Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Hotuba ya Halaiki

"Utafutaji Nyuma ya Wamagharibi Hufisidi Dunia na Akhera"

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa hotuba ya halaiki katika jimbo la Qadarif (Gedarif) mnamo 14/08/2020 kwa anwani: "Utafutaji Nyuma ya Wamagharibi Hufisidi Dunia na Akhera" baada ya swala ya Ijumaa pambizoni mwa Msikiti wa Zamani na mbele ya Uwanja wa Uhuru katika soko la Qadarif; ambapo Mhandisi Al-Bashir Ahmed Al-Bashir aliihutubia hadhira akiashiria hamu ya serikali zote mtawalia ya kuiridhisha Magharibi na kutabikisha mipango yake kwa gharama ya maisha ya watu na Aqeedah yao. Hii hapa serikali ya sasa inaendelea kuwasilisha kwa makafiri wa Magharibi kupitia kujibu maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ya kufanya marekebisho bajeti jumla, ambapo kwa mujibu wake ruzuku ya mafuta itapanda kwa asilimia 75 na umeme kwa asilimia 41, na vilevile sarafu kuelea na kupelekea ongezeko la bei na kurahisisha kuporwa wa utajiri wa nchi kupitia malighafi nafuu.

Hotuba hii ya halaiki ilishuhudia hadhira na maingiliano mazuri kabisa, ambapo hadhira ilipiga takbira na tahlil, bali baadhi yao wakataka kwamba wafanyiwe hotuba kama hizi katika mitaa na vijiji, na wakasema haya ni maneno mazuri na ni wajibu kila mmoja kuyasikia.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu