Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Lini Mateso ya Waislamu wa Uyghur Yatakwisha?

Na: Ustadha Asiya Uyghur

(Imetafsiriwa)

Leo, nitawaambia kuhusu mojawapo ya sehemu iliyojaa uhalifu muovu zaidi na mauaji, ambapo mauaji ya halaiki yanafanyika, na watu wake wanateseka mateso ya kila aina, ya kisaikolojia na ya kimwili ambayo hata akili haiwezi ikayafikiria, na imekuwa kikamilifu jela la wazi licha ya zaidi ya milioni ishirini ya Waislamu wanaoishi hapo. Kwa maana nyengine, ni sehemu ambayo ubinadamu umesahaulika. Kutokana na taarifa chache nilizozisema, unaweza fikiria nazungumzia kuhusu Turkestan Mashariki. Ndiyo, hujakosea, ni Turkestan Mashariki ambayo inajulikana kwa tanzia ya watu wake katika mikono ya mamlaka ya makafiri Wachina. Mateso ya Waislamu wa Uyghur wanaoishi hapo hayajakoma hata kidogo japokuwa mateso yao yanaonyeshwa katika vyombo vya habari kote mara kwa mara. Njia za mateso zimetofautiana na kukua kwa namna isiyoweza kufikiriwa. Unaweza kuwa umesikia kuwa katika Turkestan Mashariki, watoto wa kiume wanauawa au wanapelekwa katika kambi za watoto kwa jina la shule ya chekechea kwa mradi wa kuwafanya kuwa Wachina, wanawake wanabakwa na kulazimishwa kufanya matendo maovu na miji yao ya uzazi kutolewa, Waislamu wote wamekatazwa kufanya ibada zao, hata kusalimiana “Assalaamu Alaykum” wakati wa kukutana kumekatazwa. Kwa ufupi, ni sehemu ambapo mauaji ya kimfumo yanafanyika kwa njia ambazo hazihesabiki, vitisho visivyoelezeka. 

China ya kikomunisti huchukua kila fursa kutimiza malengo yake. Na wakati huu; mauaji ya chini kwa chini ya Waislamu wa Uyghur pia yanafuata kwa kisingizio cha kukabiliana na virusi vya Korona. Zaidi ya siku arubaini zilizopita, Turkestan Mashariki yote ilikuwa ni sehemu iliyofungwa. Kiingilio cha kijiji, vichochoro na milango ya majengo na majumba ya kuishi katika mji huo yameunganishwa kwa vyuma na ni mhunzi pekee yake anaweza kuyafungua, kwa hivyo ni vigumu sana kwa yeyote kutoka nje ya nyumba. Wakati wa uamuzi wa “Karantini ya mji wa Ghulja” ulitolewa, kwa mfano, serikali ya China ilizuia wakaazi wa mji huo kutokwenda kokote, kumaanisha walilazimika kubaki walipo; ima barabarani, au malishoni au nyumbani na hawafai kwenda sehemu yoyote ile, hata kurudi nyumbani. Waislamu wa Uyghur wana hofu kuwa ikiwa hawatafuata masharti, basi watakamatwa, na wakijaribu kuondoka na kutotii masharti ya maafisa, basi watapigwa risasi mara moja. Wakazi wa mji huo, wamenyimwa vyakula, vinywaji, dawa na mahitajio mengine msingi kwa siku ishirini. Kwa matokeo ya hivi vizuizi vilivyotiwa chumvi na malengo ya kuwaangamiza Waislamu wa Uyghur, watoto wengi, wazee, wanawake na hata watoto wachanga, wanakufa kwa njaa katika majumba yao, na wengine waliobaki wanapiga siyaa na kulalamikia maumivu ya njaa. Vilio vyao vimefika angani. Kina mama wanalia kwa kuwa hawawezi kuvumilia vilio vya watoto wao, wakisema, mimi ni mwanadamu! Watoto wangu wanakaribia kufa! Watumwa wao kwa wao wanapatiana vyakula ambavyo hata wanyama hawawezi kula! Hii ni mojawapo ya operesheni za mamlaka za China katika kuwaangamiza Waislamu wa Uyghur! 

Uhalifu huu unafanyika mbele ya Waislamu bilioni mbili, na Wachina hawaogopi kwa matendo yao ya ukatili kwa sababu wanapata ujasiri kupitia viongozi wasaliti wa Waislamu ambao wanawaunga mkono au wanayafumbia macho matendo ya Wachina dhidi ya Waislamu wa Turkestan Mashariki,

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿

“Ni viziwi, mabubu, vipofu na kwa hivyo hawaelewi.” [AL-Baqara: 171] 

Haya yote yanaonyesha kiasi cha uzembe wa watawala wa Waislamu na vilevile hizaya na uhalifu wa viongozi wa unaoitwa ulimwengu huru. Katika ulimwengu ambao unaonyesha hisia kwa kifo cha mbwa na hawafanyi lolote usoni mwa vifo vya maelfu ya watu wanaokufa kwa ajili ya njaa. Nchi za Kimagharibi, Marekani na Umoja wa Mataifa, ambao daima hudai ubinadamu na kudai kuwa watetezi wa uhuru na ubinadamu, hawajafanya lolote kukomesha uhalifu wa China; kwa sababu wao hufanya jambo wakati manufaa yao yanahusika, na huu ndio umekuwa mtindo!

Taifa hilo limeonja uchungu wa kukosekana kwa Khilafah. Kama wangekuwa na Khalifah kama Harun Al-Rashid ambaye alimwandikia mfalme mkuu wa Byzana, akisema “Majibu ni yale unayoyaona, sio yale unayoyasikia, ewe mwana wa kafiri,” na mfano wa Khalifah Al-Mu’tasim aliyejibu kilio cha mateka, mwanamke Muislamu aliyedhulumiwa kwa jeshi la Armam, na kisha akaifungua Amuriya, je, China inayomkana Mungu ingeweza kuwakandamiza ndugu zetu Waislamu katika nchi yao?! La, haitasubutu, hatujasahau jibu la mfalme mkongwe wa China kwa kiongozi Qutaybah bin Muslim Al-Bahili, Waislamu waliishi kwa hadhi chini ya dola yao ya Kiislamu. Leo, vile vile, njia pekee ya kukwepa ukandamizaji wa China ni kwa kusimamisha Khilafah Rashida, na kurejesha fahari kwa Waislamu.  

Wauyghur ni watu wenye dini, ambao walisilimu karne nyingi zilizopita na wanashikamana na dini yao licha ya kuteseka, kushikwa, mateso na ubakaji wa makafiri na hawajawahi kusalimu amri. Nao ni sehemu ya Ummah wa Kiislamu, na kuteswa wanakopitia sasa ni kwa sababu ya imani zao. Mwenyezi Mungu, Mtukufu amesema:

﴾ وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيد ﴿

“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.” [Al-Burooj: 8] 

Waislamu wapendwa; Mtume wetu, rehma na amani ziwe juu yake, amesema, akiwasifu Waislamu; 

مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ؛ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى

“Mfano wa waumini katika mapenzi yao na kuoneana hurumu kwa na kuoneana upole kwao ni kama mwili mmoja, kiungo kimoja kikipata uchungu, viungo vyengine hujibu kwa kukosa usingizi na homa.”

Kwa hivyo; ninawaalika nyote kufanya kazi kurejesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kwa sababu ndio njia pekee ya kuwanusuru ndugu zetu Waislamu wanaoteswa kote duniani, kwa kuwa ni Khilafah pekee itawaokoa kutokana na dhulma za makafiri na kuwaleta katika haki ya Uislamu, kwa maana nyengine ni kuwaleta katika furaha ya hapa duniani na kesho Akhera.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu