Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kongamano la Kisiasa la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Jijini Omdurman Muundo wa Makubaliano na Changamoto ya Khilafah 

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya kongamano la kisiasa lenye kichwa: “Muundo wa Makubaliano na Changamoto ya Khilafah”, mnamo Ijumaa, tarehe 29 Jumada al-Awwal 1444 H, sawia na 12/23/2022 M, katika uwanja wa Al-Thawra Al-Hara 42 huko Omdurman, wazungumzaji ni pamoja na Ustadh Nasser Ridha - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, Ustadh Ahmed Abkar, Mjumbe wa Kamati ya Wilaya ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, na Ustadh Ibrahim Othman ( Abu Khalil), Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan.

Ustadh Muhammad Jami' (Abu Ayman) - Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, mwendeshaji wa kongamano hilo, aliikaribisha hadhira tukufu, na Sheikh Siddiq Qasim Al-Sayyid - Mwanachama wa Hizb ut Tahrir akasoma aya za Qur'an Tukufu, kisha Ustadh Nasser Ridha aliwasilisha karatasi ya kwanza yenye kichwa: “Muundo wa Makubaliano ni mangati katika jangwa ambalo mwenye kiu hudhani kuwa ni maji,” ambapo Ustadh Nasser alitaja msingi ambao Muundo huo wa Makubaliano umegemea. Ni katiba ya usimamizi wa mawakili, inayoonyesha kuwa katiba hii iliandikwa nje ya nchi na kwamba dhamira ya muundo wa makubaliano na katiba ambayo msingi wake ni kupiga marufuku Uislamu na kuunda maisha ya Waislamu wa Sudan kwa msingi wa kutenganisha dini na maisha, kutekeleza mifumo dhalimu ya Kikafiri ya kibepari kwa watu, na kuvunja umoja wa nchi na kuusambaratisha kwa mfumo wa ufederali, na kuidhinisha Hawakir, kisha kukabidhi utajiri wa nchi kwa wale wanaowaita wawekezaji wa kigeni, akitoa mfano katika Wadi Al-Hawad na bandari ya Abu Amama.

Waraka wa pili uliowasilishwa ulikuwa kwa kichwa: "Mtazamo wa Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah," Wakili Ahmed Abkar alizungumzia jinsi maisha ya Kiislamu yanavyopaswa kuwa, akielezea ufisadi wa vifungu na sheria ambazo nchi inazifuata sasa kupitia katiba zilizotungwa na mwanadamu ambazo zinagongana na Dini ya Ummah, kwani alisisitiza kuwa kanuni ni kwamba maisha lazima yasimamishwe. Kwa Waislamu kwa msingi wa imani ya Kiislamu, akionyesha kwamba Hizb ut Tahrir inawasilisha kwa Ummah rasimu ya katiba iliyotolewa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw). Kisha akazungumzia baadhi ya ibara zinazothibitisha kuwa katiba hii ndiyo inayojenga maisha ya staha yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Katika waraka wa tatu na wa mwisho, Ustadh Abu Khalil alizungumzia nadharia ya kusimamisha dola ya Khilafah kuwa ndiyo dola pekee ya Waislamu, akifafanua nadharia hii kwa dalili ya Kisharia, akiwataka waliohudhuria kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah, ambayo kwayo Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba yenye ibara 191 zinazodhibiti nyanja zote za maisha; katika utawala, uchumi, mfumo wa kijamii, sera ya elimu, sera ya kigeni na mengineyo hadi maisha yarudi kuwa maisha ya Kiislamu. Na Khilafah hii ni wakati wake umewadia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi kurudi kwake, kama vile Mtume (saw) alivyotoa bishara njema ya kurudi kwake kama Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ili kusoma Hotuba nzima ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan: Bonyeza hapa.

Kisha fursa ikafunguliwa ya michangio, na maimamu kadhaa wa misikiti na wengineo wakazungumza, wakisifia kile ambacho hizb imekifanya, kuunga mkono yale ambayo hizb iliwasilisha katika kongamano hili, na kutoa wito wa kuendelea kwa makongamano haya. Alhamdulilah, Mola Mlezi wa walimwengu wote kwa mafanikio Yake.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu