Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je, Jamii ya Waislamu ina Dori katika Kuamua Uchaguzi wa Marekani?
Na: Dkt. Abdullah Robin

(Imetafsiriwa)

Katika mkesha wa uchaguzi wa urais wa Marekani, Waislamu milioni 2.5 waliojiandikisha kupiga kura wanauliza jinsi gani wanaweza kuleta mabadiliko. Hawakubaliani kuhusu jinsi tofauti hiyo inavyofanyika, lakini kheri katika nyoyo zao inawaunganisha katika hamu yao ya kuona mauaji na maangamizi nchini Palestina na Lebanon yanafikia mwisho kwa namna fulani. Chama cha Demokrat kiasili kimechukua kura nyingi za Waislamu. Katika uchaguzi wa 2020, wapiga kura wengi walichagua kumpigia kura Biden ili kumuondoa Trump aliyechukiwa ambaye alifurahisha umbile la Kizayuni kwa kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka ‘Tel Aviv’ hadi Jerusalem, na hivyo kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa umbile la Kizayuni. Trump alipiga marufuku kusafiri kutoka kwa baadhi ya nchi za Waislamu na kuwachukiza Waislamu. Kisha akaja Biden, Mzayuni mkubwa zaidi katika historia ya Marekani ambaye alilipatia umbile la Kizayuni shehena za silaha ambazo hazijawahi kushuhudiwa ambazo zinaweza kuua makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia. Ingawa wanadamu kote ulimwenguni wameshangazwa na kile kinachotokea, hakuna uhalifu ambao umekuwa wa kutisha vya kutosha kwa Biden kuacha kuchochea mauaji kwa silaha zake.

Sasa katika mkesha wa uchaguzi wa Marekani, huku Makamu wa Rais Harris akisimama kama mgombea wa Democrat, Waislamu wengi wanakihama Chama cha Demokrasia kwa sababu ya ushiriki wao wa uhalifu katika uharibifu wa maisha na mali huko Gaza na Lebanon. Kura ya maoni ya kitaifa ya wapiga kura Waislamu 1,449 ilionyesha Trump akiwa na asilimia 10 pekee ya uungwaji mkono wao, huku Harris akipata 41% na mgombea wa chama cha tatu, Jill Stein, alipata kibali cha juu zaidi ingawa hana nafasi ya kushinda uchaguzi huo. Kuna majimbo 7 ya Marekani ambapo kura elfu chache zinaweza kuamua iwapo Trump au Harris atashinda uchaguzi, na Waislamu wengi nchini Marekani wanataka kuwaadhibu Wanademokrat kwa kupiga kura dhidi ya Harris ingawa hilo linaweza kumfanya Trump anayechukiwa kushinda.

Trump anatafuta kura za Waislamu. Katika mkutano wa hadhara huko Detroit, Trump aliwasifu Waarabu na Waislamu akisema kuwahusu: ‘Hawakubaliani na shughuli za watu waliobadili jinsia. Hawakubaliani na wanaume kucheza michezo ya wanawake.’ Baadhi ya Waislamu wanamuunga mkono Trump kwa sababu ya maadili yake ya kihafidhina na wengine kwa sababu anaahidi kumaliza vita, ingawa hakuna anayejua atafanyaje hivyo. Imam mmoja wa Kiislamu aliutangazia umati wa watu: ‘Sisi, kama Waislamu, tunasimama na Rais Trump kwa sababu anaahidi amani, si vita … umwagaji damu unapaswa kukomeshwa duniani kote. Na nadhani mtu huyu anaweza kufanya hivyo. Binafsi naamini kuwa Mungu aliokoa maisha yake mara mbili kwa sababu’. Je, Waislamu wanaweza kufanya mabadiliko? Wanaweza kujiunga na mchezo, lakini wengine wanaweza kupanga meza na kuamua sheria. Swali kubwa zaidi linapaswa kuwa: Je, kuna Muamerika yeyote anayeweza kufanya mabadiliko, sio tu Waislamu walio wachache nchini humo? Nguvu zinazofadhili siasa nchini Marekani zitatoa kafara dunia nzima kwa ajili ya maslahi yao na zitatoa kafara wapiga kura wa Marekani pamoja nao. Wapiga kura huchagua tu kati ya vikaragosi wawili.

Wapo wanaosema kuwa Wazayuni wanadhibiti siasa za Marekani, huku wengine wakisema kuwa Marekani inatumia Uzayuni kwa maslahi yake katika Mashariki ya Kati. Yeyote unayefikiri anaendesha siasa za Marekani, unaweza kuwa na uhakika kwamba wanafanya hivyo kwa malengo yaliyo kinyume kabisa na uadilifu na maadili ya hali ya juu ambayo Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waislamu kuyatumia na kuyaeneza duniani. Kwa sababu hii, kama Trump au Harris, wawe Mayahudi au wengineo, mabepari ambao utajiri wao na uwezo wao unategemea mfumo wa riba na utiishaji wa ulimwengu wataendelea kutafuta maangamivu ya Uislamu kwa njia yoyote ile, na mfumo wa demokrasia na kauli mbiu zinazohusiana nao ni milki yao. Wanalipia kumbi za demokrasia ya umma na kuchagua watendaji ambao watasimama mbele yako. Kwa hiyo, Waislamu nchini Marekani, kama ilivyo kwa Waislamu popote pengine duniani, wana njia moja tu kuelekea kwenye mabadiliko yenye maana na hiyo ni njia ya siasa za Kiislamu kwa mujibu wa mfumo na njia ya Uislamu. Nchi za Magharibi, huku Marekani ikiongoza, zimeonyesha waziwazi uhalisia wa mfumo wake fisadi. Ujumbe umeandikwa kwa ajili yetu kwa damu nyekundu ya maelfu ya mashahidi watoto chini ya mchanga na chini ya vifusi vya ardhi zetu takatifu. Yeyote asiyeweza kusoma ujumbe huo hatanufaika hata akisoma maelfu ya vitabu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu