Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 22/05/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 14 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na 22 Mei 2024 M

Ama kuhusu “Mashirika ya Kimkakati Yanayomilikiwa na Serikali (SOEs),” Uislamu Unaharamisha Ubinafsishaji wa Mali ya Umma, Huku Unahakikisha Utawala wa Serikali juu ya Sekta ya Kijeshi

Mnamo tarehe 12 Mei 2024, Waziri wa Fedha alisema kuwa "hakuna kitu" kama mashirika ya kimkakati yanayomilikiwa na serikali (SOEs), huku akisisitiza haja ya ubinafsishaji. Mtawala huyu duni anasema anachohitaji ili kuhakikisha utiifu kwa amri za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kuhusu ubinafsishaji. Je, watu wa Pakistan hawalipii gharama ya ubinafsishaji wa sekta ya nishati, iliyoamriwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia, katika miaka ya tisiini ya karne iliyopita? Kwa kuongezea, deni la mzunguko limesimama kama mlima mrefu mbele yao. Kwa mujibu wa Uislamu, mali ya umma, kama vile nishati na madini, hairuhusiwi kubinafsishwa. Kwa kuongezea, serikali inatawala sekta za kimkakati kama sekta ya kijeshi.

08 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 16 Mei 2024 M

Watawala wa Pakistani Hawalindi Hata Maadili ya Kiislamu

Bendi ya muziki ya Marekani inayoendeleza mapenzi ya jinsia moja, "Raining Jane," ilitumbuiza nchini Pakistan mnamo tarehe 8 Mei 2024 katika Chuo cha Kitaifa cha Sanaa ya Maonyesho. Ziara ya bendi ya wafisadi ni sehemu ya Mpango wa Diplomasia ya Muziki wa Kilimwengu wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani. Waislamu wa Pakistan walikataa ukoloni huu wa kithaqafa na kulazimisha kughairiwa onyesho la bendi hii ya Marekani katika Baraza la Sanaa la Karachi na Chuo Kikuu cha Serikali cha Lahore. Kwa hivyo, kwa nini mpango huo uliruhusiwa na watawala wa Pakistan kwanza, wakati ajenda yake ya kiliberali inajulikana? Utawala huu unajenga uhusiano wa kithaqafa na utawala wa Biden, ambao mikono yao imelowa damu ya Gaza. Usaidizi wa kijeshi wa Marekani na kifedha wa umbile la Kiyahudi umehakikisha mauaji ya halaiki huko Gaza. Umefika wakati sasa wa kuwaondoa watawala hawa duni na kusimamisha Khilafah Rashida.

09 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 17 Mei 2024 M

Ugavi wa Madaraka katika Demokrasia Unaharibu Utawala kwa Kusababisha Migongano baina ya Taasisi

Kesi ya Mahakama ya Upeo iliyosikilizwa mnamo tarehe 16 Mei 2024, kuhusu uwajibikaji wa waziri mkuu wa zamani, ilishindwa kupiga hatua yoyote katika kumaliza machafuko ya kisiasa. Kuna machafuko kwa sababu ya mgongano kati ya uongozi wa kijeshi, nguvu ya kisiasa na upande wa mahakama. Mivutano ya mamlaka baina ya taasisi imeharibu utawala. Machafuko hayo yanasababishwa na jaribio lililoshindwa la kuleta utulivu wa Demokrasia kwa njia ya ugavi wa mamlaka. Bunge limekuwa uwanja wa kejeli na matusi. Katika Uislamu, Khalifa pekee ndiye serikali. Badala ya ugavi wa mamlaka, mamlaka yanatolewa na Ummah kwa Khalifa kupitia Bayah ya Kisharia, na anawajibika kwa kila suala. Khilafah ni mfumo wa utawala imara, huku demokrasia inakabiliwa na machafuko na mgawanyiko wa ndani.

10 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 18 Mei 2024 M

Kipote cha Watawala Wafisadi Huhamisha Mali Nje ya Nchi ili Kukimbia Serikali Inayozama

Mnamo tarehe 16 Mei, 2024 iliripotiwa kuwa watu 17,000 miongoni mwa watu wakubwa wa Pakistan, wakiwemo majaji, majenerali, wanasiasa na warasimu, wana mali yenye thamani ya dolari bilioni 12.5 jijini Dubai pekee. Mali hizi ni kando na mali zao zaidi zilizo nchini Marekani, Ulaya na Australia. Ni uthibitisho wa kufeli kabisa kwa serikali. Wanaohusika na uendeshaji wa serikali hii wanaogopa kuwekeza ndani yake. Badala yake, wanapendelea kuomba Mfuko wa Fedha Duniani dolari bilioni kadhaa. Ni wakati sasa wa kubadilisha mfumo huu wa unaozama. Umefika wakati sasa wa kusimamisha Khilafah Rashida ambayo itakamata mali zilizoporwa kutoka kwa mafisadi na kukusanya mali ya Ummah kuangalia mambo yake.

11 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 19 Mei 2024 M

Bila ya Khilafah, Waislamu ni Wageni katika Ardhi Zao Wenyewe

Mnamo tarehe 18 Mei 2024, Wizara ya Mambo ya Nje ilisema, "Serikali ya Pakistan imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Kyrgyzstan ili kuhakikisha usalama wa raia wake walio hatarini kutokana na ghasia za umati wa watu za jana usiku katika Jamhuri ya Kyrgyzstan. ” Sababu iliyotolewa kwa hili ni mzozo ulioanza na mapigano kati ya wanafunzi kutoka Misri na Kyrgyzstan. Hoja yoyote ile itakayokuwa, mipaka ya dola za kitaifa husababisha chuki miongoni mwa Waislamu dhidi ya Waislamu wengine. Chuki ya utaifa inazuka kwa uwepo wa ndugu wa Kiafghan nchini Pakistan, Wasyria nchini Uturuki, Wapalestina nchini Misri na Warohingya nchini Bangladesh. Mwisho wa chuki hii unawezekana tu kwa kuasisiwa Khilafah Rashida. Khilafah itafuta mipaka ya dola za kitaifa kati ya Waislamu. Itawaunganisha Waislamu kama dola yenye nguvu zaidi duniani.

12 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 20 Mei 2024 M

Marafiki wa Modi nchini Pakistan Wameizika Kashmir na Kujitahidi Kuhalalisha Mahusiano na Dola ya Kibaniani

Mnamo tarehe 18 Mei 2024, Waziri wa Mambo ya Nje alilalamika, "India iliamua kutoza ushuru wa asilimia 200 kwa bidhaa kutoka Pakistan, ilisimamisha huduma ya basi la Kashmir na biashara katika Mstari wa Udhibiti." Hii ina maana kwamba watawala wa Pakistan kiasili hawana pingamizi ya kuhalalisha mahusiano na India. Hawajali kuhusu kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir katika Dola ya Kibaniani. Watawala hawa wako tayari kuiinamia Dola ya Kibaniani kwa sababu ya maagizo ya Marekani. Watawala wa Pakistan walikuwa wamefanya makubaliano ya kuisalimisha Kashmir huko Washington, siku chache kabla ya Modi kuiunganisha kwa nguvu Kashmir mnamo Agosti 2019. Kisha watawala wa Pakistan wakatekeleza usitishaji vita mnamo Februari 2021. Enyi Waislamu! Waondoeni marafiki hawa wa Modi na musimamishe tena Khilafah Rashida nchini Pakistan.

13 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 21 Mei 2024 M

Waziri wa Mambo ya Nje Yuala Njama na Uturuki Kuusaliti Msikiti wa Al-Aqsa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alikutana na mwenzake kutoka Uturuki mnamo tarehe 20 Mei 2024, kujadili suluhisho la Marekani la dola mbili kwa Palestina, ambalo linasalimisha sehemu kubwa ya Palestina chini ya uvamizi wa Kizayuni. Kwa dhambi alipuuza kupanga shambulizi la pamoja dhidi ya Mayahudi, pamoja na mashambulizi ya droni za Pakistan na Uturuki na ndege za kivita, kuanzisha eneo lisiloweza kuruka ndege kwa Wazayuni, kufungua Kambi ya Anga ya Uturuki ya Incirlick kwa Jeshi la Anga la Pakistan na kizuizi cha jeshi la majini cha Bahari Nyekundu. Hakutoa hata onyo la shambulizi la kombora, au hata tishio la maneno tu, dhidi ya umbile la Kizayuni, ingawa kila nchi ina uwezo wa kuukomboa Al-Masjid Al-Aqsa peke yake. Ni wazi kwamba njia ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa inaanza na ukombozi wa Islamabad kutoka utumwa wa Marekani.

14 Dhu al-Qa’adah 1445 H - 22 Mei 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu