- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina pamoja na Wanaume, Wanawake, na Koo
Yatangaza Kukataa katakata Sheria ya Ulinzi wa Familia na CEDAW!
Katika mkusanyiko mkubwa wa taadhima uliofanywa na Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina mnamo siku ya Jumatano, Machi 23, 2022, watu wa Palestina walitangaza kukataa kata kata Sheria ya Ulinzi wa Familia inayotokana na CEDAW, ambayo Mamlaka ya Palestina inakusudia kuiidhinisha.
Wazungumzaji hao waliwasilishwa na Dkt. Musab Abu Arqoub, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina, ambaye aliikashifu Mamlaka ya Palestina kama yenye kufisidi ardhi katika azma yake ya kupitisha CEDAW na Sheria ya Kulinda Familia. Abu Arqoub alielezea CEDAW na Sheria ya Ulinzi wa Familia kuwa ni vita dhidi ya Umma wa Kiislamu, dini yake na thaqafa yake, na kwamba hatutasimama kama watazamaji katika vita hivi.
Kisha ikafuata hotuba na misimamo ya wanawake na koo za watu wa Palestina, hivyo mwalimu mwema Umm Abdullah akazungumza kwa niaba ya wanawake wa Palestina na kusisitiza kwamba wanawake wa Palestina leo wanasimama na baba zao, watoto wao, waume zao na kaka zao katika kukataliwa CEDAW na Sheria ya Uharibifu wa Familia. Umm Abdullah alisema, "Sisi, wanawake wa sahihi wa Palestina tunajivunia dini yetu na sheria ya Mola wetu... Ama kundi lile la wahuni ambalo haliko katika dini yetu na sheria ya Mola wetu linalodai kutuwakilisha, tunawakataa na wala hawatuwakilishi."
Alihutubia jumuiya za wanawake zinazofadhiliwa na nchi za Magharibi kwa kusema: "Nyinyi hamtuwakilishi sisi wala wanawake wa Palestina... Anayetuwakilisha ni yule anayehifadhi hadhi yetu na kulinda heshima yetu, na sisi haturidhiki na chochote isipokuwa Uislamu. na hukmu zake zinazotutawala... Heshima ya baba zetu, kaka zetu, watoto wetu wa kiume na wa kike inalindwa na hukmu za Uislamu na Sharia ya Mwingi wa Rehema. Magharibi, ambayo iliyowaajiri nyinyi, ndiyo inayosibiwa na maangamivu ya uasherati na uchafu... Ndiyo inayohitaji kung'oa hadhara yake na masuluhisho yake yaliyofeli, na ndiyo inayokosa sheria ya kiwahyi inayoregesha mizani ya usawa kwa wanadamu wote."
Kisha koo za watu wa Palestina zikatangaza msimamo wao waziwazi wa kukataa makubaliano ya CEDAW, kwa hivyo Hajj Abdul-Wahhab Ghaith, mwakilishi wa koo hizo akazungumza na kusema kuwa tukio hilo lilikuwa zito na linahitaji kauli ya mwisho, akisisitiza kuwa watu wa Ummah huu wanakataa makubaliano ya CEDAW na kwamba watu wa Ummah ndio wafanyaji maamuzi, na kwamba sheria ya ulinzi wa familia haitapita.
Viongozi kadhaa mashuhuri kutoka koo za Palestina walitangaza kukataa kwao vikali CEDAW na jaribio linaloendelea la Mamlaka ya Palestina kupitisha sheria hizo angamivu kwa watu wa Palestina zinazohujumu muundo wa familia na maadili yake.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina
Sehemu ya Amali
- Click to open image! Click to open image!

https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/palestina/2242.html#sigProIda65e6eae29
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Iliyobarikiwa - Palestina
Facebook: Hizb ut Tahrir / Iliyobarikiwa - Palestina