Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ziara Ya Biden Hadi Tulsa Haitafuta Aibu ya Mauaji Mabaya Kabisa ya Kiubaguzi wa Rangi ya Amerika.

(Imetafsiriwa)

Na: Abdullah Robin*

Raisi wa Marekani Joe Biden anataka kusafisha sura mbaya ya Marekani ndani na  nje ya nchi baada ya kuchukua hatamu kutoka kwa Trump. Hata hivyo, kunamaanisha kuhutubia urithi muovu wa kihalifu ambao ulitokea kabla Trump kuingia madarakani na kwa hilo litaendelea kuchafua maelewano ndani ya Marekani baada ya kuondoka kwa Biden. Wiki iliopita, Biden aliadhimisha miaka 100 tangu tokeo la mauwaji ya halaiki ambayo kwa utaratibu yalimaliza jamii nzima ya watu weusi ndani ya Tulsa, Jimbo la Oklahoma. Mauwaji ya watu wenye rangi nyeusi yalikuwa yamefutwa katika vitabu vya historia, lakini yaliibuka tena mwaka jana katika maandamo ya “Black Lives Matter” ambayo yaliwasha moto ndani ya Marekani baada ya matokeo ya kuuwawa kwa watu wenye rangi nyeusi na askari.

Mnamo 1921, kundi la watu wenye rangi nyeupe lilivamia eneo Jirani la watu matajiri Wamarekani wenye rangi nyeusi ndani ya Tulsa,Oklahoma, na wakateketeza moto mabiashara, mikahawa, mabenki na majumba zaidi ya 1200 ya watu weusi. Vurugu hilo lilidumu kwa siku mbili. Askari walisaidiwa na takribani wakaazi 500 wa rangi nyeupe katika kuwazunguka na kuwakamata wanaume wote wenye ngozi nyeusi ili kuruhusu ubomozi wa maeneo Jirani ya watu weusi kuendelea bila pingamizi. Baadaye, karibia watu 10,000 waliachwa bila makao na 6,000 wakalazimishwa kuingizwa katika kambi za vizuizi, na zaidi ya watu 300 kuuwawa na miili yao kutupwa katika makaburi ya halaiki. Mwaka jana, Marekani iliamua kuanza kuangalia katika makaburi hayo, na miili 5 zaidi iligunduliwa baada ya hotuba ya Biden. “Baadhi ya dhulma ni zakutisha, zakutamausha, zenye uchungu sana, haziwezi kuzikika, hata kama tutafanya bidi kiasi gani,” Biden alisema, na akaendelea, “Isipokuwa kupitia ukweli inaweza ikaja tiba. Kwa sababu historia iko kimya, haimaanishi haikutokea, jahannamu ilifunguliwa, hakika jahannamu ilifunguliwa. Hatuwezi chagua kile tunachotaka kujua, na kile tusichotaka kujua... Naja hapa kujaza pengo la ukimya, kwa sababu katika ukimya kidonda kinazidi.

Mbunge wa Congress Jerrold Nadler, mwenyekiti wa kamati ya mahakama alisema, “Mauwaji ya Tulsa Greenwood yanaweza kuelezewa kama tendo la kumaliza jamii, ambayo hatimaye ilifutwa katika vitabu vya historia kwa miongo mingi.” Ni ajabu kwamba Biden mwenyewe hakutangaza utumwa, mateso na mauwaji ya watu weusi ndani ya Marekani kama mauwaji ya kikabila, ikizingatiwa kwamba mnamo Aprili alitambua mwanzo tukio la kihistoria wakati wa vita vya kwanza vya ulimwengu kama mauwaji ya halaiki.

 Mauwaji ndani ya Tulsa yalianza baada ya mwanaume wa ngozi nyeusi alipotuhumiwa kimakosa juu ya kumshambulia mwanamke mwenye ngozi nyeupe. Mwanaume huyo aliwekwa chini ya ulinzi na kukawa na vitisho vya kuwa atanyongwa bila mashtaka wala hukumu ya kisheria, hali ambayo ilikuwa ya kawaida, kisha watu 61 wakanyongwa bila mashtaka mwaka huo huku wengi wao wakiwa wenye rangi nyeusi. Wakati wakaazi wenye ngozi nyeusi walipo kusanyana wakishinikiza kuachiliwa kwake, wenzao wenye ngozi nyeupe wakajumuika kushinikiza kuadhibiwa kwake. Kisha mauwaji yakaanza. Licha ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa miaka 60 kabla, na katika miongo mingi ya mapambano ya haki za kiraia iliofuatia na sheria za usawa katika miaka ya 1960 na 1970, Wamarekani wenye ngozi nyeusi bado hawahisi usawa wala kuwa salama. Historia imenukuu tukio liitwalo “Uhamaji Mkubwa” ambalo lilikuwa ni kuhama kwa Waamerika milioni 6 weusi kutoka kusini hadi kaskazini mwa Marekani ili kukimbia mauwaji na ubaguzi wa kirangi ambao ulikuwa zaidi katika majimbo ya kusini ambamo mababu zao walikuwa watumwa.

Visa 4,743 vya mauwaji bila mashtaka ya kisheria vimenukuliwa kutokea katika miaka ya 1882 na 1968 nchini Amerika. Waathiriwa walinyogwa ama kuteketezwa, baadhi yao walikatwa vipande sehemu ya miili yao kama ukumbusho na mara nyingi watendaji na waangalizi walikuwa na ufahari juu ya kazi yao huku wakijipiga picha kwa kujifakhiri na waliofanya. Katika ripoti moja,” genge la zaidi ya watu mia moja wenye ngozi nyeupe…. Liliufunga mguu wa Mary, na kumuangika juu chini katika mti, wakamuingiza kwenye mafuta ya gari na kumwasha moto. Alikuwa bado yuko hai wakati mmoja katika genge hilo alipo tawanya wazi matumbo yake kwa kisu. Mtoto wake ambaye alikuwa bado hajazaliwa akaanguka chini kwenye ardhi, akakanyagwa na kumalizwa. Mwili wa Mary ulimiminiwa risasi zaidi ya mia moja.” Mary Turner alikuwa mtu mweusi, na kosa lake ni kutishia kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika katika mauwaji ya mume wake – ambaye mbeleni alinyongwa pamoja na watu wengine weusi bila mashtaka. Waathiriwa wengi wa mauwaji bila mashtaka walikuwa wenye ngozi nyeusi, wengine walliuliwa kwa kuwasaidia watu weusi na idadi halisi inawezekana ikawa zaidi ya hii, na watu wenye ngozi nyeusi bado wanauwawa.

Mwaka jana, Marekani ilishuhudia hali ya maandamano na kupinga maandamano, ghasia na uporaji baada ya kuuliwa George Floyd na askari ndani ya mji wa Minneapolis. George Floyed alikuwa mweusi na aliuwawa na mbaguzi wa rangi masiku kabla ya maadhimisho ya miaka 99 ya mauwaji ya Tulsa, ambayo yalikuwa yameanza kujulikana na wengi kwa mara ya kwanza. Wakaazi wa Tulsa walichora katika barabara, "Maisha ya watu weusi Yana Maana" katika barabara ambayo mauwaji yalitokea, na katika nchi wakati wa majira ya joto taharuki ikazidi na watu wakaanza kuzungumzia vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe. Miezi kadhaa baadaye, Meya wa jiji akapanga operesheni ya siri ya usiku kurudi kwenye barabara hiyo kwa kisingizio cha kuondoa kumbukumbu ya wale waliopoteza Maisha yao miaka iliyopita na sasa. Ubaguzi wa rangi ni hali halisi ya kila siku ya Waamerika wenye ngozi nyeusi ambao ni masikini zaidi, ambao hawajaelimika zaidi na wanaokufa wachanga kuliko Waamerika weupe. Katika kura za karibuni, 48% ya watu weusi walionyesha imani uchache ama kukosa imani kabisa kwamba polisi katika jamii yao wataamiliana na watu weusi na mweupe kwa usawa.

*Imeandikwa kwa Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 342

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu