Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Muendelezo wa Unyonyaji wa Kikoloni Barani Afrika

Na: Fatima Musab*

Mnamo 2019, Luigi Di Maio, aliyekuwa naibu wa waziri mkuu wa Ufaransa na waziri wa masuala ya kigeni kwa sasa alisema “Ufaransa ni miongoni mwa nchi ambazo zinachapisha fedha kwa nchi 14 za Afrika ikizuilia ukuaji wao wa kiuchumi na kuchangia ukweli kwamba wakimbizi wanatoka na kisha kufa baharini ama kufika katika pwani zetu.” Hili ni tamko muhimu sana lililo lengwa shirika la CFA franc barani Afrika.

CFA franc, Iililoanzishwa 1945, ni jina la sarafu mbili, CFA franc ya Afrika Magharibi, inayotumika ndani ya nchi nane za Afrika Magharibi, na CFA franc ya Afrika ya Kati, inayotumika katika nchi sita za Afrika ya Kati. Sarafu zote mbili zinadhaminiwa na Hazina ya Ufaransa. Na natija yake, benki kuu ya Ufaransa (Banque de France) ilizuilia hifadhi za nchi 14 za Afrika na kuwalazimisha kuchangia “dola bilioni 500 kila mwaka” kwa hazina ya Ufaransa kama malipo ya “deni la ukoloni”.

Nchi hizi zililazimishwa kupitia mkataba wa kikoloni kutumia “pesa za kikoloni za ufaransa” na kuweka asilimia 85 ya hazina za kigeni chini ya uangalizi wa waziri wa fedha wa Ufaransa. (Chanzo: Ripoti)

Mnamo Disemba 2019, Ufaransa ilitangaza kwamba nchi nane za Afrika Magharibi za Muungano wa Kifedha na Kiuchumi wa Afrika Magharibi (WAEMU) zitabadilisha jina lao la CFA franc kuwa Eco.

Hili lilipitishwa kote kama mageuzi makubwa ya kisarafu, ambayo yangepunguza udhibiti wa Ufaransa juu ya Afrika, kwa kiasi kwamba hawataweka tena nusu ya hifadhi zao za kigeni nchini ufaransa, hali hiyo sio rahisi kama inavyo dhaniwa. Wala haikomboi eneo hilo kutokana na udhibiti wa Ufaransa.

Kulingana na Jarida la Wall Street, hatua hii inaonesha kwamba Ufaransa “imeinama kwa shinikizo la watu wengi wa Afrika Magharibi kwa kukubali kuondoa jina la CFA franc na kulegeza usimamizi wake wa muungano wa sarafu huku Paris ikitafuta kurekebisha mahusiano yake na nchi zalizokuwa koloni zake za Afrika.” Hata hivyo, “Ufaransa bado itakuwa na nguvu muhimu katika eneo hilo kupitia sarafu na uwepo wake wa kijeshi huko.”

Pia inapaswa itambulike kwamba, nchi hizo 6 za Afrika ya Kati bado zimefungika na mkataba huu na masharti yake.

CFA Franc:

Ufaransa unawaruhusu kupata asilimia 15  pekee ya pesa katika mwaka wowote. Kama watahitaji zaidi ya hiyo, itawabidi kuomba hiyo ziada kutoka kwa asilimia 65 ya pesa zao wenyewe kutoka kwa hazina ya Ufaransa kwa viwango vya kibiashara. Ufaransa iliweka kiwango juu ya idadi ya fedha nchi hizo zaweza kuomba kutoka kwa hifadhi. Kiwango ni maalumu cha asilimia 20 ya mapato ya taifa katika mwaka uliotangulia. Kama nchi itataka kuomba zaidi ya asilimia 20 ya pesa zao wenyewe, Ufaransa ndio iko na usemi wa mwisho. (Chanzo)

Hii inamaanisha kuwa nchi 14 za Afrika hazina sera huru za kifedha. Hawana haki ya maamuzi ya kimsingi juu ya kiasi gani cha sarafu cha kukiingiza katika uchumi wao ama kubadilisha thamani ya sarafu yao wanavyo taka. Maamuzi yote yanayo husiana na sera za kifedha yana dibithiwa na Paris. Hizi nchi pia zimelazimishwa kuweka asilimia 65 ya hifadhi zao za kigeni katika benki kuu ya Ufaransa. Zaidi ya hivyo, hizi nchi haziwezi kupata pesa hizi vile zinavyo taka. Kihakika, kama wanahitaji zaidi ya asilimia 20 ya hii asilimia 65, watazichukua kama mkopo kutoka kwa Ufaransa kulingana na bei ya soko iliyoko kwa wakati huo. (Chanzo: https://www.geopolitica.info/tag/french-colonial-pact/)

Eco:

Eco bado inadhaminiwa na Ufaransa na ikaambatanishwa na euro. Kulingana na Jarida la Wall Street, maelezo yake bado hayajakamilishwa lakini ni wazi kwamba nchi hizo bado zitashirikiana katika habari za kila siku pamoja na Paris. Ufaransa pia inaweza kuteua mwanachama huru katika kamati ya sera za fedha hata kama mgombea hatawakilisha Ufaransa wala hana jukumu la kuripoti. Kama hifadhi ya nchi itashuka chini ya kiwango fulani, Ufaransa inaweza kuomba kwamba mwakilishi aregeshwe kwa shinikizo kuwa kushirikiana katika habari za kila siku na Paris kutaendeleza kamati ya sera za fedha ya Eco.

Dola hizo 8 hazitahitajika kuweka nusu ya hifadhi zao katika hazina ya Ufaransa. Hata hivyo, ni wazi kutokana na masharti mengine kwamba Ufaransa haijaachana na  udhibiti juu ya eneo hilo.

Suala ni kwamba Ufaransa unadumisha udhibiti wa koloni zake, hata baada ya kuondoka.

Sarafu ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya ukoloni, ambayo Ufaransa ilitoa wito kwa nchi za Kiafrika kuyatia saini walipotaka uhuru. (Video ya Ripoti ya Atlantis). Ufaransa ikatoa pendekezo kwamba wanaidai Afrika “deni la ukoloni” kwa manufaa ambayo ukoloni wao uliyaleta.

Hili linaonekana kupitia ukweli kwamba, wakati Guinea ilipoamua kutaka uhuru kutoka kwa himaya ya Ufaransa mnamo 1958, serikali ya Charles de Gaulles ilitoa zaidi ya wafanyikazi wa ummah 4,000, mahakimu, walimu, madaktari, na wanaufundi, na kuwaelezea kuhujumu kila kitu kilichobaki. Wakachukua mali zao na kuharibu kile ambacho hawakuweza kuondoka nacho, hivi ikiwemo shule, majengo ya utawala wa ummah, magari, vitabu, madawa na vifaa vya vituo vya utafiti (Riport ya Afrika). Hili lilifanywa kwa lengo la kuonesha koloni zingine ubaya wa athari ya kutaka uhuru ulivyo.

Kuna ripoti kwamba kama kiongozi wa nchi atakataa kulipa kodi ya ukoloni, atauwawa na majeshi ya kigeni. Kulingana na ripoti, katika miaka 50 iliyopita, jumla ya mapinduzi 67 yametokea katika nchi 26 barani Afrika, nchi 16 miongoni mwazo ni zile zilizokuwa koloni za Ufaransa, hii inamaanisha asilimia 61 ya mapinduzi yametokea katika nchi zilizo koloniwa na Ufaransa barani Afrika.

Ili kutekeleza mipango ya CFA franc, inasemekana, Ufaransa kamwe haijasita kung’oa wakuu wa nchi wanaojaribu kujitoa katika mfumo. Wengi waliondolewa afisini ama kuuwawa kwa kuwapendelea viongozi watiifu wanaokwea mamlaka kwa nguvu kuje moto ama mawimbi, kama inavyo onyeswa na mataifa ya CAEMC na Togo. (Chanzo: Brookings)

Pia wako na kitu kinaitwa “Makubaliano ya Ulinzi” yalioambatanishwa na makubaliano ya kikoloni, ambayo Ufaransa iko na haki za kisheria kuingililia kati kijeshi katika nchi za Afrika, na pia kuweka vikosi vya kijeshi kudumu katika kambi na vituo vya kijeshi katika nchi hizo, vikiendeshwa kikamilifu na Ufaransa. Kuna uwajibu wa kuitumia Ufaransa salio la kila mwaka na ripoti ya hifadhi. Bila ya ripoti hii, hakuna pesa. Kando na hili, Ufaransa iko na haki ya kwanza katika rasilimali asili ambazo zinapatikana katika ardhi zilizokuwa koloni zake. Dola za Afrika zinaruhusiwa kutafuta washirika wengine pekee iwapo tu Ufaransa itakuwa haina haja ya rasilimali hizo.

Kwa kutazama ushahidi huu, ni wazi kwamba hmakubaliano haya ya kikoloni yalikuwa kwa manufaa ya Ufaransa wala si Afrika.

Mnamo Machi 2008, Aliyekuwa Raisi wa Ufaransa Jacques Chirac alisema: “Bila Afrika, Ufaransa itateleza hadi katika hadhi ya dola za ulimwengu wa tatu”. Sarafu hizi zilizinduliwa kwa “haja ya Ufaransa ya kukuuza ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa koloni zake chini ya utawala wake, na hivyo kudhibiti rasilimali zao, muundo wa kiuchumi na mfumo wa siasa”. (Chanzo: wavuti wa LSE).

Hili likuwa wazi kutokamana na kukata tamaa ambako Ufaransa ilidhihirisha wakati wa kushughulikia nchi ilizozikoloni na mwito wao wa kutaka uhuru.

Huku kukiwa na ushahidi kwamba wasomi wa Kiafrika wananufaika kutokana na machaguo haya na hivyo kusaidia eneo la CFA, nchi na watu wake hawanufaiki. Hakika, dola 14 zilizotia sahihi makubaliano ya Kikoloni ni miongoni mwa nchi zilizo na “Maendeleo ya Chini ya Kibinadamu’ na ni dhaifu kiuchumi.

Huku watetezi wa eneo la CFA franc wakikubaliana kwamba sarafu hii inapeana kipimo cha utulivu wa kifedha, wengine wanasema kwamba katika ubadilishanaji kwa udhamini unaopeanwa na hazina ya Ufaransa, nchi za Kiafrika zinaelekeza pesa zaidi kwa Ufaransa kuliko wanazopokea kama msaada. Kwa nchi kuendelea kiuchumi, zinahitajika kuachana na sarafu hizo. (Chanzo: BBC). Kwa mujibu wa makala ya Brookings, “CFA franc ni kikwazo kwa ukuaji wa viwanda na mabadiliko ya kimiundo, isiyo hudumu kama kichochezi cha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi zinazotumia sarafu hiyo, wala kuongeza mikopo ya benki kwa uchumi”. Pia inashajiisha kuchururika kukubwa kwa mtaji kwenda nje.

Nguvu za kikoloni zimekwisha, Unyonyaji bado haujakwisha na mabadiliko hayatokuja bila kubadilisha mfumo mzima wa Kimagharibi.

Nchi za Kimagharibi zinadai kwamba zama za ukoloni zimekwisha na unyonyaji wa kikoloni ni jambo la zamani. Mfano huu unaonesha kwamba, madai hayo yako mbali na ukweli – Ufaransa inaweza kuwa sio himaya rasmi tena, lakini wamedumisha udhibiti juu ya mataifa na kuhakikisha kwamba wanafaidika kwa gharama ya watu wa Afrika.

Kubadilisha sheria, kuwaondoa viongozi, kuasisi mahakama za Kiislamu katika nchi za kidemokrasia hakutoweza kubadilisha hali kama mfumo wa kirasilimali utabakia kuwepo, ukiziruhusu dola zenye nguvu na kikundi cha wasomi wao kuzitumia nidhamu za kisiasa, kiuchumi na kisheria kwa manufaa yao.

Ili kubadilisha hali hizi, tunahitajika kubadilisha mfumo. Hii inamaanisha kuuondoa mfumo wa Kibepari katika ngazi ya utawala na kuubadilisha na mfumo wa Kiislamu.

(اللّهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُواْ يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّوُرِ وَالَّذِينَ كَفَرُواْ أَوْلِيَآؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ أُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ)

“Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni mashet’ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni na humo watadumu.” [Al Baqarah: 257]

* Mwanachama wa Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

* Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 294

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 14:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu