwaacha huru na Moto. Na hilo ni kila usiku.” [Imetolewa na Al-Hakim katika Mustadrak yake].

Vile vile namuomba Mwenyezi Mungu (swt) aijaalie Idd hii iwe ni utangulizi wa kheri na baraka kwa Waislamu baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi chini yake kwa miaka 100 iliyopita, ili Idd ijayo ije hali ya kuwa tuko chini ya Raya (bendera) ya Khilafah Rashida, Raya ya La Ilaha Ila Allah Muhammad Rasool Allah. Na hilo si jambo kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfa Ib Al-Yaman, Mtume (saw) amesema: «...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» ثُمَّ سَكَتَ “...Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu atataka uwepo kisha atauondoa akitaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha yeye (saw) akanyamaza”. Hii pia imepokewa na Al-Tayalsi katika Musnad yake.

Kwa kutamatisha, natoa salamu na dua zangu za kheri kwenu, na namuomba Mwenyezi Mungu azikubali ibada zenu.

Wassalmu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

 

Siku ya Idd ul-Fitr, 1 Shawwal 1443 H        Ndugu Yenu
 01/05/2021 M  Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

           

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu