- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 03/08/2022
Muendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika maeneo tofauti ya nchi ili kupata maoni ya umma kuhusu hukmu za Uislamu (Ahkaam Shariah) na masuluhisho yake yanayohusiana na mifumo tofauti tofauti ya maisha, ambayo yanakabiliana na mapigano ya hivi majuzi ya kikabila katika eneo la Blue Nile, na tatizo la kilimo cha kutegemea mvua katika eneo la Gadharef.
Mnamo Julai 21, 2022, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika uwanja wa Al-Hurriya huko El-Obeid, kwa anwani: "Mapigano ya Kikabila, Sababu Zake, Chanzo, na Utatuzi wake," ambapo Ustadh Muhammad Qoni alizungumza kuhusu mapigano kati ya makabila ya Funj na Hausa katika Jimbo la Kusini mwa Blue Nile, idadi ya waliofariki na kujeruhiwa, na miitiko iliyotoka kwa wafuasi wa makabila hayo mawili katika miji na sehemu tofauti za nchi, kama vile maandamano, kufungwa kwa barabara, uharibifu na uchomaji wa makao makuu na afisi za serikali. Kuhusu muitiko wa serikali, haufikii kiwango cha wajibu iliyokabidhiwa kwake. Mzungumzaji pia alizungumzia sababu za tatizo hili lililoanzishwa na Kafiri mkoloni anayewakilishwa ndani ya mfumo wa Hawaker unaogawanya Ardhi kwa misingi ya kikabila, ambapo iliwafanya watu kujifunga na kabila na ardhi. Kanuni ya msingi ni kwamba watu wanafungamanishwa na fungamano la imani ya Kiislamu, na kuifanya kuwa msingi wa kupata haki na majukumu. Imani hii inaharamisha umwagaji damu na ugomvi.
Kuhusu mzozo na mapigano ya kikabila katika Jimbo la Blue Nile vilevile, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Al Kalakila, Uwanja wa Al Wahda 6, baada ya swala ya Ijumaa mnamo Julai 22, 2022, yenye kichwa: “Mapigano ya kikabila na Mtazamo wa Uislamu”, ambapo Mhandisi Basil Mustafa alizungumzia uhusiano wa wachungaji na wakulima na mzozo wa ardhi baina ya makabila mbalimbali unaotokana na mfumo wa Hawakir ulioasisiwa na mkoloni MUingereza ili kuwe na mgawanyiko na fitna baina ya Waislamu katika hili, na ni Dola ya Khilafah Rashida pekee ndiyo inayoweza kukomesha umwagaji damu wa mapigano haya ya kikabila.
Katika muktadha huo huo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika vyuo vikuu mnamo tarehe 23 Julai, 2022 katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Mafunzo ya Kiuchumi na Kijamii, yenye kichwa: “Mapigano ya Kikabila… Sababu na Masuluhisho”, ambapo mhandisi Ahmed Jaafar alieleza kuwa mapigano katika jimbo la Nile Azraq yalianza pale kabila la Hausa lilipoomba kuwa na imarati yao, na ombi hili likakataliwa na makabila ya eneo hilo, hususan kabila la Alberta, kwa kisingizio kwamba Wahausa hawana haki ya kumiliki ardhi hiyo, na kwa sababu hiyo, mapigano yakaanza kati ya makabila hayo mawili.
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Madani pia walifanya mkutano wa hadhara kwenye kituo cha mabasi katika Soko Kuu mnamo Julai 26, 2022 wenye kichwa: "Khilafah Huwayeyusha Watu, na hakuna nafasi ya mapigano ya kikabila au ya kieneo" , ambapo Ustadh Abdel Aziz alizungumza, akieleza kuwa fungamano baina ya Waislamu lazima lijengwe juu ya imani ya Kiislamu.
"Kilimo cha kutegemea mvua ... ukweli mchungu", chini ya mada hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika mji wa Gadharef mnamo Julai 28, 2022 ambapo Ustadh Muhammad Mukhtar alizungumza kuhusu uwezo wa kimaumbile wa kilimo eneo la Gadharef hasa, na Sudan kwa ujumla. Nini linayoifanya Sudan kuwa kapu la chakula la dunia, ambako kuna ardhi yenye rutuba, mvua na mito, na kisha kukabiliana na ukweli mchungu unaowatesa wakulima wa ushuru, kodi na kupuuzwa kwa makusudi kuwa mwathirika wa benki za biashara zinazolinyonya hitaji lake kuongeza faida zao.
Chini ya kichwa: "Matukio ya Blue Nile na moto wa uchochezi mkali", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Khartoum mnamo Julai 28, 2022, karibu na bandari ya ardhini jijini Khartoum. Matukio haya ya kusikitisha si mapya, bali yanajirudia mara kwa mara, na sababu za kweli za kuibuka kwa mizozo hii mwanzo ni uangalizi mbovu wa dola, na kutoweza kwa sheria zinazotekelezwa kutatua matatizo ya watu, ikiwemo Sheria ya Idara ya Wanati, sheria za ardhi, na watu kufungamana kwa misingi ya kikabila na kieneo. Serikali na mavuguvugu ya kisilaha wanachochea moto wa fitna katika utabikishaji wa mipango ya wakoloni makafiri.
Kwa kumalizia, waliohudhuria walionyesha uwajibu wa kufanya kazi ya kuunda dola hii uwanjani, kwa kufanya kazi na wafanyikazi ili kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah of Sudan
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/2460.html#sigProIdea267b792a