Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 29/05/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 21 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na 29 Mei 2024 M

Gazeti la ‘The Dawn’ liliripoti mnamo tarehe 21 Mei 2024 kwamba maisha katika Chaman yametatizika kwa karibu wiki mbili, kutokana na maandamano dhidi ya kanuni mpya za kuvuka mpaka. Maandamano yamekuwa yakiendelea tangu Oktoba 2023, wakati serikali ilipopiga marufuku kuvuka mpaka wa Pakistan na Afghanistan, bila hati halali za kusafiria, kutoka pande zote mbili, na kuanzisha "mfumo mpya wa hati moja." Watu wa makabila wamekuwa wakiandamana katika kivuko cha mpaka cha Angur Ada, kwa miezi sita iliyopita juu ya suala hili. Wafanyibiashara wa mpakani na maelfu ya vibarua wanaolipwa kila siku walikosa ajira kutokana na kanuni hizo mpya. Kukomeshwa kwa Mstari wa Durand na kuunganishwa kwa Pakistan na Afghanistan kupitia kuasisiwa Khilafah Rashida kutamaliza masaibu ya Waislamu katika eneo hilo. Khilafah itawageuza kuwa kikosi cha kutisha cha kisiasa, kiuchumi na kijeshi.

15 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 23 Mei 2024 M

"Suluhisho la Dola Mbili" la Marekani kwa Palestina ni Usaliti wa Ummah!

Tarehe 21 Mei, 2024, Waziri wa Mambo ya Nje alitoa wito wa "kuanzishwa kwa Palestina kama Dola tendakazi, salama na inayoshikamana na msingi wa mipaka ya kabla ya 1967." Waziri wa mambo ya nje wa nchi yenye silaha za nyuklia anarudia suluhisho la Marekani kana kwamba ni la Pakistan. Kwa kukataa kupeleka jeshi, watawala hawa wanawezesha mauaji ya halaiki huko Gaza. Suluhisho la dola mbili la Marekani linakabidhi sehemu kubwa ya ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kwa umbile la Kiyahudi, ambalo lilianza ukaliaji wake wa kimabavu mnamo 1948, sio mnamo 1967. Ni marufuku katika Uislamu kutoa hata shubiri moja ya ardhi ya Isra' na Mi'raj ya Mtume ﷺ. Suluhisho la kweli kwa Palestina ni lile la Salah al-Din Ayyubi ambalo ni uhamasishaji wa majeshi chini ya Khilafah.

16 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 24 Mei 2024 M

Palestina Haihitaji Kutambuliwa. Inahitaji Ukombozi na Majeshi ya Waislamu

Tarehe 22 Mei 2024, nchi tatu za Ulaya, Norway, Ireland na Uhispania, zilitangaza mipango ya kuitambua rasmi dola ya Palestina. Watawala wa Waislamu walifurahia kutambuliwa kwa mpango huo, huku umbile la Kiyahudi lilikataa. Hata hivyo, kutambuliwa ni ishara tu. Nchi 143 kati ya 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa tayari zimeshafanya rasmi utambuzi wao. Kwa hivyo utambuzi wa Ulaya utaleta tofauti gani kwa uvamizi wa Kiyahudi wa Palestina? Palestina haihitaji kutambuliwa. Inahitaji uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu. Wakati umefika kwa dola yenye nguvu ya Kiislamu kama Pakistan, Misri au Uturuki kusimamisha Khilafah Rashida. Majeshi ya Pakistan lazima yachukue hatua na kusonga na Ummah kukomboa Al-Masjid Al-Aqsa.

17 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 25 Mei 2024 M

Mkuu wa Jeshi Azuru Ujerumani Huku Inasambaza Silaha kwa Umbile la Kiyahudi

Mnamo tarehe 24 Mei 2024, mrengo wa vyombo vya habari vya kijeshi ulisema kwamba, "Mkuu wa Majeshi yuko katika ziara rasmi katika Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani." Mnamo tarehe 11 Machi 2024, Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm ilisema, "Marekani inachangia asilimia 69 na Ujerumani kwa asilimia 30 ya uagizaji wa silaha wa ‘Israel.’" Huku Ujerumani ikisambaza silaha ambazo umbile la Kiyahudi hutumia kuwaua wanawake na watoto wa Gaza, mkuu wa jeshi akutana na makruseda. Khiyana ya uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Waislamu umevuka mipaka yote. Ni juu ya Umma wa Kiislamu na majeshi yake kuwang'oa wasaliti na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah Rashida ndiyo itakayokusanya majeshi kwa ajili ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa.

18 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 26 Mei 2024 M

Kashmir Itakombolewa Kupitia Jihad na Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan, Sio Kupitia Maazimio ya Umoja wa Mataifa

Mnamo tarehe 24 Mei 2024, Wizara ya Mambo ya Nje ilikataa amri ya Mahakama ya Upeo ya India iliyounga mkono uamuzi wa upande mmoja wa serikali ya Modi wa kukomesha hadhi maalum ya Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Kuunganishwa kwa nguvu kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na Dola ya Kibaniani ilikuwa ni mstari mwekundu. Majeshi ya Pakistan lazima yajipange kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu kwa njia ya Jihad. Walakini, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan kamwe hautawahi kuhamasisha vikosi vyetu vya kijeshi, kwa sababu wao ni vibaraka wa Marekani. Kashmir ni ardhi ya Waislamu na ukombozi wake ni wajibu wa Shariah. Khilafah kwa Njia ya Utume itakusanya majeshi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, huku ikimaliza utawala wa mfumo wa dunia wa Marekani.

19 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 27 Mei 2024 M

Youm-e-Takbir Halisi ni ile Siku ambayo Jeshi la Pakistan Litaangamiza Umbile la Mayahudi

Tangazo la likizo ya umma mnamo tarehe 28 Mei, Youm-e-Takbir, kusherehekea silaha za nyuklia za Pakistan linaongeza chumvi kwenye majeraha ya Waislamu wa Gaza. Kwa nini makombora ya balistiki hayawezi kulenga Tel Aviv, ili kutoa ulinzi kwa wanajeshi wa ardhini wa Pakistan, badala yake? Kwa nini kipote cha wanajeshi wa Kikundi cha Huduma Maalum (SSG) hawawezi kutumwa Misri, kuingia Gaza kupitia Kivuko cha Mpakani cha Rafah? Kwa nini wanajeshi wa kawaida hawawezi kutumwa Jordan, kuingia Ukingo wa Magharibi, kupitia Daraja la Al-Karameh? Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ng'oeni watawala hawa na kuvunja minyororo yao ya utaifa. Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir, ili Khilafah Rashida ikusanye silaha zetu na majeshi yetu kukomboa Al-Masjid Al-Aqsa.

20 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 28 Mei 2024 M

Kudai Haki kutoka kwa Makafiri ni Ishara ya Akili Dhaifu

Mnamo tarehe 24 Mei 2024, Waziri Mkuu alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kutekeleza mara moja uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya kukomesha uchokozi wa "Israel" huko Gaza. Je, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan hauoni uadui wa wazi wa mataifa ya Magharibi dhidi ya Waislamu, huku Ujerumani na Marekani zikiendelea kulipatia umbile la Kiyahudi silaha? Hivi kwa nini wanadai makafiri watekeleze uamuzi wa mahakama, kana kwamba walishawahi kuutekeleza hapo awali? Waislamu daima wanawataka watawala kutabikisha amri ya Mwenyezi Mungu ﷻ

[وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah, 2:191]. Khilafah kwa Njia ya Utume itatabikisha mara moja amri ya Mwenyezi Mungu ﷻ, kuyakusanya majeshi ya Waislamu bila kuchelewa.

21 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 29 Mei 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu